Barua Kwa Lowassa, Zitto na Wengine: Hakuna Elimu ya Bure

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,063
2,471
Ndugu Lowassa, Zitto, na Wengine:

Hili suala ya elimu ya bure naona linajirudiarudia. Lakini umefika wakati sisi wananchi tuingilie kati na kuanza kudai elimu na huduma zingine zitakazobadilisha maisha ya watoto wetu. Na moja ya kuingilia kati huku ni kuwafahamisha wana siasa kuwa hawana uwezo wa kutoa elimu ya bure.

Kijuujuu tunaweza kusema kuna elimu ya bure. Lakini kiundani hile ni ruzuku inayotoka kwenye mapato ya serikali kulipia gharama za elimu. Na hili kupata mapato ya kutoa ruzuku hiyo ni lazima watu au makampuni yalipe kodi ya mapato. Na kwa nchi kama Tanzania ni lazima wahisani watoe misaada.

Ndio kuna uwezekano wa Tanzania kutoa ruzuku zitakazotoa elimu ya bure. Swali ni kwa mazingira gani? Sijuhi majibu ya Lowassa. Lakini kwa sababu yeye alikuwepo serikalini na alishindwa kuona uwezekano wa elimu ya bure kipindi akiwa na madaraka makubwa basi naweza kusema analeta longolongo za kupata kura. Akipewa madaraka tena ataanzisha sera za elimu ya bure ambazo hata wajukuu zake hawatazitumia.

Zitto, katika mahojiano yake na JF, anasema kuwa kama miaka ya nyuma tulitumia kahawa, chai kusomesha basi sasa tutatumia Tanzanite na Almasi. Ndugu Zitto naomba rejea athari za misaada ya kigeni. Sera za nchi zilitegemea sana misaada ya kutoa nje kusomesha na kutoa huduma zingine za jamii. Na pale walipochoka kutusaidia (donor fatigue) walitutelekeza au kutulazimisha mipango mingine. Hivyo ni kutowajibika kusema kuwa miaka ya nyuma tulisomesha bure kwa resources zetu.

Kuhusu utumiaji wa madini na rasimali zingine kuna madhara yake. Kwanza rasilimali zetu sio renewable or infinite. Hivyo tusitegemee sana natural resources. Kwani zinapokwisha zinawaacha watu mashakani. Na kwa nchi yenye watu milioni 40 si busara kuwa tegemezi.

Pili suala la kutumia rasimali ni sawa na suala la kutumia misaada kutoka nje. Linawafanya viongozi wasiwajibike. Wakati wa Nyerere tulikuwa hatumuulizi maswali, kwa sababu alikuwa anatupa elimu na matibabu ya bure. Wanafunzi walikuwa hawagomi kwa sababu, serikali ilikuwa inawapa elimu bure.

Ndugu Lowassa na Zitto tukiwapa madaraka na uwezo wa kutumia pesa za madini kutupa elimu bure, mtatununua wananchi na hamtataka kuulizwa maswali au kuwajibika.

Shida ya watanzania sio elimu ya bure. Na elimu ya bure haitafanya watanzania kuondoa matatizo yao. Shida ya watanzania ni mzunguko mdogo wa shughuli za kiuchumi.

Kiwango cha elimu cha sasa sio kizuri. Lakini tulipofikia sasa, watanzania wanaweza kujikita kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kutumia elimu na maarifa waliyo nayo. Kwa mtaji huo, badala ya kurudia rudia sera za huduma za bure. Tunataka sera za kumwezesha mtanzania.

Hivyo toeni sera za uchumi ambazo zinaongeza mzunguko wa uchumi ambao watanzania walipe kodi zitakazotumia kutoa ruzuku za elimu na huduma zingine za bure. Ni lazima kuwepo na uhusiano kati ya matumizi ya serikali na kodi za wananchi.

So Long

Z10
 
Mkuu sikuungi mkono kamwe, Elimu ya Bure inawezekana kabisa, ni Mabilioni mangapi yanaliwa kila mwaka? Kuhuhu kutegemea Natural Resources hakuna Nchi isiyo tegemea natural resources na hata huko kwenye Viwanda bado kuna Matatizo, Marekani na kutegemea Viwanda kwa sasa Uchumi wake unsuasua sana,

Serikali ingeweza Kubana Matumizi yake watoto wakitanzania from Secondary hadi chuo kikuu wangesoma Bure, tena Bure ile ya kukuta kila kitu shuleni kuanzia, Uniform,vitabu,madaftari, kalamu na kazalika, Hii nchi pesa zinaishia kununua ma V8, Kulipana posho, kulipana mishahara kwa watumishi wasio kuwa na kazi kama wakuu wa wilaya na Mikoa,

Kaa piga mahesabu ya Nikiwango gani cha pesa kinahitajika kulipia elimu bure kwa Mwaka mzima na ni kiwango gani hupotea kwenye Posho, kununua Magari, Misamaha ya Kodi na kazalika, Utaona kwamba ingetosha na tena Kubakia
 
Serikali haiokoti pesa au kuchapisha tu. Ni mapato ya serikali yanayotolewa kama ruzuku ndio yanayosababisha huduma za bure. Hivyo kimsingi hakuna kitu cha bure.

Kuhusu suala la matumizi ya mabaya kama vile v8 na posho, charity starts at home. Ndugu Lowassa na Zitto ni wabunge ambao wanatembelea V8 na kutumia posho ambazo zingetumika kutoa elimu ya bure kama unavyodai.

Sasa kwanini uwe na imani nao wakati matumizi yao ya kawaida hayaonyeshi kuwa yanaweza kusaidia kuondoa matumizi mabaya ya pesa za serikali?
 
Nashindwa kukuujibu,
Ushahuri tu kakojoe hulale au kama una shuri kaoge uende club, since its friday!

Labda nikupe hint kidogo tu,
Je wajuwa faida ya kusomesha mtu mmoja angalau hata kwa elimu ya degree ?
As long as unakiri kuwa redsource zetu sio renewable the u should know that the best investment ni kichwani au kuelimisha.
Kama hujuhi ilo kajifunze qatar, wanafanya sasa kilo tunachopaswakifanya na ama ambacho mwalimu alifanya.
 
  • Thanks
Reactions: PhD

Sahihisho dogo tu. Zitto hatumii V8 na hachukui posho.
 
Kwa maliasili tulizonazo( mbuga za wanyama, madini, bandari na ardhi nzuri ya kilimo) elimu bure inawezekana kama ukiwa na serikali makini na iliyojaa viongozi wazalendo. Lakini kwa hawa mafisadi na wahujumu uchumi kwao haliwezekani.
 
Ndugu Lowassa, Zitto, na Wengine:

Hili suala ya elimu ya bure naona linajirudiarudia. Lakini umefika wakati sisi wananchi tuingilie kati na kuanza kudai elimu na huduma zingine zitakazobadilisha maisha ya watoto wetu. Na moja ya kuingilia kati huku ni kuwafahamisha wana siasa kuwa hawana uwezo wa kutoa elimu ya bure.

Kijuujuu tunaweza kusema kuna elimu ya bure. Lakini kiundani hile ni ruzuku inayotoka kwenye mapato ya serikali kulipia gharama za elimu. Na hili kupata mapato ya kutoa ruzuku hiyo ni lazima watu au makampuni yalipe kodi ya mapato. Na kwa nchi kama Tanzania ni lazima wahisani watoe misaada.

Ndio kuna uwezekano wa Tanzania kutoa ruzuku zitakazotoa elimu ya bure. Swali ni kwa mazingira gani? Sijuhi majibu ya Lowassa. Lakini kwa sababu yeye alikuwepo serikalini na alishindwa kuona uwezekano wa elimu ya bure kipindi akiwa na madaraka makubwa basi naweza kusema analeta longolongo za kupata kura. Akipewa madaraka tena ataanzisha sera za elimu ya bure ambazo hata wajukuu zake hawatazitumia.

Zitto, katika mahojiano yake na JF, anasema kuwa kama miaka ya nyuma tulitumia kahawa, chai kusomesha basi sasa tutatumia Tanzanite na Almasi. Ndugu Zitto naomba rejea athari za misaada ya kigeni. Sera za nchi zilitegemea sana misaada ya kutoa nje kusomesha na kutoa huduma zingine za jamii. Na pale walipochoka kutusaidia (donor fatigue) walitutelekeza au kutulazimisha mipango mingine. Hivyo ni kutowajibika kusema kuwa miaka ya nyuma tulisomesha bure kwa resources zetu.

Kuhusu utumiaji wa madini na rasimali zingine kuna madhara yake. Kwanza rasilimali zetu sio renewable or infinite. Hivyo tusitegemee sana natural resources. Kwani zinapokwisha zinawaacha watu mashakani. Na kwa nchi yenye watu milioni 40 si busara kuwa tegemezi.

Pili suala la kutumia rasimali ni sawa na suala la kutumia misaada kutoka nje. Linawafanya viongozi wasiwajibike. Wakati wa Nyerere tulikuwa hatumuulizi maswali, kwa sababu alikuwa anatupa elimu na matibabu ya bure. Wanafunzi walikuwa hawagomi kwa sababu, serikali ilikuwa inawapa elimu bure.

Ndugu Lowassa na Zitto tukiwapa madaraka na uwezo wa kutumia pesa za madini kutupa elimu bure, mtatununua wananchi na hamtataka kuulizwa maswali au kuwajibika.

Shida ya watanzania sio elimu ya bure. Na elimu ya bure haitafanya watanzania kuondoa matatizo yao. Shida ya watanzania ni mzunguko mdogo wa shughuli za kiuchumi.

Kiwango cha elimu cha sasa sio kizuri. Lakini tulipofikia sasa, watanzania wanaweza kujikita kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kutumia elimu na maarifa waliyo nayo. Kwa mtaji huo, badala ya kurudia rudia sera za huduma za bure. Tunataka sera za kumwezesha mtanzania.

Hivyo toeni sera za uchumi ambazo zinaongeza mzunguko wa uchumi ambao watanzania walipe kodi zitakazotumia kutoa ruzuku za elimu na huduma zingine za bure. Ni lazima kuwepo na uhusiano kati ya matumizi ya serikali na kodi za wananchi.

So Long

Z10

Sijasoma mpaka mwisho. Ila nimesoma one line nikatambua muelekeo wa mawazo yako.

Its is a fact: WElimu tunayosema bure inawezekana kwa sababu ukweli siyo kwamba haitalipiwa, Kodi za watanzania (ulizoita heal za serikali) will pay for that free education.

Tanzania ina raslimali nyingi sana siyo tu kutoa elimu bure in that context, but kufanya mambo mengine kwenye sector kama afya n.k yaende na mtanzania asike nafuu ya maisha.

Naomba nikukumbushe kitu kimoja: The greatest resource that any country has is people. To this fact of truth - "Good leaders manage people and develop systems while Great leaders manage systems and develops people". Tafakari then chukua hatua za makusudi.
 
"Ndio kuna uwezekano wa Tanzania kutoa ruzuku zitakazotoa elimu ya bure" - Zakumi
 
Hapana. Hakulizungumzia nadhani kwa sababu hakuulizwa. Lakini amesema ana magari mawili.

Kwa hiyo hilo limekutosha wewe kumsahihisha Zakumi kuwa hana (ama hajawahi kuwa na) 'V8' ya Wabunge/Ubunge?
 
Nashindwa kukuujibu,
Ushahuri tu kakojoe hulale au kama una shuri kaoge uende club, since its friday!

Labda nikupe hint kidogo tu,
Je wajuwa faida ya kusomesha mtu mmoja angalau hata kwa elimu ya degree ?
As long as unakiri kuwa redsource zetu sio renewable the u should know that the best investment ni kichwani au kuelimisha.
Kama hujuhi ilo kajifunze qatar, wanafanya sasa kilo tunachopaswakifanya na ama ambacho mwalimu alifanya.

Ungempa na kiroba cha konyagi na valuu kabisa alale na apumzike kwa amani, muulize nyerere aliwaomesha watanzania kwa pesa zipi na wakati hata madini tuilikuwa hatuchimbi, nyerere kawasomesha kwa kahawa, pamba , katani na korosho , hivyo leo dhahabu tu inatosha kuwasomesha wanafunzi wetu vyuo vikuu, ni suala la mipango tu.
 
Yaani tukiamua kama Taifa (na kama hatutapigwa kwa sababu hiyo) tunaweza kuishi kwa kukusanya kodi (rents) za rasilimali zetu - almasi, dhahabu, tanzanite, gesi, upepo, maji, jua, wanyama n.k. - na kuzitumia kutoa elimu, afya, maji n.k. 'bure' na bwerere!

kp21112012.jpg
 
Wee kama kwako unaona elimu bure ni ndoto acha kutuaminisha kwamba wewe ni kilaza...elimu bure inawezekana...zamani walitumia mikorosho kahawa na sisal sasa tuna tanzanite dhahabu na almasi kwanini isiwezekane???
 
Hivyo toeni sera za uchumi ambazo zinaongeza mzunguko wa uchumi ambao watanzania walipe kodi zitakazotumia kutoa ruzuku za elimu na huduma zingine za bure. Ni lazima kuwepo na uhusiano kati ya matumizi ya serikali na kodi za wananchi.

Nimechukua mstari wako wa mwisho ili kuweza kufafanua kwani siku fahamu ulipo sema kuhusu madini kuwa yanaweza kutusomesha wewe ulichukulia vipi?

si kama na pinga kama madini hayatakwisha, au kama ulivyo sema kwa kurejea maneno ya Zitto kuwa kama zamani kahawa iliweza kutusomesha then why not now kwenye madini, ukweli ni kwamba kama unasema sera za uchumi then ndio zitto anachokisema kuwa kama kweli serekali ikiwa makini kwenye usimamizi bora kwenye sector hiyo basi uchumi wetu utaondoka kwenye utegemezi, hivyo elimu ya bure na mambo mengine yote yanaweza kufikiwa.

hivyo elewa kuwa zkk anaposema madini anamaanisha kuwa kupitia jambo hilo tunaweza kukuza uchumi wetu na kutimiza ndoto za kila mtanzania kupata elimu kama haki yake ya msingi kikatiba
 
Unless I have information otherwise I have to take him at his own word.

Which word of his own while you have already agreed that he didn't talk at all about the use of V8 za Wabunge/Ubunge - au ndio mambo ya ku-infer if not ku-put words into his mouth?
 
Back
Top Bottom