Barua Kutoka Ughaibuni - Kwanini Katiba Mpya na Si Kubadilisha ile Iliyopo

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Mods ningependa uiache mada kama ilivyo na isiunganishe na mada zingine.

Kama kawaida, ningependa kutoa salaam kwa waZalendo wenzangu. Katika mjadala huu wa katiba kuna mambo mengi yanajitokeza. Moja ya jambo lililojitokeza ni kutaka kufanyia amendment ya vipengere ya katiba ya sasa. Mzee Mwinyi amesimamia hilo jambo. Kwanza nilimuunga mkono lakini kwa sasa naona kuwa umefika wakati wa katiba mpya.

Kwanini tunahitaji katiba mpya na sio kubadilisha? Zifuatazo ni sababu zangu za kutaka katiba mpya. Kumbuka hizi ni sababu za kutaka katiba mpya na sio vitu vitakavyokuwa ndani ya katiba hiyo.

Kwanza: Katiba ya sasa ni ngumu kiuandishi. Imeandikwa kwa lugha ya mwanasheria. Inatakiwa iandikwe kwa lugha ambayo itamfanya mtu yoyote kuelewa katiba hiyo.

Pili: Katiba ina muundo wa check and balance ya chama kimoja. Katika mfumo wa chama kimoja, chama tawala kilikuwa ni mhimili mwingine wa utawala na chujio la kupata viongozi. Kwa sasa check and balance iwe mikononi mwa watu. Watu wawe na uwezo wa kumwingiza mtu madarakani na vilevile kumvua madaraka. Shughuli za bunge, mahakama na serikali ziwe za kutazama utendaji mzuri na sio kulindana.

Tatu: Baada ya uhuru marais wengi wa Africa walijilundikia madaraka hili kufanya reforms au kuzuia mgawanyiko wa kidini na kikabila. Wengi waliboronga na wachache walitumia madaraka yao vizuri. Hivyo wimbi la marais kuwa na madaraka mengi hili kuondoa tofauti za kikabila na kidini zimepitwa na wakati. Kwa Tanzania ni muda wa kurudisha madaraka kwa wananchi wenyewe. Hakuna sababu mtu ambaye hana interests na maendeleo ya watu wa Mtwara awe mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Nne: Katiba inawakilisha historia ya nchi na watu wake. Katiba ya sasa inawakilisha maoni viongozi wa juu. Viongozi hao walitaka nchi iwe kwa mtazamo wao. Kwa mfano kujenga taifa la kijamaa ni madhumini ya katiba ya sasa. Hivi toka tumepata uhuru kuna mtanzania wa kawaida aliyetaka kujenga Ujamaa kwa hiari yake?

Tano: Katiba lazima imlinde na kumpa haki mtanzania katika kushiriki katika shughuli za uongozi wa nchi yake. Katiba ya sasa ina mpa haki mwanachama wa chama cha kisiasa.

Kwa vipengere nilivyoweka hapo juu na vingene vitakavyokuja, dai katiba mpya. Itasaidia kama utasoma katiba ya sasa. Lakini hakuna ulazima wa kuisoma katiba yenyewe.

Wenu:

Z10
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,471
2,000
Another rubbish from Great thinkers they wanna be seen starting new thread ...... Mods leave this here do not remove pleaseeeeeeeeeee... khe khe kheeeeeeeee
 
LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
Another rubbish from Great thinkers they wanna be seen starting new thread ...... Mods leave this here do not remove pleaseeeeeeeeeee... khe khe kheeeeeeeee

i agree.... typical replicate
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Guys:

Imesoma nilichoandika au mnakurupuka. Hii thread ni original. Kwa sababu nadai katiba mpya bila kuangalia vipengere vya katiba ya sasa.
Vilevile ukumbi huu ni wa mabadiliko ya katiba. Sasa kama unashindwa kuchangia si unanyamaza.
 
George Jinasa

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
395
225
Nimeguswa na namna mchangiaji toka ughaibuni alivyoweza kufanya uchambuzi yakinifu kuhhusiana na mapungufu yaliyomo katika katiba yetu. Ila ningemuomba anipanue mawazo kidogo. Anazungumzia tatizo la matumizi ya lugha ya kisheria inayowafanya wananchi wa kawaida kushindwa kuielewa. Lakini katiba kama waraka wa kisheria inaweza kuepuka kuandikwa katika lugha ya kisheria? Wataalamu wanatuambia kwamba lugha ya kisheria ni mhimu katika kuzuia utata katika tafsiri ya dhana mbali mbali mbali zilizotumika katika kuunda kanuni, amri na makatazo. Tukiepuka moja kwa moja matumizi ya lugha hiyo hatuwezi kupelekea matatizo katika ufasiri wa katiba? Ningeomba pia tujadili hili. Vinginevyo kama tatizo la lugha ni kubwa, uandikaji wa katiba mpya hautaepukika.

Kwa upande wa mapungufu mengine kama vile madaraka ya Raisi, mjadala zaidi unahitajika ili kupima uzito kati ya katiba mpya au marekebisho zaidi ya hii tuliyonayo. Nasema hivyo kwa sababu, mtu anaweza kusema kwamba mapungufu hayo yanaweza kuondolewa kwa kurekebisha katiba. Baadhi ya vifungu vinavyompa madaraka makubwa Raisi vinaweza kufutwa, kuongezewa au kupinguziwa maneno na vifungu vingine zaidi vinavyowapa wananchi nguvu zaidi ima za moja kwa moja au kupitia wawakilishi wao vikaongezwa. Nategemea wachangiaji zaidi watanikosoa na kunirekebisha.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
George Jinasa:

Katiba yoyote ni document ya kisheria. Pamoja na hayo sio document yoyote ya kisheria ni lazima iandikwe kwa lugha wanayotumia wanasheria. Nilipokuwa primary school, tulitumia katiba ya chama cha mapinduzi kama kitabu katika somo la siasa. Watunzi kwa sababu walitunga wakijua kuwa ni lazima siasa ya chama hicho ieleweke na mtu wa kawaida, hivyo walitumia lugha ya kawaida.

Mlengwa wa katiba ya JMT sio mtanzania wa kawaida. Sidhani kama mtoto wa shule ya msingi Tanzania anaweza kutumia katiba hiyo kama kitabu cha rejea. Katiba sio rocket science na tusijaribu kuifanya iwe.

Kuhusu madaraka ya rais, ni lazima kukubali kuwa demokraisa ina gharama zake. Moja ya gharama zake ni majadiliano ya kuvutana ambayo wakati mwingine hayana msingi. Hivyo viongozi wa mwanzo wa nchi za kiAfrika walijiongezea madaraka, wengine kwa nia njema kabisa. Walitaka kufanya reforms. Mfano mzuri ni Nyerere, Kaunda na Mugabe. Lakini umefika wakati kwa wananchi kurudishiwa madaraka yao.
 
Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,812
2,000
Aitakua na maana kuandika katiba mpya unless tuna taka kubadilisha mfumo mzima na namna ya uongozi wa sasa ulivyo Tanzania. Na ukisema uibadilishe maana yake unataka kutoka kwenye mfumo wa katiba ya sasa ambao ni 'unitary' na kwenda kwenye mfumo wa 'federal'. Hizo ndizo katiba mbili kuu duniani, kila nchi inayo badilisha imejifunza kuziba viraka vya katiba wanazotumia lakini si kuibadilisha yote.

Kenya ni nchi ambayo kwa sasa unaweza sema wamejaribu badilisha katiba karibu yote kutoka 'unitary' kwenda 'federal' na ina make sense kwa matatizo waliyonayo ya ukabila. Federal governance aims to release autonomy in a segregated society kama Kenya ambako kuna madai ya kutotendewa haki baadhi ya wanajamii au America ambayo iliundwa chini ya vita na unshared ideology (ndio mpaka leo kwingine kuna capital punishment kwingine hakuna) hivyo hiyo ndio basis ya Federal constitution kuunganisha watu lakini kuachia baadhi ya maamuzi locally. Whereby a unitary governance is much more advanced and aim to govern a society that has almost a similar ideology and values. Na ukisema tu-adapt a federal one atuendi mbele tutakuwa tunarudi nyuma as a tolerant society.

Tatizo kubwa la katiba yetu ni madaraka ya raisi na too much power of the executives, hii imeondoa nguvu ya bunge na judiciary. Ukitaka kuona ni tatizo mahakama hazina nguvu independently za kusikiliza kesi za katiba sasa where is the check in judiciary. Au mmbunge hawezi leta motion ya katiba bungeni ikajadiliwa na kupigiwa kura without the authority of the executive hili ni tatizo ambalo lina wafanya hata majambazi wajilimbikie mali kwa kuwa the parliament is weak and the judiciary is like the branch that doesnt exist and has no independent voice hili ndio tatizo kubwa kwenye katiba yetu.
 
Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,518
2,000
Kwanza: Katiba ya sasa ni ngumu kiuandishi. Imeandikwa kwa lugha ya mwanasheria. Inatakiwa iandikwe kwa lugha ambayo itamfanya mtu yoyote kuelewa katiba hiyo.

Katiba ni sheria pekee katika sheria za tanzania ambayo imetungwa kiswahili na version inayojulikana na kutambulika kisheria ni version ya Kiswahili.

Tatizo tulilonalo ni kuwa watanzania hatupendi kusoma, nakumbuka mwaka 2009 kwenye maonesho ya Sabasaba, wizara ya sheria na katiba ilikuwa na banda na walikuwa wanagawa katiba bure . Watu waliokuwa na interest ya kuchukua katiba ili waisome na kuielewa walikuwa wachache sana.
 
Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,812
2,000
Katiba ni sheria pekee katika sheria za tanzania ambayo imetungwa kiswahili na version inayojulikana na kutambulika kisheria ni version ya Kiswahili.

Tatizo tulilonalo ni kuwa watanzania hatupendi kusoma, nakumbuka mwaka 2009 kwenye maonesho ya Sabasaba, wizara ya sheria na katiba ilikuwa na banda na walikuwa wanagawa katiba bure . Watu waliokuwa na interest ya kuchukua katiba ili waisome na kuielewa walikuwa wachache sana.
Kaka
kama katiba ni sheria yenye principles za muongozo uoni kama mahakama ni sehemu kuu ya ku-interpret katiba na kuleta mabadiliko ya kikatiba.

Ebu niambie hizi mahakama zina nguvu gani katika taifa letu zenyewe? uoni ni tatizo si lazima kila mtu lazima ajue katiba lakini ni muhimu viongozi wa upinzani kujua pa kuanzia na kwenye kuibadilisha hii katiba. Chombo kinachotakiwa kubadilisha akina sauti ya kuikosoa the same thing they're supposed to supervice. The judiciary branch of the check ni tatizo la kwanza before anything, kwenye mabadiliko ya katiba. Serikali aiwezi sema au amua kama katiba ina makosa ni haki ya watu kitaifa kusema kama ina makosa. Na representative wa watu tayari wameshasema kuna makosa, mahakama chali aina nguvu yoyote kisheria.
 
Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,268
2,000
nakumbuka mwaka 2009 kwenye maonesho ya Sabasaba, wizara ya sheria na katiba ilikuwa na banda na walikuwa wanagawa katiba bure.
mpaka Sabasaba ndio watoe Katiba?

Nimetafuta ma bookstore yote hakuna Katiba mjini hapa, duka la Serikali Jamhuri street ndio wazembeeee wa kutupwa mtaroni
 
George Jinasa

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
395
225
Kuhusu madaraka makubwa ya Raisi nakubaliana nanyi kuwa ni tatizo. Hata baba wa Taifa amewahi kuungama kwamba chini ya Katiba yetu angeweza hata kuwa dikteta kama angetaka. Hata Bunge lenyewe lina mamlaka makubwa sana chini ya Katiba yetu. Kwa hivi sasa wabunge wana uwezo hata wa kuibadilisha Katiba ili kujiongezea muda wao kuwepo Bungeni. Hamna kifungu katika Katiba kinachowazuia ili mradi kura zitoshe. Kuliondoa hili kungekuwemo vifungu katika Katiba ambavyo ndio msingi wa Katiba, vifungu ambavyo visiweze kurekebishwa bila kupata ridhaa ya wananchi.

Mapungufu haya katika Katiba yalijidhihirisha katika kesi maarufu ya Mgombea Binafsi ambapo Mahakama ya Rufaa ilishindwa kutengua marekebisho ya Katiba yanayoonekana kukinzana na vifungu vingine katika Katiba kwa kuwa chini ya Katiba yetu hamna kifungu chenye nguvu kuliko kingine na kwamba Bunge limepewa nguvu ya kisheria kurekebisha kifungu chochote cha katiba. Mahakama ililiona suala la kama sheria ndani ya katiba inayozuia wagombea binafsi ni halali au la, ni suala la kisiasa ambalo Mahakama haiwezi kuliingilia. Japo Mahakama ya Rufaa inalaumiwa kwa hili, lakini kwa maoni yangu tatizo halikuwa Mahakama ya Rufaa bali ni mapungufu yaliyomo katika Katiba. Mahakama ilijielekeza kiusahihi kabisa kwamba kwakuwa Bunge kwa kutumia mamlaka yake chini ya Katiba limetunga sheria hiyo kwa kuzingatia taratibu zote za kurekebisha sheria zilizomo ndani ya Katiba, isingekuwa busara na haki kwa Mahakama kutumia kofia yake ya mahakama kurekebisha mapungufu yaliyomo katika Katiba, Hiyo ingekuwa kuingilia mamlaka ya watu na wabunge. Ndio maana Mahakama ikashauri kwamba mapungufu ya kikatiba ni matatizo ya kisiasa siyo ya kisheria na yanaweza kutatuliwa na wananchi wenyewe ima kwa kupiga kura dhidi ya wabunge wao au kuwaagiza wabunge wao waondoe mapungufu hayo katika njia za kibunge. Lakini pia wananchi wanauwezo wa kisiasa kuchagiza mabadiliko ya katiba ili kuondoa matatizo hayo.

Suala la lugha nakubaliana kwamba kwa kadili itakavyowezekana jitihada zitumike kuifanya Katiba ieleweke kwa wananchi. Hilo lifanyike pia kwa kuzingatia kwamba Katiba ni waraka wa kisheria hivyo unapaswa kuwa katika lugha isiyotoa nafasi ya utata wa kitafsiri. Kama itabidi kwa sababu za kitaalamu kubaki katika lugha ya kisheria utaratibu utumike kuandika vitabu vya kuifafanua kwa lugha ya kawaida ili kila mtu aweze kuielewa kiurahisi. Kwa hilo nafikiri itabidi tuwaachie wataalamu.
 
Uoni kama ni tatizo kama mahakama inakuwa over ruled na bunge katika maswala ya uongozi wa kitaifa. Mfano tume ya uchaguzi ina nguvu kushinda mahakama, where do we go for justice then kama tukitaka kuhakiki matokeo yenye utata. Mi nadhani serikali yetu imepotosha mno maana ya mahakama kama mhimili wa dola na hili ndio tatizo la haki kupatikana Tanzania.

Bunge ndio linaweza tunga sheria lakini mahakama lazima iangalie na ijue interpretition ya hiyo sheria, sasa kama sheria inasema mahakama aina nguvu ya kuingalia sheria (mfano tume ya uchaguzi) uoni ni upuuzi huu na uporaji wa demokrasia.
 
George Jinasa

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
395
225
Bwana Juma nakubaliana nawewe kwamba kwa hali ya kawaida Mahakama baada ya kutamka kwamba kifungu katika Sheria ya Uchaguzi kilichokuwa kinamtaka mgombea ubunge na Uraisi kutoka katika chama cha siasa ni haramu kwa kukinzana na Katiba halikupaswa kuweka kifungu katika Katiba kinachofanya masharti hayo kuwa sehemu ya katiba. Hoja yangu ya msingi ni kwamba kutokana na mapungufu yaliyokuwemo katika katiba Bunge lilikuwa na mamlaka ya kufanya lilichofanya. Mapungufu yaliyomo katika katiba kwa maoni yangu yasingeweza kutatuliwa kwa njia ya tafsiri kwakuwa yalikuwa yanaenda katika mzizi wa mamlaka ya Mahakama. Kwamba mara baada ya marekebisho hayo kuingia ndani ya Katiba yalikuwa moja kwa moja ni sehemu ya Katiba na Mahakama isingeweza, labda kungekuwa na sababu za kidhalura (necessity) kujipa hayo mamlaka. Suluhisho halali ni kulipeleka suala kwa wenye Katiba (wananchi) ambao wana mamlaka ya kulitoa au kuliacha ndani ya Katiba kama wanaona linafaa. Kama Bunge lingekiuka masharti yoyote katika katiba yanayoratibu mamlaka yao ya kurekebisho Katiba, Mahakama ingekuwa na uwezo wa njia ya ufasilina kutamka kwamba kilichotungwa na Bunge hakikuwa Katiba kwakuwa Bunge halikufanya kisheria. Lakini Bunge wanapofanya marekebisho kwa kukidhi masharti ya kikatiba bila kujali kama katiba ni nzuri au mbaya, Mahakama kama zao la katiba inakuwa haina uwezo zaidi ya kushauri kama ilivyofanya. Uwezo wote unabaki kwa wananchi.

Suala la matokeo ya mgombea Uraisi kutopingwa Mahakamani limewagawa wanasiasa na wataalamu wa katiba kwa sababu za kiusalama zaidi. Raisi anapotangazwa na Tume alafu baadae Mahakama ikabadilisha matokeo hayo iwe kwa usahihi au vinginevyo kuna uwezekano mkubwa sana wa kuwepo na machafuko kama yalivyotokea Ivory Coast. Sababu hizo hizo zitakazotolewa kwamba Tume ilipendelea zinaweza pia kutolewa kwamba Mahakama ilipendelea au ilikosea. Chukulia Raisi aliyeshinda katika Tume na kushindwa katika Mahakama ataamua kukata Rufaa, ni nani atakuwa kiongozi wa dola kwenye kipindi cha kusubiri matokeo ya Rufaa? Hoja yako naiona na ina nguvu pia, lakini umakini, busara na hekima vinahitajika zaidi katika suala hili hasa kwa nchi zetu ambazo bado zinakuwa katika demokrasia. Kabla hatujaamua katika hili ni bora pia tukapata uzoefu katika nchi mbalimbali ambazo zina vifungu kama hivyo na zisizonavyo. Suala la mhimu zaidi kuzingatiwa, kwa maoni yangu, ni kuwa na Tume huru na yenye uadilifu ambayo wananchi wataiamini kama wananvyoziamini Mahakama.
 
Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,812
2,000
Kaka una valid arguments lakini mi nadhani unaliangalia bunge kama chombo chenye sauti ya juu kushinda vyombo vingine na hili ni tatizo especially bunge ambalo ni weak.

Katiba inatakiwa kutoa legitimacy ya kuongoza baada kushinda kura za wananchi na jinsi kiongozi anvyotakiwa ku behave under the constitution guidelines. Sasa kama kura inaibiwa kunatoa legitimacy nzima ya uongozi na tayari katiba imeshavunjwa kwa sababu uongozi wako unakuwa si sauti ya watu. By commonsense bunge aliwezi kuamua kitu hapo zaidi ya katiba inasema nini kama kuna utata na hiyo ndio demokrasia. Kama nilivyokwambia mchambuzi wa katiba ni mahakama, sasa hili ni suala la mahakama kuhakikisha amna kilichovunjwa kisheria. Mahakama yenyewe ndio unaambiwa aiwezi bishia maamuzi ya tume ya uchaguzi. Uoni tayari the legitimacy ambayo inamtambua raisi kikatiba tayari imeshavunjwa.

Na katiba hii ya sasa kama wengi tunavyoitambua ni ya kizamani na yenye muundo wa ki-totalitarian aiwezi restrain viongozi wa juu wala aiwezi wajibisha authorities kujua there limitations. In normal circumstances una washitaki, kwa kuingilia sheria isiyo wahusu au hawana uwezo wa kuizuia, mfano halisi ni suala hili hili la katiba ambayo viongozi wa CCM wanadhani wanahaki ya kuamua ni lini ibadilishwe huu si ufalme wanadhamana tu ya uongozi lakini hawawezi amua mambo ki utemi utemi tu.

Tatizo lingine labda tunazani katiba inatakiwa hiwe rigid kama vile tupo China, katiba inatakiwa hiwe flexible hili kama inapungufu challenges ziwe zinapelekwa mahakamani hili kurekebisha loopholes kama tume ya uchaguzi ambayo clearly it is a problem, si lazima kila kitu kirudi bungeni kujadiliwa kwanza. Kama kuna matatizo unaenda mahakamani na mahakama ikiona kweli kuna makosa ni sharti lazima ibadilishe. Atuwezi eti subiri kila kitu bunge liamue what is the role of the judiciary then.

Huku UK wanakitu kama judicial review ambayo wanacheck 'ultra vires' (meaning acting beyond powers) kama serikali inavyotaka kupoteza muda na hili suala la katiba. lakini kwetu (tanzania) mahakama aina independent voice at all na ni kama sehemu ya executive tu, hili ni tatizo na UK vile vile majaji wanakuwa vetted kisawa sawa kabla majina hayaja pendekezwa kujaribu kuweka watu walio politically neutral kuliko huko kwetu ambapo rahisi anaweka puppets wake tu.

Usiku mwema
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Katiba ni sheria pekee katika sheria za tanzania ambayo imetungwa kiswahili na version inayojulikana na kutambulika kisheria ni version ya Kiswahili.

Tatizo tulilonalo ni kuwa watanzania hatupendi kusoma, nakumbuka mwaka 2009 kwenye maonesho ya Sabasaba, wizara ya sheria na katiba ilikuwa na banda na walikuwa wanagawa katiba bure . Watu waliokuwa na interest ya kuchukua katiba ili waisome na kuielewa walikuwa wachache sana.

Kuna ukweli kuwa watanzania hatupendi kusoma. Swali linakuja, je tungekuwa tunapenda kusoma, tungependa kuisoma katiba ya sasa? Kitu cha kusomwa ni lazima kiwe na mvuto.

Katiba moja yenye muda mrefu hapa duniani ni katiba ya Marekani. Kitu kinachofanya waMarekani kuwa na interests na katiba yao, ni kuwa katiba hiyo inalinda uhuru wa mwananchi na vilevile inalinda madai ya uhuru. Hakuna raia wa Marekani anayekubali serikali ya Marekani iendeshwe kama serikali ya mfalme au kiongozi kuwa mfalme.

Kwa Tanzania, toka tumepata viongozi ni wafalme. Siku zote wao wanajua ni kitu gani cha kumwambia mwananchi. Una kiwanja au nyumba Kigamboni, serikali inakuja na kukwambia unatakiwa kuhama. Polisi anakukamata anakuuliza kitambulisho, wakati nchi haina sheria ya mtu kutembea na kitambulisho.

Unalazimishwa kuchangia ujenzi wa shule, wakati hakuna sheria ya kukulazimisha kutoa mchango. Hivyo hakuna umuhimu wa mtu kusoma katiba na sheria wakati wenye mamlaka ya kulinda sheria hizo ni wakiukaji wakubwa.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Aitakua na maana kuandika katiba mpya unless tuna taka kubadilisha mfumo mzima na namna ya uongozi wa sasa ulivyo Tanzania. Na ukisema uibadilishe maana yake unataka kutoka kwenye mfumo wa katiba ya sasa ambao ni 'unitary' na kwenda kwenye mfumo wa 'federal'. Hizo ndizo katiba mbili kuu duniani, kila nchi inayo badilisha imejifunza kuziba viraka vya katiba wanazotumia lakini si kuibadilisha yote.

Kenya ni nchi ambayo kwa sasa unaweza sema wamejaribu badilisha katiba karibu yote kutoka 'unitary' kwenda 'federal' na ina make sense kwa matatizo waliyonayo ya ukabila. Federal governance aims to release autonomy in a segregated society kama Kenya ambako kuna madai ya kutotendewa haki baadhi ya wanajamii au America ambayo iliundwa chini ya vita na unshared ideology (ndio mpaka leo kwingine kuna capital punishment kwingine hakuna) hivyo hiyo ndio basis ya Federal constitution kuunganisha watu lakini kuachia baadhi ya maamuzi locally. Whereby a unitary governance is much more advanced and aim to govern a society that has almost a similar ideology and values. Na ukisema tu-adapt a federal one atuendi mbele tutakuwa tunarudi nyuma as a tolerant society.

Tatizo kubwa la katiba yetu ni madaraka ya raisi na too much power of the executives, hii imeondoa nguvu ya bunge na judiciary. Ukitaka kuona ni tatizo mahakama hazina nguvu independently za kusikiliza kesi za katiba sasa where is the check in judiciary. Au mmbunge hawezi leta motion ya katiba bungeni ikajadiliwa na kupigiwa kura without the authority of the executive hili ni tatizo ambalo lina wafanya hata majambazi wajilimbikie mali kwa kuwa the parliament is weak and the judiciary is like the branch that doesnt exist and has no independent voice hili ndio tatizo kubwa kwenye katiba yetu.

JC:

Mfumo mzima wa kiutawala inabidi ubadilike. Utawala wa Central Government haufai. Ukichukua karibu nchi zote zilizoendelea kuna utawala wa majimbo japokuwa nchi hizo hazina tofauti kubwa sana za kikabila au kidini.

Kuwa na decentralized system inasaidia viongozi wa majimbo kuwa customized solutions ambazo zitakidhi mahitaji ya majimbo yao. Kwa mfano, watu wa Kilimanjaro tayari walijiendeleza katika shule za sekondari. Hivyo mpango mzima wa sekondari za kata hauna manufaa yoyote kwa mkoa huo. Lakini kwa sababu tuna mipango ya kitaifa, inabidi nchi zima ifuate mipango ya haina moja wakati kuna variations.

Hivyo masuala ya mfumo wa Federal sio lazima yawepo kujibu hoja za mgawanyiko wa kikabila au kidini tu. Utunzaji na matumizi ya resource peke yake ni sababu nzuri ya kufanya kuwepo kwa decentralization.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,067
2,000
Kaka
kama katiba ni sheria yenye principles za muongozo uoni kama mahakama ni sehemu kuu ya ku-interpret katiba na kuleta mabadiliko ya kikatiba.

Ebu niambie hizi mahakama zina nguvu gani katika taifa letu zenyewe? uoni ni tatizo si lazima kila mtu lazima ajue katiba lakini ni muhimu viongozi wa upinzani kujua pa kuanzia na kwenye kuibadilisha hii katiba. Chombo kinachotakiwa kubadilisha akina sauti ya kuikosoa the same thing they're supposed to supervice. The judiciary branch of the check ni tatizo la kwanza before anything, kwenye mabadiliko ya katiba. Serikali aiwezi sema au amua kama katiba ina makosa ni haki ya watu kitaifa kusema kama ina makosa. Na representative wa watu tayari wameshasema kuna makosa, mahakama chali aina nguvu yoyote kisheria.

JC:

Vilevile ni lazima tukubaliane kuwa mindsets za watu nazo zinachangia katika masuala ya kuelewa haki za kikatiba. Pamoja na kuwa kituvo cha sheria pale UDSM ni miongoni mwa vitivo vya mwanzo kama sio cha kwanza, ukosefu wa kutotilia maanani utawala wa kisheria umedumaza mawazo yetu.

Siku zote katika katiba ya nchi vipengere vya haki ya binadamu au raia vina uzito kuliko vipengere kumchagua rais au mbunge au vipengere vingine.

Ni haki ya mtazania kushiriki katika uchaguzi wa aina yoyote pale anapokuwa na sifa za kiraia. Kuwa mwanachama wa chama fulani sio haki ya kiraia. Hivyo kusema kuwa mgombea wa urais au ubunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa ni kukiua vipengere muhimu vya katiba.
 
George Jinasa

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
395
225
Bwana Juma mamlaka ya Mahakama kureview maamuzi ya Bunge na Serikali Kuu yameanishiwa vizuri katika Ktiba yetu tofauti na ya Uingereza. Uingereza nijuavyo mimi, Bunge likitunga sheria yoyote Mahakama haina uwezo wa kuibatilisha hata kama Bunge limekosea. Kuna execeptions chache sana katika kanuni hii. Hiyo ni kwa sababu Uingereza kuna kitu kinaitwa Parliamentary Sovereininty (utawala wa Bunge).

Tanzania kinadhalia tuna utawala wa Katiba. Wakati Uingereza Bunge liko juu ya Mahakama na Serikali Kuu pamoja na sheria yenyewe, Tanzania Katiba ipo juu ya Bunge, Mahakama na Serikali Kuu. Baina ya Mahakama, Bunge na Serikali Kuu kuna checks and balance. Kwamba Mahakama kwa mfano, kwa njia ya Judicial Review, inauwezo wa kutamka kwamba sheria fulani ya Bunge ni haramu kwa kukinzana na Katiba. Kwani uhalali wa sheria yoyote Tanzania unapimwa na Katiba. Kwamba sheria yoyote ni haramu kama inapingana na Katiba. Tatizo hapa ni kama Katiba inakinzana yenyewe kwa yenyewe kama ilivyokuwa katika kesi ya Mgombea binafsi. Tatizo hili linakuwa tatizo kwa kuwa Katiba ipo juu ya Mahakama na ni mzazi wa Mahakama. Lakini nani mzazi wa Katiba? Ni watu wenyewe. Hao ndio wanaweza kuiondoa au kuibakisha kama hawaitaki au wanaitaka. Tatizo lingine lililopo ni kwamba mamlaka ya kubadilisha katika Tanzania yamewekwa katika Bunge ambalo likifanya kazi ya kurekebisha Katiba linakuwa sio Bunge la kawaida bali Bunge la Katiba (Constituetent Assemble). Marekebisho ya katiba yanapopitia hatua zote yanakuwa ni sehemu ya Katiba ile ile iliyo juu ya Mahakama, Bunge na Serikali kuu.
 
George Jinasa

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
395
225
Ndugu yangu JC kwamba ni haki ya kila mtanzania raia kupiga kura, nakubali. Issue hapa ni nini chimbuko la haki hiyo? Kwa maoni yangu chimbuko la haki hiyo linapaswa kuwa katiba na sheria za nchi. Mtu anaweza kuuliza kama kila raia mtu mzima ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa na mtu mzima ni yule aliyejaaliwa miaka kumi na nane na kuendelea iweje haki ya kugombea uraisi imuangukie yule aliyejaaliwa miaka 40 na zaidi na sio kuanzia miaka 18? Jibu la haraka ni kwamba kwakuwa wananchi wenyewe waliamua hivyo katika katiba yao. Kama jibu hilo ni sahihi, haiwezekani kuwa sharti la kuwa mwanachama wa chama cha siasa nalo likawa na jibu hilo hilo. Kama Katiba ingekuwa imetamka kwamba mgombea binafsi ni ruhusa kungekuwa na tatizo?

Kwa maoni yangu maadamu kifungu cha kutaka mgombea uraisi na ubunge kuwa mwanachama wa chama cha siasa kitabaki kwenye Katiba, hapatakuwa na uvunjaji wowote wa haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwani wananchi wana uwezo wa kuweka masharti yoyote ya kutumia haki zao kwa njia ya Katiba. Tatizo mimi ninaloliona ni ushirikishwaji wa watu katika uandikaji wa katiba. Niliwahi kutoa maoni huko nyuma kwamba vipengele mhimu kama vile vinavyogusa haki za binaadamu visirekebishwa bila kupata ridhaa ya wananchi. Kama hili litakuwepo katika Katiba wananchi wenyewe wanaweza kuamua kama masharti hayo yanafaa au la. Kwa sasa hivi tuna ushahidi gani kama wananchi wengi wanataka mgombea binafsi? Au kwa kuwa kuna baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama fulani waliwahi kusema? Lakini wapo watanzania wengi pia wanapinga mgombea binafsi. Yawezekana maoni ya Mchungaji Mtikila na wengine kwamba tunataka kuwepo mgombea binafsi ni maoni yao binafsi na watu wanaowaunga mkono bali watu wengi hawapendi mgombea binafsi. Ikiwa hivyo ndio ndivyo tutasema suala la mgombea binafsi linavunja haki za msingi zilizowekwa na kutakiwa na nani?

Watanzania tunatatizo kubwa la elimu ya sheria na uraia ambalo linatokana na ukweli kwamba wakati wa utawala wa chama kimoja elimu hiyo ilikuwa kwa watu maalumu. Ni kutokana na tatizo hilo kwamba wasomi wengi tumejivalisha sauti ya wananchi bila kuwa na ushahidi wa ridhaa yao. Mtu atasema wananchi wanataka mgombea binafsi wakati hana ushahidi kwamba japo hata asilimia kumi ya watanzania wanamuunga mkono. Tuwaelimishe zaidi wananchi uraia, sheria na katiba ili wapate uwezo wa kuamua.
 
Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,812
2,000
Kaka Zakumi,

Amna katiba inayokataza local society's efforts kama zinaleta nguvu au zinaendana na namna yao ya kimaisha ndio maana hata katiba yetu inasema freedom of choosing a religion and guidance popote ulipo ndani ya mipaka. Hivyo mjomba hata ukitaka kubadili kabila kazi kwako mababu tu wakutambue. Tofauti kubwa ya federal govs, si kwamba decentralization bali its the manner with which a nation was formed. Mfano American history inatuambia sababu kubwa ya states kuanza ku-join forces zama hizo, ilikuwa ni kupambana na mwingereza na tax zake za ajabu ajabu kama stamp duty ambazo waliona hazipo fair.

Jamaa walishachoka hila wakajua mmoja mmoja hawawezi mpiga hivyo ilikuwa ni lazima kuunda a state federation. Kwa kuwa umuhimu wa kujiunga ulikuwa kupata nguvu na sauti ya pamoja hili kupambana na adui, mwisho wa siku kila state ilipenda kubaki na values zake na some local autonomy. Hiyo ndio misingi ya Federal constitution na mpaka inakuja american civil war wasiotaka ilibidi waunganishwe kwa lazima. Ndio mpaka leo American state despite the central gov, each states has its own constitution hii ni kutokana na historia na namna katiba yao ilivyotungwa based on the context of the era.

Na misingi hiyo ndio imekuwa 'bench mark' ya katiba za nchi ambazo zina different ethnicity, religious, values and ideologies hili sehemu zilizokuwa na popular ideology ziweze kuwa na autonomy zao.

Kama tanzania leo ingekuwa ni nchi ya federal Zanzibar wangekuwa na sauti au uwezo wa kutunga katiba yao na kufuata hiyo mahakama ya kadhi. Lakini under a unitary constitution unakuwa na freedom yako lakini lazima huwe in toe with the regulation of the whole nation and no group should receive special treatments.

Suala la maendeleo ya taifa tatizo si kwa sababu ya kuwa na central governments, it is much to do with political naivity. Kama kuna ardhi yenye rutuba nzuri na serikali inaamua kulima, hivyo watakao pata ajira ni local people. Hila kama local people awaoni umuhimu wa kulima serikali aina budi zaidi ya kui-encourage immigration hili shamba lilimwe.

Tatizo kubwa si central gov, bali politicians (wabunge) wasiojua kuchambua policies, kwa sababu hata ukisema watu wajiendeshe wenyewe locally, still the right policies ought to be formulated. Mfano look at this policy Serikali ina mmpango gani kuhusu matatizo ya elimu Tanzania?

Mimi na wewe hapa tukisema tulumbane tutakuwa wenda wazimu kwa serikali isiyo toa policies zake hadharani au kutujuza matumizi yake katika kufikia lengo hilo. Hili ni suala la wabunge kujua kwa nini elimu hipo chini, matumizi ya budget yanatumikaje, hela inapotea wapi, au inaibiwa wapi, kiasi gani cha intended sums kinawafikia the intended institutes. Au upinzani na wao watoe mapendekezo yao based on a realistic budget au spending priorities zao based on the budget. Mwisho wa siku wapiga kura wajue alternatives zilizopo na wapige kura ki maslahi zaidi kuliko party loyalty.

Pili ukitaka kujua wabunge ni useless, wewe lini umeona mmbunge kuja hadharani na kukemea policy fulani ambayo kwake aifaidiki au aiwafikii watu wake even on something as universal as education or medical needs. Kuna watu wanatembea kilometa kadhaa kwenda kujifungua tu kwa kuwa amna clinic karibu wala usafiri wa kuwapelekesha huko. Wakati mmbunge huyo huyo anatembea na VX ya sh million280 kwa mujibu wao. If a representative can not scrutinize on obvious wasteful spending based on simple needs how do you expect him to fight policies that causes inflation, taxation policies, production or even national priorities.

Kwa maana hiyo tatizo sio central gov bali ni weak reps, kama sehemu ina maliasili obvious jamii ya hapo itafaidika kwanza kwa namna ya employment na faida inatakiwa kuwa shared nationally through investments either on health, education or economic production based on a plan. Hiyo ndio principles behind unitary na local gov has a role to play in supervising and monitoring local assets, hila vitu vinafanywa kwa manufaa ya taifa si kwa watu.

Kuna siku niliwahi kuuliza kuna watu wanalalamika tunaagizia samaki, wavuvi wanalalamika jamaa wanaua biashara na kupunguza idadi ya wavuvi wadogo wadogo. Ni lini umeona mmbunge wa sehemu usika kasema si sawa hawa samaki wa kuagiza wanaua local economy ambapo samaki wanapatikana. Haya si matatizo ya central gov entirely but rather poor politicians.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom