Governor of Bettors-GB
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 10,476
- 9,601
Wakuu nimeona hili niliandike maana humu hakuna kinachobakia humhumu lazima ujumbe utafika.
Hii ni kutokana na hali ya Usalama kuwa ya kutisha saana Zanzibar kwa sasa kwa wenye Kumiliki simu.Kupigwa watu Mapanga na visu mchana kweupee na Polisi kuzembea na Hata maafa kutokea
Hii ni kuonekana kwa dhahiri kabisa kushindwa kwa jeshi la polisi.
Kumekuwa na ongezeko kubwa saana la vikundi vya wala unga na wavuta bangi,ambao kiuhalisia polisi imeshindwa kuwadhibiti licha ya kwamba woote wanafahima makwao na wala hawakimbii mtu.
Haya makundi mwanzo yalianza kuwa kwa mtu mmoja mmoja,ila sasa ni vikundi vikubwa saana.
Na Kwa uelewa wangu,na kwa jinsi Kamanda Mkadam alivyo,naamini atalishughulikia,na hii ni baada ya wachini yake kushindwa kabisaaa na watu hawa na kumpa taarifa za Uongo.
Matukio ni kama haya,na nimeandika baada ya leo kuona moja jingine.
Sasa hivi maeneo ya FUONI,JITMAI,KINUNI,MBORIBORINI,BUBUBU yanatisha saana kwa mcheo huo.
Unakuta vijana wanamapanga na visu,tena unakuta mmoja tu,anakupiga baka uachie sim,na wao ni sim tu hawataki kingine,labda uwe sim yako mbaya ndio wanakusachi.Sasa mwanzo alikuwa mmoja mmoja.
Sasa baada ya kuona usalama wao upo,basi ndio wakaanza kuwa kwenye Makundi Makubwa saana.
Maeneo ya BUBUBU na JITMAI unaweza kukuta kundi la watu 20 wapo na mapanga,na ukipita wanakupukutisha kila kitu.
Karibia wastan wa simu 50 - 100 zinaibiwa kwa siku,maana wanakuwa na mfuko kabisaa wanazijaza.
Matukio niliyoyaona na kusikia
a)Kuna mtu alipwa panga mchana na jamaa akachukua sim,akasepa
Jamaa akaenda Polisi na huwezi amini,polisi walienda kuchukua maelezo kwa watu wa karibu baada ya mwezi.
b)Kuna mama alitaitiwa na jamaa,kwanza walimdhalilisha saana,wakamwambia awape sim kisha wakamwambie atoe maziwa amnyonye,jamaa mbele ya watu akanyonya maziwa akasepa kwa jeuri
c)Kuna Mtu kwenye uwanja wa mazoezi alikuwa na sim,basi wakatokea wakachukua sim kama yake
d)Kuna mtu juzi tu hapa jamaa alichukua sim yake,alivyoatak kuleta mkwala jamaa alipigwa ngum mbili usoni na akamuambia ukileta kuremba tu nakupa panga.Jamaa akakimbia
c)Kuna mtu mzima wa kiarabu,alibanwa na jamaa atoe sim,alivyobisha wakamlamba mabapa ya panga na alivyokomaa wakampa mapanga wakasepa
d)Kuna maeneo ya Maharibiko,kuna jamaa walikata watu mapanga kibaooo,kwa kujihami,ukienda utakuta kuna watu kibao wana makovu mikononi walipokuwa wakipambana na hawa watu
e)Leo,na ndio imenikera zaidi,kuna mwanafunzi ameshikiwa Panga,na kupukutishwa kila kitu,mkoa wake na vilivyomo jamaa kasepa,wakatokea watu kusaidi jamaa akatembeza Panga,na wakati huo kuna wenzie walikuwa wanasubiri tu walianzishe.
Na ukienda Kituo cha polisi,unaambiwa tu huyu mtu na kundi lake la upande huu faili lao limejaa majina yao.Sasa waulize je hawawajui makwao,utaambiwa usitufundishe kazi.Vijana woote wanajulikana.Na ukienda polisi au ukijidai kimbelembele basi utashangaa jama wanakufuata na kukuambia kwamba tumepata taarifa zako kwamba unajifanya kwenda polisi kutuchomea.Na hii imepelekea kwamba watu kibao wanafanyiwa matukio na polisi hawaendi teena,na wengine wamesema hakluna atakaeenda polisi teeena,maana hakuna jipya wala faida ya kwenda.
Kwa fuoni tu Kesi zaidi ya 100 za watu hawa.
Sasa cha kukera ni kwamba Maeneo hayo ya matukio niliyotaja ni Fuoni.Na Mtuhumiwa huyu anakaa maeneo hayo tena 400m kutoka kituo Cha polisi cha fuoni,na huwezi amini utashangaa eti polisi wanasema wanamtafuta kumbe geresha,maana kila siku mchana yupo pale kwao.
Na nikwamba kuna siku Maeneo ya Fuoni chunga,kuna mzee wao wa huo alifanyiwa tukio la kukatwa panga na kuchukuliwa sim,kama saa sita mchana,basi siku ya pili vijana wale walichoka na hali hiyo na kuanza na wao Kuhamasishana kwamba hakuna msaada wowote Polisi,na kauli zao zile zile za kwamba Polisi ingekuwa wafuasi wa CUF basi sekunde wamo ndano,au umamsho.
Basi Ikabidi waanze kujilinda wao wenyewe kwa kutembea na Mapanga,tena cha kushangaza kuna Mmoja kati yao alikuwa na Silaha ya moto(gobole),kutwanza nzima wanajilinda wao na kutembea maeneo yoote na walifika hadi kituo cha Polisi kutoa malalamiko kwamba Wakipata hili kundi lazima wawauwe.
Sasa revenge ya ya hao walaunga na Bangi,Jamaa alichukua Canter nzima ya wahuni wenzie,na kupita mitaa ya hao vijana,na kusema kwamba anawalia timming,wakimzingua tu basi team hiyo nzima itavamia mtaani na kuuwa mmoja baada ya mwingine.Na Kundi ile lilitokea maeneo ya BUBUBU.
Ningeomba jeshia la Polisi,tusifanye kazi kwa mazoea,Zanzibar ni ndogo saaana kutawaliwa na Wala Unga.Leo hii Jeshi la ndani la KVZ linaonekana mahiri zaidi kwenye matukio kuliko hata Polisi.
Sasa hivi wanafunzi wote roho juu,baada ya mwenzao kufanyiwa tukio la kutisha.
Cha ajabu zaidi,mtuhumiwa kila mmoja kila siku anapita maeneo yao tena mbele ya kituo cha polisi,halafu wanasema wanamtafuta.Na kila siku hali ikipoea unamkuta yupo kwao,anafanya tukio leo basi kesho kutwa anarudi mtaana,akipata tena mchongo anaweka team yake sawa wanapiga issue wanasepa.Unaona eti usiku polisi wanapiga doria,na mchana mtu yupo kwao.
Kimechokera wananchi ni kwamba,ukienda polisi unaambiwa ukimuona utuite,basi ukigusa tu polisi basi unashangaa yeye mwenye anakuambia oyaa umeenda polisi basi tutakufanyizia,sasa kila mtu muoga saana.
Miaka ya nyuma mliopo Zanzibar mtakumbuka haya makundi,kuna Jamaa tena Mzee wa watu na Mkewe wakati wanarudi,basi njiani jamaa waliwazuia,then wakamshika jamaa mikono na kumuingilia mkewe woote huku jamaa akiona live,inauma saana hii hali.
Mtaniwia radhi nimeandika,kwa haraka na bila mpangilio,ni baada ya kukera na hii hali.
Ujumbe wangi kwa Mkuu wa polisi Zanzibar,Kamanda Mkadam,uwezo wako tunaujua vizuri saana.Na huwa hukurupuki.Sasa naona ulifuatilie hili mwenyewe,ila ukituma tu wakuu wa vituo vyako watakupoteza.Maana ndio wale wale taarifa zinafika kwao wao wanazembea na kukufikishia wanavyojua wenyewe.
Nakuomba Tembelea mwenye sehem hizo upate maelezo kutoka kwa wananchi na watakupa majibu ya moja kwa moja wanayopewa na vituo vya Polisi,ni aibu saana kuona kwamba raia wanajilinda wenyewe.
Itakumbuwa kwamba,kwa kuachia hawa watu,ndio ilifanya hadi wafike Stonetown.
Ambapo kuna siku walichukua sim kwa mtu,na alipojaribu kugoma wakampiga kisu na kumuuwa papo hapo tena mchana kweupee.