Barrick Wajibu Mapigo ya Acacia, Take It or Leave It. If You Take, You Get Something, If You Leave It, You Get Nothing!. Hawaongezi Hata Sentano!

Hawa viumbe wenye nywele za KUTELEZA(wazungu) Wana akili mno wanajua wanachokifanya kama Mali wameshachuma vyakutosha na wameshiba kilichopo hapa ni maongezi ya baina ya ndugu wawili.

Mzugu gani Fala atakuja kulipa hizo pesa za kishika uchumba?
 
Wanabodi,

Hii ngoma ya mvutano wa bei ya Acacia kati ya baba na mtoto, inaendelea, Barrick anasema, taarifa ya Acacia, haina chochote kipya ambacho Barrick walikuwa hawajakijua, hawataongeza hata senti tano!.

Barrick continues to believe that the terms of its Proposal (as defined in the Barrick Announcement) reflect the fair value of Acacia, not taking into account any further discount which could be applied to reflect the significant risk inherent in the Acacia business and remaining uncertainties of any settlement with the Government of Tanzania. In the absence of a take-private transaction, Barrick does not consider there is any credible alternative solution which will preserve, to the extent possible, value for all stakeholders. Barrick has considered the statements made in the Acacia Announcement and has concluded that the Acacia Announcement contains no information of which Barrick was not already aware. Barrick therefore remains firmly of the view that certain assumptions made by Acacia in relation to its mine plans are not appropriately risked or supportable and that adjustments should be made

Mgogoro wa Baba na Mtoto, alianza kama ifuatavyo
  1. Rais Magufuli alisimamisha kusafirisha mchanga wa makinikia ya dhahabu baada ya kuhisi tunaibiwa.
  2. Akaunda tume mbili, zikathibisha ni kweli tunaibiwa, TRA wakapiga hesabu ya tulichoibiwa, bili ikaja tunawadai Dola bilioni 190, fedha inayotosha kumnunulia kila Mtanzania gari aina ya Noah.
  3. Baba wa Acacia, Barrick akaingilia kati, tukafanya mazungumzo, yalipofika katikati, Barrick akaahidi kutulipa kishika uchumba cha dola milioni 300, wakati tukijadiliana jinsi ya kulipa mahari kamili ya ile dola bilioni 190.
  4. Mazungumzo yalipofika mwisho, serikali yetu ikaamua kwa nia njema kabisa, kuwasamehe Acacia lile deni kubwa la bilioni 190, na badala yake, sasa tutalipwa kifuta machozi cha kile kishika uchumba cha dola milioni 300.
  5. Acacia itavunjwa na kuundwa kampuni mpya ya ubia, na Tanzania, ambapo tutamiliki hisa za asilimia 16%
  6. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, 50/50.
  7. Kabla Acacia hajapelekewa mapendekezo haya, Serikali ikaziandikia barua migodi mitatu ya Acacia kuwa haiitambui Acacia, hivyo kuokoa jahazi, Barrick akaonyesha nia ya kuinunua Acacia kwa fedha kiduchu, kwa kuwagaiya wanahisa wote wa Acacia hisa za Barrick.
  8. Acacia akagoma kununuliwa kwa bei kiduchu, hivyo Barrick wakaomba muda zaidi kabla hawajatoa bei ya mwisho, Acacia akakubali kuipa muda zaidi Barrick wapandishe dau.
  9. Barrick, akamwaga ugali hadharani kuwa wametoa dau dogo kwa sababu Acacia haina thamani kivile, na bado ni very risk.
  10. Baada ya Barrick kumwaga ugali, Acacia akakasirika, na yeye akamwaga mboga, kwa kujionyeshea ana thamani kubwa sana hivyo Barrick lazima aongeze dau.
  11. Ndipo leo Barrick kajibu mapigo kuwa hakuna kipya chochote Acacia alichokisema, hawataongeza hata senti tano.
  12. Tarehe ya mwisho kwa Barrick kutoa offer rasmi ni tarehe 9 Julai.
  13. Kesho Acacia watajibu mapigo haya.
  14. Hizi piga nikupige kati ya baba na mtoto zinaendelea.
  15. Swali ninalojiuliza huu ni ugomvi wa kweli kati ya baba na mwana, au wanajuana, kuna game fulani inataka kuchwezwa?.
Mnaweza kufuatilia kwa karibu huku
Response to Acacia’s announcement - June 26, 2019

P
All in all Tanzania remains determined to enforce, and is actually enforcing, ammendments in the Mining Act with or without Barrick/Acacia deadlock negotiations.

In view of that Tanzania has nothing to loose after having been "shamba la bibi" for decades.

Barrick/Acacia waache watafunane na madini yetu yatabaki palepale mpaka hapo kizazi kingine kitakapoona kiko tayari, kiuwezo, kuchimba kwa faida ya Watanzania.
 
mwengeso wewe acacia anaendelea kuchimba na wewe unatwambia madini yanabaki!
 
