Barua Kwa Rais Jakaya M Kikwete-Usipoangalia Utaiacha Nchi Imevunjika Vipandevipande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua Kwa Rais Jakaya M Kikwete-Usipoangalia Utaiacha Nchi Imevunjika Vipandevipande

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaldinali, Oct 28, 2012.

 1. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  RAIS WANGU KIKWETE BILA UMAKINI UTAIACHA NCHI KATIKA VISASI!

  Rais wangu niliyasikiliza kwa makini sana mawaidha yaliyotolewa katika
  swala ya Ijumaa iliyopita kama yalivyorushwa na kituo cha televisheni
  cha TBC. Sheikhe alielekeza mawaidha yake katika maisha ya kiongozi wa
  uma mtume Mohamad (SAW) na mafundisho yake.

  Alisema mtume aliwafundisha waumini wake kuwapenda wengine hata kama
  wale wengine siyo waislamu. Akahubiri amani na kuwataka waumini wake
  kuwa watu wenye subira. Akasema hata ilipokuwa lazima kuingia katika
  vita aliwaasa kutowadhuru akina mama, watoto, miti na mimea mingine.
  Mawaidha yale yanamfanya mtu yeyote makini kujua na kuelewa kuwa
  vurugu kama zile za Mbagala na zile za ijumaa iliyopita Kariakoo
  haziko kwa mujibu wa dini ya kiislamu. Siyo uislamu ule! Ni vurugu na
  fujo za wahuni fulani wanaotaka kuitumia dini vibaya.

  Rais wangu ugaidi hauna dini. Ugaidi hauna kabila. Isipokuwa magaidi
  wanapotaka kutekeleza matakwa yao ya kigaidi hutafuta mwavuli kwa
  lengo la kutaka kuungwa mkono na maamuma na magaidi wenzao wengine.
  Ndiyo maana utakuta magaidi wanaotumia ukabila kama wasomali au dini
  kama ukristu au uislamu. Watu wa namna hii ni magaidi tu popote
  wanapopatikana duniani, hata kama ni hapa kwetu Tanzania!
  Unateteaje uislamu kwa kuvunja vioo vya gari la mwislamu mwenzako?
  Tena ni muislamu tunayemjua kuwa ni swala tano! Hiki si kitendo cha
  kiislamu, hiki ni kitendo cha kigaidi.

  Ndugu Rais ni nani ameleta ugaidi nchini mwetu? Ugaidi nchini mwetu
  umeletwa na wanasiasa uchwara, wachovu, waliofirisika kisiasa.
  Wanasiasa dhaifu walipoona kampeni za chaguzi mbalimbali zinawaelemea
  na hasa uchaguzi mkuu 2010, ndipo wakaanza kupandikiza sumu ya udini
  ambayo sasa namshukuru Mungu imeanza kuwatafuna wenyewe. Nayo
  itawamaliza vibaya muda si mrefu kwasababu sheria za magaidi ziko
  wazi.

  Siku zote Watanzania wamekuwa hawana udini lakini viongozi dhaifu
  wakawa wanalazimisha wananchi waone kama kuna udini miongoni mwetu.
  Watanzania kwa jadi yao siyo wadini. Tumekuwa na umoja, upendo na
  mshikamano kwa muda mrefu sana. Na hata sasa Watanzania hawana udini.
  Lakini tunao baadhi ya viongozi wanaolazimisha udini kwa maslahi yao
  binafsi. Maamuma hawakosekani, wanawapata baadhi wanawaunga mkono.
  Hali hii ya sasa inaweza kutazamwa kama ifuatavyo; Malofa hawa wa
  kisiasa na hawa ambao wao walidhani ni maamuma wa kila kitu wakaunda
  timu ya ushindi huku wanasiasa hawa wachovu wakiwaahidi karibu kila
  kitu. Makundi haya mawili ambayo sasa yakawa kundi moja kila kundi
  likiwa na lengo la kutaka kutawala nchi. Wakati kundi la wanasiasa
  likianika wazi lengo lake, wenzao walifanya siri. Ili kufanikisha
  lengo kila kundi liliona ni muhimu kupanda kwenye mgongo wa kundi
  mwenza.

  Wanasiasa ndio walioanza kuwapanda wenzao, wakafanikisha. Ushindi
  ulipopatikana utekelezaji wa ahadi ukawa mgumu. Kuwaachia wenzao nao
  wawapande mgongoni ili watimize lengo lao ni sawa na kuwaachia nchi.
  Ikawa haiwezekani.

  Rais wangu vurugu zote hizi ni kundi mwenza kulazimisha kundi la
  wanasiasa kutimiza ahadi zao kama walivyokubaliana. Hapa hakuna dini.
  Hapa kuna ‘dili!’ Watu wamegeukana wenyewe kwa wenyewe. Ndiyo maana
  hata kuwakamata imekuwa ngumu kwao. Watu wanasimama hadharani na
  kukashfu dini za wengine serikali inachekelea tu. Magazeti yanatukana
  huku radio na TV fitinishi vikitumika kukashfu dini zingine, serikali
  inachekelea tu! Mungu mkubwa sasa yamewafika!

  Ndugu Rais waliosema mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa binadamu mchungu,
  hawakuwa wajinga! Yanapochomwa makanisa serikali inacheeka huku ikitoa
  machozi ya Mamba! Sasa mkuki umegeuka, serikali inashangaa, ‘Ala,
  kumbe! Jambo la hatari, tunachekelea?’ Lakini wamechelewa!
  Katikati ya kadhia hii anatokeza waziri na kupiga marufuku mihadhara
  ya kashfa kwa siku thelathini pekee. Yaani baada ya siku thelathini
  kashfa ruksa ziendelee! Kupiga marufuku moja kwa moja kashfa
  zinazotolewa dhidi ya dini nyingine kupitia mihadhara, magazeti, radio
  na televisheni haiwezekani kwasababu ukifanya hivyo utakuwa unavunja
  makubaliano. Na bado kidogo wanajua watawahitaji hawa; uchaguzi si
  umesogea? Ni kweli kabisa, ‘tutapata wapi waziri kama huyu!’ Hawa
  ndiyo viongozi wetu! Sijui ni mikosi gani awamu hii ilizaliwa nayo!

  Rais wangu katika hali kama hii wananchi watamsahau vipi Waziri wa
  Mambo ya Ndani wa ukweli, Augustine Lyatonga Mrema? Nikikumbusha
  utendaji wa mtu mahiri mjinga anadhani anabebwa mtu. Ni mbebe Mrema,
  nimpeleke wapi? Umahiri wake katika utendaji kazi ndiyo unaombeba.
  Naandika kuililia nchi yangu na amani kwa watu wake. Siandiki
  kumfurahisha mtu. Ninaandika ninachokiamini kuwa ni sahihi. Kudhani
  naweza kuandika anavyotaka mtu fulani au kwa upambe na kushabikia, ni
  udhalilishaji. Badala ya kukumbatia vinavyowaunganisha wapuuzi
  wameving’ang’ania vinavyowatofautisha!

  Rais wangu sitasita hata siku moja kuhoji ukimya wa waziri mkuu wangu
  katika wakati huu ambao taifa linapita katika majaribu magumu hata
  kama kwa kuhoji huko kutaifanya milima itikisike! Amani imetoweka.
  Hofu katika mioyo ya wananchi imetamalaki. Wananchi wanaishi katika
  wasiwasi mkubwa huku kanisa likilia machozi! Kwa tishio kubwa kwa
  amani ya nchi kama hili waziri mkuu kuwa kimya na kuonekana kama
  hayupo haliwezi kunyamaziwa hata kidogo!

  Mwanamwema Kija kutoka Njiro, Arusha akaniandikia, “Umesema kweli
  mwalimu mkuu wa watu, Pinda siyo kama hayupo ni hayupo kabisaa! Mimi
  naona serikali yote haipo. Nchi imewashinda sasa wanyonge hatumwoni
  wakumshika mkono! Pamoja na yote Edward Lowassa ndo waziri mkuu pekee
  angalau alifanya kazi! Yaani haingii akilini mpaka sasa Pinda hajasema
  chochote, ama ni mgonjwa wametuficha?”

