Barua: Kutoka kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi kwenda kwa Rais wa JMT

So sad........................!
I love my teachers, but I'm afraid of your pay.
 
Maisha ni magumu kila mahali hata huku mtaani pia, afadhali ya wewe mwalim ambaye unapata mshahara. Kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kufikiria hata biashara ndogo ya kukupatia kipato mbadala tofauti na mshahara. Hata wanaolipwa milioni kumi kwa mwezi haziwatoshi nao wanataka waongezewe. Don over spend, don misuse...be economical

Economical zaid ya hivo alivoelezea hapo?mkuu tafadhali usi-tuudhi hapa,rasilimali ngapi za nchi hii zinatumika hovyo?unajua thaman ya roho zenu ninyi ni sawa tu na ya roho zetu?kutuambia habari za million 10 hazitoshi je wataka kuturingishia mnacholipana?tunafahamu hayo yote,ila tunaomba mtuonee huruma na sie watoto wetu waende chooni!tunajua hatuwez kula na kuendesha mnavoendesha bt tuoneeni huruma mtupe haki zetu.
Au mnafikiri mtaishi milele?kumbukeni all great leaders na matajiri wa dunia hii waliokwisha kufa,je walikufa tofauti na maskin wanaokufa?waliondoka na mali zao?jamani tendeeni watu haki,maana hata mkiringa siku moja wote tutakufa,na tutarudi mavumbini wote bila ubaguzi!hakuna atakayezikwa mawinguni!
In short alichoeleza huyo mwalimu kimenigusa sana,na wewe unachojibu ni kuwa umeshiba hujui wenye njaa!
 
Sasa wewe mbona
unaishi kwa kujipendekeza kwa akina Napelwa pale Lumumba na wanakutuma
tuma kutpost utumbo huku ili upate shs 5000 kwa siku za kuendesha
maisha. Huoni mwenzako anafanya kazi za mikono yake na kuishi vizuri.

Boss wako Mwigulu aliiba mke wa kada mwenzio pale Igunga saa saba za
mchana kweupee, na wewe angalia vizuri ndoa yako maana hicho chama chenu
kuaminiana kuko chini sana

kwenye historia ya kupora wake za watu ni chadema. ona baba lenu halina hata haibu. limeukuzwa upadre kwa tamaa za kimwili. likaoa likatelekeza familia. kana kwamba haitoshi likapora mke wa mtu. looo aibu!
 
Mi namsaport huyo mwl sana tuko nyuma yake na mbaya zaid utake kujiendeleza mikwara kibao wakiona wameshindwa utasikia kajisomeshe ukikubali unaambiwa walimu wachache, jaman serikal mnataka nini? Hamtak sekta ya elimu iwe na walimu? Kama hamtak bas achen kuajir na mpunguze manyanyaso hao mnaowaita wachache. Tunataka taifa la wasomi na taifa lenye watu wanaoogopa kudai haki zao na tusimamie sheria tunazotunga sisi wenyewe
 
baada ya kusoma hoja
zako, nmemtafuta ticha aliyenipa hii barua na kumuuliza, majib yake ni
kama ifuatavyo:
"hapa Dar sina ndugu, kama yupo bac hatufahamian, nlihitim kitado cha
nne mwaka 2010, matokeo yang n division IV ya point 26 kama
Civ- C, Hist- C, Kisw-B, Eng-D, Geo-D, Bio-F na Math-F= kwa kuwa ckuweza
kusomeshwa private nlienda kusomea ualimu ila kwa sasa nmeanza kusoma
masomo ya advance pale Aman centre na mwakan Mungu akipenda natarajia
kufanya mitihan ya form six.
wazaz wang wapo Mbeya na hata leo asubh nmeongea nao anayesema
nimewatosa wazaz wang ana lake jambo, hata kwa bahati mbaya siwezi
kuwatosa wazazi wangu.
kukopa n kweli nlikopa NMB lakin sio million 10, nlikopa million moja,
nkanunua shamba (Mbozi) laki 5, familia nliipa laki 2 (baba na mama laki
1 na nusu, mdogo wang elf 50) lengo n kwamba waanzishe biashara ili
wapungze utegemezi kwang. kiaskilichobaki nlitumia kukipendezesha chumba
chang, naamn watu wanajua n kiasi gani cha pesa walim tunapewa kwa ajil
ya kuanza maisha.

mkuu, utetezi wako ni dhaifu sana . sina hakika kama ulichoandika kimetoka kwa mhusika. umekuwa too general. hujasema mbozi kijiji gani wazazi wake wanaishi, hujasema amemaliza shule gani kidato cha nne. mambo chungu nzima ambayo ni ya kusadikika. mie naujua ukweli wake na wala sina shaka katika hilo. kajipange upya
 
Kama mshahara wa mwalimu ni huu kwa mwezi na nikifananisha na mishahara ya wabunge, ukweli sina la kuchangia.
Hiyo sio take home, ni basic salary, bado kuna makato mbalimbali kama kodi, NSSF, sijui nini, n.k, kinachobaki hapo ndio mwalimu anachukua.
 
anayajua yote haya yaani aache kusafiri awaze wewe mshahra wako haukutoshi wakatai anasema anaenda kuomba msaada
 
Hata waongeze mishahara kwa 100% bado hali itaendelea kuwa ngumu endapo mfumuko wa bei hautadhibitiwa. Kinachotakiwa hapa ni kubadili utawala ili tupate mawazo mbadala kwani ccm wamefika mwisho wao wa kufikiri hawana tena ubunifu. Sasa wanawaza usiku na mchana namna ya kuiua cdm badala ya kuwaza namna ya kuondoa kero za wananchi ikiwemo shida ya maji, umeme, miundombinu mibovu, kufa kwa elimu, kushamiri kwa udini, ufisadi, rushwa, nk. Mungu ihurumie tanzania.
 
Nikilinganisha uwezo wa walimu wa primary, ni dhahiri uwasilishaji huu wa maelezo umefanywa na mwalimu halisi kama alivyojitambulisha. Ila nimecheka sana namna alivyotoa maelezo yake na NIMEHUZUNIKA sana namna alivyowasilisha dhima yake. Huyu mwalimu amesema chai asubuhi 200/ unadhani ni chai ya namna gani hii?

Kila kitu ameweka katika lowest estimates lakini huo mshahara wake hautoshi maskini. Kwa kifupi Rais wa Nchi hii ambaye watu kama huyu waliowasilisha mawazo kama haya walisimama (wengine) masaa 10 ili wakupigie kura jukumu lako la kwanza ilikuwa kuondoa class hii kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Kwa sisi ambao tunajua thamani ya rasilimali zinazopatikana tanzania, tunajua kuwa ni uzembe na wizi tu unaosababisha class hili kuendelea kuwepo hapa tz, na kwa minajili hiyo Huenda PEPO ya Mungu hautainusa.

Ndiyo, dini inasema ukijiona si muadilifu usitake uongozi kwani utakupeleka motoni na ukijiona muadilifu watu watakuomba uwe kiongozi na utakupeleka peponi-I hope kwa lugha niliyotumia hapa ina-match na ya mwalimu wangu Mwambije

Ndiyo maana tunasema watu wanaishi kiujanja-ujanja. Hiyo bajeti haitekelezeki. Ni lazima shule itafute hela ya mlinzi, mitihani, choo, usafi nk ili walau waweze kugawana kidogo. Mnakumbuka wale walimu waliokuwa wanawapa adhabu wanafunzi ya sh.500? Ni kwa sababu ya bajeti ya namna hii. Something should be done to alleviate the problem.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Naamin ujumbe umefika.....ila duh nilikuwa na mpng wa kusomea ualim,naanza kukata tamaa

usikate tamaa mkuu,wanetu watafundishwa na nani,halafu kakaa,uchaguzi ukifika nyie walimu ndo wanaoipitisha ccm,wakija huku wanajifanya wana machuuungu,mshahara mdogo kweli ila mbona promo kwa ccm ni kama kazi na dawa?
 
Maisha ni magumu kila mahali hata huku mtaani pia, afadhali ya wewe mwalim ambaye unapata mshahara. Kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kufikiria hata biashara ndogo ya kukupatia kipato mbadala tofauti na mshahara. Hata wanaolipwa milioni kumi kwa mwezi haziwatoshi nao wanataka waongezewe. Don over spend, don misuse...be economical

no bidii kazini if there is no motivation and recognition for what you are calling kufanya kazi kwa bidii. in this country kuna sehemu ambazo hujafika wewe. mwalimu anakaa zaidi ya wiki bila kuoga wala kunywa maji. hapo kuna kufanya kazi kwa bidii? serikali inashindwa tu hata kujenga matank ili maji ya mvua yasipotee angalau hata walimu wapate maji. wewe unachofanya ni kama kumkuta mtu kafiwa then unampatia pole na kumwambia kuwa ni mambo ya kawaida na inatokea tu kwa kuwa msiba si wako.
 
MKUU, kumbe lengo la hiyo barua ni kujenga hoja ya jumla kwa walimu wote? ila kumbuka hiyo barua ni personal na wala si ya kikazi. kajieleza yeye na si walimu wote. ukiangalia kwa makini matumizi yake utagundua kuwa hayana uhalisia kama nilivyofafanua hapo juu. pia nimeeleza kuwa huyu mwalimu namfaham na hastahili kuwa mwalimu kama serikali itaamua kubana na kufuata haki. hastahili pia kudai kitu ambacho hastahili kukipata. huyu ni miongoni mwa watu waliokimbilia ajira ya ualimu baada ya kufanya vibaya kwenye mtihani wa form four. ni kielelezo kiigizo kibaya cha fani ya ualimu.

Khaa, kuna watanzania wana vichwa vibovu hivi halafu wamepenya hawa leo wachambuzi; kwa akili yako hiyo barua ambayo ni personal ikitokea Mhe. Rais aifanyie kazi kwa kuongeza mshahara, unadhani ataongeza personal kwa mwalimu huyu tu? Nikukumbushe tu kama ulipita O'level katika kiswahili na English kuna uchambuzi wa vitabu, vile vitabu vimeandikwa in-persnal life, lakini reflection yake ni ya kijamii. Kuhusu maisha yake binafsi lete thread nyinggine inayohusu maisha yake lakini kuhusu hili, yuko sahihi kijana wa watu. Ujinga nyie watu mlioko huko govt kudharau tatizo/kauli/action hata kama itakuwa na chembe ya "sisimizi".
 
Mishahara ya walimu na watumishi wa umma kwa ujumla inapanda katika bajeti inayoendelea dodoma
Wewe kwa akili zako unadhani serikali itaongeza zaidi ya 20,000/-Tanzania hii ys ccm sio ya kufanya maajabu hata siku moja,, nauli zimepanda maisha yamepanda watakachoongeza utacheka mwenyewe, utarudi hapa kuniambia
 
kwenye historia ya kupora wake za watu ni chadema. ona baba lenu halina hata haibu. limeukuzwa upadre kwa tamaa za kimwili. likaoa likatelekeza familia. kana kwamba haitoshi likapora mke wa mtu. looo aibu!
Haya inatosha turudi kwenye mada.
 
Mi ni mwalimu wa daraja 3a.nafundisha kijijini.wakuu maisha ya ualimu ni magumu kuliko watu wanavyo chukulia.sishauri mwanao/ndugu yako awe mwalimu.naunga mkono kwa mtoa hoja ya mwl mwambije
 
Naamini hiyo ndo hali ya maisha wanayoishi walimu wengi hapa nchini.Walimu wanaishi maisha duni sana, makazi yao ya hovyo, wengi wao wako mbali na huduma za kijamii, licha ya kwamba wanafanya kazi kubwa na ngumu lakini nchi hii imeamua kwa makusudi kuwatelekeza na kuwasahau wao na sekta nzima ya elimu.Hii nchi ya kipumbavu kabisa, pamoja na namna wanavyowa treat walimu wa nchi hii bado wanategemea miujiza kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa....!HUYO MWALIMU HAPO BADO HAJAWEKA FEDHA ZA NAULI KWENDA KUUFUATA HUO MSHAHARA WENYEWE. Wapo walimu na watumishi wengine wanaosafiri zaidi ya kilomita 100, kufuata mshahara, tena inampasa kuanza safari saa 10 usiku, na analipa nauli zaidi ya shilingi 10000/kwa safari.KUNA HAJA YA KUSIMAMA NA WALIMU KATIKA KUDAI MASLAHI NA HALI BORA ZA MAISHA ILI HATIMAYE WAWEZE KUTUFUNDISHIA WATOTO WETU VEMA.
mkoa wa ruvuma wilaya ya mbinga kuna shule za msingi ziitwazo dar pori,lunyere,mpepo na mitomoni ziko zaidi ya km 190 toka makao makuu ya wilaya na nauli ni sh50,000.00 kwenda na kurudi.na ukifika mbinga ambapo ni mji lazima ukae kuanzia siku 3
 
Back
Top Bottom