Barua kwa mkuu wa nchi kuhusu waziri wa utamaduni, sanaa na michezo

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,458
4,049
MH..Mkuu wa nchi pole kwa shughuli ngumu ya kuhahikisha unatetea maslahi ya wanyonge Nchini kwako.

Pia nikupongeze kwa jitihada mbali mbali unazozifanya katika kuhakikisha watanzania wote tunaishi katika usawa na haki.

Mheshimiwa miongoni mwa jitihada ulizozifanya katika kuhakikisha Kuwa maisha ya watanzania tunaishi katika haki na usawa ni hizi hapa.

1. Ukaguzi wa watumishi hewa
2.kukagua na kuhakiki vyeti halisi vya watumishi

Mheshimiwa ama hakika Jitihada hizi ziliamsha hisia nzuri kwa Wazalendo wa Taifa letu kwani masuala hayo yalikuwa na umhimu mkubwa sana kwa watanzania ikiwemo kuongeza fulsa mbali mbali kwa watu wenye vigezo na wamezikosa fulsa hizo ambazo zilikuwa zinakaliwa na watu wasio na vigezo.

Mheshimiwa wangu raisi wangu mtukufu nina imani kuwa na wewe ni binadamu na siku zote binadamu hatujakamilika kwa kila tutendalo kuna kujisahau au kuna kupitiwa hivyo basi kwa mantiki hiyo tunahitaji kukumbushwa kwa machache tunayojisahau.

Sitaki kwenda mbali sana napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuwa kutokana na sera ya Taifa letu kuwa ni nchi ya demokrasia hivyo nina uhuru wa namna moja au nyingine kumfikishia mheshimiwa kipeperushi changu pale nitakapo kuwa nimeshindwa kuwasiliana na wawakilishi wangu (wabunge).

Lengo la kipeperushi hiki ningependa mkuu wangu raisi wangu apitishe zoezi la uhakiki wa Taaluma za watumishi wako kulingana na vitengo vyao au idara zao wanazofanyia kazi.

Hii nimeiona ina umhimu mkubwa sana hata zaidi ya lile zoezi la uhakiki wa vyeti feki na uhakiki wa watumishi hewa kwani kuna watumishi wapo kwenye idara ambazo si taaluma yao jambo ambalo hupelekea kupunguza ufanisi wa kazi na maadili ya kazi pia vilevile huchangia kupoteza haki za msingi za wanajamii pamoja na kupelekea ufinyu wa nafasi kwa watu wenye taaluma mbalimbali.

Mheshimiwa nimeliona hili kutokana na kauli ya WAZIRI WAKO MH...HARISON MWAKIEMBE ambae ameonesha hadharani mbele ya jamii kuwa taaluma yake haiendani na idara yake, kwa sababu zifuatazo....

1.Waziri wa SANAA, UTAMADUNI na MICHEZO
Katika taaluma hii inahusisha vitu hivi,,

1. UTAMADUNI ni jumla ya njia zote za kimaisha zinazomzunguka mwanadamu katika mazingira yake.

2. MICHEZO, ni jumla ya vitu vyote vinavyotumika kupumzishisha, au kuliwaza akili ya mwanadamu.

3 SANAA,,neno sanaa linamaana ujuzi, uzuri,mbinu ya kipekee inayotumika katika jambo fulani,,

Kuna vipengere vingi sana katika sanaa ambavyo sitaweza kuvielezea vyote ila nitakijikita katika kipera kimoja cha mhimu na cha msingi ambacho kinaitwa FASIHI....!

FASIHI..ni mojawapo ya tawi sanaa ambayo hutumia lugha ya maneno au maandishi ili kufikisha ujumbe katika katika jamii kusudiwa.

MWANAFASIHI....Ni mtu anehusika kutunga au kuandaa kazi ya kifasihi.

Mheshimiwa Rais Kwa maelezo hayo sina lengo kuwa nataka nikufikishie taarifa kuhusu ni namna gani nilivyokuwa makini na kumwelewa Mwalimu wangu wa kidato cha pili

Ila ninalengo la kutaka kukumbusha kuwa sanaa ya Fasihi inahusu binadamu na Mwanafasihi ni chombo kinachotumika kuchambua masuala ya yaliyopo katika jamii na kuyafikisha katika jamii kwa njia ya ufundi.

Ikumbukwe kama hakuna jamii basi hakutakuwepo na sanaa vile vile hakutakuwepo na utamaduni na michezo pia, Kwani vitu hivi hutegemeana

Mheshimiwa naomba kuihusisha kauli ya mheshimiwa waziri MWAKIEMBE na na ujumbe wangu kuwa simlaumu kwa kauli yake aliyoitoa ila hii imeonesha wazi kwamba atakuwa hana Taaluma nzuri juu ya idara yake kwa kitendo alichokifanya kuwakemea wanafasihi wasifanye kazi zao kwa kuzihusisha na masuala ya kisiasa, kwa kutumia kigezo cha kuwa haina manufaa yoyote kwao ile hali ni vitu ambavyo vipo katika jamii yetu ya kila siku.

Napenda kuuliza mheshimiwa MWAKIEMBE atutajie angalau Dhima moja ya mhimu ya kazi ya sanaa,

Mheshimiwa nijuavyo mimi kwa taaluma yangu niliofundishwa na Mwalimu wangu wa kidato cha pili aliniambia kuwa kazi ya sanaa Huhamasisha maendeleo, Hukosoa, Huonya,Huelimisha, huburudisha nk...

Pia nilijifunza kupitia misemo ya Wazee wa busara kuwa akili ni nywele kila mtu anazo na ndio maana tunatofautiana hana vipato na kimaisha,
Je ni kweli kuwa wote waliofanikiwa kimaisha huimba mapenzi??

Iko wazi Mtaalamu wa macho hawezi tibu sikio hivyo ningependa mheshimiwa asiharibu sifa ya utamaduni wetu ambao Mababu zetu walimwaga damu kuutafuta.

Asiharibu sanaa yetu ambayo kutwa watanzania tunaumiza vichwa kuikuza

Asidhoofishe fasihi yetu ambayo vijana kila siku tupo darasani kuisoma na kuitengeneza.

Nahitimisha kuwa Mh... kama umeamua kutumbua majipu hebu angalia kuna majipu yaliyojificha ambayo hupelea kupoteza ufanisi katika kazi.
 
Back
Top Bottom