  Rais wangu, Pinda lazima aliliwe hata kama mbingu zitaanguka kwasababu
  alipoteuliwa kuwa waziri mkuu aliwapa matumaini makubwa wananchi
  ingawa yeye mwenyewe hakujua! Wananchi walijawa na matumaini makubwa
  kwasababu Mizengo Pinda wakati hila za kutafuta madaraka zilipokuwa
  zikifanywa na baadhi ya viongozi waliopo madarakani hivi sasa yeye
  hakuwa mmoja wao! Hivyo wananchi walidhani angekuwa na nafasi nzuri ya
  kuwa upande wao kwa maana wametelekezwa! Yeye hakuwa katika
  majadiliano na wafanya vurugu wa sasa! Hawamdai kitu chochote.
  Kama vile haitoshi, serikali imetangaza balaa la njaa! Ukimya huu wa
  mtendaji mkuu ukiendelea unadhani nini kitatokea? Siyo kwakutaka kwetu
  bali tunalazimishwa kukumbuka balaa la njaa lililopita. Tulishuhudia
  Waziri mkuu Edward Lowassa alivyokuwa wakihaha nchi nzima kuhakikisha
  maisha ya Watanzania hayapotei kwa sababu ya njaa. Nani asiyekumbuka
  ziara ya Waziri mkuu Edward Lowassa kule Same? Njaa imeshika kasi,
  wananchi wanataabika kwa njaa, mkurugenzi kakaa na mahindi ya njaa
  ofisini! Eti Same yote hakukuwa na mtu mwenye uwezo wa kuyasafirisha.
  Mtu huyu hakuwa na kile wadhaifu wanaita maamuzi magumu. Aliamua
  mahindi yagawiwe kwa wananchi akiwepo! Wakati wakuondoka kurudi Dar es
  salaam akaondoka na mkurugenzi; kazi ya mkurugenzi ikawa imeisha.
  Mwangwi wake ukaenea katika masikio ya wakurugenzi wote nchi nzima!
  Nani ataichezea serikali kwa kuwatesa wananchi? Kungekuwa na ukimya
  kama huu kule Same wangekufa wananchi wangapi?
  Lazima Waziri mkuu atokeze aseme na wananchi wanaoishi kwa wasiwasi
  katika nchi yao. Atokeze awajibu Maaskofu wanaolia! Asimame akemee
  ugaidi huu!

  Maaskofu wanahoji, “Watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe?
  Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai
  washtuke? Wamue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa
  usalama wa Taifa letu?”

  Ni nini hiki wanachosema Maaskofu kuwa, “Katika mateso haya kanisa
  litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala Tanzania mpya
  itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana?”

  Kabla yakusema hayo walisema, “Kilichotokea Mbagala katika wiki ya
  kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa baba wa Taifa tu,
  bali kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa.”
  ‘Kebehi kwetu sisi wenyewe tuliokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa’.
  Ni nani huyu aliyekalia kiti cha Baba wa Taifa anayefanyiwa kebehi hii
  halafu hajiwezi hata kujibu? Ninachokiona hapa ni kuchokwa na kutengwa
  kwa waliokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Kwasababu mbegu
  waliyoipanda na kuaicha ikomae imeamua kupeleka machungu yake Ikulu,
  basi matumaini ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, umoja,
  mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini kuzaliwa,
  yatatimia! Ukombozi wa kweli utapatikana!

  Tumeona katika kundi la watu waliofikishwa mahakamani ni mchanganyiko
  wa makabila mbalimbali. Ni mchanganyiko wa dini tofautitofauti. Ni
  mchanganyiko wa kada mbalimbali, vibaka, waporaji na wakora wote pia
  wamo.

  Hivyo siyo sahihi hata kidogo kuwatambulisha waliokamatwa wakifanya
  uhalifu kwa kutumia kigezo kimoja tu cha dini. Kuwaita hawa wafanya
  vurugu waislamu ni kutaka kuidhalilisha dini ya Mwenyezi Mungu kwa
  kuihusisha na ugaidi. Uislam ni amani, upendo na uvumilivu! Kuchoma
  makanisa ni ugaidi bila kujali kama waliochoma makanisa hayo ni
  Wanyamwezi kwa kabila lao au Waislamu kwa dini yao!
  Ni vema jamii na hasa viongozi wetu wa serikali na vyombo vya habari
  kuacha kupotosha kwa kuwatambulisha waliotenda ugaidi huu kuwa ni
  wanaharakati wa dini ya kiislamu. Waumini wema tuwakatae watu hawa na
  hasa wakati huu ambao baadhi ya viongozi wetu wamekuwa kama samaki
  waliomeza chambo chenye ndoani. Imebaki kuvuliwa tu!

  Rai yangu kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba
  na wanatume wenzake wote watambue kuwa nao pia ni wananchi, hivyo
  wasisahau kutoa maoni yao. Kati ya maoni yao wahakikishe katiba
  itakayopatikana inaelekeza kwa uwazi njia halali ambazo wananchi
  watazitumia kuitoa madarakani kabla ya muda wa uchaguzi, serikali
  itakayothibitika kuwa imeshindwa kuongoza.

  Moja ya sababu kubwa ambayo itoshe kuiondoa serikali iliyoko
  madarakani ni pale itakapofikia uamuzi wa kuligeuza Jeshi la Ulinzi
  wa wananchi JWTZ kuwa jeshi la kupambana na wananchi. Matumizi ya
  Jeshi bila idhini ya Bunge ndivyo walivyokuwa wanafanya akina Iddi
  Amin, Bokassa, Hittler na wenzake! Katika utawala uliostaarabika
  kidemokrasia hii ni dhambi kubwa haikubaliki.

  Nyingine iwe ni serikali kutuhumiwa kwa unyama na mauaji ya raia wasio
  na hatia na hivyo kuwafanya wananchi waishi maisha ya hofu! Nchi kujaa
  migomo na vurugu zinazowafanya wananchi kukosa amani nchini mwao.
  Rais wangu hapa mlipowafikisha wananchi, nchi inatengeneza visasi
  vingi! Bila kuwa makini kitakachofuata baada ya wewe kuondoka itakuwa
  ni kulipizana visasi tu! Tutawaficha wapi watoto wetu na wana wa nchi
  hii?

  Robert Manumba mkurugenzi wa upelelezi nchini, akimlilia kamanda wa
  Polisi wa mkoa wa Mwanza aliyeuawa na majambazi amewaamrisha Polisi
  walipe kisasi dhidi ya raia. Ni tamko la bahati mbaya kwa wadhifa
  alionao!
  Wanawema wakaniambia mwalimu mkuu tushitakie huyu mtu kwa baba yako!
  Kumbe baba ulikuwa Oman. Iweje uahirishe safari ya kwenda nje kutokana
  na kifo cha mwigizaji wa michezo huku ukitoa ubani wa milioni kumi
  halafu uende Oman wakati mauti yamemfika Kamanda wa Polisi wa mkoa wa
  Mwanza, Liberatus Barlow?

  Madhali baba Mwenyezi Mungu amekujalia umerudi salama wajibu watu
  wako! Watu wa Mungu wanauliza je, na raia nao watumie amri hiyohiyo ya
  Manumba kulipiza kisasi kwa Polisi majambazi waliowapora mali zao na
  kisha kuwaua kinyama wanawema wafanyabiashara wa madini wa Ulanga na
  dereva Taxi katika msitu wa Pande? Baba bila kuwa makini utaiacha nchi
  katika visasi vya maangamizo!

