Barua kwa Mhe. Zitto kutoka Mtwara

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
SALAM KWA RAIS WANGU MPENDWA…..MTWARA KUNA TATIZO.

Na Baltazar B.komba.

Nianze kwa nukuu za jumbe kutoka kwa ndugu zangu na rafiki zangu wa Mtwara jumbe hizi zimezagaa katika simu za mkononi huko Mtwara jumbe hizi zinaashiria kuna jambo linahitaji kushughulikiwa kwa mstakabali mwema wa Mtwara na Tanzania kwa ujumla

Mali za kusini zilichukuliwa wakati kuna makambi ya wapigania uhuru na mali hizi zilitumika kuletea sifa taifa na mikoa mingine, Leo gesi yetu inahamishwa kwenda huko huko tunaambiwa ni mali ya taifa, je kusini ni taifa gani?Tusikubali kuondolewa gesi yetu ndio urithi wa vizazi vyetu kama wewe ni mzalendo tuma sms hii kwa watu ishirini kama na wewe unakubali kuwa fisadi kujidhulumu urithi wa watoto wako, basi nyamazia kusini bila kanda zingine inawezekana amka jitambue okoa vizazi vyako.(0652 137989)

Mikoa ya kusini ndio ilikuwa mikoa ya kimkakati katika mapigano ya vita kusini mwa afrika,Mazao yetu kama mihogo,Mpunga,ufuta na mahindi yalichukuliwa kwa ajili ya kuwachangia ndugu zetu walio kuwa wanapigana vita , na mikoa hii ilikuwa kama yenye vita kwa kipindi kirefu hali hii ilitufanye tukose fursa za maendeleo mpaka sasa, Lakini pia tukumbuke kuwa reli iling'olewa bila sababu kuwekwa wazi na sasa gesi inaondolewa bila sababu kuwekwa wazi ndgu wana Mtwara tusikubali tukatae tuma ujumbe huu kwa watu wengi uwezavyo(0715616006)

Rais wangu hizi ni jumbe zilizo ingia katika simu yangu siku ya Tarehe 24/11/2012 na 25/11/2012 zikiwa zimetumwa na wananchi wakazi wa Mtwara na siku ya tarehe 14/11/2012 nilihudhuria mkutano ulioandaliwa na TPDC katika ukumbi wa Makonde pale Mtwara mjini mkutano huu ulikuwa na lengo la kuchuka maoni ya wananchi juu ya utengenezaji wa rasimu ya sera ya gesi. KIlicho tokea katika mkutano huu unaweza kumuuliza mkurugenzi wa TPDC na najuwa hawezi kusema uongo tena kwa kuwa aliambiwa kuwa atakuja kukudanganya kuwa wananchi wa Mtwara wamefurahia sera hiyo ingawa haikuwa hivyo kilicho tokea ni wananchi kumwambia mkurugenzi wa TPDC hawaihitaji maswala ya sera wakati tayali gesi imekwisha ondoka na mikataba imekwisha ingiwa dhidi ya zao hilo na wananchi hawakutoa mawazo yao kama ilivyo kusudiwa walikataa kutoa maoni wakidai kuwa hawaja shirikishwa katika hatua zozote za uchakatuaji mradi huo muhimu kwa mustakabali wa maisha yao.

Katika salam hizi sitaki kurudia kilicho wakuta mawaziri walio ambatana na msafara wa sekretarieti mpya ya chama chetu haya najua umeshaambiwa na katibu mpya wa chama cha CCM Mzee kinana, lakini si mbaya nikakudokeza kuwa Yule mama aliye jitambulisha kwa jina la Rukia Ismail Athumani ni mama mmachinga muuza samaki katika beseni usafiri wake miguu trela yake kichwa maisha yanaenda, nafikiri umeambiwa namna alivyo mshambulia dada yetu,mbunge wetu waziri wetu Hawa ghasia juu ya suala hili hili la uchakatuaji mradi wa gesi na usafirishaji wa gesi kwenda Dar salaam, Si rahisi kwa utamaduni wa wanawake wa mikoa ya pwani wewe unajua hilo, kuwa na ujasiri mkubwa wa kuongea mbele za watu katika hadhira kama ile tena kuongea kwa kukemea kwa jazba na kumkemea mwanamke mwenzie zile ni dalili kuwa kuna tatizo linalo hitaji kushughulikiwa mapema na wewe mwenyewe ,sitaki kuongea kuhusu zile zomea zomea za wahuni…..!

Muh,Rais salam hizi sijui kama zitakufikia kwa wakati, ila kuzileta niliapa tokea siku ile nilipo hudhuria mkutano wa kutoa maoni kuhusu sera najua kipindi hiki muheshimiwa utakuwa unapumzika kutokana na majukumu mazito uliyo yafanya ya kupanga safu katika chama chetu chadema…lakini naomba unisamehe nimeoana nizitume mapema ili ratiba yako ya majukumu itakapoanza kwa siizoni hii basi ikiwezekana uje uongee na wananchi (si wazee wa chama chetu peke yao) wa Mtwara.

Muheshimiwa Rais wangu naomba unisikiliza kuhusu masuala mawili makubwa yanayo zizima hapa Mtwara swala la kwanza ni suala la gesi, wananchi hawajui chochote kuhusu gesi na unajua kama ulivyo sema siku ile ukihutubia pale Dar salaam wakati timu yetu ya ushindi ikiwa inapongezwa nakumbuka ulisema hivi nanukuu wao wakisema tusipo jibu hata kama ni uongo utakuwa ni ukweli.

Mheshimiwa Rais Mtwara wananchi wana hamu ya kujua kwanini gesi imepelekwa Dar salaam kwa bahati mbaya hakuna hata kijana wako mmoja aliye mudu kuwaeleza wananchi kwa ufasaha juu ya suala hili na dalili zinaonyesha kuwa hawajui, kwa bahati mbaya zaidi hata hawa wabunge wetu maarufu kwa jina la Kaka(mjini) na Dada(vijijini) nao wapo kimya tena hawana muda kabisa wakuongea na wapiga kura wao juu ya suala hili na wananchi wameshindwa kuwashinikiza chochote wanadai kuwa kaka alifanya mambo yetu yale wakati wa kumchagua naogopa kusema moja kwa moja kwa kuwa sina evidensi ila huyu kaka anaonekana hajui chochote juu ya wajibu wake kwa wananchi walio mchagua na wala hili ninalo kuambia kuwa ni fukuto sijui kama hata anajua ila ukweli ni kuwa Mtwara si shwari kuna tatizo


Muheshimiwa Rais jambo la pili ni Ardhi muheshimiwa Rais Mtwara ya leo sisi watoto wa Kudihalika, Nammohe, Minjale, Lupanda, Namdimba na wengine hatuna tena uwezo wa kununua ardhi hata kipande cha robo ekari kwa matumizi yeyote ardhi katika mji huu imeshakuwa ni bidhaa adimu, Manispaa wako kimya kupima ardhi na wakipima tayari imekwisha ombwa na kunamaombi mengi ya muda mrefu sijui sasa kizazi hiki kitapata wapi ardhi, na tunachoshuhudia hapa ni wanasiasa kuotesha majumba na kuporomosha vitega uchumi na kuendelea kujilimbikizia viwanja si hivyo tu muheshimiwa hata viongozi wa serikali yako nao wanajipatia maeneo huku kwa kasi ya ajabu na kwa habari tulizo zichomoa zikiwa mbichi ni pamoja na malalamiko ya madiwani eti kila wanapo kaa katika vikao vyao wanapo taka kupima viwanja wanakutana na maombi kwa ajili ya matumizi maalum maombi ambayo hayatakiwa kuhojiwa wala kuulizwa kwa kuwa ni maalum mimi mwandishi wa salam hizi nakumbuka niliandika maombi kwa njia ya barua kuomba kiwanja mwaka 2008.mpaka naandika waraka huu kwako hata jibu sijapatiwa…!

Jambo jingine ambalo kelele zake inawezekana umezizowea ni kuhusu zao la korosho kuna minong'ono huku mitaani kwetu kuwa wanao angusha bei ya zao letu hili la korosho ni hawa viongozi wetu tulio waamini kuwapa nafasi za kutuwakilisha huku katika jumba la maamuzi na kutungasheria na kisa kikubwa kinazungumzwa huku ni kuwa hao nao ni miongoni mwa wenye makampuni haya ya kifisadi yanayo jifanya yananunua Korosho kwa mfumo usiotakiwa na wananchi mfumo wa stakabadhi gharani,


Muheshimiwa kama kuna vita inakuja Mtwara ni vita ya Ardhi kwa kuwa wananchi wa kawaida wamepoteza matumaini kabisa ya umiliki Ardhi na hakuna kiongozi wetu tuliye mchagua anaye onyesha utashi wa kisiasa wa kuja na mbinu au mkakati wowote wa kumilikisha wananchi Ardhi.

Muheshimiwa Rais kupitia salamu hii tunaomba utusaidie haya yafuatayo kwanza uje utuambie tusiuze tena kura mwaka 2015, Na utuambie umuhimu wa hicho kitu kinacho itwa ARDHI katika maeneo yanayo patikana Rasilimali kama gesi au mafuta hivyo tusiraghaiwe kwa kuwauzia mafisadi wenye tamaa ya kuinunua nchi yote hii, na uje uwaambie mafisadi na viongozi wa kisiasa na serikali wanao jilimbikizi a ardhi kuwa hawataweza kuikalia kwa starehe kama hawa maskini wengi wataendelea kuitwa wavamizi katika ardhi ya mababu zao, lakini kubwa zaidi uje na mkakati maalumu wa kuwafanya vijana wa Mtwara walio poteza matumaini ya kuwa wana Mtwara kwa kuwa hawana uhakika wakuendelea kuwa Mtwara kwa kukosa ardhi uwasadie wapate ardhi,

muheshimiwa Rais yanayotokea katika nchi za wenzetu yaweza tokea kwetu na dalili zimeanza kuonekana maana viongozi wakisiasa na serikali wanajilimbikizia maeneo kwa kuendelea kuwalaghai wazee maskini wawauzie bila kujali kuwa maeneo ya Ardhi hayapanuki na watu wanaongezeka hali hii inasababishwa na uwepo wa uwekezaji wa gesi na mafuta.

Lakini umaskini, kukosa elimu kutokana na mlimbikizo wa mkoa huu kukosa fursa ni sababu za msingi za wakazi wake kutokuelewa umuhimu wa masuala ya umiliki wa ardhi, sawa na sheria ya ardhi na 5 ya mwaka 1999.


Tukumbuke kuwa wajukuu zetu watahoji asili zao na wataambiwa kuwa wao ni wana Mtwara achilia mbali wamakonde,wayao,wamakuwa,wangoni,wamwela na wataonyeshwa makaburi ya baba,bibi,babu zao wakiwa wamezikwa katika Ardhi ya Mtwara lakini wakati huo watakuwa hawana hata kipande cha Ardhi na watakuwa wanaiona ardhi inayo milikiwa na Mushi, Shirima, Mrema, Mfinanga, Mkama, Bundala katika hali kama hiyo maswali yatakuwa mengi kuliko majibu na mwisho wake watakuwa hawana cha kupoteza na hatua ya kukosa cha kupoteza ikifika maamuzi yeyote yanaweza kufuatwa tusishangae kuona ya Biafra yakitokea pia hapa kwetu mungu apishe mbali

Mimi ninaye kuandikia salaam hizi ni miongoni mwa wamachinga wenye jina kutokana na shughuli zangu na sina tumaini la kumiliki ardhi leo wala kesho kwa muujiza wowote zaidi yakuendelea kuitwa mvamizi tu katika ardhi ya mababu zangu hii ni hatari sana,Naelewa muheshimiwa Rais maandishi haya yanaweza kunibadilisha jina sijui nitaitwaje, mwongo, mgombanishi,mpinzani au hata mchochezi au hata vyovyote ,lakini nimeyaandika nikijua kuwa maandishi hayafutiki na hasa maandishi kama haya yaliyo beba sauti ya kutafuta haki za watu wengi wasio na sauti.

Muheshimiwa rais mungu amekujalia wewe binafsi kuwa na huruma hebu tuhurumie sisi vijana wa Mtwara, hebu tumia hiyo huruma yako kuiokoa Tanzania, hebu tumia huruma yako kuondosha balaa, na katika hili usimuamini mtu njoo uongee na sisi wamachinga, uongee na sisi bodaboda na wengine wengi

Muheshimiwa Rais nisikuchoshe na ujumbe huu usio na maana sana kwako lakini kabla sija hitimisha ni vema nikakujulisha majibu nilyo wapa wale wana Mtwara wenzangu walio nitumia ujumbe pale juu niliwajibu hivi.

No.. No..Situmi ujumbe huu kwa mtu yeyote kwa kuwa huu ni ujinga wetu wa kuuza kura kama chapati na sasa tunakumbuka shuka asubuhi, hivi kweli gesi hii ingekuwa katika jimbo la Mchungaji Msigwa, Mnyika, au January makamba, mwiguru nchemba, zitto kabwe ingesafirishwa bila wananchi kujua au bila kuzingatiwa maslahi ya jimbo husika au mkoa husika No situmi NO,huu ni uzembe wetu Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo.

Haya ndiyo majibu yangu kwa jumbe nilizotumiwa na rafiki zangu hao hapo juu kutoka Mtwara.
Ahsante muheshimiwa rais wewe pekee ndio tumaini letu okoa Mtwara okoa Tanzania.
(Mtumwa wa watu)
+255 786-821744,767 821744,779 8217144.

(HAPA KUNA BANGO LENYE BENDERA MBALIMBALI LIKIWA MBELE YA OFISI YA
JIMBO MTWARA MJINI)
Bango lenye maneno ya…. Gesi kwanza vyama baadaye hakitoki kitu hapa….. likiwa limewekwa nje ya ofisi ya Jimbo ya chama cha NCCR-Mageuzi siku ya Tarehe 12/12/2012 siku ambayo vyama vyote vya siasa isipokuwa CCM vimeungana na kufanya mkutano wa Pamoja wenye ajenda ya kupinga kusafirishwa kwa gesi kutoka mnazi bay Mtwara kwenda Dar-es-salaam

huuu ujumbe(kama ulivyo) nimetumiwa kwenye email nifikishe kwa zitto kabwe.
 
Picha ya aliyetuma na eneo bendera zilipowekwa naomba uni pm nikutumie kama unahitaji
 
Muumini, sijaweza kumaliza kusoma uzi wako, ila kwa ufupi "Rais" wako/wenu ni nani? Na pia ni nini maudhuiya waraka huu mrefu?
 
Muumini, sijaweza kumaliza kusoma uzi wako, ila kwa ufupi "Rais" wako/wenu ni nani? Na pia ni nini maudhuiya waraka huu mrefu?

MKUU hii email nimeipokea na kuiweka kama ilivyo.
zitto ni rais kwa kusini mwa tanzania,Mhh kijana anakubalika kweli kweli.Dalili za mvua ni......_____________
 
Mi sijaelewa jamani ina maana rais wa kusini ni zito?kama ni zito kwani yeye ndie aliwaambia wachague magamba na si walipewa kanga na pilau sasa wanalalamika nini?wacha gas ije dar wao wao wabaki kulalama tu,chezea mafisadi wewe
 
Mi sijaelewa jamani ina maana rais wa kusini ni zito?kama ni zito kwani yeye ndie aliwaambia wachague magamba na si walipewa kanga na pilau sasa wanalalamika nini?wacha gas ije dar wao wao wabaki kulalama tu,chezea mafisadi wewe

Zitto anangekewa????Duhh kutoka Kigoma to Mtwara anaitwa Rais?Hongera zitto kabwe,unaonekana wewe si mtu wa kawaida nchini
 
Mi sijaelewa jamani ina maana rais wa kusini ni zito?kama ni zito kwani yeye ndie aliwaambia wachague magamba na si walipewa kanga na pilau sasa wanalalamika nini?wacha gas ije dar wao wao wabaki kulalama tu,chezea mafisadi wewe

:angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry:
 
Kweli umepokea email. Ila ungewajulisha CHADEMA kwa ujumla wao, au angaliwajulisha CHADEMA kwa ujumla wao na siyo ZZK. Huu ujumbe una-touch
 
Zitto ni magwanda halisi bungeni,naweza sema ni rais wa chadema bungeni ila awapo njee dr.slaa ndilo jembe na kila mtu analijua hilo. Kuitwa Zitto kusini mwa Tz sipati shda sana kwani wengine mikoa ya huko kusini wanaamini kuwa, Hayati Nyerere yupo hai na bado ni rais wao pia. Ninachoweza sema ni kwamba,ktk uchaguzi ujao 2015, Zitto awe bega kwa bega na dr.wa ukweli nchi nzima hasa kusini kwani wananchi pia wanamkubali sana na jimbo kwake hana mpinzani hvyo hakuna haja ya kupoteza muda kupiga kampeni.
 
Zitto ni magwanda halisi bungeni,naweza sema ni rais wa chadema bungeni ila awapo njee dr.slaa ndilo jembe na kila mtu analijua hilo. Kuitwa Zitto kusini mwa Tz sipati shda sana kwani wengine mikoa ya huko kusini wanaamini kuwa, Hayati Nyerere yupo hai na bado ni rais wao pia. Ninachoweza sema ni kwamba,ktk uchaguzi ujao 2015, Zitto awe bega kwa bega na dr.wa ukweli nchi nzima hasa kusini kwani wananchi pia wanamkubali sana na jimbo kwake hana mpinzani hvyo hakuna haja ya kupoteza muda kupiga kampeni.

Rais Bungeni,Kusini Mwatanzania,Kigoma na mwaka 2015 siatakuwa rais wa nchi nzima!!!!
 
Back
Top Bottom