Barua Kwa Mpenzi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Dear ,

Mwaaa

Habari zako , za moyo wako , za tabasamu lako , za kicheko chako , sauti yako na kila kitu kizuri chako ? Najua kila kitu kitakuwa safi sana kuanzia moyo wako mzuri na mtamu uliojaa upendo na mapenzi ya dhati kabisa ulio mkweli na mvumilivu .

Angalia ndani ya moyo wako , utakuta hakuna kitu cha kuficha , pengine unaweza kuficha kwa sababu ni wajibu wa kila mtu katika maisha yake , lakini linapokuja suala la kupendana basi mambo ya kuficha hakuna tena kama ukiwa na uhakika kuhusu uhusiano wako .

Nikifikiria kuhusu wewe , nafikiria kuhusu dunia ya mapenzi iliyo nyooka na iliyo katika njia sahihi kabisa , mpaka hapo jua tu mimi na wewe mpaka milele kwenye mabonde twende , baharini tuogelee hata hewani tutapaa .

Tabasamu lako ambalo ndio nalipenda zaidi , na kila mara huwa nalihisi liko mbeleni mwangu lakini kama unavyojua muda mwingi uko mbali najaribu kufikiri tu je kama tungekuwa tuko wote masaa 24 siku 7 usiku na mchana sijui ningesema maneno gani kusema za ukweli namisi tabasamu lako maridani .

Kicheko chako ambacho nikisikia moyo wangu huenda kasi kuliko wakati wowote ule , Dear labda nikuambie kitu Fulani , mimi napenda sana kusikia vicheko , unajua kuna wakati ukiwa sehemu Fulani Fulani jinsi unavyocheka ndio watu wale wanavyoweza kukuweka katika kundi gani , wewe kicheko chako nakuweka katika kundi la wanadamu maridani .

Hiyo sauti yako ni zaidi ya Coco Lee , honey kama hujui au hujawahi kusikia , Coco Lee ndio mwanamuziki wa kike mwenye sauti ya mvuto zaidi duniani mpaka sasa hivi , moja ya nyimbo nzuri kabisa aliimba na Julio Iglesius inaitwa WHEN U TELL ME THAT U LOVE ME kwahiyo wewe ni zaidi yake , pengine ungeamua kuimba leo ningekuwa naandika kuhusu kitu kingine cha zaidi .


Honey huwa napata furaha sana kila ninapopata wasaa wa kukuandikia email , kila ninapopata nafasi ya kukusalimia wewe , wengine hawapati nafasi hii kutokana na sababu zao mbali mbali , wengine hawana mikono ya kuandika , wengine wameachana na wapenzi wao , wengine wamegombana na wapenzi wao na kadhalika lakini mimi nafurahi nakuandikia email hii kwa furaha kuu kuliko zote .

Kikomo naishia hapa , naomba tuendelee kuwasiliana siku nyingine tena , mwisho wa barua moja ndio mwanzo wa barua nyingine nzuri na bora zaidi , kwahiyo usijali sana mrembo wangu .

Natamani ningekuwa kengele
Ningelia unisikie hapo ulipo
 
sawa, tumeipata hiyo iko bomba ile kinyama, ila unaweza jarbu kututumia zingine fupu fupi? wish u gud day!!
bi.
 
Ebwana Kwautamu Wamaneno Nakupa Big Up Chakuchosha Ni Urefu Wa Barabara Hadi Unasahasu Ulikotoka Na Ulivyoona Njian Kwa Kifupi Umeboil
 
jaribu tena, umechemsha vinoma. barua ya aina hii yawastahiki wanafunzi wa shule za msingi. ni demu gani wa kisasa mwenye elimu yake ya chuo kikuu unaweza mwandikia barua ya kihuni kama hii akusikilize. in short be specific and direct to the point. be realistic and smart in your approach
 
Barua kama hizi ni vigumu sana kuendelea nazo katika maisha, na punde ukiacha kuandika kama hivi mwenza wako atajua tayari una mwingine kumbe wapi umekosa muda na maneno yote umeshayamaliza. Kwa maana hiyo ni rahisi sana kuachana!
 
Ukiniandikia barua kama hii ujue sifiki mwisho na kama nilikuwa na nia ya kusema ndiyio nakacha. Imagine unaimba mshairi ya Saadan nani asikilize. Wapenzi kama hawa kwa kulalama ndiyo wa kwanza. Mungu tuepushe na wasanii kwenye mapenzi.
 
daaah! Maneno yte yake? Ila ndefu sn bna! Ataisoma ck ngp? Manake kmbka wkt anasoma aktokezea m2 anaifcha hark! Namhurumia hyo mwny saut nzr!
 
Mmmmh, ataona maneno yooote ni uongo. Bora maneno machache yenye kubeba ujumbe mzito.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom