Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,486
- 2,332
Ni muda mrefu umepita tangu historia iandike wewe kupigwa na Makonda wakati wa sekeseke la katiba mpya. Katika utetezi wake Makonda anadai alikuwa anajaribu kukutoa nje, usidhurike na fujo zilizokuwa zimejitokeza.
Hata hivyo jamii hadi leo haijaamini utetezi huo wa Makonda hali inayoleta sintofahamu kuhusu ukweli wenyewe. Ila kiukweli wewe mh. ndio unaujua ukweli.
Kama ni kweli Makonda alichosema ni sahihi naomba uliweke wazi hili kwa watanzania kabla hujalala na kama sio kweli basi msamehe bure.
Kwanini nasema uliweke wazi? Makonda bado kijana na ana nyota ya uongozi, huko mbeleni atakuja kufika mbali sana na kuisaidia nchi hii, hivyo historia kubaki namna hiyo kuwa aliwahi kukupiga itakuwa ni doa sana katika safari yake na historia yake kwa vizazi vijavyo