Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Ndugu Lowassa, Zitto, na Wengine:
Hili suala ya elimu ya bure naona linajirudiarudia. Lakini umefika wakati sisi wananchi tuingilie kati na kuanza kudai elimu na huduma zingine zitakazobadilisha maisha ya watoto wetu. Na moja ya kuingilia kati huku ni kuwafahamisha wana siasa kuwa hawana uwezo wa kutoa elimu ya bure.
Kijuujuu tunaweza kusema kuna elimu ya bure. Lakini kiundani hile ni ruzuku inayotoka kwenye mapato ya serikali kulipia gharama za elimu. Na hili kupata mapato ya kutoa ruzuku hiyo ni lazima watu au makampuni yalipe kodi ya mapato. Na kwa nchi kama Tanzania ni lazima wahisani watoe misaada.
Ndio kuna uwezekano wa Tanzania kutoa ruzuku zitakazotoa elimu ya bure. Swali ni kwa mazingira gani? Sijuhi majibu ya Lowassa. Lakini kwa sababu yeye alikuwepo serikalini na alishindwa kuona uwezekano wa elimu ya bure kipindi akiwa na madaraka makubwa basi naweza kusema analeta longolongo za kupata kura. Akipewa madaraka tena ataanzisha sera za elimu ya bure ambazo hata wajukuu zake hawatazitumia.
Zitto, katika mahojiano yake na JF, anasema kuwa kama miaka ya nyuma tulitumia kahawa, chai kusomesha basi sasa tutatumia Tanzanite na Almasi. Ndugu Zitto naomba rejea athari za misaada ya kigeni. Sera za nchi zilitegemea sana misaada ya kutoa nje kusomesha na kutoa huduma zingine za jamii. Na pale walipochoka kutusaidia (donor fatigue) walitutelekeza au kutulazimisha mipango mingine. Hivyo ni kutowajibika kusema kuwa miaka ya nyuma tulisomesha bure kwa resources zetu.
Kuhusu utumiaji wa madini na rasimali zingine kuna madhara yake. Kwanza rasilimali zetu sio renewable or infinite. Hivyo tusitegemee sana natural resources. Kwani zinapokwisha zinawaacha watu mashakani. Na kwa nchi yenye watu milioni 40 si busara kuwa tegemezi.
Pili suala la kutumia rasimali ni sawa na suala la kutumia misaada kutoka nje. Linawafanya viongozi wasiwajibike. Wakati wa Nyerere tulikuwa hatumuulizi maswali, kwa sababu alikuwa anatupa elimu na matibabu ya bure. Wanafunzi walikuwa hawagomi kwa sababu, serikali ilikuwa inawapa elimu bure.
Ndugu Lowassa na Zitto tukiwapa madaraka na uwezo wa kutumia pesa za madini kutupa elimu bure, mtatununua wananchi na hamtataka kuulizwa maswali au kuwajibika.
Shida ya watanzania sio elimu ya bure. Na elimu ya bure haitafanya watanzania kuondoa matatizo yao. Shida ya watanzania ni mzunguko mdogo wa shughuli za kiuchumi.
Kiwango cha elimu cha sasa sio kizuri. Lakini tulipofikia sasa, watanzania wanaweza kujikita kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kutumia elimu na maarifa waliyo nayo. Kwa mtaji huo, badala ya kurudia rudia sera za huduma za bure. Tunataka sera za kumwezesha mtanzania.
Hivyo toeni sera za uchumi ambazo zinaongeza mzunguko wa uchumi ambao watanzania walipe kodi zitakazotumia kutoa ruzuku za elimu na huduma zingine za bure. Ni lazima kuwepo na uhusiano kati ya matumizi ya serikali na kodi za wananchi.
So Long
Z10