Barua kwa mh. Jk na mh. Pinda - sehemu ya mwisho

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,068
183
Ubadhirifu
Kwa ufupi tu! Hakuna kitu kinatukera watanzania kuonawatendaji wa serikali wanapotumia hovyo kodi ya mkulima na mfanyakazi!! I nakera kuon anyie mnapeta na Toyota Landcruser VX au GX (V8) huku pale Mwananyamala Hospital au Ilala Hospital wagonjwa wanalala mzungu wa nne!! Inasikitisha tukiona serikali inanunua ndege kwa mabilioni (tena ndege mbovu) kwa jili ya kuvinjari nje ya nchi huku watoto wetu wanasoma kwenye shule ambazo hazina hata madawati….achilia mbali kukosa walimu!! Mimi sijue hesabu sana, ila hebu mtumieni hata Ludovick (AG) awaeleze ni Bilioni ngapi serikali ya TZ inatumia kwenye haya magari ya kifahari na ni kiasi gain kati ya hizi zingeweza kutatua matatizo ya elimu/afaya kwa mfan? Ningekuwa mimi ni mmoja wapo kati yenu, ningeamua kwa makusudi kutoa maelekezo kuacha matumizi haya kwa nchi changa na masikini kama yetu!! Kwa mfano badala ya kununua magari haya ningeamua say kupunguza bajeti yake by 50% Niaminini mimi, tungekuwa tumeisaidia sana nchio yetu!! WATANZANIA WANACHUKIA KUWAONA NYIE MNATESA KWENYE MAGARI HAYA YA KIFAHARI!! NI UBADHIRIFU NA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA MLIPAP KODI!!
Hivi ule utaratibu wa kutangaza mali haukubaliki nini kwenye chama chetu? Naona kama umeachwa vile?? Mimi binafsi nitafurahi sana kusikia mkuu wa kaya na mtendaji wake mkuu wametangaza mali walizochuma Kabla hawajaingia madarakani na sasa baada ya kuingia madarakani!! MSISAHAU PIA KUWAOMBA WAKE NA WATOTO WENU NAO KUTANGAZA ZAO…Maana nasikia kuna WATOTO WA WAKUBWA WANAWEZA KUNUNUA MAJUMBA KWA MABILIONI YA SHILINGI!! WANAZITOA WAPI HIZI?? JE WAZAZI HAWAHUSIKI?? Kwa kazi/biashara gain ya kuzalisha mali na faida kwa kasi hivyo??

Huduma za Afya
Kwa hili sina la kusema; nawaombeni mtembelee zahanati na vituo vya afya kila wilaya mnayokwenda! Waangalieni watendaji kule, tazameni mishahara na posho za wafanyakazi wa afya; angalieni idadi ya wananwake na watoto wanaokufa wakati wa kujifungua; tazameni upungufu wa madaktari na wataalamu wa maabara nk, zaidi ya yote hebu angalieni idadi kubwa ya wataalamu wetu wanaokimbilia kwenye hospitali za binafsi au nje ya nchi…hii inadhihirisha nini?? Huduma za Afya upande wa serikali, kwa wagonjwa na watoa huduma haziridhishi!! Nini cha kufanya nawaachia nyie, nitafurahi kusikia mnachukua jitihada za makusudi kabisa kutatua tatizo hili!!

Maslahi kwa wafanyakazi serikalini
Kwa hili sihitaji maelezo!! FANYENI UTAFITI na pia msione haya kufuata maombi/maoni ya TUCTA!! Mishahara ya wafanyakazi wetu jamani ni midogo sana!! Kwa pesa hizo hawawezi kuhudumia familia zao ipasavyo; watakimbilia kwenye wizi na kuomba rushwa!! Mnadhani ni kwa nini? Wao si hawana “tripu”, hawana semina, hawana makongamano etc kama viongozi wakubwa serikalini!! HEBU SIKILIZENI KILIO CHAO! Labda swali la kizushi tu; hivi nyie waheshimiwa nikiwagawia 300,000/= kila mmoja, ulipe kodi ya nyumba (say 100,000 kwa mwezi) bila kuumwa (kwenda hospitali kupata matibabu) ila usiwe na hela nyingine yeyote ile, hiyo pesa itawatosha?? Say kulipa nauli ya watoto shule, kununua chakula, etc?? SITAKI KUJUA MAJIBU YENU KWA SASA, nitashukuru majibu kwa vitendo!!

Marupurupu na Mishahara ya Wabunge
Wakuu; hiini njozi ya mchana, lakini hawa watu wanakula mabilioni ambayao kwa kweli hatuoni wanafanya nini!! Hebu chukueni mikanda ya kikao kilichopita cha bunge…wabunge wachache kwenye ukumbi wa bunge; au kulala usingizi wa pono ukumioni na kutia aibu!!(si mliona hata juzi tu siku ya ufunguzi wa Bunge jamaa wakaanza kuuchapa??) inalet apicha gain hii?...
Niwaambie kitu wakuu?Kwanza wabunge walipwe wanapohudhuria vikao hadi mwisho, wekeni security sytems ambazo kila mbunge akiingia ukumbini kunakuwa na records za muda alioingia na kutoka, ni mashine zinauzwa chini ya dola 50,000

Uwajibikaji
Wakuu, ni wazi dhana ya kuwajibika imesahaulika kabisa sasa!! Hivi wako wapi watendaji kama walivyokuwa wanafanya kazi kina Timoth Apiyo?? (mfano mmoja wapo)!! Siku hizi watendaji wakuu na wafanyakazi wa serikali muda mwingi sana wako bize na mambo binafsi, uwajibikaji ni zero!! KWA NINI TUSIAZIME LILE FAGIO LA CHUMA LA MZEE RUKSA??...Au limevunjika?? Hatuwezi kutafuta letu jingine? Hata la bati tu….? Nawaombeni wakuu, WASHUGHULIKIENI WATENDAJI WANAOLALA!! Wale wasiowajibika wawekwe pembeni….!! Tena niwakumbushe tu, uwajibikaji siyo kwenda kazini na ku-spend muda mwingi kwenye simu na kuchat kwenye fb, ni ku-deliver!!

Utunzaji wa Mazingira
Waheshimiwa, nyie mmetembea zaidi yangu hapa nyumbani!! Jambo moja ni wazi, utunzaji wa mazingira (kupunguza hewa chafu, kupanda miti, usafi wa miji na mitaa nk) unahitaji msukumo wa hali ya juu! Sijui kama mna mikakat yoyote ile katika hili; nafahamu watanzania pia wanawajibika katika hili, lakiniiii….HEBU LIWEKEENI MSUKUMO WA KISHERIA KIDOGO!! Si mmeona kule Moshi mjini? Mji unapendeza!! Kwa nini tusianzishe kampeni ya kupanda miti kwa kila kaya kwa mfano?? Kama serikali itafanya mkakati, (tena naamini hata UN-HABITAT na mashirika mengine watatupa support kwenye hili)…kwa mgfano kila mtendaji wa kata/mtaa ahakikishe kwamba watu wake wanapanda mti mmoja kila nyumba!! DSay serikali inatoa bure miche ya miti kwa wananchi wanaohitaji…kwa kampeni maalum ya kupanda miti…nina uhakika ndani ya miaka mi5, 75% ya hiyo miti itakuwa imekuwa na tutakuwa tumeboresha mazingira!! Hali ya hewa itaboreshwa,..na faid anyingi zitakuja!!
Uchafu wa mazingira…kwa mfano mkiamua iwepo sheria ya kuwakamata wanaovamia maeneo ya wazi, wanokojoa hovyo, wanaotupa taktaka hovyo na kadhalika!!! Jamani mbona mimi naon a hili linawezekana??? Kama nilivyosema mwanzoni, tuione haya, twende kwa jirani zetu pale Kigali, waulizeni wamewezaje??? Jibu ni rahisi tu…SHERIA KALI YA MAZINGIRA!!

Michezo
Hii ni sekta inayotia aibu sana nchi yetu!! Riadha, msumbwi, soka, netiboli nk…kot etumekuwa “kicha cha mwendawazimu”!! TATIZO NI KWAMBA BADO ELIMU YA MICHEZO MASHULENI HAIJABORESHWA!! Kuna wakereketwa wachache wanafanya kazi kubwa kwenye sekta hii, bado serikali haijawa na jitihada za dhati!! Michezo mashuleni pia inasaidia afya ya wanafunzi/watoto wetu!! N atuboreshe michezo basi….


Watendaji wakuu wa Serikali
Mkuu wa Kaya, pamoja na Kiranja Mkuu; Mtaniwia radhi kama kuna sehemu ya baru a hii nilipoteleza na kuwa kosea kimaadili; NI UCHUNGU TU WA NCHI YANGU!! Natamani ningekuwa DC wa Wilaya mojawapo nionyeshe mfano wa kuigwa kwa wengine! Natamani niwatajie majina ya watu waliopo na ambao wana uwezo mkubwa sana kupewa U—DC lakini kwa bahati mbaya zamu zao hazijafika!! Wao baba zao sio wanasiasa mashuhuri wa kuwalipa fadhila; Wao si wanachama wakerekletwa wanaokubalika na “mtandao”; wao, kama mimi tutaendelea kushuhudia teuzi hizi kwenye nafasi nyeti kwa watu ambao kwa kweli hawana uwezo!! Lakini tufanyaje? Labda ninachoweza kuwashauri wakuu wangu, HEBU TUANGALIE UWEZO BASI!! Hata mtu awe na sura nzuri kiasi gain, hata awe na support ya viongozi waandamizi wa chama au serikali, hata wawe watoto wa mabilionea, hat kama wakiwa wanapata sapoti ya mizimu ya waasisi wa taifa hili, KAMA HAWANA UWEZO TUSIWAPE NAFASI!! You know what? Hebu jaribuni kuzigeuza nafasi za U-DC kuwa kazi za kuajiriwa!! Watu wenye sifa waombe na kusailiwa!! WAPEWE WENYE UWEZO!! Kama hili haliwezekani basi tuendelee na utaratibu uliopo ila nawakumbusha tu; MAISHA YA MTANZANIA WA KAWAIDA YANADIDIMIA KWA KUWA KULE KWENYE NGAZI ZA CHINI ANAKOISHI, kule wilayani kule, kule vijijini, WATENDAJI WENU NI WAFALME/MALKIA, WENGI WAO WANASHINDWA KUSIMAMIA VEMA UTEKELEZAJI WE SERA MLIZOJIWEKEA!!
Endelezeni ‘grass root level” (kule si ndiyo ile 80% ya wananchi ipo??), mkifuat ahili mtagundua kule kunahitajika WATU MAKINI!!

Salamu sana kwa familia zenu; kwa Mheshimiwa JK salamu kwa mama kufikisha miaka 47, naona umri unasogea!! Kwa kampeni zake zile za 2005 na 2010 naona atakuwa mwansiasa mzuri sana! Hivi anagombea 2015?? HAPPY BELATED BIRTHDAY 1st LADY. Kwa mjomba PM, nimependa maamuzi yako ya kuamua kuacha siasa ifikapo 2015, ila wanasema SIASA NI MCHEZO MCHAFU!! Huwe mkinogewa hamuachi!! Pongezi kwako kwa ule mchango wa Milioni 50 pale UDSM, umeonyesha mfano…washauri basi kina Lowassa, Rotsam Azizi, Chenge, Mramba, Mh, Mkapa na wengineo….unadhani wanakosa milioni 50 kila mmoja kuchangia maendeleo ya elimu Tanzania?
Nawatakia afya njema (najua kwa matibabiu yenu hakutakuwa na shaka), Mtanijulisha kama mmepata barua yangu;
Asanteni sana.
Ni mimi, nipo kama bwegebwege, je ni *****?
Imeandikwa leoleo
 
Kaka umenena sana na hongera kwa kuandika vitu kama hivi vya maana sana nakuonysha uzalendo, lakini je hao vibaka wenyewe unaowaambia wanapita humu JF na kusoma? au hizi habari zinawafikia?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom