Barrick yadaiwa kuwanyanyasa wafanyakazi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barrick yadaiwa kuwanyanyasa wafanyakazi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Aug 14, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h] MENEJIMENTI ya Kampuni ya Barrick Gold Mining ambao wanaendesha mgodi wa Bulyanhulu, imetupiwa lawama ikidaiwa kupindisha sheria za nchi na kuwafukuza wafanyakazi kinyume na utaratibu. Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo ambao walifika jijini Dar es Salaam ili kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walijikuta wakiachishwa kazi mwaka 2007 baada ya kugundulika kupata ugonjwa wakiwa kazini. Wakizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wafanyakazi watatu wa kampuni hiyo, walisema kuwa menejimenti imekuwa ikitumia kigezo cha ugonjwa, na kupeleka majina katika Bodi ya Tiba na kisha kuwaachisha kazi. Wafanyakazi hao ambao wanakabiliwa na maumivu makali ya magonjwa yaliyotokana na kazi walizokuwa wakizifanya, walisema kuwa Barrick hutumia nafasi hiyo ili kukwepa kulipa fidia inayohitajika kimataifa. Baadhi ya wagonjwa hao wanahitajika kufanyiwa upasuaji, na mmoja anatakiwa kupelekwa nje ya nchi kutokana na kukosekana wataalamu nchini, lakini wameendelea kutaabika pasipo kuelewa hatima yao. Mmoja wa wagonjwa hao ambaye amepangiwa chumba katika Hoteli ya Durban, Khalfan Lukensa, alisema kuwa alipata matatizo ya kuziba kwa njia ya hewa pamoja na kuvuja damu sehemu za siri baada ya uti wa mgongo kuathirika kutokana na kuendesha mashine nzito. “Unajua nilianza kusikia matatizo ya kiafya mwaka 2006, lakini ilipofika 2009 yalizidi, nilikuwa naendesha moja ya mashine iitwayo Scoop,” alisema. Alisema daktari wa kampuni aliamua kumwandikia rufaa na kuja Muhimbili na baada ya vipimo aligundulika kuwa aliathirika katika mfumo wa hewa na uti wa mgongo, hivyo kutakiwa kupelekwa nchini India katika Hospitali ya Bangalore kwa ajili ya upasuaji. Alisema cha kustaajabu, alibaini taarifa za kopi ya ripoti yake kuibwa na kubadilishwa, ikawapo iliyoonesha kuwa tatizo lake alilipata tangu awali akiwa hajaajiriwa katika kampuni hiyo. “Walifanya hivyo ili kukwepa gharama, maana ninatakiwa kulipwa hisa tano na kunitunza hadi kifo, kwani kuna mfano wa mzungu mmoja (anamtaja) alipata tatizo kama langu, hadi sasa analipwa na kutunzwa, na walimgharamia tangu yupo hapa hadi aliporudi kwao,” alisema. Alisema kuwa hadi sasa hajui hatima yake, na madaktari walimweleza kuwa iwapo upasuaji hautafanyika kwa haraka,

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
Loading...