Barua kutoka Ughaibuni - Kura za Maoni na Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua kutoka Ughaibuni - Kura za Maoni na Uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zakumi, Oct 11, 2010.

 1. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Salaam Ndugu zanguni:

  Ama baada ya salaam ningependa kuwatakia heri na pilikapilika za uchaguzi. Pamoja na hayo ni lazima tuendelee kupanuana mawazo na kuacha kuchukulia siasa kama ushabiki wa Simba na Yanga.

  Nimefuatilia kura za maoni zinazoendelea sasa. Na kwa kifupi tu, msije kupata ugonjwa wa moyo siku ya uchaguzi pale matokeo yatakapotoka kwa sababu kura nyingi za maoni zinazofanyika sasa sio za kisayansi. Na hizi ni sababu ninazotoa.

  1. Kura za maoni zina maana yake na tafsiri zake. Hivyo maswali yanayoulizwa na watu wanaoulizwa ni kitu muhimu.
  2. Kuna kura za maoni za kuhamasisha watu kupiga kura na zinatumika wapiga kampeni. Hivyo swali linaweza kuulizwa je kati ya JK na Dr. Slaa unampenda nani? Hili swali ni tofauti na kwenye siku ya uchaguzi utampigia kura nani? Na vilevile ni tofauti na nani anafaa kuwa rais.
  3. Watu wanaoullizwa maswali nao ni muhimu. Hili kura ya maoni iwe na maana basi wale watu watakaopiga kura siku ya uchaguzi watoe maoni yao. Mtanzania aliyopo Marekani anaweza kuwa-influenced na uchaguzi wa Obama na kutaka mabadiliko. Wakati watanzania waliopo sehemu mbalimbali Tanzania wana mitazamo tofauti.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red hata mimi nimekuwa na hofu kama hiyo.
   
 3. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Kama taasisi za kufanya tafiti na kura za maoni zinafanya kama zinavyotueleza, then tuna safari ndefu gizani mbele.
  Watanzania tujitahidi kutumia elimu zetu kufanya mambo kihalisia zaidi, sampling methods, size etc. za matokeo yaliyotangazwa na taasisi hizo zinatia shaka 100%!
   
 4. monge

  monge Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 10, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napata shida sana ku-analyze akili za hawa wasomi wetu wa kitanzania! Hivi inakuwaje wasomi wa
  kiwango hicho na wanaoishi katika hii dunia inayobadilika kwa kasi namna hii wanakubali kutumiwa na
  wanasiasa uchwara wa kibongo pasi na hofu ya kudhalilisha elimu walizotumia muda mwingi mashuleni kuzitafuta.! Wakati umefika sisi watanzania tuache mambo ya kijinga kijinga na tuanze kukimbizana na
  mambo ambayo yanafaida kwa jamii na kizazi chetu kijacho.  Monge omunyabhikerya.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,957
  Likes Received: 420,622
  Trophy Points: 280
  Vigezo hivi vyathibitisha ya kuwa SYNOVATE na REDET ni wababaishaji tu na wala siyo vinginevyo
   
 6. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 80
  CCm full kutapatapa.... Hukumu yao ni 31/10/2010......
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Lebabu11:

  Kama nilivyodokeza kura za maoni zina maana yake. Hata hapa Marekani Pollsters wanatumika ku-influence matokeo ya uchaguzi. Na hata hapa JF watu wanatumia polls ku-influence matokeo.

  Kuna mtu hapa alikwenda kwenye msiba. Ubishi ukatokea msibani kuhusu uchaguzi na Dr. Slaa akapita. Kilichotolewa hapa ni asilimia za matokeo. Lakini hazikutolewa idadi za wapiga kura.

  Kwenye mila zetu, kwenye msiba wanawake na wanaume wanakaa tofauti. Hivyo kuna uwezekano mkubwa ni vijana wa kiume waliotoa maoni yao. Wakati wapigaji kura wengi ni wanawake.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  Good to see you back in JF. It has been long. I thought by now you would have new sandals, no?:tonguez:
   
 9. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180

  Unafanya makosa makubwa unaposema kuwa wanasiasa wa bongo ni uchwara. Wengi wao ni educated na wanavyo-vipaji. Matatizo yaliopo ni kuwa wanashindwa kutumia vipaji na elimu yao kwa manufaa ya nchi ( Realization of potential).
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Si ndio uchwara wenyewe mkuu?
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Jasusi:

  Kwikwikwi.

  I am not looking for new scandals, but will try to write a manifesto for 2015. This manifesto will be in a satirical format. The goal is to recapture our identity and spirit.
  Anyway, next year, the nation will celebrate 50 years of mainland independency. This is a milestone. But, I am not sure if we are better off today than we were 50 years ago. Today, we can claim a number of achievements such as schools, hospitals, roads etc; however, without international handouts we cannot sustain our live style.  On the other hand, our grand-mothers and grand-fathers did not have all of those fancy things we have today; nonetheless, their systems were complete and sustainable.  So SUSTAINABILITY is my new thing.
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Metaphorically, I am with you. They are Wacharwa.
   
Loading...