Kama anaendelea kuchimba ni kwa masharti ya mkataba mpya ukizingatia marekebisho ya Sheria ya Madini. Kwa msingi huo amefyata mkia.
Acha kusema uongo wa wazi; lini ACCACIA wameitwa kusign mkataba upya kutokana na marekebisho wa sheria mpya? uliisoma hiyo sheria kua inaanza kufanya kazi.lini na kwa mazingira gani? acha kuleta ushabiki.
 
Sina tatizo na taarifa zilipotoka, mbona hata mkuu Pascal Mayalla ameweka source ya taarifa hizo? Mimi naongelea hilo Saga jinsi linavyochezwa, halichezwi katika ustaarabu wao bali wa kwetu.
Naweza sema ujasusi wa kiuchumi unatumika utupoteza kutokana ulelew wetu mdogo katika maswala haya. But acacia na barrick are just company names owned by different people of the same mission and vision all of them are Investor and are looking for supper proft, tunapoteza muda wetu bure kuwakataa acacia na kuwataka barrick.
 
Mkuu, Swali ulilouliza kwenye kipengele cha 15 liko wazi kabisa, Barrick na Acaccia ni fungu moja lililogawanywa kimkakati ili kujinufaika kibiashara katika huu mradi wa uchimbaji madini ndani ya bara Africa.

Ikumbukwe kuwa mbinu hizi za kibiashara zilianza pale walipoanza kuchimba madini hapa Tanzania na baadaye kuja na mkakati wa kuuza hisa zake kwenye soko la LSE, kama African Barrick. Nakumbuka jinsi ununuzi wa hisa zake za awali kwenye soko la LSE ulivyokuwa na utata kwa mwekezaji wa kitanzania aliyetaka kununua hisa za African Barrick akiwa Tanzania mimi nikiwa mmoja wao.

Alichofanya Rais ni sahihi kabisa na muda ukifika wataumbuka wote wawili, tunatakiwa tuwe macho katika kila hatua ya sarakasi wanazofanya sasa, ni maigizo tu ambayo mwisho wake ni kunyoosha mikono.
 
Naweza sema ujasusi wa kiuchumi unatumika utupoteza kutokana ulelew wetu mdogo katika maswala haya. But acacia na barrick are just company names owned by different people of the same mission and vision all of them are Investor and are looking for supper proft, tunapoteza muda wetu bure kuwakataa acacia na kuwataka barrick.
Well spoken, you nailed it.
 
Kama nchi tuache ufara tuwaulize waliosababusha yote Haya ni kina Nani na kama walikufa makaburi yao yapigwe pingu na viboko hapa ndipo tunaona tofauti na baba wa Taifa na hawa madalali waliotangulia . Makampuni yanashinda kuzimuni kisa mali tulizopewa na mwenyezi Mungu
 
Mbona umeandika kishabiki sana? Hizi lugha za mabavu ni za serikali hii usiwasumbue wasiojua kiingereza kuhangaika
 
Kama anaendelea kuchimba ni kwa masharti ya mkataba mpya ukizingatia marekebisho ya Sheria ya Madini. Kwa msingi huo amefyata mkia.
mwengeso, , sheria mpya ilisema wazi kabisa haitagusa makubaliano ya nyuma
 
Ni kweri mkuu
Kama nchi tuache ufara tuwaulize waliosababusha yote Haya ni kina Nani na kama walikufa makaburi yao yapigwe pingu na viboko hapa ndipo tunaona tofauti na baba wa Taifa na hawa madalali waliotangulia . Makampuni yanashinda kuzimuni kisa mali tulizopewa na mwenyezi Mungu
 
Hawa jama Accacia wasije wakawa wanataka kutupandisha hasira tuharibu watupeleke mahakamani ili wapate zaidi ya dau la Barrick. tukae macho
 
Wanabodi,
Hatimaye huu mtanange wa Acacia kununuliwa na Barrick, hatimaye umefika mwisho jana, kwa Barrick kutoa tangazo la kuinunua Acacia, na Acacia kutoa tango la kukubali kununuliwa na Barrick.

Tangazo la Barrick la Kifo cha Acacia ni Hili
PRESS RELEASES
Recommended Final Offer For Acacia Mining Plc By Barrick Gold Corporation – July 19, 2019

Tangazo la Acacia kukubali kununuliwa na Barrick ni hili

Hii maana yake ni
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
Huu ndio utakuwa ushindi wa kwanza wa kishindo wa rais Magufuli na awamu ya Tano kwa kuanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini.
Hongera Kabudi, Hongera Magufuli, Hongera Watanzania, ila kwenye makinikia, bado kuna lakini!.
Leo tupongezane kwanza, lakini tuzijadili baada ya kusainiwa makubaliano yenyewe!.
Paskali
 
Back
Top Bottom