Barua Kwa Lowassa, Zitto na Wengine: Hakuna Elimu ya Bure

Companero,

Kama wachagga wangehamua kuchukua mapato yao ya kahawa na kuipa serikali hili iwape huduma bure, je wangeweza kusomesha watoto wao na kufanya vitu vingine vya maendeleo?

Sehemu kubwa ya maendeleo yao inatokana na wao ku-control mapato yanayotokana na mazingira yao. Mapato ya migodi yanalipwa DSM na yanafanyiwa maamuzi DSM ambayo haina hata mgodi mmoja.

Shii nyamaza wasikusikie watakuita mkabila....niliwahi sema haya.Kuwa DSM ndio imefunga mikoa minyororo na hiyo gari la mendeleo likiondoka wao huchomoka.

Kw aujumla dara haina think tanks wa kuweza master mambo ya mikoa fulani fulani.Mikoa mingine ina mipango ambayo dar hawajafikia, matokeo yake dar wakileta yao wanarudisha hiyo mikoa nyuma.Watu wengi wanaopewa ulaji dar ni wale walioweza tawala maungumzo vijiweni, walifanikiwa kufanya matukio moja moja, na kupewa kitengo, ndio maana utasikia sijui Kova anaiwezea dar, si utasiki mwaibula, etc halafu wanadhaniwa kuwa walichofanya ni sahihi sana kwa vile kimetoa matokeo wanayoyapenda.Baadaye hulazimisha kwenda mikoani.

Nimefurahishwa sana kusikia sasa wanataka wakuu wa mikoa watoke mika husika.Niliwahi lalamika sana kuwa wakuu wa mikoa wengine wametoka mikoa ambayo kuna sector kwani hakuna kabisa, na hivyo wakienda ktk mikoa ambayo hizo sector zipo juu , wao huona kuwa wenzao walipofikia kuna tosha na mikoa yao ndio inastahili sasa kuangaliwa kma si kubebwa
 
Serikali haiokoti pesa au kuchapisha tu. Ni mapato ya serikali yanayotolewa kama ruzuku ndio yanayosababisha huduma za bure. Hivyo kimsingi hakuna kitu cha bure.

Kuhusu suala la matumizi ya mabaya kama vile v8 na posho, charity starts at home. Ndugu Lowassa na Zitto ni wabunge ambao wanatembelea V8 na kutumia posho ambazo zingetumika kutoa elimu ya bure kama unavyodai.

Sasa kwanini uwe na imani nao wakati matumizi yao ya kawaida hayaonyeshi kuwa yanaweza kusaidia kuondoa matumizi mabaya ya pesa za serikali?


ukiwa milionea kama lowassa haya mafao ya waziri mkuu mstaafu ambayo kisheria na protocal hastahili kupata ya nini? kama siyo ubinafsi uliopindukia. charity starts at home, uliona Nyerere alivyokua, thats the guy unaweza kujua anaongea ukweli na atafanya anachokisema siyo hawa wasanii
 
tathmini iliyofanwa 2010 ilionekana inawezekana nasi tumebaki na hili wazo kuwa kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa na hili hata halina shida yoyote; mfano kodi ya makampuni ya simu tu ya 20% ikikusanywa vizuri nadhani kodi hii inatosha.
 
Serikali haiokoti pesa au kuchapisha tu. Ni mapato ya serikali yanayotolewa kama ruzuku ndio yanayosababisha huduma za bure. Hivyo kimsingi hakuna kitu cha bure.

Kuhusu suala la matumizi ya mabaya kama vile v8 na posho, charity starts at home. Ndugu Lowassa na Zitto ni wabunge ambao wanatembelea V8 na kutumia posho ambazo zingetumika kutoa elimu ya bure kama unavyodai.

Sasa kwanini uwe na imani nao wakati matumizi yao ya kawaida hayaonyeshi kuwa yanaweza kusaidia kuondoa matumizi mabaya ya pesa za serikali?

Mkuu, nilidhani mada yako ilikuwa ni kujadili ukweli kuhusu uwezekano wa kutolewa elimu ya bure kwa wa-TZ. lakini katika mchango wako nimebaini kuwa kumbe unawajadili watu (wahe. Zitto na Lowasa)

Na jingine nimeshindwa kukuelewa hoja zako zinapokinzana hususan, unaposema ati pesa ya serikali hutolewa kama ruzuku kwa hiyo kimsingi hakuna kitu cha bure! Ulitaka kusema nini hasa kimantiki?
Serikali ni nani? Na hiyo pesa unayodai ni ruzuku ameitoa wapi? Kwa maana nyingine chanzo cha mapato ya serikali makini ni nini?
Mkuu, ninakushauri urudi ukajipange upya maana hoja zako zinapwaya sana.
 
Tangu tupate uhuru, watanzania hawajawahi kusomeshwa elimu. Waliingia tu madarasani. Kipindi chote cha utawala wa CCM zaidi ya miaka 50 tangu enzi za TANU mpaka sasa hivi hakuna wakati Watanzania wanaweza kusema wakati huu tulipata elimu ya kutosha kutawala mazingira yetu na kuweza kuiendesha nchi yetu kwa kutegemea rasilimali watu tu na nchi ikawa tajiri. Huwezi kusema kuna watanzania waliosoma wakati katika kipindi chote cha zaidi ya miaka 50 tangu tupate uhuru nchi haijawahi kuwa na hata kiwanda cha kutengeneza sindano ambacho tunaweza kujivunia kwamba kimeundwa na wasomi wa kitanzania watupu!!!!
Lazima Watanzania tulielewe hili amasivyo tutakuwa tunapiga kelele tu kila siku na wanasiasa wataendelea kutupumbaza na kutugawa kwa ajili ya misele yao ya kwenda ikulu.
CCM kimeshindwa kutawala nchi hii. Hatuwezi kuendelea kuwaruhusu waiweke nchi yetu kwenye majaribio ya kiutawala na kiuongozi wakati wameshindwa kufanya hivyo zaidi ya miaka hamsini. Watanzania tusitazame sura, kabila au dini ya mtu aliyepo CCM na kufanya maamuzi kwa vigezo hivyo. Nchi yetu itaendelea kuwa masikini milele kama tutafanya hivyo. CCM hawafai kuongoza hata mtaa. Watanzania wasiwape hata kura moja ya udiwani katika uchaguzi ujao ili tupate utawala na uongozi mwingine. Potelea mbali hata kama ukiwa wa kubahatisha kuliko kuendelea kuwaweka CCM madarakani wakati tunajua kabisa kwamba hata ashuke malaika kutoka mbinguni hawa jamaa hawataweza kuwa na mtazamo sahihi kuhusu nini cha kufanya nchi hii ili nchi itoke kwenye lindi kubwa la umasikini wa hiari!!!!!
 
Elimu bure aliyosema Lowasa heti ni elimu ya sekondari,hiyo siyo concern kubwa ya watanzania kwani hada ya sekondari ya elfu 20 na boarding laki moja wengi wanaimudu,kero kubwa ni elimu ya chuo kikuu ya mamilioni,watanzania wengi hawawezi kumudu ada ya chuo kikuu kwa watoto wao.Hao voingozi wasituadae ,watanzania wanataka elimu bure ya chuo kikuu na serikali inaweza kabisa,mfano ikiziba mianya yote ya ukwepaji kodi,wawekezaji wakalipia kodi inavyotakiwa,mikataba yote ya rasilimari zetu ikafanyika kwa uwazi na kwa manufaa ya nchi,mafisadi wakabanwa na wizi wa fedha za uma ukakomeshwa,na pia wizara ya elimu ya juu ikasaidiwa kuwa na vitega uchumi vya hali ya juu vyenye kuingiza kiwango kikubwa cha pesa nina hakika pamoja na mbinu nyingine zikitafutwa ikiwemo ya kuhakikisha asilimia angalau 5 ya faida itokanayo na mafuta na gesi inapelekwa kwenye elimu nina hakika elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu inaweza kuwa bure.
 
Zakumi,
Unaweza kunambia ni kiasi gani cha fedha kutoka nje (hisani) kilitumika ktk kuendeleza ELIMU bure nchini wakati wa Nyerere!..
 
Kwa hiyo hoja yako ya kwanza tumemaliza, Wananchi ndio wenye Nchi, hatujui HAKI, WAJIBU wetu kama Wananchi aka Watanzania, wengi wetu tuafuata Upepo, hatuwezi aka hatuna ujasiri wa kuuliza, kukataa maovu na mengineyo.

Tukihamia hoja ya pili, hauwezi kutoa Elimu bure bila kuboresha upande wa pili, means upande wa Waalimu, unawalipa vizuri unawaandalia mazingira mazuri yao ya kazi, wana vitendea kazi, Je hizo shule zina vifaa vyote vya kufundishia pamoja na Lab ???

Mwananchi ni lazima awe na haki na wajibu wake. Kuna msemo unaosema 20%/80% Ukiwa na maana kuanzisha itakugharimu 20% lakini kuendesha na kusimamia itakugharimu 80%.

Mishahara ya waalimu na marupurupu yao. Jinsi ya kuendesha shule na labs hipo kwenye 80%. Lakini hoja nyingi zetu kuhusu huduma za umma zimelenga sana kwenye 20%, uanzishaji. Mfano mzuri ni shule za kata ambazo Mheshimiwa Lowassa anahusika sana.

Tukirudi kwenye haki. Mwanasiasa akishashika madaraka na kuanza kutumia pesa, atakwambia mafanikio ya serikali yake. Hakuna mwanasiasa anayesema kwa pesa zenu wananchi, tumefanikiwa kufanya hiki na kile. Siku zote mwananchi anakuwa hayupo kwenye equation ya utumiaji wa pesa. Hivyo haki ya yeye kuwa katika maamuzi au kusimamia mchango wake haipo.

Kukiwepo na uhusiano kati ya mapato na matumizi ya serikali yanayomuhusisha mwananchi, basi mwananchi atawajibika.
 
Mkuu umeongea vyema sana ila unapaswa jua kuwa makosamadogo sana ktk mazao ya fikra yanaweza pelekea kufanya wazo zila likawa la kijinga sana.

Sabau ulizokataa nazo rasilimali ndizo zina apply ktk kila kitu.Hakuna kitu kisichoisha, ndio maana watuw anawekeza ktk mipango endelevu, na diversity.pamoja na financial discipline fulani.

Hata waomi nao huisha au kuwa absolete,Wasomi baada ya kizazi kimoja kama hapakuwa na mipango endelevu hutokea kukawa na mapungufu yanayoweza spiral down ktk nyanja nyingi.

Ninachotaka sema hapa ni kwamba Zitto anavyodai kuna madini wakati mchango wake ktk uchumi ni mdogo kuliko wa TBL, tayari kaonyesha kuringia vitu visivyo halisi.Ingekuwa serikali na wazawa wana upper hand basi tunegone kuwa Hizo rasilimali zikisaidia sector nyingine kama za ujenzi, viwanda etc.Na si tuu suala la kuwa hizo rasilimali zitakwisha.Suala ni kwamba kama zitakwisha mchango wake nao utakwisha?Nini kifanyike mchango wake usife?Hizo rasilimali zinapaswa kuwa ndio mtaji wa kuelekea ktk maisha yasiyotegemea tena chanzo cha mtaji.Mtaifa yame move kwa kuwa na raia wasiojiibia, rais wanaoweka malengo ya muda mrefu na kutoayaacha hata kama kutakuwa na mtikisiko.Hapo ndipo tunapata diversity.Serikali ya CCM haijaweza fikia vigezo hata vidogo kabisa vya kufanya haya.Ndio serikali iliyotuaibisha sana nje ya mipaka yetu kwa kutupelekea viongozi wenye ujinga wa wazi, na kuwapa watu picture mbaya sana kuhuru sisi.

Kutoa majenshi nje kwa tatizo la msingi ni sehemu ya majeshi kujifunza, na kuongeza influence yetu ktk mataifa yanayotuzunguka.Kw aujumla ni uhai wa taifa.Kuwa na ushawishi kwa mataifa jirani ni silaha ya ulinzi, kwani mara zote unakuwa ukiwafanya wasifikiri kuanzisha vita na wewe, na hata atakayenzisha basi unakuwa na kundi fulani nchin mwao unalowez litumia kukusaidia kushinda hiyo vita.Kama unavyooona mitaani watu wachokozi, waporaji etc ktk level ya mataifa pia hizo hali zipo, kw amataifa yanayolinda wafanya biashara wao nje ya nchi ambao wanalipa kodi nchi zao za asili, wanaosupport nchi zao, wanaofanya biashara huku wakieneza policies za nchi yao kwa nchi za ugenini, watakapozurika ktk ushindani na wafanya biashara za nchi ya ugenini,panaweza tokea hali ya ajbu ghafla na vita kupigwa.Barclays bank inaweza sababisha vita kati ya mataifa mengi ikiwa itahujumiwa ktk nchi za ugenini, kwnai imeshikilia uchumi w amataifa mengi sana duniani pamoja na UK.Vita zitakuwepo na kutojiweka tayari ni kutaka jiua au kutawaliwa.Kamwe amani na mataifa kama Rwanda, Burundi, malawi, Uganda, DRC, Zambia, Malawi military muscle tuliyo nayo, na viongozi wa hizo nchi wana mahusiano gani nasi, wanategemea nini kwetu, otherwise akija kioongozi kichaa atataka vita na cc wachukue raw material, na kufungua njia hadi baharini, hizo nchi zina watu wapo very aggressive na determined to expand thier sphere of influence.

Mlawi si tuu kuwa wanataka Ziwa Nyasa,ila wanataka pia waclaim himaya ya zamani na chief wao iliyokwenda hadi bahari ya Hindi, Rwanda wapo tayari kujenga reli hadi bahari, Uganda hivyo hivyo, zambi hivyo hivyo,Congo hivyo hivyo, burundi ndio kabisa wanataka chukua kabisa ndio maana kila leo wanaingia watu ktk ardhi yetu kw avisingizio kuwa wanafuata waasi.Sabau wanayotumia akina Uganda, Rwanda kuiba congo.

Hembu tujiulize kw ajinsi CCM wanavyotoa sababu za kijinga na kuwa na uwezo mdogo wa kuongoza nchi , wangekuwa na nchi isiyo na kitu kama Rwanda nautalii wao ukawa ni Masokwe tuu sijui wangtufikisha wapi?Au pengine tusingekuwa na mila duni za kiswahili zinazoharibu fikra kuu za nchi na kuzipunguza hadi kuwa kungombea migao tuu, n ahaki zisizokuwepo badala ya kufanya kazi na kuweka watu ktk nafasi kwa weledi.Bila kuwa na watuw anaowakijibika kabla hawajwajibishwa.

Nakusikia Mkuu,

Kutumia rasimali asilia kama mtaji wa kuanzia ni kitu kinachoeleweka. Lakini ni lazima kuwa makini katika kufanya hivyo. Mtu anapokuja na kutuambia kuwa anatujengea shule na kutupa elimu bure tunampigia makofi. Tunashindwa kujua kuwa anapofanya hivyo anatufanya tubadilike kimawazo na kufikri kuwa ni wajibu wa serikali kutupa wananchi kila kitu bila sisi kufanya kazi.

Jamii ambayo hipo nyuma kielimu ni jamii ambayo serikali isipojenga shule, basi wananchi nao wataacha kujishughulisha kielimu. Jamii ambayo imeendeleza kielimu, itajaribu kwa njia yoyote kuelimisha watoto wao.

Vitu vya bure vina behavioral and physiological consequences zake.
 
Mkuu, nilidhani mada yako ilikuwa ni kujadili ukweli kuhusu uwezekano wa kutolewa elimu ya bure kwa wa-TZ. lakini katika mchango wako nimebaini kuwa kumbe unawajadili watu (wahe. Zitto na Lowasa)

Na jingine nimeshindwa kukuelewa hoja zako zinapokinzana hususan, unaposema ati pesa ya serikali hutolewa kama ruzuku kwa hiyo kimsingi hakuna kitu cha bure! Ulitaka kusema nini hasa kimantiki?
Serikali ni nani? Na hiyo pesa unayodai ni ruzuku ameitoa wapi? Kwa maana nyingine chanzo cha mapato ya serikali makini ni nini?
Mkuu, ninakushauri urudi ukajipange upya maana hoja zako zinapwaya sana.

Toka mwanzo. Mada inasema HAKUNA ELIMU YA BURE. Kwa mantiki kuwa ni lazima ziwepo resources za kugharimia elimu.

Pili nimesema serikali inapotoa elimu bure inakuja na masharti yake. Hivyo ni bora kujadili hayo masharti yake pia. Moja ya masharti hayo ni kupewa mashule bila wao kuhusishwa kwenye maamuzi. Serikali itakupangia kila kitu. Mbili vitu vya bure ni mtaji wa wanasiasa kuingia madarakani. Lakini sekta ya elimu ni muhimu kama ya ulinzi. Tatu resources ambazo serikali inalipia elimu bure zina muda wake. Ukisema utasomesha watanzania bure kwa kutumia Tanzanite ni lazima ukumbuke Tanzanite itaisha.

Kwa watu wanaonifahamu hapa JF, wanajua mimi si mpenda vitu vya bure (Mjamaa). Kama kuna uwezekano, ni afadhari rasilimali itumike kujenga viwanda vitakavyonipa kazi ambayo itaniwezesha kulipia gharama za mtoto wangu shule.

Nipo tayari kulipa kodi na kutoa jasho hili mtoto wangu apate elimu anayostahili kutoka chekechea mpaka chuo kikuu. Kwa mtaji huu naomba ndugu Lowassa, Zitto na wengine watoe economic models ambazo zitawapa watanzania vipato vya kusomesha watoto wao.
 
kwa kweli aliyejiita profesa wa siasa za Kenya mzee sana Moi alisema ni ndoto kwa Kenya kutoa elimu bure.NARC walisema inawezekana elimu bure na wakaenda mbali zaidi kusema Kenya bila KANU na MOI inawezekana.Sasa anayebisha haiwezekani hana takwimu za mapato na matumizi ya serikali .Huyu hajui mapato yanayotoroshwa serikali ikaachwa mdooooooomo wazi,hajui matumizi yasiyo ya msingi ya serikali yake,na kwa njia hiyo hana haja ya kuleta hoja hadi atakapopata takwimu na aweze kufikiri vizuri.
Vinginevyo Elimu ni public good, na ni vizuri ingetolewa bure sambamba na maji umeme,na huduma za afya ya msingi!
 
mtu akisoma mada anaona unajua basic economics lakini sijui hukuambiwa kuwa models/frameworks zingine wala siyo za huku kimazingira?Finnland,Sweden na kwingineko waliwezaje?
 
kwa kweli aliyejiita profesa wa siasa za Kenya mzee sana Moi alisema ni ndoto kwa Kenya kutoa elimu bure.NARC walisema inawezekana elimu bure na wakaenda mbali zaidi kusema Kenya bila KANU na MOI inawezekana.Sasa anayebisha haiwezekani hana takwimu za mapato na matumizi ya serikali .Huyu hajui mapato yanayotoroshwa serikali ikaachwa mdooooooomo wazi,hajui matumizi yasiyo ya msingi ya serikali yake,na kwa njia hiyo hana haja ya kuleta hoja hadi atakapopata takwimu na aweze kufikiri vizuri.
Vinginevyo Elimu ni public good, na ni vizuri ingetolewa bure sambamba na maji umeme,na huduma za afya ya msingi!
mtu akisoma mada anaona unajua basic economics lakini sijui hukuambiwa kuwa models/frameworks zingine wala siyo za huku kimazingira?Finnland,Sweden na kwingineko waliwezaje?


Kombesana;

Nimekaa Sweden. Na moja ya sifa ya Sweden ni wananchi kukubali kulipa kodi kubwa hili serikali iweze kutoa huduma kwa jamii. Hivyo public good inatokana na wananchi wa Sweden kuwajibika kuchangia. Na vilevile kutokana na wananchi kutoa kodi, wapo makini sana kuangalia matumizi ya serikali.

Tukirudi Tanzania, huduma za jamii hazitegemei mchango wa mapato ya wananchi serikalini. Huduma zinategemea sana wahisani, rasilimali kama utalii na madini. Hii model ya matumizi ya jamii sio nzuri, (unsustainable).

Kuhusiana na Kenya ni lazima uwe makini. Wakati Moi yupo madarakani, bajeti ya wakenya ilitegemea 9% misaada kutoka nje. Hivyo bila misaada ya kutoka nje wakenya walitunda tu. Wakati huohuo, watu waliokwenda shule kwa kujilipia wenyewe tayari walifika kati ya 60%. Hii ni rekodi nzuri sana kwani watu tayari walijua wajibu wa kwenda shule.


Kwa watanzania tunaomba elimu bure, kwanini tusiombe kuacha kutumia misaada kutoka nje kwanza? Nchi nyingi za Asia zilizofanya mapinduzi katika sekta za uchumi, kilimo, na elimu, zinafanya hivyo zikiwa zinategemea 2% misaada kutoka nje.

Hivyo kuna umuhimu wa kuonyesha kuwa tunajitegemea kwanza kabla ya kuanza kutoa handouts kwa wananchi.
 
Zakumi,
Unaweza kunambia ni kiasi gani cha fedha kutoka nje (hisani) kilitumika ktk kuendeleza ELIMU bure nchini wakati wa Nyerere!..

Katika miaka ya 70s kuna takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ilipokea kama 3Billion USD. Kama pesa hizi zingetolewa mwaka 1975 pekee yake, zingekuwa na thamani ya 12Billioni ya leo. Ni kiasi gani kilienda kwenye elimu sina data kamili.
 
Nakusikia Mkuu,

Kutumia rasimali asilia kama mtaji wa kuanzia ni kitu kinachoeleweka. Lakini ni lazima kuwa makini katika kufanya hivyo. Mtu anapokuja na kutuambia kuwa anatujengea shule na kutupa elimu bure tunampigia makofi. Tunashindwa kujua kuwa anapofanya hivyo anatufanya tubadilike kimawazo na kufikri kuwa ni wajibu wa serikali kutupa wananchi kila kitu bila sisi kufanya kazi.
Hapo kwenye red ndipo kuna shida, jamii yetu imejaa ujinga sana, hata wasomi pia ni waoga wa kufikiri critically, mwishowe wanaachia wapiga debe kulazimisha matamshi ya viongozi yaonekane kuwa ni mawazo mapya na yenye kuleta mapinduzi.
Jamii ambayo hipo nyuma kielimu ni jamii ambayo serikali isipojenga shule, basi wananchi nao wataacha kujishughulisha kielimu. Jamii ambayo imeendeleza kielimu, itajaribu kwa njia yoyote kuelimisha watoto wao.

Vitu vya bure vina behavioral and physiological consequences zake.
Mazoea na binadamnua ni vitu ndugu sana, ndio maana kuna palan nyingi sana ziliwekwa na wenzetu, ktk dini, ktk utendaji wa umma etc, mtumishi wa taasisi hakupasw akaa mahali pamoja muda mrefu, kuna ushuhuda hadi viongozi wa dini /serikali na watumishi wengine wamekuwa wakikaa sehemu kwa kiasi cha kuiingia ktk jamii kama wenyeji, huku wakijifunza tabia zao kwa ufasaha kabisa.Utakuta haw aatumishi wanajuana na wenye fedha, wakijua na watu maarufu, wakiwapa hawa watu maarufu haki kuliko hawa akina kobelo.

Vivyo hivyo hata hiyo bure inatadanganya watu waanze idai na ku abuse, mwishowe watajikuta haijawa mtaji ili ni ATM na siku inasimama jamii inashindwa kwenda na mapinduzi huanza iva.Tatizi ni kuwa na counter and check ktk hii mifumo ili kuhakikisha uzembe hauruhusiwi.Ila tujuavyo nchi yetu hakuna kitakachofanyika kisigeuzwe kuwa mazoea.Believe me hata mimi na wewe tukifikia miaka fulani tunaanza amini life limeharibika na best way kufanya vitu ia kama tunavyofanya leo ktk miaka ijayo.
 
Katika miaka ya 70s kuna takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ilipokea kama 3Billion USD. Kama pesa hizi zingetolewa mwaka 1975 pekee yake, zingekuwa na thamani ya 12Billioni ya leo. Ni kiasi gani kilienda kwenye elimu sina data kamili.
Sawa lakini nachouliza mimi ni mahusiano baina ya ELIMU bure wakati wa Nyerere na fedha hizo..

Kumbuka miaka ya 70s misaada yote ilokuwa ikitolewa ilikuwa ni Project aid yaani inahusiana na project zenyewe hivyo mwalimu kupewa Bil 3 na akaweza kujenga reli na miundombinu yote tunayoitumia hadi leo hii siwezi kupingana na kiasi hicho. Hivyo leo hii ukitaka kujenga reli toka Dar hadi Tunduma tu zinaweza kuwa hazitoshi kulingana na hali ya maisha ya leo hata kama fedha hizo zina thamanishwa sawa na bil 12 lakni pia umesahau ya kwamba baada ya mageuzi ya Uchumi mwaka 1985 misaada hiyo hiyo ilifika bil 7 ambazo leo sijui utasema ni kiasi gani, na miaka ya 90s ya Mkapa ilifika bil 8 na kati ya zote project aid zime declinewhile more emphasis ipo ktk general budget support kwa matumizi ya ndani kama elimu na Afya na kulipana mishahara mikubwa, safari na semina zao..

Miaka hii misaada inatolewa kama programme aid ndio hiyo sijui MKUKUTA na kadhalika ambayo macho wya watu wote yapo hapo kuiba... na ndio maana nasema toka mwaka 2000 - Corruption is our biggest problem japokuwa misaada ya leoi inakuja na masharti magumu pia ni mitego ya nchi tajiri kutuweka ktk madeni, hawa hawatusaidii isipokuwa kwa faida yao - basi hata elimu jamani tuwategemee wahisani?.

Nachitaka kusema miye, na ndio sababu ya kuuliza hivyo ni kwamba ELIMU bure inawezekana kabisa ikiwa tuliweza kuendesha elimu a Afya kwa kutumia Tumbaku, korosho, Chai na Pamba ambazo zilikuja poromoka bei na ikawa mwisho wetu hivyo hata hizo Almasi, Dhahabu na vinginevyo vinaweza kwisha lakini bei yake haiwezi kudondoka kama tumbaku na Pamba maana ndio uchumi wa leo na kesho. Kwa hiyo hoja nya Zitto na Chadema kwa Ujumla inawezekana kabisa japo Lowassa kaidakia isipokuwa huyu ana lengo lake kisiasa kama ilivyo misaada tunayopokea.


Tatizo liko wapi wapi? tatizo kubwa letu ni kujengewa misingi ya maendeleo yetu na hawa IMF na world bank ambao wao hawajui matatizo yetu zaidi ya kuelewa sisi ni maskini na tunahitaji msaada. kwa hiyo wanaitoa misaada yao kwa mashatri ambayo wanahakikisha fedha yao itarudi na kwa kufanya hivyo they tend to apply a top-down approach and instead of identifying the needs of the poor maana necessity is the mother of invention na hwa njamaa kusema kweli they don't know what is necessity to us, isipokuwa maskini anayetaka msaada kama yule unayempa shilingi 100 pale Salender Bridge..


L
a pili ni utawala bora ambao mawazo yao ni kuiona Tanzania kama Dubnbai ama Ulaya.. Hizio ndio hadithi za viongozi wetu ambao wanashindwa kuelewa kwamba asilimia zaidi ya 50 ya vija awetu leo hii hawana ELIMU ya kutosha, hawala ujuzi wa kazi ambazo zinaweza kutuletea maendeleo, hivyo hata ajirra zetu mwajiri ata prefer kuajiri mgeni mwenye elimu na ujuzi wa kazi hizo.

Hivyo basi ELIMU bure ni muhimu sana kwa nchi yetu na ndio sababu ya kujenga shule za kata. na tunataweza tu kuwapa watoto wetu Elimu bora ikiwa tutaweka nguvu kubwa kifedha ktk project yenyewe badala ya kutaka watu wajitolee kufundisha ama kujenga shule hizi. Binafsi yangu nitaendelea kuwa mpinzani mkubwa wa mfumo wa Elimu nchini hasa pale tunaposisitiza kulipia elimu kwa fedha inayotokana na kodi za wananchi..Serikali inakuwa wezi kama wahisani wetu maana kodi zetu ndizo zinajenga na kuendesha shule (mtaji) halafu bado wazazi wanalipishwa ada kubwa kuwasomesha watoto hao hao.. WE pay double for same thing... Hii nasema hapana huu ni UFISADI mkubwa unafanyanyika!
 
Katika miaka ya 70s kuna takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ilipokea kama 3Billion USD. Kama pesa hizi zingetolewa mwaka 1975 pekee yake, zingekuwa na thamani ya 12Billioni ya leo. Ni kiasi gani kilienda kwenye elimu sina data kamili.
hakuna senti ilokwenda ktk ELIMU maana miaka hiyo misaada ilitokana na project sio Programme aid kama leo hii.. Hivyo mwalimu hakutumia fedha za misaada kujenga wala kuendesha elimu nchini isipokuwa fedha zetu wenyewe maana hukuna haja ya kununua Catapillar wala ndege kutoka nje kuendesha elimu..
 
hakuna senti ilokwenda ktk ELIMU maana miaka hiyo misaada ilitokana na project sio Programme aid kama leo hii.. Hivyo mwalimu hakutumia fedha za misaada kujenga wala kuendesha elimu nchini isipokuwa fedha zetu wenyewe maana hukuna haja ya kununua Catapillar wala ndege kutoka nje kuendesha elimu..

It doesn't matter where Nyerere found the money to fund free education. He might used foreign aid, local resources or the combination of the two. The point is he managed to provide free education and by doing so he created at least two things: the process which was used to dispense the education, and the outcome of that process.

So rather than discussing the financial sources which was used to keep the system up and running, could we talk about the process and the outcome? I think we could. For example, one could argue that in order to educate Tanzanians in huge number, we sacrificed, and unfortunately we have continued to scarify, quality for quantity. In simple words the process of educating Tanzanians has been of poor quality for many years.

In terms of the outcome, I don't need to talk a lot. On his recent tour to the USA, Mr. Mbowe said that there are four priorities if CHADEMA take power: 1-Education, 2-Education, 3-Education, and 4-The rule of law.

He spent a half of his speech to explain why Tanzanians can't complete globally due to poor education. Mind you, he wasn't talking about the current crop of students, but the older ones that received education for free.

I am not saying free education isn't possible in Tanzania. It is possible. However, we the people, the stakeholders, need to have a serious discussion on this issue. Just because Kenya and Sweden have done it doesn't mean we are capable of achieving their feet with the same degree of success.
 
Back
Top Bottom