Barrick Yaitangaza Vibaya Tanzania “Considered a higher risk",na "Acacia Mining reflects Tanzania risk". Jee ni Kweli?. Kama Sii Kweli Tukanushe Au?.

Mchimbaji mdogo aliyeuza almasi ya billion 3 atamsikiliza Lisu kwamba atashitakiwa MIGA baada ya kuuza almasi yake kwenye soko la madini lililofunguliwa baada ya Magufuli kubadili sheria za madini??
Hivi si ni serekali ya CCM inayo tuhumiwa kuwafukia wachimbaji wadogo ili kuingia mikataba ya kinyonyaji. Taifa lilikuwa likinufaika zaidi na madini kabla ya kumilikisha migodi kwa wazungu....by TAL.
 
Ni kweli Tanzania ni high risk, sheria na sera zetu hubadilika overnight. Ni kawaida kukuta shughuli halali leo kesho ikaharamishwa bila kujali walio kuwa wamewekeza upande huo watapata hasara kiasi gani, mifano hai ipo. Tanzania haipo stable politically,..kila anaye ingia huanza kivyake unadhani tumepata uhuru siku hiyo yahani hatuna mwendelezo wa mipango na sera, sheria zetu zinabadilika badilika Ku favor matakwa ya viongozi. .......,.
 
Nazifahamu links ndugu ila sioni nyodo hapo makosa yetu wenyewe
P
 
Mkuu Paskal salaam sana!! Kinachotutesa wabongo ni uwepo wa serikali kurupushi tu basi!! Usihangaike kujitetea maana hata huyo unayesema analinda rasimali aliridhia madini yetu kutokukaguliwa na CAG! (Kama sijakosea)

Afu kaka, sisi tutajitetea wapi, tbc, itv, au channel ten?? Wenzetu wanazungumzia kwenye global media, na wanaeleweka maana wana reference ya Acacia kuwa tz sio rafiki tena kwa investors. Personally sifurahii ila serikali yetu inatakiwa ijitazame sana aisee!!
Tuache kujiuma uma ni kweli Tz si rafiki kwa investors wa ndani na wa nje period.
 
Mchimbaji mdogo aliyeuza almasi ya billion 3 atamsikiliza Lisu kwamba atashitakiwa MIGA baada ya kuuza almasi yake kwenye soko la madini lililofunguliwa baada ya Magufuli kubadili sheria za madini??
Mkuu turudi kwenye mada maana ata kabla ya apo wachimbaji walikuwepo na walikua na uza almasi au dhahabu zao.
Vipi ACACIA wameanza kulipa au bado?
Vipi kishika uchumba na urafiki mwema ?
Africa is A Capital Risk Continent.. kama utaki basi nakuacha ulivyo ukisubiri mtukana Mh.Lissu
 
Wakuu, itifaki imezingatiwa.
Ndio, umuhimu wa kusikia upande wa siri-kali kutoka serikalini... Upo

na kuongeza haya kwenye kaya....

Isitishe mazungumzo yanayoendelea
Deni la 1billion na ushee liwepo pale pale
...na kwa jeuri hiyo hiyo, badala ya kutoitambua tu hiyo acacia, wabatilishe makubaliano yote toka mwanzo.

Lazima Watanzania tuendelee na Jeuri ama tutaendelea "...kuchezewea kweli kweli,tumechezewa sana,.."

Pascal, asante kwa kutujulisha Watanzania wenzako, matumaini maswali ambayo yamejitokeza kutokana na hizo " t.t.t" s yanadhihirisha mapungufu,na nyufa katika "mkataba" wa awali na hawa Acacia...vijikandarasi. kwani wanaendelea kwa kejeli pamoja na jeuri wakijuwa kuwa wametukaba sehemu...hatari sana hawa na wanahatarisha Usalama wa Taifa letu.

Ndio, na nitarudia Hao Acacia wanataka kusababisha hisia zisizo na maslahi kwa Taifa letu na hivyo kuhatarisha Usalama wa Taifa letu kwa kusambaza yasiyo ya kweli, au yasiyothibitika.

Wafungishwe virago. Deni libaki pale pale. "...Dhahabu haiozi.." tutajua mbele kwa mbele lakini hawa sasa basi....sisi Ashoka!
Eti tutajua mbele kwa mbele! Usifanye decision ukiwa umefurai sana au ukiwa umechukia sana
 
Mkuu SYLLOGIST, sisi Tanzania wastaarabu sana, ukiisha samehe, umeisha samehe, deni la dola bilioni 190 tumeisha samehe kwa ahadi ya kifuta machozi cha dola milioni 300. Sasa tunachosubiri ni dola milioni 300.
P.
Wastaarabu? Tutaendelea na uzi ule ule? wa kusameheana kwenye rushwa za ajabu Hakika hakuna kijana atakaye kuwa mstaarabu wakijua tuna staarabikaa na hizi millioni mia tatu, historia itatuumbua.

Nafikiri tumepiga hatua kubwa kama nchi, na tuendelee kusimama kidete na maamuzi magumu ya Mh. Raisi. Hakika ni magumu, na nina uhakika maswali kama hayo ambayo umeuliza amejiuliza, anayafanyia kazi.
Wanatapatapa, tatcicts hizo wamejaribu huko mashariki mwetu na kusini mashariki, na bado wanavurundana. Akashia si lolote wala lelote bila dhahabu ya Tanzania, na ni pamoja na Bariki.
 
Eti tutajua mbele kwa mbele! Usifanye decision ukiwa umefurai sana au ukiwa umechukia sana
Mkuu, hayo ni yako. Sina uwezo wewote wa kufanya maamuzi kama hayo, ila kama mwananchi, nina wajibu wangu wa Kikatiba kunyoosha kidole,

Ninao wajumbe, madiwani, wabunge niliowapigia kura yangu, na hivyo chukulia hili kama mbiu yangu kwao, kwa niaba yangu binafsi na mtanzania yeyote mwenye jeuri na kutambua kuwa nyakati zimebadilika.
SIkuwa na jazba hizo.
Aluta Continua
 
Ha ha ha Paye,holdholding tax,levy,vat etc zote acacia wamelipa kwa kutumia hilo jina
Dse si wamesajiliwa?
Kama acacia hawajawahi kufanya malipo ya aina yoyote TRA na kupewa receipt kuonyesha kuwa Acacia wamelipa Tsh..... Nitaiunga mkono serikali kuikana Acacia.
 
Wakichelewa watamkuta Magufuli keshanunua mtambo wa kusafisha dhahabu hapahapa ndani; kama amewezea kununua madege 7 kwa mpigo atashindwa kweli kujenga smelting plant moja? Yeye mwenyewe akiwa mkemia. Watakuja kumbuka shuka wakati kumekucha na bulldozer keshabomoa chumba cha kulala.
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali, hawa Barrick wanaitangaza vibaya Tanzania kwa kusema kuwa Tanzania is Considered a higher risk",na kuwa mgogoro wa "Acacia Mining reflects Tanzania risk". Jee ni Kweli?. Kama Sii Kweli jee tukanushe kwa kuusema ukweli au tuendelee kujinyamazia na kumuachia Mungu?.

Uongo ukisemwa na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, sio tuu unaweza kuonekana kama ndio ukweli, bali unaweza kabisa kugeuka kuwa ukweli kwa sababu baadhi ya kauli huumba!.

Maneno haya ni matamshi wa Bosi wa Barrick kwenye interview na shirika la habari za Uingereza Reuters kuhusu mgogoro wa Acacia ambapo siku ya Jumapili iliyopita, licha ya kuwa sio siku ya kazi, lakini siku hiyo, inasemekana serikali yetu iliziandikia barua migodi mitatu ya Acacia nchini kuiambia kuwa serikali haaitambui Acacia, hali iliyoilazimu kampuni mama ya Barrick, kutoa offer ya kununua hisa zote za Acacia, hivyo kuifungisha virago, na kutekeleza yale makubaliano na serikali yetu.

Kabla sijaendelea, naomba kukiri nimekuwa inspired na bandiko hili
Mkuu Winnerian, asante kwa taarifa hii.
Kiukweli sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana!, huyu mtu anatutangaza vibaya hivi kimataifa kuwa Tanzania ni higher risk nation for investors, halafu watu humu wanashangilia!.

Taarifa hii kaitolea Reuters na sio kwenye haya magazeti yetu ya kufungia maandazi.
What does this tell about our nation to the rest of the world as far as investment climate is concerned?.

Hoja kuu ya bandiko hili, hawa jamaa wanasema vibaya, wanatungaza vibaya ulimwenguni, jee ni kweli sisi Tanzania tuko Considered a higher risk kwenye investments?. Kauli hii ina maana gani kwa investors?.
Jee ni kweli the situation ya Acacia Mining in reflects Tanzania risks?

Naomba kuziweka hoja zangu in number formats ili iwe rahisi kueleweka, na mtu ukiuliza, uweze kuuliza kuhusu specific kipengele.

  1. Ila naomba kutoa angalizo muhimu kwa serikali yetu, hii saga yote ya Acacia na Barrick, mara kimepanda, mara kimeshuka, to me it looks like a game that people plays. Hawa ni baba na mwana, na huu ni mchezo tunachezewa, the bottom line ni lile deni letu la kodi kutoka US$190 bilioni hadi just $300milioni, this is peanut, ila tukiamua kuiita ndio a win win situation for the sake ya uzalendo kwa uwezo wa viongozi wetu ku negotiate, then Watanzania tutawakubalia, na kujifunza somo kuwa na wanasheria nguli tuu peke yake bila watu ambao ni negotiators, hakutoshi. Japo tutapata 16% na kugawana 50/50 za economic benefits, mimi naona kama hapa tunapigwa mchana kweupe huku tunajiangalia.
  2. Kama sasa tunaanza kuchafuliwa na huku makubaliano ya mwisho hayajasainiwa, naona kama vile tunanyanyaswa, kusimangwa na kunyanyapaliwa wakati dhahabu ni yetu, sisi wenye mali tuko kimya tunafanya mambo kimya kimya, halafu wavunaji wa rasilimali zetu wao ndio kila siku press release, na press conferences Toronto na London, hiki kimya chetu kinaashiria nini?.
  3. Msingi mkuu wa yote haya ni mgogoro wa makinikia. Tulizuia makontena ya mchanga, kwa sababu tulihisi tunaibiwa kwa kutokujua kilichomo ndani ya mchanga ule, tukaunda tume mbili kuchunguza, tukajiridhisha kuwa ni kweli tunaibiwa na TRA wakaja na figure ya dola bilioni 190. Ili tuthibitishe madai yetu ya tunaibiwa nini, ilibidi ule mchanga uchenjuliwe ndipo tupigiane hesabu za kweli. Kitendo cha kusamehe deni la dola bilioni 190, kwa kifuta jasho cha dola milioni 300, kinaeleweka kwa wenye akili wote kuwa kule kwenye majadiliano, tumeshindwa kuthibitisha hicho kiwango cha dhahabu. Maadam makinikia bado yapo, tunashindwa nini kuyachenjua na kuwathibishia?. Mpaka sasa, sijasikia tena kuhusu ununuzi wa kichenjulio, kiukweli mchanga ukiondoka bila sisi kujua kilichomo, sio tuu nitashangaa bali, bali kiukweli kabisa nitaamini sisi Watanzania .... naomba nisimalizie
  4. Hitimisho.
    Watanzania wote wazalendo wa kweli wa taifa hili, tumuunge mkono rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli katika vita vya kulinda rasilimali zetu dhidi ya mabeberu, na kama una jicho la tatu la kuangazia visivyoonekana na wenye macho mawili tuu, then share what you see which others don't see so that we can all see, kwenye hili, la mgogoro wa makinikia, kuumaliza bila mchanga ule kuchenjuliwa tukajua kilichomo, hili ni kosa kubwa tutafanya kwa sababu, tuliuzuia mchanga kwa kuhisi tunaibiwa kwa sababu hatujui kilichomo, tukiumaliza huu mgogoro bila kujua kilichomo, tutakuwa tunafanya makosa makubwa kwa sababu tutaendelea kuibiwa.
  5. Mwisho. Kwangu mimi kwenye hili, I feel there is either something fishy or there is something wrong with us somewhere somehow katika uelewa wa haya mambo, dawa pekee ni kwa pande zote lets come clean, honest, truthfully, na very transparent ili ku establish trust kwa pande zote ikiwemo kwa sisi Watanzania kuamini serikali yetu kuwa its doing the best kwa nchi yetu Tanzania na kwa Watanzania, hivyo namaliza kwa kuuliza tena hili swali, huku kwa Baarick kututangaza vibaya, Jee ni kweli?. Kama ni kweli, hatuna jinsi tujikalie kimya, lakini kama sii kweli jee Tanzania tuendelee kujinyamazia kimya huku nchi yetu ikichafulia kimataifa kwa upande wa uwekezaji kwa kuwachia Mungu, au tukanushe kwa kuusema ukweli ili dunia iujue ukweli kuhusu nchi yetu.

    Mungu Ibariki Tanzania,
    Jumatatu Njema.
    Paskali
Jamani hawa tunaowaita mabeberu wa Ulaya wamewekeza matrilioni ya pesa zao kufukua mawe yaliyoumbwa na Mungu sio CCM wala serikali yake iliyoyaweka huko ardhini.

Ndio maana babu zetu hawakujua kazi yake mana wao nao walikuja wakayakuta sio asili yao wala hawakua na kazi nayo.
Wamekuja wakoloni weusi wasio na mtaji hata mia zaidi ya mashati yao ya kijani na figisu za Uchaguzi wamejilimbikizia utajiri mkubwa unaokaribiana na hao mabeberu na ugomvi wao uko hapo .
Sioni manufaa ya kuwaibia wazungu mitaji yao Wakati tumepewa Mgodi uliojengwa vizuri wa Tulawaka hakuna kilichofanyika unajifia tu.

Nyerere alimfukuza mzungu mmoja aliyesema tu kuwa serikali ameiweka mfukoni matikeo yake alifukia vifaa vyake vyote ardhini na kuondoka zake na mashimo yake mpaka leo hakuna anayeweza kuyachimba. Hawa watu wana mambo Fulani ya haki wanayotenda ndio maana Mungu amewapa maarifa makubwa sana.

Waafrika tuna roho mbaya sana.
Gesi inajifia kwa sababu za roho zetu za kwa nini.
Kuwekeza kwenye kisima kimoja cha gesi ni matrilioni ya Pesa lakini mtu anakuja tu analeta figisu mradi unakufa na haueleweki.
Mwishowe wachina watachimba mitaro ardhini na kuibeba tunabaki tukishanga kama majoka ya mdimu yanayolinda ndimu Wakati hayali ndimu.

Haiwezekani kugawana faida 50/50 ukapata wawekezaji bila kuwapa kwanza grace period ili walinde mtaji wao wa matrioni.
Kama turakua na watawala wanaoangalia maslahi yao tu bila kujali mitaji ya wawekezaji hatutapata wawekezaji zaidi ya Wachina wanaokuja kuwekeza kwenye viti vya plastiki, juisi, mikeka , masufuria na vikombe na vifungashio.

Dunia sasa hivi ina madini mengi sana.
Kuna zaidi ya aina 100 za Germistone duniani na wenzetu wanayatumia kwa wanavyojua wenyewe Wakati sisi hatuna matumizi nayo leo zaidi ya kuota kesho.

Naamini kama sio Mkapa Tanzania isingepata mwekezaji wa maana.
Tafuteni taarifa kwa watu wa chini sio kwa watawala.
Nendeni vijijini hasa Yale maeneo yaliyowahi kukaliwa na wakoloni wazungu ndio mtapata picha halisi ya uwekezaji na uchekeshaji wa wakoloni wa leo tunaowaita majina mazuri kama waheshimiwa watawala.

Tunataka tuuze malighafi iliyoko ardhini kwa bei ya bidhaa tunajidanganya na kudanganywa sana ili tuwasifu wasaka madaraka.
Gharama ya kuipata hiyo malighafi ni kubwa mno .

Kama serikali inaona kuwa kuna soko holela tu la dhahabu na madini mengine kwa bei unayotaka basi wanapoyachimba serikali iyanunue yote kama ilivyofanya kwenye KOROSHO iuze ili ipate mapesa. Tena madini hayaharibiki .
Tafakari!!
Awamu hii siasa kwanza uchumi baadae.

Jiulize tena ; Kwa nini Serikali isiuze MADINI ya matrilioni ya pesa kwenye hayo MAKINIKIA kama Walivyotuaminisha, kisha wakachukua Tril . 400 tunazowadai tukagawiwa Noah zetu. Hela zinazobaki wakawarudishia Wadeni wao.
Kama unamdai mtu kwa haki kabisa, kisheria unaruhusiwa kuuza Mali yake na kuchukua Deni lako kinachozidi unamrudishia mdeni wako.
Tafakari!!

Awamu hii ni madaraka kwanza uchumi wa nchi baadae. Kuwadanganya watanzania kwa lengo la kupata kura kisha baada ya 2020 watarudi kwenye uhalisia baada ya kuwavuruga vuruga wasomi,wanasiasa,asasi za kiraia ,wafanyabiashara ,mashirika ya dini ,wafanyakazi n.k ili kundi kubwa la watu wa vijijini na wasiotafakari kwa umakini wawapigie kura bila ufahamu wa kutosha kupitia propaganda hewa za uzalendo(usio na tija) na kulinda rasilimali za nchi .
 
Mindset yako ni ya kinyonge sana; ndiyo hiyo ya wailing to be enslaved! Mbona hawafanyi hivyo kwa China na mpaka leo China imeweza kushindana nao? Kama hukumbuki, miaka 25 iliyopita China ilikuwa maskini sana, na waliyakaribisha makampuni ya Magharibi kwa masharti kama haya haya ya Magufuli, ndiyo maana wamenyanyuka na kuwa washindani wakuu leo.
 
Mimi bado nasubiri Noah zetu, haya mengine sijui!
Mkuu Mbinguni Kwenu, maadam kwenu ni Mbinguni na hapa Duniani ni mapito tuu, then hiyo Noah yako endelea kusubiria tuu na utasubiri sana, mwishowe utakutana nayo kwenu na kuendeshea barabara za huko.
P
 
Wakichelewa watamkuta Magufuli keshanunua mtambo wa kusafisha dhahabu hapahapa ndani; kama amewezea kununua madege 7 kwa mpigo atashindwa kweli kujenga smelting plant moja? Yeye mwenyewe akiwa mkemia. Watakuja kumbuka shuka wakati kumekucha na bulldozer keshabomoa chumba cha kulala.
Mkuu Kichuguu, hili la kuchenjua, ndio neno, na hapa ndipo wizi ulipolalia, tunaibiwa katika makinikia kwa sababu hatujui kilichomo, na bila kuchenjua hatuwezi kujua.

Siku ya kwanza Boss wa Barrick anakuwa kumuona Magufuli, alizungumzia kutujengea kichenjulio, mwisho wa mazungumzo sijasikia tena kuhusu kichenjulio, bali alia hiding kutupa zawadi ya dola million 300 za nia njema ambazo zinatosha kujengea kichenjulio.
Hivyo niliuliza

P
 
Mkuu, hayo ni yako. Sina uwezo wewote wa kufanya maamuzi kama hayo, ila kama mwananchi, nina wajibu wangu wa Kikatiba kunyoosha kidole,

Ninao wajumbe, madiwani, wabunge niliowapigia kura yangu, na hivyo chukulia hili kama mbiu yangu kwao, kwa niaba yangu binafsi na mtanzania yeyote mwenye jeuri na kutambua kuwa nyakati zimebadilika.
SIkuwa na jazba hizo.
Aluta Continua
Kumbuka ata rais ulimpigia kura lakini kuna pesa ambazo mpaka sasa hatuna majibu zilipo na zimetumika je. Aya si yangu ila niya ripoti ya CAG ..vipi umemyoshea kidole mbunge na Rais wako kuhusu ili?
 
Back
Top Bottom