Barua inayowatesa Mangula na Membe hii hapa!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Kabla ya Mangula kuitwa na mtandao wa Membe tayari alikuwa katika tope la Rushwa ambapo alijhusisha na mtandao wa Waziri Gerson Lwenge ambaye tuhuma zake zipo PCCB Njombe.

Hata hivyo Mangula alipenda apite kama mjumbe wa NEC lakini kikwazo kikubwa alikuwa ni YONO KEVELA. Baada ya kushindwa katika kinyang'anyilo hicho aliamua kupambana na YONO Kwa CHUKI na akajiunga na kundi la akina Lwengwe ambao taarifa za 2010 zinaonyesha kuwa alikamachwa na Kamanda wa PCCB Richard akitoa Rushwa.

Hata hivyo Mangula alijihusisha na siasa chafu kwa kumutukana Mangufuli na YONO kuwa wanatibiwa Mirembe kwa magonjwa ya Kichaa.

Mangula alihojiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama Njombe akakiri kuwa ana Ushahidi jambo ambalo walimuona anachanganyikiwa!!!

Kilichomfanya kikwete kumuibua Mangula ambaye ni adui yake Mkubwa ni kasi ya Lowassa kutaka kutenganisha Kofia Mbili ambapo tayari Uvccm walishatwangana DSM.

Kilichowaumiza ni hatua ya Yono Kevela Kuandika barua ya wazi makao makuu CCM kabla hata Mangula hajateuliwa kuwa makamu mwenyekiti CCM kumurithi Pius Msekwa!!!

Barua hiyo imewaumuza sana akina Membe lakini Wakaona ni Bora Kuifumbia macho!!

Mangula ametoa siku sita kwa Waliotoa Rushwa kujisalimisha na kwamba wanapitia Rufaa zote lakini hii rufaa ya Njombe ni Mwiba Mchungu:


Ili Mangula aonekane ni Muumini wa kweli ni bora akaanza na Rufaa za Nyumbani kwake Njombe Kwani Usafi unaanza ndani kwako ndipo Uende Sehenu Nyingine kama Arusha:


Habari kamili ipo katika gazeti la Mwananchi leo Lead Story soma hapa chini
Na Zabro..........


ALIYEKUWA Mbunge wa Njombe Magharibi (CCM), Yono Kevela amemtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula kwa kuvuruga uchaguzi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya chama hicho, Wilaya ya Wanging'ombe kwa kuwabeba baadhi ya wagombea.

Katika madai yake ambayo ameyakatia rufani, Kevela amesema katika uchaguzi huo uliofanyika Julai 29 mwaka huu, mbali na kuwabeba wagombea hao, Mangula alishiriki kutengeneza makundi ya vitisho, rushwa na lugha za kejeli dhidi yake.

Alisema siku ya uchaguzi akiwa amekaa meza kuu, Mangula alipopewa nafasi ya kuhutubia, aliwaambia wajumbe kuhakikisha Kevela na mgombea mwingine Hamisi Nurdin hawapiti.

"Mangula alisema watu hao wasichaguliwe kwa kuwa wana malengo tofauti na yale ya kukitumikia chama," alidai Kevela. Malengo yaliyodaiwa katika rufani hiyo ni kuwa Kevela anautaka ubunge wa Njombe Magharibi na Nurdin ana nia ya kutaka Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe yawe Igwachanya.

Rufani hiyo imetaja tuhuma nyingine dhidi ya Mangula kuwa ni timu yake kutangaza kuwa Kevela amejitoa kwenye uchaguzi… "Hili liliathiri pia ushindi wangu katika uchaguzi huo."

Rufani hiyo ya Kevela nakala yake imepelekwa kwa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa CCM, Idara ya Usalama na Maadili ya CCM, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe.

Kevela katika rufaa yake hiyo, anataka matokeo ya uchaguzi huo yafutwe kwa kuwa ulikiuka vifungu kadhaa vya kanuni kikiwamo cha Miiko ya Shughuli za Uchaguzi na Uteuzi wa wagombea ukurasa wa 39, cha Kanuni za Uteuzi toleo la Februari 2010, Kifungu namba 22 (1-6). Hata hivyo, pamoja na kukata rufani hiyo, Kevela amesema ana shaka kwamba haki itatendeka kwani, mtu anayemlalamikia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ambayo kulingana na Kanuni za Uchaguzi za CCM, ndiyo itakayopitia malalamiko hayo na kuyatolea uamuzi.

Kamati hiyo inatakiwa iwe imekamilisha kazi yake ndani ya miezi sita na Mangula alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo dhidi yake alisema hazijamfikia na wala hazijui.

"Hayo hayajanifikia na siyajui. Hata hiyo rufaa haiji kwangu. Malalamiko yote yanashughulikiwa na jopo la wataalamu kabla ya kufikishwa kwetu. Hivi sasa malalamiko yote yako katika hatua ya uchambuzi na kimsingi yatakayoshughulikiwa ni yale yanayohusu rushwa pekee."

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu madai hayo alisema asingeweza kufanya hivyo kwa kuwa alikuwa na siku chache tangu alipoanza kazi hiyo na kutaka aulizwe Katibu wake wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Alipoulizwa, Nape alimtaka mrufani kutokuwa na wasiwasi juu ya kutendewa haki akisema kwa kawaida rufani hazisikilizwi na mtu mmoja.

Alisema baada ya kuchambuliwa, rufani zote zinafikishwa katika kikao cha sekretarieti ambayo huzipitia na kuzipeleka katika Kamati ya Usalama na Maadili kisha Kamati Kuu na yapo ambayo huishia katika ngazi hiyo na mengine kupelekwa hadi Halmashauri Kuu kwa hatua zaidi.

Nape alisisitiza kuwa hakuna uamuzi utakaofanywa na mtu mmoja … "Labda aseme (Kevela), kuwa hana imani na Kamati Kuu ya chama chake na hapo ndipo labda tutaangalia kanuni zinasemaje lakini kwa sasa hali halisi ndiyo hiyo," alisema.



Fuatilia kwa Makini Barua inayomtesa Mangula :

YONO S. KEVELA
MGOMBEA NEC TAIFA.
S.L.P 46 ILEMBULA,
WANGING'OMBE – NJOMBE.




KATIBU MKUU WA CCM TAIFA


YAH: MALALAMIKO YA UCHAGUZI WA NEC TAIFA WILAYA YA
WANGING'OMBE MKOA WA NJOMBE KUWA HAUKUWA HURU NA HAKI.
ULIJAA VITISHO KASHIFA, RUSHWA NA DHULUM
Rejea kichwa cha habari hapo juu. Mimi Yon S. Kevela niliyekuwa mgombea katika uchaguzi huo katika nafasi ya NEC Taifa, natoa malalamiko yangu juu ya uchaguzi huu uliofanyika mnamo tarehe 29,07.2012 siku ya Jumamosi eneo la soko kuu la Igwachanya katika wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe kuwa uchaguzi huu haukuwa huru na haki kwa sababu zifuatazo:-

I. Viongozi wa CCM wilaya na mkoa waliwabeba baadhi ya wagombea akiwemo mgombea Nepchardi Msigwa ambaye pia aligombea nafasi ya NEC Taifa kupitia wilaya ya Wanging'ombe. Walimbeba mgombea huyu kwa kutoa hotuba zilizojaa vitisho na kunikandamiza mimi Yono S. Kevela ili nisichaguliwe na badala yake achaguliwe ndugu Nepchardi Msigwa ambaye ndiye walimuandaa badala ya Philipo Mangula (katibu mkuu mstafu wa CCM Taifa). Pia mheshimiwa Philipo Mangula ambaye naye alikuwa ameomba kugombea nafasi ya NEC Taifa na ambaye jina lake halikurudi, alipewa nafasi ya kukaa meza kuu na pia kutoa hotuba iliyojaa ukandamizaji ulioelekezwa kwangu (Yono S. Kevela). Mheshimiwa Mangula katika hotuba hiyo aliendelea kuse kuwa jina lake halikurudi ili kuwa mgombea, kwasababu Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Serikali ya Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alimtuma Nchini Msumbiji akiongozana na mheshimiwa Rais mstafu ndugu Benjamini W.Mkapa, mheshimiwa Ali Hassani Mwinyi na mheshimiwa Hashim Mbita. Pamoja nayo alihoji kwa nini jina lake halikurudi na kikubwa kwa kuwasiliana na Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa.

1. Hotuba hiyo ya mheshimiwa Mangula iliungwa mkono na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya na Taifa kwa kudai kuwa mheshimiwa Mangula atapewa kuwa Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa. Kutokana na hoja alizo sema yeye (Mangula) kuwa chama kinayumba bila yeye, kwakuwa yeye ni mzoefu na kwamba alikuwa mkufunzi wa Makada wa CCM kaika Chuo cha Kivukoni kilichopo Dar – es – Salaam na kuwa yeye ndiye anayesimamia Ilani ya CCM. Maneno haya yalinitisha mimi kama mgombea kwani msimamizi huyu wa Ilani alikuwa akimtetea Mpinzani wangu (Nepchardi Msigwa) ambaye wanatoka tarafa moja ya Imalinyi huku mimi nikitoka katika tarafa nyingine ya Wanging'ombe. Mkakati huo haramu wa kunikandamiza ulifanywa chini ya Mh. Eng. Gerson Lwenge ambaye pia ni Naibu waziri na Mbunge wa jimbo la njombe magharibi. Lengo lao wakitaka mimi (Yono. S. Kevela) niliyegombea NEC Taifa na aliyekuwa mgombea uwenyekiti CCM wilaya ya Wanging'ombe mheshimiwa Hamisi Nurdi hatupati nafasi katika uongozi wakidai kuwa mimi Yono. S. Kevela nina lengo la kuhitaji Ubunge 2015 na Hamisi Nurdin analengo la kuhamisha makao makuu ya wilaya toka Igwachanya na kuhamia Wanging'ombe ambayo ni Taifa anayotoka yeye (Hamisi Nurdini).

Akiwa katika ziara jimboni, Mheshimiwa Lwenge alikuwa akitoa hotuba akidai kuwa Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Taifa anamuandaa yeye Lwenge kuwa Waziri kamili kwani Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Dr Magufuli hafai na haelewani na Mheshimiwa Rais (Dr. Jakaya M. Kikwete) kwa kuwa Dr Magufuli ni mgonjwa na maamuzi yake si makini ndio maana anabomoabomoa nyumba za watu hovyo. Hayo aliyasema akiwa katika kata ya Saja. Huku akidai kuwa Yono.S. Kevela aliondolewa katika kura za maoni 2010 na kuteuliwa yeye mtu wa tatu(3), akinituhumu kuwa mimi Yono S.Kevela sikuwaletea wananchi wajimbo la Njombe magharibi maendeleo na akiwaambia watu kuwa mimi ni mgonjwa wa akili, Ukweli ni kwamba kura ambazo nilimzidi katika kura za maoni zilikuwa zaidi ya kura mia tano (500) dhidi yake Mh Lwenge. Na amekuwa akijisifu kwamba yeye aliteuliwa na NEC na siyo wananchi
.

Mpinzani wangu Nepchardi Msigwa alikuwa akifanya kampeni kinyume na utaratibu uliopangwa na CCM Taifa, kwani alitoa kampeni zake kupita redio Ibon Fm iliyopo mkoani Iringa siku ya alhamis tar 27.09.2012 katika kipindi cha Morning talk kinachorushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 asubuhi – 0.1:00 asubuhi, kipindi hicho kiliongozwa na watangazaji Malegesi Gilshon, Neema Msafiri na Raymond Franscis. Baada ya kuhojiawa na baadhi ya wajumbe kuwa kwa nini unafanya kinyume na utaratibu alisema kuwa ameruhusiwa na ofisi ya CCM Wilaya na Mkoa na mlipojaribu kuuliza kwa Katibu wa CCM Wilaya alikataa kuwa sikumruhusu mtu yeyote kwani kanuni haziruhusu na kwamba kama ninaushahidi nimpelekee. Lakini inaonekana kwamba aliruhusiwa na ndugu yake (Adam Msigwa) ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe. Na ndio maana hata siku ya uchaguzi viongozi wa meza kuu walianza kutoa hotoba na salam za kumbeba ndugu

2. Nepchardi Msigwa ili ashinde uchaguzi na akashinda kama mkakati wa safu yao ya uongozi walivyoupanga. Pia ndugu Adam Msigwa alikuwa akitamba kuwa, kwa kuwa yeye ameshinda katika nafasi ya uwenyekiti wailaya ya Njombe hivyo atahakikisha kwamba mimi Yono. S. Kevela na Hamis Nurdin pamoja na Scholastika Kevela hatutapata uongozi wowote wala kushinda nafasi yoyote katika CCM. Mipango yote hiyo ilikuwa ikifanywa pamoja na Katibu wa CCM Mkoa ndugu Hosea Mpagike chini ya usimamizi wa Gerson Lwenge.

3. Kampeni za kunichafua na kunidhalilisha, mnamo tar 06/09/2012 Nepchardi Msigwa alikuja nyumbani kwangu Ilembura majira ya saa moja usiku akiwa ameongozana na rafiki yake Lupenza na kusema kuwa wametoka kwenye kampeni na kutembelea wajumbe, siku iliyofuata nilianza kupokea simu za watu wakiniambia kwamba mbona Nepchardi anasema kwamba wewe umejitoa na kusema kuwa mimi nina matatizo ya akili. Lakini pia hata siku ya uchaguzi, Nepchardi Msigwa alitoa kampeni za kunidhalilisha kwa kusema kuwa yeye hachekicheki kwani wanaocheka cheka ni warembo na hawezi kuvaa suti kwani yeye ni askari. Ukweli siku hiyo ya uchaguzi nilikuwa nimevaa suti na tai. Nahii ni baada ya kuulizwa swali na mjumbe mmojawapo siku hiyo ya uchaguzi.

Mwisho naomba kusema yafuatayo:-

1. Athari nilizopata ni kubwa sana katika familia, katika jamii na katika nafasi mbalimbali za uongozi kuwa huenda nimepangiwa kitu kibaya sana. Tatizo hili ni kubwa na nilishawahi kuambiwa kuwa mimi sio raia wa Tanzania na kuwa mimi ni raia wa Afrika Kusini mwaka 2003, idara ya uhamiaji ilinisumbua sana hadi wakaniandikisha uraia.

2. Mimi nilikuwa mbunge wa CCM wa Jimbo la Njombe Magharibi (2005 – 2010) Sijawahi kuonywa wala kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu. Matusi na ubbabe ni sera za CHADEMA siyo za CCM, CCM ina sera za amani na upendo. Hivyo naomba Chama kichukuwe hatua zinazostahili dhidi ya mgombea huyo Nepchardi Msigwa. Hivyo naweka pingamizi la kuomba uchaguzi upande wa NEC Taifa kupitia Wilaya ya Wanging'ombe utenguliwe kwa manufaa ya Wilaya na CCM.

3. Upendeleo wa waziwazi uliokuwa na lengo la kunikandamiza, Yono Stanley Kevela lilitakiwa kuwa jina la mwisho katika mpangilio wa kialfabeti lakini hali ilikuwa ndivyo sivyo jambo ambalo linadhihirisha wazi upendeleo. Jina langu lilipewa kuwa la kwanza, kwa makusudi kabisa Mkurugenzi wa uchaguzi – Katibu wa CCM (W) aliamua kuvunja utaratibu wa jina la Yono kuwa la mwisho akaamua niwe wa kwanza ili Nepchardi Msigwa aweze kunitukana matusi ya nguoni ili nikose kura nisiweze kujitetea sehemu yoyote, mkakati huo ulifanywa kwa makusudi na ofisi ya wilaya na Mkoa CCM. Siyo bahati mbaya au kosa dogo kwani kanuni za kialfabeti zinataka majina ya wagombea yawe katika muonekano huu Mfano: 1. Juliet Kadodo 2. Nepchardi Msigwa 3. Yono S.Kevela Hivyo sikutendewa haki na siku ya uchaguzi nililalamika, nikazomewa na kupuuzwa. Na nikalazimishwa nikubali matokeo la sivyo watanifukuza chama au kupewa onyo kali. Kwa vile ninakipenda chama (CCM) na kwakulinda heshima ya chama na heshima yangu nilitii kwa kuwa nilijua ninayo haki ya kutoa malalamiko yangu ndani ya siku kumi na nne (14) ilibidi nifuate matakwa ya wakubwa hao wa wilaya na Mkoa. Matusi ya nguoni pamoja na kuwa nina chekacheka kama mwanamke na tahira (kichaa). Uso wangu wa kike na kutabasamu kauli za matusi na fujo ni sera za CHADEMA na ambazo chama chetu kimakuwa kikisimama kidete kupinga sera za kuchafuana. Na ilipangwa vizuri na ngazi ya wilaya na Mkoa kwani hakuna kiongozi yoyote aliyekemea au kumsimamisha ili kupinga sere za matusi alizokuwa akizitoa mgombea Nepchardi Msigwa. Nilidhalilishwa sana naomba Chama kinilinde na wamchukulie hatua zinazostahili huyo mgombea wa NEC -Taifa ndugu Nepchardi Msigwa ambaye ni ndugu wa Adam Msigwa – Mwenyekiti wa CCM – Njombe. Chama sasa ni mali ya watu Fulani au ukoo wa Msigwa. NEC-Nepchardi Msigwa Edson Amri Msigwa M/Kiti Wanging'ombe CCM (W) M/kiti – Adam Msigwa – Njombe CCM (W) Na mipango yote ya kugombea ndugu Nepchardi Msigwa iliandaliwa na ndugu yake Adamu Msigwa (mwenyeki CCM wilaya ya Njombe) kwa vile anadai tuna ugomvi na sitakuwa na nafasi katika Chama (CCM).

Ni kweli kabisa ukoo wetu (Kevela) kaka yangu Elias Kevela alioa dada yake Adam Msigwa (binamu yake) aitwaye Rehema Kambo wamezaa watoto wawili wa kiume Danieli Kevela na Wito Kevela. Bahati mbaya kaka yangu alimtalika huyo dada binamu Rehema Kambo. Dada huyo amelelewa na ukoo wa Adam Msigwa akiwa mdogo na mjomba wake mzee Kambo alikuwa Kanamalenga ninakotoka mimi Yono S.Kevela, kitendo ambacho anajenga chuki ameamua kumbeba kwa hali na mali ndugu Lwenge, Naibu Waziri na Mbunge. Hata siku ya uchaguzi wa Wilaya ya Wanging'ombe akawa anamsifia sana Mh Lwenge. Kuwa anamjazia mafuta kwenye gari na kumpa fedha na misaada mbali mbali. Hivyo anakuwa anaungana na Katibua wa CCM Mkoa Hosea Mpagike, kujenga mikakati ya kunimaliza kisiasa. Akina Lupyana Fute wao wanatumika tu. Na siku za nyuma alikuwa anambeba sana Thomas Nyimbo wa CHADEMA sababu kubwa ilikuwa kwa vile alikuwa amemsaidia sana kupata Uenyekiti akiwa Mh Nyimbo Mbunge hadi nilipomshinda mwaka 2005 bado waliendelea kushirikiana hadi alipohamia CHADEMA.

4. RUSHWA ilishamiri siku ya uchaguzi wahusika wakagawa fedha za Mh Lwenge na Mangula ili ashinde mgombea Nepchardi Msigwa katika NEC –Taifa kupitia wilaya ya Wanging'ombe na hawa ni baadhi ya waliopewa pesa hizo chafu na wao kuwagawia wapiga kura wakiwasihi kumchagua Nepchard Msigwa:- i. Stephano Kinyangasi – Mkandarasi amehusika kugawa kata fedha za kampeni. ii. Anna Upendo – Diwani Mdandu iii. Makwata – Diwani Igwachanya iv. Zawadi Mgani – Mwenezi Ilembula – amekamatwa na PCCB kuhojiwa.

Wote hawa walipewa pesa na Mangula na Mh Lwenge ili wawapatie wajumbe awape na kumpigia Nepchard Msigwa.
Bahati nzuri TAKUKURU inawashikilia na kuwahoji Zawadi Mgani kwa tuhuma ya rushwa Tsh 360,000/= zilikuwa zinagawiwa kwa baadhi ya wajumbe nje ya mkutano na kwenye vyoo nabar bila ya kuandikishwa sehemu yeyote.wakati wanatoa hiyo rushwa walikuwa wanaelekezwa kuwa wamchague Nepchardi Msigwa siyo Yono Stanley Kevela na tayari alikuwa kwenye mtandao wa Mh Lwenge na kunichafua kuwa sifai kuwa NEC Taifa, alikuwa akinichafua Zawadi Mgani.

Zawadi Mgani alipewa kazi ya kugawa pesa ya posho kwa wajumbe, kazi ambayo yeye hakutakiwa kuifanya kwani yeye si Katibu wa CCM Kata, Ila yeye na mjomba wake Richard Ngwale Diwani wa Ilembula
Ndio waliopanga kuwa Zawadi Mgani ndiye agawe pesa za posho mtandao wa mheshimiwa Lwenge wakanichafua na kupinga nisipate NEC –Taifa. Na akatumia nafasi hiyo kutoa rushwa. Yote haya yaliyotendeka yalikuwa ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uchaguzi, baadhi ya vifungu vya kanuni vilivyo kiukwa ni: Miiko ya shughuli za uchujaji na uteuzi wa wagombea ukurasa wa 39 katika kanuni za uteuzi wa wagombea toleo la februari 2010 Kifungu namba 22(1-6) Sababu ya kupinga uchaguzi huo kwa nafasi ya UNEC

5.
Utangulizi: Katika kikao cha NEC kilichokaa Dodoma chini ya Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete kilitoa maelekezo kuwai ni marufuku kwa mgombea yeyote Yule kufanya kampeni za kuzunguka mitaani kwa lengo la kushawishi ama kuomba kura kwa wajumbe. Kwa mujibu wa kanuni hiyo inapaswa mgombea huyo aombe kura ndani ya ukumbi siku ya uchaguzi na si vinginevyo. Kwa maelezo hayo ndugu Nepchard Msigwa amefanya kinyume na utaratibu unavyotaka kama ifuatavyo; · Kunako tarehe 27/09/2012 katika kipindi cha morning.talk kinachorushwa kuanzia majira ya saa 12:00 alfajiri hadi saa 4:00 asubuhi,kipindi hicho kiliongozwa na watangazaji waitwao. a) Malegesi Gilshon b) Neema Msafiri na c) Roymond Francis Ndugu Nepchard Msigwa alifanya kampeni za wazi wazi kinyume na utaratibu wa CCM akiwataka wajumbe wampe / wampigie kura kupitia Redio Ibon FM na ushahidi wa tukio hilo upo kwenye CD naambatanisha kwenye taarifa hii.

2. Kashifa
· Kinyume na maadili ya mwanachama wa CCM ndugu Nepchard Msigwa alidiriki kunitolea kashifa kwa wanachama wenzangu wa CCM kwa kudai kuwa mimi niliwahi kuugua kichaa, ni mwndawazimu nisiyekuwa na sifa ya kuwa kiongozi na akadai kuwa nimelazwa Hospitali ya Milembe katika wodi ya vichaa na mpaka sas naendelea kutumia dozi na niko chini ya uangalizi maalum ya mke wangu, kaulihizi zinanidhalilisha kifamilia na kijamii kauli kama hizi mara nyingi hutolea na vyama vya upinzani. · Aliye kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini ndugu Godbless Lema kwa ticketi ya Chadema. · Katika kampeni zake aliwahi kutoa kauli kama hizi dhidi ya mgombea wa CCM Mh Buturido Buriani na kwa kitendo hicho mahakama kuu iliamua kutengua ubunge wake.

6.

3. MATUSI
Ndugu Nepchard Msigwa siku ya uchaguzi tarehe 29/09/2012 katika ukumbi wa uchaguzi mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu (w) mpya ya Wanging'ombe, Alidiriki kunitukana wazi wazi kuwa mimi ni kiongozi mwenye kupenda kucheka cheka ovyo kama mwanamke na nisiyokuwa na maamuzi ni mjinga na kibaya zaidi matusi hayo ametukana mbele ya viongozi wa wilaya na mkoa pamoja na katibu mkuu mstaafu Mh. Philipho Mangula. Kauli hizi zilitolewa kwenye ukumbi wa uchaguzi na zilishuhudiwa na vyombo vya habari ulinzi na usalama wa Taifa na Maafisa / waandamizi kutoka kitengo cha Idara ya uchaguzi makao makuu. Ikumbukwe kauli hizi hutolewa na viongozi wa chadema Mfano: · Mbunge wa jimbo la Ubungo ndugu John Mnyika akiwa Bungeni aliwahi kumtukana mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwamba, Anacheka cheka ovyo hana maamuzi na mdhaifu. · Kwa kupitia kauli hizo, Naibu Spika Mh. Job Ndugai alimtoa nje ya bunge. ·

Mh. Mwenyekiti wa CCM kitendo alichofanya kijana huyu analenga kukichafuaChama cha Mapinduzi na kukikosesha ushindi kwenye uchaguzi mkuu 2015-2020. Kwani kitendo hicho kisipo shughulikiwa kitaathili chama kwa sababu mimi niliwahi kuwa Mbunge 2005 – 2010 hivyo nitakapo amua kugombea uchaguzi mkuu ujao Wapinzani wanaweza kuweka pingamizi iwapo nitateuliwa na chama change kwamba aliyeteuliwa CCM ni tahira, kichaa na anacheka cheka ovyo na kusababishwa kuenguliwa na kuwapatia upinzani nafasi kubwa ya ushindi kwa kosa la mtu kama huyu. Pamoja na maelezo haya naambatanisha na CD ya kampeni aliyoifanya tarehe 27/09/2012 kupitia redio Ibon Fm. Ambapo nikinyume cha kanuni zilizotutaka tufanye kampeni katika ukumbi wa uchaguzi siku hiyo ya uchaguzi. Niko tayari wakati wowote kutoa ufafanuzi.

Ni Mimi
………………………………….
YONO STANLEY KEVELA
Mgombea wa NEC Taifa



NB: Pamoja na kashifa na kunidhalilisha kuwa mimi ni mgonjwa wa kichaa, nakanusha kuwa mimi si mgonjwa nimwenye akili timamu na nimesoma shahada ya pili katika Chuo Kikuu cha Dar –es –Salaam na nina uzoefu wa shughuli za chama na Serikali na nilikuwa Mbunge wa jimbo la Njombe magharibi kuanzia 2005-2010 pia ni mcha Mungu.



KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.


Nakala:
· Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
· Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa.
· Idara ya Usalama na Maadili.
· Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa.
· Mkuu wa wilaya Wanging'ombe.
 
wewe gamba umetumwa na nani? humu
tokaaaaaaa kwa jina la mwenyekiti
kidumu chama tawala ,zidumu fikra sahii za mwenyekiti
 
wewe gamba umetumwa na nani? humu
tokaaaaaaa kwa jina la mwenyekiti
kidumu chama tawala ,zidumu fikra sahii za mwenyekiti
Jina linalo Toa Mapepo ni jina la YESU na sio Mwenyekiti,
Kumbuka hata Kikwete akiwa Mweyenyekiti alianguka jangwani 2010. Jitazame kama hujatumwa!!!
 
Kevela atakua na matatizo ya akili kweli kwani hawezi kutoa tuhuma zake bila kuihusisha CDM? Lakini amenisaidia kujua siri ya uteuzi wa Mangula na siasa za majitaka na kikabila zinazoendelea mkoa mpya wa Njombe.
 
Kevela atakua na matatizo ya akili kweli kwani hawezi kutoa tuhuma zake bila kuihusisha CDM? Lakini amenisaidia kujua siri ya uteuzi wa Mangula na siasa za majitaka na kikabila zinazoendelea mkoa mpya wa Njombe.
Inakuaje mwenye matatizo ya akili anakusaidia ??? Au na wewe huna akili???
Kama kweli Kevela ana matatizo ya akili basi kwa kauli yako hupaswi kutumia ripoti ya mweye matatizo ya akili vinginevyo na wewe huna akili katika hilo!!!
 
Sasa huyu chizi naye si aende huko machizi wenzake wanapokimbiliaga?
 
du ina bidi uwe na ujasiri kusoma barua hii ... Jamaa ameshuka hakuna aya wala nini sijui anshahada ya kitu gani ya chuo kukuu iliyompa ujzi huu wa kuandika!
 
Matusi ya nguoni pamoja na kuwa nina chekacheka kama mwanamke na tahira (kichaa). Uso wangu wa kike na kutabasamu kauli za matusi na fujo ni sera za CHADEMA na ambazo chama chetu kimakuwa kikisimama kidete kupinga sera za kuchafuana.

Hayo maneno yanafanania Lusinde a.k.a kibajaji.. Waache kuiingiza Chadema.. Kibajaji ndo kinara wa aina hiyo ya matuci..
 
Tiba mbadala inahitajika ili kuwatibu hawa wanaoshindwa katika chaguzi zinazofanyika maeneo mbalimbali kuwa wakishindwa wawe wanakubali matokeo bila tatizo la kuuwaza uongozi huo muda mrefu. Uongozi ni kipaji. Kubali matokeo utajikuta unakubalika kwa wananchi hata bila hotuba ndeeeeeeefu.

Veya piluhe hu-vanging'ombe Kavafugamile Avavaha!!! Vitahiwa vapeete lulenga
 
(Ndani ya miezi 6 tutakisaficha chama. Wale wote walio shinda chaguzi kwa rushwa tutawafuta) Da kauli hiyo ya abuniasi ndani ya serikali iliyo shidwa kujivua gamba mpaka leo ilinichekesha sana Ha Ha Ha Haa!
 
Mangula Kumbe ndivyo ulivyo, kelele nyingi kuhusu rushwa, vitimbi kama Kibajaji, na Mwingulu, hivi ndivyo wanafunzi wako wa kivukoni ulivyowafundisha, mtu anakuwa mbunge miaka 5 unamuita ahende mirembe, kweli wewe ni wakuogopa kama ukoma
 
Siku zote alikuwa hajui kuwa huo ndio utaratibu wa CCM...? Sipendi watu walioshindwa halafu wanabaki kulalamika tu...! Kwetu uswahilini ukishaona mpira umejaa rafu unajiandaa, maana either utie mpira kwapani uondoke au subiri ngumi zilike....!
 
Jamani jamani hapa JF, mbona tunaharaka sana? Hatutaki kuhoji japo kidogo, tunakuwa na haraka ya kumjibu mtoa uzi.

Mfano mzuri jamaa katoa hata watu gani wamepewa nakala za barua hii.

Cha kwanza tunatakiwa tuhakikishe kama hii barua ni kweli ipo au imetungiwa humu humu JF? Na kwa kupitia wenye nakala je ilivyoandikwa hiyo barua na ilivyorushwa humu JF ni kama ilivyo na hakuna chumvi zilizoongezwa kwa malengo yeyote yale?

Tukishakuwa na uhakika wa hayo hapo ndipo tunakuwa na haki ya kisomi ya kumjibu mtoa uzi. Hapa wachangia wamekimbilia tu UCCM na UChadema. Hivi havitusaidii sana.

Hoja ya msingi hapa ni hii tuhuma ya rushwa.
 
kweli KEVELA ni tahila anayemalizia dozi mirembe....anaandika barua ktk JF anajifanya ameituma kwa chairman?
Barua gani haina SAHIHI? ameshindwa hata ku-scan hiyo original letter? na kwa nini akihusishwe chama cha CHADEMA?

....amulize nyimbo FITINA zake zimedunda kwa Eng.Lwenge,sasa wewe KIHIYO mwenye SHAHADA feki utaweza kwa MATHEMATICIAN and senior ENGINEER?....MANGULA ni kiboko ya wala RUSHWA subiri pigo la mwisho
 
kweli KEVELA ni tahila anayemalizia dozi mirembe....anaandika barua ktk JF anajifanya ameituma kwa chairman?
Barua gani haina SAHIHI? ameshindwa hata ku-scan hiyo original letter? na kwa nini akihusishwe chama cha CHADEMA?

....amulize nyimbo FITINA zake zimedunda kwa Eng.Lwenge,sasa wewe KIHIYO mwenye SHAHADA feki utaweza kwa MATHEMATICIAN and senior ENGINEER?....MANGULA ni kiboko ya wala RUSHWA subiri pigo la mwisho
 
Hiyo barua ya msomi Kevela ameshindwa hata kuweka aya ili isomeke kwa uzuri zaidi? Ndivyo original copy ilivyoenda makao makuu?
 
Back
Top Bottom