  PASCHALLY MAYEGA: MAKALA GAZETI LA TANZANIA DAIMA 10-24-2012
  TEL 0713334239
   
 2. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Long insha
  Umejitahidi
  Ila tatizo sio uongozi ama rais wetu
  Kikwete ni madhubuti na mtanzania kweli
  Lakini kuna tatizo la ubaguzi na chuki nchi hii kila akiwa kiongozi Muislam basi kuna njama za chini kwa chini ku sabotage utwala wake lengo asitokee kiongozi hasa muislam kuweza kumpita kwa utendaji Nyerere
  Huu ndo msimamo wa viongozi wa kanisa kwa hiyo kama mnapenda kweli amani na utulivu basi waambieni pia viongozi wenu wa kanisa kwamba mahubiri yao ya ubaguzi kwa Rais hauna maslah kwa taifa
  Lakini haya yaliotokea sasa ya kuchoma makanisa sasa kuna kila dalili kwamba makanisa yalia jiri wahuni kuchoma na kuharibu lengo
  Ni kutafuta nafasi ya kuwafitini viongozi wa waislam na pia kutaka kuonesha kikwete anashindwa
  Hivyo tunajua karibu viongozi wote wa makanisa wana passi 2 za uraia hivyo chonde chonde wasituharibie nchi kama Rwanda walivofanya
  Waliwaua watu ndani ya makanisa na wao wapo vatican na huko Pope
  Hakubali kuwaleta kushtakiwa
  Hivyo tuwe makini na makanisa na malengo yao
  Makanisa yote makao yapo nje ama ujerumani au vatican ama uingereza au marekani
  Huko ndipo kunakotolewa maagizo kwa kutumia makanisa na yanatumika kama agents wa ukoloni mwengine Africa na. Amerika kusini na mbinu wanazo zitumia ni pamoja na ugaidi ili kufikia malengo yao ya kuendelea kuwa na sauti katika mataifa haya na Tanzania ikiwemo
  Nadhani Warioba na wenzake waweke maslahi ya taifa mbele
  Katiba isiruhusu mfungamano wa dini ambao viongozi wa hapa wanakua wapo chini ya mamlaka ya nchi nyengine , uongozi wao uwe mwisho na viongozi wa taasisi za dini wachaguliwe hapa hapa tanzania
  Nyerere alivunja jumuia ya waislam kwa sababu kiongozo wao mkuu hakua Mtanzania alisema wenyewe wanaweza
  Lakini akasahau upande wa pili wa kanisa ambao nao mabosi wapo nje na ni hatari sana linapokuja conflit of interest
  S
  China wamefanya haya na mpaka leo juu ya wingi wa watu utengamano upo
  Pia katiba litambue kuwepo dini Tanzania na kuunda wizara jamii na masuala ya imani
  Na iundwe tume huru kuchunguza uchomwaji makanisa zanzibar na mbagala kwani kuna dalili za mikono ya watu wengine kama makanisa kuhusika


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 3. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]CHRISTIAN MISSION FELLOWSHIP[/FONT]
  [FONT=&quot]P.[/FONT][FONT=&quot]O. Box 55024 Dar Es Salaam Tanzania, E-mail:[/FONT][FONT=&quot]info@cmftz.org[/FONT][FONT=&quot], website: [/FONT][FONT=&quot]www.cmftz.org[/FONT][FONT=&quot][/FONT]​
  [FONT=&quot] Tel: 0715200551, 0755200550 : Tarehe 28/10/2012[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI NCHINI[/FONT]
  [FONT=&quot]Neno la Mungu limetuagiza katika 1Timotheo 2:1-2; kuwa, kabla ya mambo yote nataka DUA, SALA, MAOMBEZI NA SHUKURANI vifanyike kwa watu wote; kwaajili ya Wafalme na wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Tukiwa Kanisa la Mungu, tumechukua hatua hii ya kuanza kuliombea Taifa kwa kuugua mno ili Amani tuliyopewa na Mungu na kuenziwa na waasisi wa Taifa hili iweze kudumishwa.[/FONT] [FONT=&quot]Ndugu zangu Watanzania sote tufahamu kuwa, msimamo tuliyojiwekea katika Katiba yetu ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, ni kupiga marufuku kila namna ya ubaguzi ukiwemo wa kijinsia, rangi na kidini. Katiba Ya 1977 Ibara 13(5).[/FONT] [FONT=&quot]Kwa upande wa madhehebu ya Dini Tanzania tuna dini kubwa tatu na nyingine ndogondogo; Dini kubwa ni Ukristo, Uislamu na Dini za Kijadi. Wakristo na waislamu tumekuwa tukishirikiana pamoja katika misiba, sherehe mbalimbali, kuoleana, kuishi katika Nyumba moja na kufanya shughuli za Kijamii kwa pamoja bila kubaguana kabla na baada ya miaka hamsini (50) ya uhuru Nchi yetu. [/FONT][FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]Ndugu zangu wakristo na watanzania wezangu kwa ujumla napenda kuwafahamisha kuwa, hakuna nchi yeyote katika bara la Afrika yenye idadi kubwa ya wakristo na waislam wanao ishi kwa amani na upendo kama Tanzania.Ila kwa sasa watu wasioitakia amani Nchi yetu wanataka kupenyeza chuki za kidini ili isiwe nchi ya amani bali vurugu.[/FONT] [FONT=&quot]Hivi karibuni, tumeshuhudia kuwepo kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa kidini kwa baadhi ya vikundi toka makundi ya dini kubwa kudai haki zao ambazo kimsingi wanaona wanastahili kuwa nazo sawa na Dini nyingine. Hali hii imefanya vikundi hivi vitumie vyombo vya habari; Mathalani: Redio, Magazeti na Machapisho mbalimbali kueleza hisia zao kwa Jamii, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgawanyiko katika Jamii iliyokuwa imeshikamana. Aidha, mgawanyiko huu unazidi kukua na kusababisha hali ya Chuki kwa mamlaka ya Nchi, na hatimaye Dini moja na nyingine. [/FONT] [FONT=&quot]Baada yakufanya utafiti wa kina kwanini kuwe na Chuki baina ya makundi ya Dini na Serikali tumeona kuwa, makundi haya ya Dini yanaiona serikali inawanyima haki zao na inapendelea Dini moja na hivyo kutumia mfumo wake katika utawala. Hata hivyo, Madai ya kundi hili yanawapelekea kuwafanyia Vurugu waumini wa kundi wanalosadiki kuwa linapendelewa na Serikali, jambo ambalo linawafanya (wanaofanyiwa vurugu) wasitumie uhuru wao wakufanya ibada ambao kimsingi wamepewa Mungu na kuandikwa katika Katiba ya Nchi Yetu.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]Tukiwa Kanisa la Mungu, hali hii inatupelekea kuona kuwa bado serikali yetu haijawajibika ipasavyo katika kuelekeza sera na shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria za Nchi zinalindwa na kutekelezwa. Kimsingi, haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma vinapaswa kutoathiriwa kabisa na matumizi mabaya ya uhuru wa haki za watu binafsi. [/FONT] [FONT=&quot] Hivyo, Kanisa baada ya Kumlilia Mungu kwa machozi na maombi mengi, tumeamua kuchukua mwelekeo wa uwajibikaji usio wa maneno tu; kwani suala la kutoa matamko ya kulaani limefanywa na Dini na Serikali kwa mkazo mkubwa. Kwa upande wa Serikali, watawala wa Nchi yetu wamekuwa wakilaani na kukemea, ubaguzi wa Dini, rushwa na ufisadi katika Taifa hili bila mafanikio na hata leo tunawaona vijana wanatwangana hadharani kutokana na kushamili kwa rushwa ,hii yote ni kwa sababu hii ni vita ya kiroho na inapaswa kukemewa na viongozi wa dini na watawala wanapaswa kuchukua hatua. Kwa jinsi hii, Kanisa limelitazama jambo hili kiroho zaidi kwa kutambua kuwa chuki na rushwa ni roho kamili inayotoka kwa Shetani; hivyo watu wa kiroho tunalo jukumu la kuziopinga hila za Shetani kwa DUA, SALA NA MAOMBI ili kuleta amani ya kudumu katika Taifa letu, ambalo linasifika kuwa ndiyo kitovu cha amani Afrika na Duniani. Ndugu zangu wakristo na viongozi wa dini; ikumbukwe na izingatiwe kuwa nyumba za ibada ni sehemu ya kumwabudu Mungu, hivyo zitumike kuhubiri dini tuliyo amuriwa na Mungu na sio siasa, na pasiwe mahali pa kuandaa na kuchochea vurugu na chuki miongoni mwetu. Viongozi wa dini wanaaminiwa sana na waumini wao na lolote watakalo waambia waumini, huaminiwa kuwa limetoka kwa Mungu. [/FONT] [FONT=&quot]Aidha tukumbuke kuwa, tunafanya kila kitu vizuri zikiwemo ibada zetu kwasababu ya amani tuliyonayo. Amani isipokuwepo hakuna kitu kinaweza kufanyika katika Nchi; iwe kwa waumini na wasio wauimini, iwe kwa maskini au matajiri. Amani ikishaondoka, matajiri au wenye pesa watakimbia na kuwa wakimbizi wa Nchi zingine, huku masikini wakikosa mahali pa kwenda na kuishia kuuawa na kupoteza maisha. Kawahiyo ni vema kuitunza amani yetu na kuilinda; kamwe tusiichezee amani tuliyonayo katika nchi yetu; hii ni tunu tuliyopewa na Mungu na kuachiwa na waasisi wa Nchi yetu ili tuienzi, hivyo kila mmoja wetu ni mdau wa amani. Mkulima anahitaji amani ili aweze kupata mazao shambani mwake; daktari anahitataji amani ili afanye kazi zake vema Hospitalini, kadhalika mfanya biashara na mwanasiasa wote wanahitahi amani.[/FONT] [FONT=&quot]Nichukue fursa hii kumpongeza Kamanda Suleiman Kova kwa juhudi zake za kuifanya Dar-es-salaam iendelee kuwa bandari ya Amani; Kamanda Kova ameonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa katika kauli zake, kwani mchango wake umeleta heshima iliyotukuka katika vyombo vya dola nchini na kwa watanzania wote. Kanisa la Mungu ambao tumeitwa kw[/FONT][FONT=&quot]a Jina la BWANA, leo hii tunaomba na kuutafuta Uso[/FONT][FONT=&quot] wa BWANA tukiwakilisha zaidi ya makabila 120 ya Tanzania kwa Kutumia Lugha Zetu za Makabila kama alama ya Umoja na mshikamano wetu, tukimsihi Mungu aiponye Nchi yetu. Tunaitakia Nchi yetu amani na Utulivu, katika Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Amini.[/FONT]
  [FONT=&quot]NDIMI NDUGU YENU KATIKA KRISTO YESU [/FONT]​
  [FONT=&quot]……………………………………………….[/FONT]​
  [FONT=&quot] ASKOFU MKUU DKT. MGUL[/FONT]
   
 4. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,867
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  Leadership styles 1 Authoritarian (Dictotarship) 2. Democratic 3. Live them alone. Tanzania turudi kwenye Authoritarian tutaheshimiana na hata Wazungu hawatatutenga kwa kuwa tuna Sababu
   
 5. Mzee Msemakweli

  Mzee Msemakweli Senior Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watanzania tunayo kazi Kubwa sana ya kufanya. Maana kuuondoa huu ukoko vichwani mwa watu kama hawa si kazi ya miaka michache. Tunahitaji miaka si chini ya 50 tena yenye kazi ngumu sana ili angalau watu Kama huyu wawe na mtazamo wa kiyakinifu. Mtu hajui hata ni kwanini maiti nyingi za Watusi na Wahutu wenye msimamo wa Wastani zilionekana sana Makanisani na Mashule ya Roman Catholic. Pia hajui kuwa Nchi ya Rwanda 98% ya Wananchi ni Roman Catholic na kwamba Majeshi ya UN waliweka kambi za Kijeshi Mashuleni na Makanisani. Watu wengi sana walikimbilia huko ili wapate hifadhi ya malazi na chakula. Mara baada ya Majeshi ya UN kuuondoka; Wahutu wenye msimamo mkali wakavamia Mashule na Makanisa na kuwaua Watutsi na Wahutu wote waliokuwamo mle.

  Mtu anayewaza hata KATIBA ya Nchi iwatambue watu kwa imani zao; lazima UELEWA wake uwe wa mashaka sana. Nakushauri sana punguza mda wa kukaa madrasa kasome vizuri historia ya Rwanda utajua ni kwanini Watawala wa Kikoloni walichangia sana ubaguzi uliyopo kati ya Makabila matatu ya Rwanda yaani Wahutu ambao ni 84% wakifuatiwa na Watutsi ambao ni 15% na Watwa ambao wao ni 1% ya idadi ya Wanyarwanda.

  Jamani someni hii Elimu Dunia muondokane na upofu wa akili na muweze kuongeza vitu vya maana mbele ya Wanaume.
   
 6. x

  xlife Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very astonished that the son of president of Tanzaniariziwan was caught in china 1st jly 2012 with cocaine. And released afteragreement of massive investment and permanent for china as a bond for riziwanito escape the rope. this happen after tz ambassador in china telephonedpresident kikwete 2nd jly 2012 and give him info about riziwan saga. Andpresident phone to hu jintao and their in line for about an hour but no solution has been made. after a while bitj. kikwete phone again to hu Jintao andthen they're in line for about 18 min. after jakaya order a trip to china withfew official, arrived china 2pm and president give call to hu jintao briefinghim that he was already touching the land of china. and hu jintao sent 2official to take them before him. Then follow 8 hrs of bargain how to releaseriziwani. A concrete promise to hujintao was a massive and permanent investment for china in south corridor tosave riziwani to face death penalty. Hu Jintao accept the deal and riziwanreleased. Source one official embedded with president to china. Post a threadon Jf today after a shot time mod remove it. I think it was an order frommagogoni office.   
 7. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nashukuru kwa kumpa huyu mtu tuition maana niliposoma maoni yake sikujua hata pakuanzia. Sasa ndio naelewa kwanini kuna watu wenye msimamo kali wanaouweza kupiga mabumo hata viongozi wao wenyewe. Yaani ha watu wana uelewa mdogo sana ata ukitaka kufanya nao discussion unakuwa ujui uanze wapi
   
 8. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe tunahita Paul Kagame wa Tanzania (Authoritarian Leader)
   
 9. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kibaya duniani kama kufilisika kimawazo. Mbona Mwingi alifanya vizuri? Hakuwa mwislamu?
  Itatuchukua karne nyingi kumaliza ukoko huu vichwani mwa watu kama hawa.
  Mimi nawajua waislamu ambao wana capacity katika maeneo yao na wanafanya vizuri.
  Utaishia kudhani unaposhindwa kuna mbinu za chini kwa chini... Hakuna kitu kama hicho.
   
 10. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  M.k.w.e.r.e kutwa angani kama tai atapata muda wa kusoma waraka wote huu? Umepoteza nguvu zako bure ndugu yangu, labda mpelekee Salva akautoe kwenye Press Release! M.k.w.e.r.e anapenda Tv hapo atacheki, lakini kusoma? Hilo lilimshinda tangu akiwa UDSM.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  "Lakini haya yaliotokea sasa ya kuchoma makanisa sasa kuna kila dalili kwamba makanisa yalia jiri wahuni kuchoma na kuharibu lengo
  Ni kutafuta nafasi ya kuwafitini viongozi wa waislam na pia kutaka kuonesha kikwete anashindwa "

  Hivi kweli kuna Mtanzania mwenye akili timamu anayeamini hivyo?
   
 12. k

  kajembe JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  pole sana aisee!
   
 13. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,763
  Likes Received: 8,037
  Trophy Points: 280
  Kukosa akili ni janga kwa kweli. Nani unayemwambia awe makini na kanisa?

  Pope ndio analeta ukoloni? Kweli wewe muhuni. Kukosa kwenu uongozi unaoeleweka ndio kumepelekea leo hii mnakuwa na vikundi vidogo vidogo vyenye kupingana na kila kimoja kina msimamo wake.

  Inawauma sana kuona kanisa katoliki ni stable na lina maendeleo. Mmezoea kushindania nani kiongozi wa msikiti fulani na mambo ya uhuni unaofanana na huo. Dini yetu haiamuliwi na katiba kama ilivyo yenu ambayo hata mahakama ya kusuluhisha ndoa inataka ifanyiwe na serikali. Petro (Pope wa Kwanza) alipokabidhiwa Kanisa na Yesu, hakuambiwa kuwa aligawe kila nchi, bali aliambiwa alisimamie. Unavyoona Kanisa linasali somo fulani Jumapili hii huko vingunguti, basi jua kuwa ni somo hilo hilo linasaliwa katika kanisa la Urusi. Tutatofautiana lugha tu, lkn Kanisa Katoliki ni moja tu duniani na ndio maana hujasikia Katibu wa Kanisa kapigwa bomu kama mambo yale ya Arusha kwa kuwa hakuna anayemiliki kanisa kama ilivyo misikiti
   
 14. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2013
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  napenda mh rais aipitie tena thread hii
   
 15. scatter

  scatter JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2013
  Joined: Feb 15, 2013
  Messages: 1,200
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  hatari tupu
   
 16. akenajo

  akenajo JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 1,578
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  elimu nzuri sijui kama wakuu wanazipitia hizi dondooo
   
 17. m

  maingu z Senior Member

  #17
  Feb 17, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo mbona ndo lengo lake , ila kwa ujinga anadhani atapona, kwakuwa aliingia madarakani kwa mgongo wa ubaguzi(makundi) hivyo dhambi hiyo haitamwacha, lazima imtafune,
   
 18. Nswima John Edward

  Nswima John Edward JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2013
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 614
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Kaka umenisaidia, kweli, maana nilikuwa nafikiria namna ya kumtoa tongo tongo huyu jamaa. Kweli tuna kazi kubwa, tena nahisi hata hiyo miaka hamsini ambayo umeisema haitoshi, kazi ni kubwa sana kaka yangu. All in all, ASANTE SANA KWA MSAADA.
   
Loading...