Barrick wamekubali kulipa malipo ya madai yote muhimu ya kodi ya awali, faida watagawana na Serikali 50/50 na mengine mengi

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
210
250
Wenzangu wapendwa,

Kufuatia uamuzi wa mahakama leo, Acacia Mining Plc na shughuli zake sasa zinakuwa sehemu ya Barrick Gold Corporation na tunawakaribisha katika familia yetu. Barrick ilidhamiria kupata hisa zote ambazo hazikuwa zake katika mpango ulioidhinishwa na mahakama ambayo ilipanga utaratibu kwamba wanahisa wachache wa Acacia kama onyesho la kujiamini katika uwezo wa mali za kazi za Acacia, jiolojia ya nchi, nchi yenyewe, na watu wake. Tunaamini kabisa kuwa tunaweza kusimamia rasilimali vizuri kama sehemu ya Kampuni kuu na kwa pamoja na Serikali ya Tanzania kama mbia mwenye asilimia 16 ya hisa, kuliko utaratibu wa Soko la Hisa la London uliokuwepo hapo awali.

Katika mchakato wa kujadili utaratibu huu mpya, Barrick na Serikali ya Tanzania walikubaliana kuwa na mfumo ambao utaonyesha mgawanyo sawia wa 50/50 katika faida za kiuchumi kutoka katika shughuli hizo, na pia kuhusika moja kwa moja kwa Serikali katika kusimamia rasilimali kupitia kampuni maalum ya usimamizi, na malipo ya madai yote muhimu ya kodi ya awali.

Tunatambua kwamba hapo awali Acacia haikuweza kusimamiwa vizuri, jambo lililopelekea kusitishwa kwa leseni yake ya kufanya kazi nchini Tanzania, huku jamii, makundi toka kada mbalimbali, na viongozi wa kisiasa wakitaka migodi ya Acacia ifungwe na/au usimamizi wa Acacia ulibadilishwe kwa nguvu. Ingawa Barrick ilikuwa mbia zaidi wa Acacia, haikuwa na udhibiti wa usimamizi wa Acacia kupitia ugumu wa kanuni za uuzaji wa hisa kwa makampuni yaliyo orodheshwa wenye soko la Hisa za London. Kufuatia hali hiyo, Barrick iliamua kuchukua hisa ambazo ilikuwa haizimiliki, na kama mbia mkuu wa Acacia mwenye nafasi ya kwanza, ilichukua jukumu la kurekebisha kasoro zilizokuwepo hapo awali.

Kwa pamoja tutarekebisha hali hii kwa kusimamia mali za sasa kwa lengo la kuongeza thamani kwa wadau wote - pamoja na wanahisa, jamii, wafanyakazi na nchi kwa ujumla. Hatutakubali tabia yoyote isiyofaa au isiyo na uwajibikaji na tunakusudia kwa mara nyingine kuona fahari tena kufanya kazi na kampuni inayoonekana kufaidisha wadau wote. Timu yangu ya watendaji na mimi mwenyewe tumejipanga kufikia malengo haya kwa asilimia 100.

Ili kujenga upya shughuli na hadhi ya madini katika jamii itahitajika kufanya kazi kwa bidii na, katika mazingira mengine, kufanya maamuzi magumu. Shughuli na miradi yetu iliyo Tanzania itakuwa sehemu ya Barrick ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati na itawajibika kupitia kwa Willem Jacobs (COO) na timu yake ya wakuu wa Kanda. Tunakusudia kutolegeza nia yetu ya kutaka uwajibikaji wa kila mtu katika harakati zetu za kuwa darasa la ulimwengu. Tutawapa thamani kubwa wataalamu wa jiolojia, wahandisi, wapangaji na wasimamizi kuwa salama, wabunifu, wafanisi na wazalishaji katika kila kitu wanachofanya kila siku, kulingana na maadili yetu.

Ninawakaribisha katika familia ya Barrick na ninatarajia kukutana nanyi kwenye safari zangu zijazo za kiutendaji. Tunafurahi kulifunga jambo hili na tumejitolea kuufanya mradi huu ufanikiwe kwa wadau wote.


Mark Bristow
President and CEO of Barrick
Screen Shot 2019-09-15 at 15.21.37.png
 

Attachments

  • File size
    221 KB
    Views
    9

kapongoliso

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,341
1,500
Hivi tunaelewa lakini maana ya economic benefit au faida ya kiuchumi? Au tunajitia upofu na kushangilia kil ujinga
 

kapongoliso

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,341
1,500
Tumeliwa sana kuliko hats mwanzo mfuatilieeni Zito anafafanua vizuri sana tulivyoingizwa mkenge
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom