Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Mods ningependa uiache mada kama ilivyo na isiunganishe na mada zingine.
Kama kawaida, ningependa kutoa salaam kwa waZalendo wenzangu. Katika mjadala huu wa katiba kuna mambo mengi yanajitokeza. Moja ya jambo lililojitokeza ni kutaka kufanyia amendment ya vipengere ya katiba ya sasa. Mzee Mwinyi amesimamia hilo jambo. Kwanza nilimuunga mkono lakini kwa sasa naona kuwa umefika wakati wa katiba mpya.
Kwanini tunahitaji katiba mpya na sio kubadilisha? Zifuatazo ni sababu zangu za kutaka katiba mpya. Kumbuka hizi ni sababu za kutaka katiba mpya na sio vitu vitakavyokuwa ndani ya katiba hiyo.
Kwanza: Katiba ya sasa ni ngumu kiuandishi. Imeandikwa kwa lugha ya mwanasheria. Inatakiwa iandikwe kwa lugha ambayo itamfanya mtu yoyote kuelewa katiba hiyo.
Pili: Katiba ina muundo wa check and balance ya chama kimoja. Katika mfumo wa chama kimoja, chama tawala kilikuwa ni mhimili mwingine wa utawala na chujio la kupata viongozi. Kwa sasa check and balance iwe mikononi mwa watu. Watu wawe na uwezo wa kumwingiza mtu madarakani na vilevile kumvua madaraka. Shughuli za bunge, mahakama na serikali ziwe za kutazama utendaji mzuri na sio kulindana.
Tatu: Baada ya uhuru marais wengi wa Africa walijilundikia madaraka hili kufanya reforms au kuzuia mgawanyiko wa kidini na kikabila. Wengi waliboronga na wachache walitumia madaraka yao vizuri. Hivyo wimbi la marais kuwa na madaraka mengi hili kuondoa tofauti za kikabila na kidini zimepitwa na wakati. Kwa Tanzania ni muda wa kurudisha madaraka kwa wananchi wenyewe. Hakuna sababu mtu ambaye hana interests na maendeleo ya watu wa Mtwara awe mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Nne: Katiba inawakilisha historia ya nchi na watu wake. Katiba ya sasa inawakilisha maoni viongozi wa juu. Viongozi hao walitaka nchi iwe kwa mtazamo wao. Kwa mfano kujenga taifa la kijamaa ni madhumini ya katiba ya sasa. Hivi toka tumepata uhuru kuna mtanzania wa kawaida aliyetaka kujenga Ujamaa kwa hiari yake?
Tano: Katiba lazima imlinde na kumpa haki mtanzania katika kushiriki katika shughuli za uongozi wa nchi yake. Katiba ya sasa ina mpa haki mwanachama wa chama cha kisiasa.
Kwa vipengere nilivyoweka hapo juu na vingene vitakavyokuja, dai katiba mpya. Itasaidia kama utasoma katiba ya sasa. Lakini hakuna ulazima wa kuisoma katiba yenyewe.
Wenu:
Z10