Barua hii ya wazi imfikie naibu Waziri wa elimu mh. William Ole Nash

Smkwawa

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
651
964
BARUA HII YA WAZI IMFIKIE NAIBU WAZIRI WA ELIMU MH. WILLIAM OLE NASH.

Na
Abdul Nondo.

Habari za majukumu, Mh.Naibu waziri Mimi Naitwa Abdul Nondo, ni mkurugenzi idara ya haki na wajibu wa Wanafunzi kutoka mtandao wa wanafunzi Tanzania.(TSNP).

Jana nimekuona ukiwa bodi ya mikopo pia ukaunganisha hadi tume ya vyuo vikuu pia ukatoa maagizo.Sura yako ilioneshwa uhitaji mkubwa wa maagizo aliyotoa Mh.Rais John Pombe Joseph Magufuli kutekelezwa haraka, ili wanafunzi waliopata mkopo wasipate taabu.

Mh.Ole Nash, kuna masuala mawili ambayo kama Mkurugenzi wa haki za wanafunzi ,Naomba kukufikishia katika wizara yenu.

1. Vyuo kuzuia wanafunzi kusaini fedha zao hadi wafanye usajili na kulipa ada zote na michango yote

Mh.Naibu waziri,bodi ya mikopo wanatoa mikopo kwa wanafunzi ambao wapo chuo ,wamedahiliwa na wanaoendelea,hakuna mwanafunzi aliyedisco anapewa mkopo.hii inamaana mikopo yote inayoenda vyuoni ni ya wanafunzi halali wa chuo ,ila tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka vyuo vikuu vingi Tanzania. (Vya dar na nje ya dar) kuwa mwanafunzi haruhusiwi kusaini fedha yake ili ingie ktk akaunti sababu hajalipa ada,kila jina la mwanafunzi katika sheet(karatasi ya kusaini kuna akaunti namba yake) ,hivyo sio rahisi fedha kuingia sehemu nyingine.

Wanafunzi wengi wanapewa fedha ya chakula na malazi tuu(boom) ,hawalipiwi ada hivyo hutegemea saana fedha hiyo ya chakula na malazi kuongezea kulipa ada,wengine hawalipiwi ada yote hutegemea fedha ya chakula na malazi kuongezea katika ada.

Hivyo kwa kufuata maagizo ya Mh.Rais wanafunzi wapate fedha(mkopo huu kwa wakati) haitawezekana kwa sababu hii ,watu hukaa hata wiki 2 hawajapewa fedha zao ,ambazo tayari bodi ya mikopo huwa wamezipeleka chuo husika ila vyuo huwa wanakataa mwanafunzi kusaini hadi alipe Ada na Afanye usajili,fedha hizo ndio hutegemewa kuongezea katika kulipia ada,Tusaidie Mh.Naibu waziri huu mfumo sio rasmi na upo vyuo vingi vya dar na nje ya dar na umekuwa ukileta usumbufu mkubwa kwa wanafunzi kupata fedha zao kwa wakati.Tuna imani kubwa na wizara ya elimu hamuwezi kulifumbia macho suala hili hata kidogo,tunaomba muwasaidie wanafunzi ili haya malalamiko tunayoyapata yaishe.

2. Wanafunzi wengi hawajapata Mkopo

Mh.Naibu waziri ,tunaipongeza serikali na wizara yenu ya elimu namna mnavyopambana kuleta mabadiliko katika elimu.

Ila kama Mkurugenzi wa haki za wanafunzi kutoka TSNP,tuna ombi maalumu kwa serikali juu ya mikopo elimu ya juu.bajeti ya mikopo elimu ya juu mwaka huu 2017/2018 ni Bil.427 kuanzia mwaka wa Kwanza hadi wa 4.

Mwaka wa kwanza wametengewa sh.bil.108.8 kwa wanafunzi elf 30,mh.waziri walioomba ni wanafunzi elfu 61 sio kweli Mh.waziri kuwa hao elf 31 hawana sifa ,sio kweli bodi wenyewe wanalijua hili ndio maana ,unaweza shangaa bodi ili tangaza kutoa mkopo kwa wanafunzi elf 30 tuu ,hata kabla ya wanafunzi kuanza maombi ya mkopo.

Hii ni dhahiri kuwa wengi wenye vigezo wamekosa pia,tunapokea simu nyingi,meseji nyingi wanafunzi ni yatima,ni walemavu,na waliambatanisha kila nyaraka ila wamekosa.

Jibu linabaki ni moja tuu,kuwa bajeti haitoshi ,ni kweli haitoshi kwa namna hii wanafunzi wengi ndoto zao zimekatika hawajui hatma yao,tunawaomba wizara ya elimu mfikishe kilio hiki cha wanafunzi wengi kupitia sisi kwa Mh.Rais John pombe Joseph Magufuli. Anafanya vizuri ,anasomesha bure sekondari wanafunzi wanafaulu kwa idadi kubwa ila huku chuo wanapoteza ndoto zao huku kileleni ,wengi hawana uwezo wa kugharamia elimu ya juu.pia kuna wanafunzi wanaoendelea waliokosa mwaka Jana wakaomba tena mwaka huu wengi hawajapata.

Tunamuomba Mh.Rais John pombe Joseph Magufuli, Tunamuomba,Tunamuomba Mh.Rais asikie kilio hiki cha wanafunzi kwa Moyo wa huruma alio nao,Tunamuomba afanye maamuzi kwa niaba ya wanafunzi aongeze bajeti ya mikopo elimu ya juu,Aongeze kiasi fulani cha fedha ili kiweze kukidhi wanafunzi kadhaa walioachwa na wanasifa sababu ya ufinyu wa bajeti.

Wanafunzi wengi wapo nyumbani ,hawajui hatma yao,mh.Rais amewasomesha bure hawa kwanini tuwapoteze bila kujua,tuwasaidie.

Shukrani natumai Wizara mtafanyia kazi maombi yetu ,na mtafikisha maombi yetu pia Kwa Mh.Rais John pombe Joseph Magufuli,Rais wa wanyonge. Kama taarifa hizi zikimfikia hakika lazima afanye maamuzi.

Abdul Omar Nondo.
0659366125.
0762082783
Abdulnondo10@gmail.com
(Mkurugenzi idara ya haki na wajibu wa wanafunzi TSNP).

5a60633cab171839db17860d0231cec2.jpg
 
nice fanyen mipango iwafkie wahucka maana m mwenyewe npo nyumban cna ada wanaweza wakatfkria
 
Naatumai ujumbe huu umefika mahali husika na utaleta tumaini kwa vijana waliovunjika moyo na kupoteza tunaini la ndoto zao za elimu ya juu.
 
Haki aiombwi haki inatafutwa kwa mwendo huu wa kuandika barua za kusifia na kutia huruma haito saidia kitu.
 
Sasa mkuu ulitaka awalazimishe au? na hyo haki anaitafuta kwa njia ipi kama sio hii acha ajaribu tuone kama itasaidia au lah!
 
Dawa ni migomo mikubwa ya vyuo vyote nchi nzima hiyo ndo inayo weza kuwasaidia maana huyo Rais ni mpenda sifa hataki kuonekana kama anaharibu wakati kumbe hana lolote maana unaona alivyo wai kujitangaza kua kisha idhinisha pesa ili tu jamiii imuone kua anatimiza ahadi zake kumbe wanafunzi wenyewe wanao pewa hawafiki nusu ya walio omba.
 
Kweli kabisa mkuu hapo umenena sifa tu jamaa kabarikiwa
 
EEH MUNGU wangu wa mbinguni tusaidie kwa kweli wenzetu wapo orientation sisi adi leo hatujui hatma yetu fanya wepesi wako katika hili
 
WASOMI wa nchi hii ndiyo mnaiharibu nchi.Hammwambii uweli mfalme;mnafichaficha kutafuta sifa.Eti mpaka uanze na kusifia!!!!!
 
Iyo changamoto ya kwanza inatutesa sana tulio vyuon yan kupata boom mpaka usajiliwe kusema kweli wanatutesa.mimi nililipa ada awakat nasajiliwa lakin boadi wakanipa mkopo iyo pesa niliyo lipa mpaka leo sijapewa nikiomba waamishie kwenye michango mingine hawataki
 
Nondo ungesema pia mtindo uliotumika mwaka huu wa kubadili wanafunzi siyo mzima. Mwaka kesho wasiutumie tena
 
et watu wanazan rais hajui kua kuna kilio hiki duh!!!! sasa kwa taarifa nikwamba amajua na watu watakao pata ni 30elf tu na tuliokoswa niwale ambao hatukumchagua so tupambane na hali yetu
 
Haki aiombwi haki inatafutwa kwa mwendo huu wa kuandika barua za kusifia na kutia huruma haito saidia kitu.
Watu hutumia strategy mbali mbali kupata kile wakitacho. Unaweza kujaribu nyingine.
 
Back
Top Bottom