Barua Kutoka Ughaibuni - Kwanini Katiba Mpya na Si Kubadilisha ile Iliyopo

Bwana CJ suala la watu wanaozunguka rasilimali fulani kunufaika na mapato ya rasilimali hiyo kwa mtizamo wangu halihitaji serikali za majimbo. Chini ya mfumo tulionao sasa, mbali ya serikali kuu tuna local goverments ambazo sipo katika mtindo wa majiji, manispaa, miji, mitaa na vijiji. Chini ya utaratibu huu inaweekana sheria ikawekwa kwamba asilimia fulani ya mapato yanayopatikana kwa mfano katika madini itumike kuboresha huduma za kijamii katika jamii inayozunguka rasilimali husika.


GJ:

Kwa Tanzania serikali za majimbo kwa namna fulani zipo. Tatizo ni kuwa wananchi hawana madaraka nazo. Wananchi hawana madaraka ya kumchagua Mkuu wa mkoa au wilaya.

Local authorities zipo. Lakini technocraties wa local authories hizi bado wanateuliwa na rais au ofisi ya waziri mkuu. Mkuu wa mkoa anasikiliza amri kutoka kwa rais kwa sababu ndie aliyempa nafasi hiyo. Lakini akichaguliwa na wananchi, basi ni lazima ajiandae kufanya vile wananchi wanavyotaka.
 
Wanamtandao waliopo bongo kesho profesa Issa Shivji na Twaha Ulimwengu wataongoza mdahalo mkubwa wa katiba katika ukumbi wa Nkuruma Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Kwa mujibu wa makamu Raisi wa Jumuiya ya Wafanyakazi wa Chuo KIkuu cha Dar Es Salaam DR Kitila, kongamano hilo litakuwa ni mwanzo wa mfululizo wa makongamano ya wanazuoni na wananchi wengine kuhusiana na katiba yatayochukuwa kipindi cha mwaka mmoja. Lengo kuu kwa mujibu wa makamu Raisi ni kuwaelimisha watu juu ya katiba na umhimu wa madadiliko na kudhihirisha maoni na mitazamo ya watu juu ya mjadala wa kitaifa unaoendelea juu ya mabadiliko ya katiba. Ningewaomba wanajamii forum wenzangu tujitokeze kwa wingi ili tuwe na mengi ya kujadiliana yatakayotokana na kongamano hilo.

Umahiri wa Profesa Shivji katika taaluma ya sheria na katiba hapa Afrika Mashariki hauelezeki na uaminifu na uhuru wake katika mijadala kama hii ni wakujivunia. Nakumbuka toka miaka ya 90 wakati tunaamua kwenda vyama vingi mmoja kati ya wanazuoni waliokuwa wakihamasisha juu ya katiba mpya ni Profesa Shivji. Mimi binafsi nilikuwa mmoja wa waathirika wakubwa wa hoja zake japo kadili muda unavyozidi kwenda kuna baadhi ya mambo machache ambaye natofautiana naye. Nategemea kujifunza mengi zaidi katika kongamano la kesho na kupata nafasi ya kuuliza na kujadili pia juu ya yale ninayotofautana naye
 
Hivi,hapa nchini pana vyuo vikuu vingapi?Ni zaidi ya 32.Kila siku mambo mazuri yanatokea Udsm?Hivi hao wanataaluma wa vyuo vingine wao huwa wanafanya nini?Wanachoamini wao ni kukomoana na wanafunzi kama hapa mzumbe na kule Udom?Vinginevyo ajira zao zinatia shaka na ubopa wao wa kitaaluma!!Kila la kheri Prof.Shivji na wadau wengine ila pia uwatembelee tena UDOM ambako wakati unaenda kuwatoa moshi ubongoni walikukatia umeme.
 
Mimi nadhani Chuo Kikuu cha DSM kimeonesha njia na vingine bado vina mda wa kutosha kuipita. Tukubaliane kwamba UDSM ni baba kama sio babu wa Vyuo Vikuu vyote Tanzania achilia mbali vitivo vya sheria na elimu ya siasa ambavyo mambo ya katiba yanavihusu zaidi. UDSM ina miaka zaidi ya 40 ikisheheni maprofessa na madakitari wenye uzoefu unaliotukuka katika fani zao. Chuo Kikuu cha Mzumbe hakina hata miaka kumi toka kilivyopata hadhi ya chuo kikuu. Lakini kimepiga hatua hakipaswi kupuuziwa. Chuo Kikuu cha Dodoma hakina hata miaka mitano. Ni kitoto kama nikisema. Fani ya sheria haina hata miaka miwili kati chuo hicho. Tukitarajia kifanye makubwa kama UDSM itakuwa ni sawa na kukamua damu toka katika jiwe.

Tukirudi katika kongamano la katiba la jana limetoa muelekeo mzuri sana katika mstakbari wa Taifa kuhusiana na Katiba mpya licha ya mapungufu machache yaliyojitokeza. Wachokoza mada PROF SHIVJ na ULIMWENGU walidodosa mada kwa umahiri mkubwa na bila kuonesha ushabiki wa kisiasa jambo ambalo liliwahamasisha hadhira iliyokuwepo kuweza kuchangia kwa mafanikio. Prof Shivji aliweka wazi umhimu wa kuwa na katiba mpya kwa kujikita zaidi la uhalali wa kisiasa (political legitimacy)wa ya katiba tuliyonayo kwa sasa. Kwa mujibu wa Prof Shivji, Katiba tuliyonayo japo uandikwaji wake haukuwahusisha sana wananchi kuna wakati ilikuwa inapata uhalali wake kutokana na itikadi mbali mbali za kisiasa zilizokuwepo wakati huo. Kubwa zaidi ilikuwa ni itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Baada ya kuzikikwa kwa Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar na kuivusha nchi toka kwenye ujamaa kwenda ubepari, uhalali wa kisiasa wa Katiba yetu, kwa mujibu wa Prof Shivji, ulipoteza muelekeo. Hivyo palikuwa na ulazima kwa serikali kutafuta uhalali mwingine wa kisiasa kwa kuja na katiba mpya itakayoweka misingi mipya ya muelekeo wa nchi katika mfumo mpya wa kisiasa na uchumi.

Kwa mujibu wa Prof Shivji tatizo la Katiba sio sana katika vifungu vya kanuni na maelekezo yaliyomo katika katiba bali ni mfumo mzima wa upatikanaji wa katiba na namna inavyokubalika kwa watu. Kwa hili, Profesa alikuwa anaowanisha katiba kama mwongozo na sheria kuu na kama nyenzo kuu ya uhalalishaji wa matumizi ya mamlaka. Msimamo wa Profesa Shivji uliungwa Mkono na Ulimwengu ambaye alienda hatua mbele zaidi kwa kusisitiza kwamba Katiba kama nyaraka ya kisheria na chimbuko la madaraka na ukomo wa madaraka kwa dola na vyombo vyake haiwezi kuwa na maana yoyote kama hamna maadili ya uongozi na utashi wa dhati wa kuitii. Bila shaka ni kutokana na ukweli huo kwamba nchi kama Uganda ambayo ilikuwa ni ya kwanza kuandika Katiba mpya wakati wa vuguvugu ya kuingia kwa mfumo wa vyama vingi bado haina mafunzo ya maana katika nchi nyingine kuhusiana na demokrasia na utawala wa sheria.

Kwa upande mwingine mh Tundu Lisu alijaribu kutofautiana na Professa Shivji kwa kusema tatizo kubwa katika katiba sio kukosa uhalali wa kisiasa bali ni kutokuwa na uwezo wa kuifikisha Tanzania kesho. Hakutoa ufafanuzi sana kuhalalisha hoja yake pengine kutokana na uchache wa muda aliopewa. Mimi binafsi sikupata bahati ya kupata nafasi ya kuchangia kutokana na watu wengi kutaka nafasi hiyo licha ya uhaba wa muda. Kwa uelewa wangu wa haraka haraka Mh. Lisu alikuwa anamaanisha kwamba Katiba yetu inamapungufu sana katika kanuni na maelekezo yake kiasi kwamba haiwezi kutufikisha kesho. Baadhi ya mapungufu ambayo wachangiaji wengine pamoja na wazungumzaji wakuu waliyoyagusia ni pamoja na madaraka makubwa ya Raisi, kutokuwepo Tume Huru ya Uchaguzi, haki za binaadamu kutolindwa ipasavyo, matatizo ya muungano nk.

Suala la kujiuliza ni kwanini kilio cha katiba mpya kimepata kasi zaidi kuanzia kipindi tulipokwenda vyama vingi na mfumo wa kibebari? Kwa nini hayakujitokeza katika kipindi cha Mwalimu kipindi ambacho "kicontents" katiba ilikuwa na mapungufu mengi ya msingi kuliko sasa?. Kwa mfano, katiba yetu haikuwa na vifungu vinavyolinda haki za binaadamu na mamlaka ya Raisi na wanasiasa yalikuwa makubwa zaidi. Mimi nadhani Professa Shivji yuko sahihi katika hili japo pia kuna mambo mengi ya kihistria yanayoweza kusemwa kuhusiana na uhalalishaji wa matumizi ya mamlaka kipindi cha ujamaa na kujitegemea.


Jambo lingine la msingi, ambalo hata mimi nimeshalizungumzia huko nyuma, ni namna mchakato wa katiba mpya unavyopasa kuanza. Prof. aliunga mkono Raisi kuunda Tume na kuwataka wananchi kupiga kelele kuhakikisha kwamba Tume hiyo inakuwa huru na inawakilisha makundi yote mhimu ya kijamii. Prof aliainisha hatari ya mchakato huo wa awali kuanzia Bungeni.

Mapungufu madogo madogo yaliyojitokeza ni pamoja na hili ambalo linatukabiri katika Forum yetu la wachangiaji kuwa na jazba na kukosa uvumilivu wa hoja zinazopingana nao. Baadhi ya wanakongamano walionekana kuwazomea wale wanaotoa hoja tofauti na misimamo yao bila hata kujali umri na heshima zao. Ikubalike kwamba panapoitishwa kongamano la watu mbali mbali tofauti za kimitizamo zinatarajiwa na washiriki wanapaswa kuvumiliana na kuheshimiana katika toafuti zao. Tatizo la ushabiki kwa baadhi ya wachangiaji toka katika hadhira pia lilikuwepo.

Mchangiaji mmoja raia wa Kenya aliikosoa Katiba kwa kudai kwamba inamruhusu ofisa wa polisi kumupiga raia risasi na kufafanua jinsi ambavyo hakuridhishwa na Mh. Kikwete kuwa Raisi. Alieleza zaidi kwamba yeye mwenyewe ni muathirika wa mapungufu haya lakini hakufafanua zaidi ilikuaje. Raia wa nje mwenye busara na kujua mipaka yake ya kuwa katika nchi za watu asingetarajiwa kusema hayo. Kenya jeshi la polisi mara kadhaa limepiga risasi raia wake lakini sidhani kwamba walikuwa wanatekeleza haki yao ya kikatiba. Askari polisi waliouwa huko Arusha katika maandamano hawakuwa wanatekeleza haki yoyote katika katiba. Ifahamike kwamba chini ya Katiba na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai polisi hawaruhusiwi kuuwa raia. Uhali wa kuuwa katika nchi zote unakuwepo katika mazingira ya dhalula (necessity) pale kuuwa kunakuwa lazima kwaajili ya kulinda maisha ya watu wengine zaidi au maisha ya askari wenyewe. Kama kwenye sakata la Arusha mazingira hayo ya dhalura yalikuwepo au la hilo ni suala la kimantiki na ukweli wa mambo. Kwa hivi sasa kuna madai kinzani toka Jeshi la Polisi na Chadema huku kila mmoja akimsukumia mwingine lawana. Hoja ya Chadema sio kwamba polisi hawaruhusiwi kutumia silaha za moto katika mazingira yoyote bali ni kwamba hayakuwepo mazingira yaliyohalalisha matumizi ya risasi za moto. Kwa kuwa suala hili liko Mahakamani ni sheria za nchi zinaruhusu maofisa wa jeshi la polisi kushitakiwa kama walikiuka sheria tuache hatua za kisheria zichukuliwe.
 
Katiba katiba yetu mpya suala la haki ya wananchi kuamua kujiunga au kutojiunga katika ushirikina wa aina yoyote lazima lizingatiwe. Wananchi wawe na haki ya kuulizwa na kuridhia kama kwa mfano, wanataka kujiunga na Ushirikiano wa Afrika Mashariki au ushirikiano wowote unayoihusisha nchi.
 
Sasa tumeshapata Sheria ya Uundwaji wa Tume ya Katiba ambayo kwa bahati nzuri imezingatia maslahi ya makundi mengi ya kijamii pamoja na vyama vya siasa. Tujadili sasa kwa kina mabadiliko ya Katiba. Naona kuwasilisha
 
Ndio nimemaliza kuisoma Katiba ya Muungano; sikujua mambo kadhaa na imenisaidia;

Lakini kama aliyeanzisha hii topic; Katiba iliyopo inajitosheleza kama kungefanyika 'mabadiliko' na sio 'kuibadilisha' yote!?

Mimi hata sijui wakiibadilisha hizo sentensi zitakuwaje? kwasababu, nina wasiwasi kwamba itabidi waandike mambo yale yale... na kufanya marekebisho kidogo;
 
Ndio nimemaliza kuisoma Katiba ya Muungano; sikujua mambo kadhaa na imenisaidia;

Lakini kama aliyeanzisha hii topic; Katiba iliyopo inajitosheleza kama kungefanyika 'mabadiliko' na sio 'kuibadilisha' yote!?

Mimi hata sijui wakiibadilisha hizo sentensi zitakuwaje? kwasababu, nina wasiwasi kwamba itabidi waandike mambo yale yale... na kufanya marekebisho kidogo;

Kama tulivyosikia Tume ya Kuratibu Marekebisho ya Katiba imeshaundwa chini ya wenyekiti wa Mh Sinde Warioba akisaidiwa na Mh Jaji Mkuu Mstaafu Ramadhani. Pia Tume imesheheni vigogo wenye histroria nzuri ya kulitumikia taifa kama DKT Salim Ahmed Salimu. Kina mabingwa wa Sheria ya Katiba na Siasa kama akina Dr Mvungi, Prof Kabudi na Prof Balegu. Kwa kiasi kikubwa Tume imeundwa kwa kuzingatia uwakilishi wa makundi ya kijamii na kisiasa. Kwa kipindi hiki cha vuguvugu ya mageuzi wajumbe wa Tume wana nafasi nzuri ya kutumia hekima na busara yao ili tupande Katiba nzuri itakayotufikisha kesho na kesho kutwa. Tumuombe Mungu awazidishie hekima na busara ili tupite salama katika haya mapito mhimu kwenye historia yetu.
 
Kaka George

Sasa huko unako kwenda unahitaji wataalamu wa kutunga sheria, mahakama, na watu wanaojau sheria vizuri. Mi naelewa siasa kiasi lakini si sheria.

Ni kweli ndugu yangu kwa hilo nikiri kwamba nimetumia nguvu kupita kiasi.

Tatizo la mfumo wetu wa sheria ni kwamba kila mtu anachukuliwa kama anajua sheria japo mikakati ya kuwafanya watu wengi wajue sheria haipo
 
Back
Top Bottom