Barua: Kutoka kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi kwenda kwa Rais wa JMT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua: Kutoka kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi kwenda kwa Rais wa JMT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ndugu yako, Apr 11, 2013.

 1. ndugu yako

  ndugu yako Senior Member

  #1
  Apr 11, 2013
  Joined: Mar 30, 2013
  Messages: 195
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Japo barua imechelewa kufika hapa takribani wiki mbili lakini hakijaharibika kitu, mwalim huyu anaomba yeyote atakayeweza amsaidie kuifikisha hii barua katika meza ya mheshimiwa rais na itakuwa vizuri zaidi kama rais atakabidhiwa hii barua mkononi mwake!


  BARUA YANGU KWA RAIS
  (Serious).
  Habari yako mheshimiwa Rais? Kwanza kabisa heshima yako, shikamoo na Pole sana na kazi za kulitumikia Taifa letu.
  Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi Matakapola, iliopo Ilala hapa Dar.

  Haina aja ya utambulisho sana, naomba niende kwenye dhumuni la hii barua. (Ila ombi, naomba hii barua usome wewe mwenyewe Rais, kama kuna servant anakusomeaga, aishie hapa. Aiweke store siku ukiwa na muda wa ziada wewe ndio isome taratibu. Tafadhali sana).

  Ijumaa iliopita mshahara wangu uliingia kwenye account yangu. Asante sana ingawa ni jasho langu.

  Basi yafuatayo ni matumizi yangu yangu tokea Ijumaa hadi leo:

  1. Kodi ya chumba (miezi 3)- Tsh 60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya umeme Tsh. 5,000

  2. Chakula cha akiba kwa huu mwezi (Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage 5kg, Mafuta 2lts)-Tsh 42,000.

  3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vitu vidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni kama majani ya chai, chumvi, mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,000

  4. Mwalimu usafi, imebidi nipitie mitumbani (huku ni sehemu unakoweza pata kitu cha bei kubwa kwa bei nafuu) nipate nguo za kubadilisha, maana hizi wanafunzi wamenizoea nazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000 na nkazipeleka kwa fundi kuzirekebisha (Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani ni kawaida kua oversize, ombea isiwe undersize, na ukishanunua hakuna guarantee wala kurudisha) hapa nkatumia tena Tsh 5,000.
  Pia nikaenda duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5000), Mafuta ya BabyCare (Tsh.1000).

  5. Wazazi wangu wameteseka sana kunisomesha, hivyo fadhila muhimu kuwarudishia kwa hiki hiki kidogo nipatacho.
  Nika wa M-Pesa Tsh.40,000 ili watumie kubadilisha mboga juma pili na nusu iwasaidie kumalizia ada ya mdogo wangu Riziki, yupo ile shule uliokuja izindua mwaka 2011/May/13 kijijini kwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi, sidhani kama unakumbuka, maana ulituhaidi visima, barabara, madawati shuleni na kujenga bweni la wasichana, ila hadi leo umetuachia manyoya. Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati la drafti drafti jeupe. Na ulikuja na mama, yeye alivaa full vitenge vya chama! Kumbuka?)

  6. Kuna hela ya nauli kwenda na kurudi kila siku shuleni (Tsh.600 per day), vitafunwa asubuhi kila siku (Tsh.200 per day), na vitu visivyo nunulika kwa wingi, maana vitaharibika kama vitunguu, sabuni, nyanya, nazi,karoti, etc nakadilia Tsh.10,000 kwa mwezi.

  7. Mheshimiwa kuna vitu havizuiliki kama vocha, nyama wakija wageni, kwenda hospitali, bado kutoka out mara moja moja (Yaani kama wewe unavoendaga Sydney kula mbuzi, na sisi tunaendaga kwa mama Lucy sinza, kula vifaranga).

  8. Kuna Hiyo pesa tunaiita hela ya emergence kama michago ya mtaani, sadaka, misiba, kiatu/nguo kwa fundi...etc

  Mheshimiwa kama ulisoma vizuri hesabu kama mimi, roughly hapo ni jumla kama Tsh.210,000 nikiongeza na pesa ya hitaji no.7&8 jumla kama Tsh.250,000.

  Mheshimiwa kutaja mshahara wangu hapa si vizuri, lakini kwakua mama hapo nyumbani ameshawahi kua mwalimu naomba nikusumbue, ebu muulize walimu grade A, tunaoanza kazi tunalipwaje?

  Kumbuka hapa bado niko peke yangu (Single Boy), sina ata mpenzi. Hivi nna ndoto za kuoa kweli ukitizama iko kipato? Nikiwa na mtoto je? Akianza kusoma je?

  Nawaza sijui nikakope NMB au FINCA au VICOBA sijui Bay Port au SACCOS?

  Yaani sijielewi. Sikushawishi uniongeze mshahara, ninachoomba tu, fananisha kazi yangu na hiyo wanayofanya wabunge "wako" niliowachagua, au ata kazi unayofanya wewe. Ndio, Wewe Mheshimiwa!

  Kuna watu wananishauri nianzishe tuition, lakini mimi ni mzalendo wa pili baada ya Nyerere, itakuaje watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this is not fair (Sijui kama umeshawahi waza ili Mh.)

  Wengine wamesema nianzishe biashara. Sijui hata pa kupata mtaji, pili sio vizuri maana ntaelekeza nguvu nyingi kwenye biashara kuliko kazi ya kuelimisha ili Taifa, narudia tena mm Mzalendo.

  Hawa waliosema niache kazi wapotezee (achana nao).

  Ok Mh, naomba nisiongee sana maana unakazi, safari na mambo mengi sana. Nisikuchoshe.

  Natumaini ombi langu (Kama umesahau la kuweka hapo matumizi yako ya mshahara) litasikilizwa na kufanyiwa kazi.

  Wako katika kujenga, kuelimisha na kuandaa Taifa lijalo
  Mwl. G.C. Mwambije
   
 2. k

  kikoito Member

  #2
  Apr 11, 2013
  Joined: Apr 10, 2013
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dah its pain
   
 3. k

  kikoito Member

  #3
  Apr 11, 2013
  Joined: Apr 10, 2013
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inaumiza kiukweli
   
 4. C

  COPPER JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2013
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 1,572
  Likes Received: 267
  Trophy Points: 180
  Pole Mwalimu Mwambije, bila shaka ujumbe utafika.
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2013
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,041
  Likes Received: 674
  Trophy Points: 280
  Mh,
  Mwambije anawaakilisha maelfu ya waalimu, ni dhahiri tuuendako kama hakuna mabadiliko sioni kama kuna usalama!
   
 6. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2013
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nikilinganisha uwezo wa walimu wa primary, ni dhahiri uwasilishaji huu wa maelezo umefanywa na mwalimu halisi kama alivyojitambulisha. Ila nimecheka sana namna alivyotoa maelezo yake na NIMEHUZUNIKA sana namna alivyowasilisha dhima yake. Huyu mwalimu amesema chai asubuhi 200/ unadhani ni chai ya namna gani hii?

  Kila kitu ameweka katika lowest estimates lakini huo mshahara wake hautoshi maskini. Kwa kifupi Rais wa Nchi hii ambaye watu kama huyu waliowasilisha mawazo kama haya walisimama (wengine) masaa 10 ili wakupigie kura jukumu lako la kwanza ilikuwa kuondoa class hii kwa kutumia rasilimali zilizopo.

  Kwa sisi ambao tunajua thamani ya rasilimali zinazopatikana tanzania, tunajua kuwa ni uzembe na wizi tu unaosababisha class hili kuendelea kuwepo hapa tz, na kwa minajili hiyo Huenda PEPO ya Mungu hautainusa.

  Ndiyo, dini inasema ukijiona si muadilifu usitake uongozi kwani utakupeleka motoni na ukijiona muadilifu watu watakuomba uwe kiongozi na utakupeleka peponi-I hope kwa lugha niliyotumia hapa ina-match na ya mwalimu wangu Mwambije
   
 7. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Hakika maoni yangu tofauti kidogo kwa kuwa ametaja Shule aliko na jina lake hilo hapo Mwl G C Mwambije, msije shangaa mkakuta ameokotwa Mabwepande akiwa hana meno wala kucha.
   
 8. k

  kigoda JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2013
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 1,784
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Umeona eeh! Maana hii serikali ya CCM ikiambiwa ukweli tu WANA KUULIMBOKA
   
 9. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,044
  Likes Received: 1,512
  Trophy Points: 280
  Mishahara ya walimu na watumishi wa umma kwa ujumla inapanda katika bajeti inayoendelea dodoma
   
 10. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,044
  Likes Received: 1,512
  Trophy Points: 280
  Serikali imeahidi kupandisha mishahara ya walimu katika bajeti ya mwaka huu..kutakuwa na ongezeko kubwa sana tuvumilie kidogo
   
 11. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2013
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 14,392
  Likes Received: 2,537
  Trophy Points: 280
  Mliambiwa hataki kura zenu bado mkajipendekeza.
   
 12. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,044
  Likes Received: 1,512
  Trophy Points: 280
  Maisha ni magumu kila mahali hata huku mtaani pia, afadhali ya wewe mwalim ambaye unapata mshahara. Kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kufikiria hata biashara ndogo ya kukupatia kipato mbadala tofauti na mshahara. Hata wanaolipwa milioni kumi kwa mwezi haziwatoshi nao wanataka waongezewe. Don over spend, don misuse...be economical
   
 13. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2013
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 20,950
  Likes Received: 12,829
  Trophy Points: 280
  Unamtaka mwalimu asi-over spend, em rejea kwenye expenditure yake useme wapi ana over spent, nyie wenzetu mna rushwa mbalimbali, mnabajeti za kungoa watu kucha bila ganzi, hatulingani
   
 14. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2013
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 20,950
  Likes Received: 12,829
  Trophy Points: 280
  Bila shaka Mwl. Mwambije anahitaji ulinzi wa nguvu sana dhidi ya Chama, anaweza kumfanyia kitu mbaya
   
 15. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,044
  Likes Received: 1,512
  Trophy Points: 280
  tumia kichwa kufikiri pia sio kufuga nywele peke yake
   
 16. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2013
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,420
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Huu ni uvivu wa kufikiri, kutoa maoni ya jumla jumla kuwa maisha magumu bila kuweka data ili kupingana na aliyesema maisha magumu kwa data unajivua nguo tu mkuu. Huyu jamaa ameonesha anafanya kazi kwa bidii na hataki ubabaishaji kama tution, anatamani biashara lakini mtaji na muda wa kufanya biashara ni kikwazo...

  Nilitegemea Mtanzania mwenzie umuunge mkono kwa kumuombea kwa Mh Rais angalau awafikirie kwa nyongeza ya asilimia 300 ili walimu nao wajione watu kama watu wengine.
  Suala la mshahara wa milioni kumi kutotosha litolee ufafanuzi kwa kutupa mchanganuo hazitoshi vipi, hapo tutajua na wewe ni Great Thinker

  All in All Big up kwa walimu wote Tanzania kwa uvumilivu wenu, nchi hii ni yetu sote na adui yetu ni mmoja tu, naye ni CCM
   
 17. Baraka Roman

  Baraka Roman JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 16, 2013
  Messages: 694
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa hali hii kwel kazi ni wito

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 18. muhandu

  muhandu JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2013
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi bado ualimu ni wito au ni kazi kama kazi zingine?
   
 19. MANI

  MANI Platinum Member

  #19
  Apr 11, 2013
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,296
  Likes Received: 1,684
  Trophy Points: 280
  Mpwa Elli njoo huku uone mateso ya walimu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. P

  Paul Erasto Member

  #20
  Apr 11, 2013
  Joined: Apr 8, 2013
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamin ujumbe umefika.....ila duh nilikuwa na mpng wa kusomea ualim,naanza kukata tamaa
   
Loading...