Barua" fupi" kwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Magufuli

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
Salaam Wana JF,

Naanza andiko hili fupi kwa kumshukru Mungu kwa wema wake wote kuendelea kutupenda sisi Watanzania na kutujalia kheri za kila namna katika shughuli zetu za kila siku.

Baada ya Salaam hizo niangazie kusudi la barua hii fupi, Andiko hili kimaudhui ni kutambua Mchango wa kipekee kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na kiutamaduni uliofanywa na awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli katika miaka yake 5 ya awali, Bila shaka hakuna Mtanzania yeyote asiyetambua mchango wa Mzalendo huyu namba moja.

Awamu ya tano imekuwa awamu ya kipekee katika falsafa mpya za uwajibikaji tofauti na awamu nyingine zilizopita, Aidha Kitu kinachoitambulisha awamu hii ni "Utu wa Watu, Kazi na Maendeleo ya nchi Kwanza" Falsafa hii kimaudhui inaendana na ile ya Mwl. Nyerere ya "Ujamaa" Kwa nukta hiyo unaweza kuziona fikra za John Pombe Magufuli katika utawala wa watu dhidi ya Mwl. Nyerere na fikra zake.

Rais Wangu John Pombe Magufuli Salaam Kwako na pongezi sana kwa kulihe shimisha taifa langu la Tanzania, umefanya makubwa ambayo Sisi Watanzania wenye nia njema na nchi yetu tunajivunia na uwepo wako, Mhe. Rais maneno yote unayoyasikia kutoka kwa wakosoaji wako yapo yenye tija katika ujenzi wa taifa letu, lakini wengi kati ya wakosoaji hao ni Wanafiki sawa na Mafarisayo waliokuwa wakimjaribu Yesu kwenye Masinagogi huku wangali wanaujua ukweli wa mambo, Aidha ni Watu wanaotumika kuivuruga nchi yetu kwa maslahi yao binafsi na familia zao ambao asilimia yao ni kidogo kulinganisha na sisi tunaokuunga mkono.

Mheshimiwa Rais wapo wanaotumia jina vibaya la Mwasisi wa taifa hili kuwa "Kama angelikuwa hai asinge kubaliana na utaratibu wa sasa katika dhana ya demokrasia inavyotendewa" Wanaojenga hoja hii ni "Washamba kisiasa na pengine hawaijui historia ya taifa letu tokea tulipo pata uhuru" Pengine warejee maandiko ya Prof. Shivji watapata mantiki ya demokrasia katika mataifa ya Afrika.

Mheshimiwa Rais ukweli wa kitafiti ni kwamba Mwalimu Nyerere angekuwepo bado angeungana na wewe na kukupa sifa unazostahili kwa hiki unachokifanya kwa sasa, rejea viongozi wastaafu wa awamu zilizopita wamekukubali na kukupa ushirikiano unaohitajika Why Nyerere? bila shaka hii si hoja Rais wangu zaidi ya kuipuuza na kutambua ugumu wa siasa za Kiafrika kwa maana uongozwa na hila, chuki na uasi kwa waafrika wenyewe hivyo basi puuza na chapeni kazi kwa tija ya taifa zima.

Mheshimiwa Rais nimalizie barua hii fupi kwa kukutakia heri ya mwaka mpya wa 2021, Aidha niombe Falsafa na mitindo yako ya kiutawala uliyoitumia katika kipindi chako cha kwanza cha miaka mitano ya awali uendelee nayo katika kipindi chako hiki cha pili unapoelekea kuhitimisha miaka yako kumi, tunakuombea na sisi Watanzania wazalendo tupo tayari kusaidia kwa namna yoyote tutakapo hitajika kufanya hivyo, Kila la Kheri na Mungu akutangulie.

Ndimi, Deogratias Mutungi.
 
Safi sana ni vizuri Mzalendo JPM akapewa moyo namna hii, umefanya vyema sana kama unavyoona mawakala wa shetani ni wengi na hawapendi kuona nchi inasonga mbele.

Tumsupport Rais wetu.

Viva JPM
 
Wakina Mutungi mnaeleweka hata bila kuacha Namba ya simu teuzi utapata tu vilevile ni homeboy. Mnamsifia msifiwa anaonekana mjinga kuliko ninyi!
 
Safi sana ni vizuri Mzalendo JPM akapewa moyo namna hii, umefanya vyema sana kama unavyoona mawakala wa shetani ni wengi na hawapendi kuona nchi inasonga mbele.

Tumsupport Rais wetu.

Viva JPM
Wewe utakuwa ni mushuti
 
Back
Top Bottom