Barrick to construct a road from Bulyanhulu to Mwanza according to the contract signed today

Hadi mtaji urudi si leo. Kiufupi sisi tumekubali maana wangeenda mahakamani tungepoteza sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Barrick Wana migodi 47 duniani kuanza kushitakiana na ka nchi Kama Tanzania nikujidhalilisha ndio maana wamekuwa waungwana, makubaliano ya Leo tu ndani ya robo saa hisa za barrick newyork zimepanda
 
and will also commit up to $40 million to upgrade the road between Bulyanhulu and Mwanza as well as constructing a housing compound and related infrastructure.
Sentensi kama hizi zinazoachwa zinaning'inia; ndipo mahali pa kupigia hapo!
 
Hapo kwenye "After recoupment of capital investments" ndipo kuna mambo kwani inavyoonekana Tanzania haitachangia chochote kwenye huo uwekezaji.

Wewe hauna stake yoyote kwenye mtaji lkn unapewa hisa za bwerere 16% halafu eti tena faida mnagawana pasu...!!! Hapo kwenye gharama za uendeshaji hizo ambazo huchangii lazima uliwe tu.

Kipindi fulani niliiwahi kuona orodha ya suppliers wa Barrick North Mara ilikuwa ni orodha kubwa mno kutoka ndani na nje ya nchi kitu kinachoonyesha kuwa kwenye mining industry operating expenses ni nyingi mno na pia kampuni ya uchimbaji ina uwezo wa kucheza na hao suppliers ili ku-inflate bei za bidhaa na huduma na isitoshe sisi bado hatuna qualified personnel in this complex industry, lazima tu tutakuwa 'Shortchanged'.

Hapa there will be nothing to smile about.
Shemu pekee itakayoleta tofauti ni ongezeko la mrabaha na 16%.

16% ipo kwenye divident wakati makampuni mengi makubwa ya uchimbaji madini hayatoi dividents. Faida kubwa kwa wanahisa wa makampuni ya madini ni kutokana na mauzo ya shares wakati zinapokuwa zimepanda. Kwa mfano tangazo hili tu la kusema Barrick imefikia maafikiano mazuri na serikali ya Tanzania, hisa za Barrick zitapanda, na baadhi ya wanahisa watauza hisa zao na kutengeneza faida. Kwa bahati mbaya serikali haitaziuza hisa zake kipindi chote, na hivyo kutokufaidi faida itokanayo ya kuongezeka thamani kwa hisa zake.

Jambo la pili, hata kama watatoa gawio, itakuwa ni baada ya muda mrefu maana kwenye migodi uwekezaji huwa ni mkubwa na haukomi. Bahati mbaya gawio ni mpaka baada ya Barrick kurudisha pesa yake aliyowekeza. Atarudisha lini wakati uwekezaji unaendelea? Ndiyo swali la msingi.

Namwona Mwenyekiti mpya ambaye amepatikana kwa gharama kubwa sana toka Randgold, kwa mara nyingine, akifanikiwa kuonesha weledi wake wa kuweza kufanya kazi katika mazingira ya Afrika na kutengeneza faida kubwa, kama Barrick walivyotarajia. Barrick wamehangaika sana kumpata huyu bwana. Na inaonekana kuhangaika kwao haikuwa kazi bure.

Barrick katika hili wamefanikiwa sana kuliko hata mazingira ya mwanzo. Sasa wataweza kuipata hata miradi ambayo zamani wasingeipata. Maana ndani ya Barrick, sasa ipo serikali.

Kule kusakamwa kuwa mara Barrick wametiririsha maji ya sumu, mara Barrick wanawaonea wafanyakazi wazalendo, mara Barrick ni majizi na mabeberu - yote hayo sasa wameyashinda. Yamefikia mwisho. Hii sasa ni kampuni yetu. Kampuni ya Taifa letu inayobeba nembo ya Taifa, TWIGA. Mwenye kutaka kuihujumu kampuni hii kwa namna yoyote ile, anaihujumu kampuni ya serikali, atakuwa analihujumu Taifa. Na anayelihujumu Taifa amekosa uzalendo.

Hakika mazingira ya sasa, yatakuwa ya manufaa makubwa sana kwa Barrick kuliko kipindi chochote. Kwa mara nyingine tena Barrick wanaonesha uwezo wao wa kuiishi falsafa yao ya, 'Every best person must work with Barrick' . 'The biggest asset of Barrick is its people, not the machinery, not its gold in the ground, not its money in the bank, it is the PEOPLE. These are the people who have made Barrick to flourish while others were dying'. Nayakumbuka maneno haya ya Rais wa Barrick tukiwa pale Toronto, tukiwa kwenye mkutano wa wakubwa wote wa operations za Barrick Duniani kote. Kwa maneno yake ni kuwa Barrick tangu ianzishwe, kwa ujumla wake, haijawahi kushindwa kufikia malengo yake.

Kama GGM wana weledi wa kutosha, ni vema na wenyewe wakaomba kufanyiwa kama walivyofanyiwa Barrick.

Kwa ujumla, kama nchi tutafaidika zaidi na uwepo wa makampuni haya makubwa kuliko kutokuwa nao. Sawa na ilivyo - ni aheri kuwa karibu sana na mataifa haya makubwa kuliko kuwa mbali nao.

NADHANI SASA NI WAKATI WA SERIKALI KUTOA KAULI NZITO DHIDI YA YEYOTE ATAKAYETUMIA NENO MABEBERU DHIDI YA WAWEKEZAJI.
 
Asilimia inategemea na ukubwa wa namba mfano 10% ya Wamarekani milioni 300 ni watu milioni 30 lkn 10 % ya Watanzania millioni 45 ni watu ~ milioni 4, hivyo ni swala la namba, hiyo 16% ni ya kiasi gani cha fedha? Inaweza ikawa ni mabilioni ya fedha kulingana na mfano wangu wa 10% ya Watu wa USA vs 10% ya Watu wa Tanzania.

Namba hazina Siasa ,bado tofauti ya Asilimia 16 kwa 84 ni kubwa sana .
 
Hizi double standards siyo nzuri hapa Serikali tiyari imeshapigwa, huu mkataba kabla haujasainiwa kwanini wameharakisha badala ya kuupeleka bungeni kwanza ukajadiliwe kama Jinsi Mh Rais alivyojinadi kwamba ndio utaratibu hadi kupelekea Lugola kung'olewa? Yani Rais tu na wapambe wake kina Kabudi wanajifungia Ikulu na kupitisha mikataba mikubwa kamaa hii peke yao siyo Sawa! Ni suala la muda kila kitu kitajulikana na hasa utawala huu pale utakapomaliza muda wake kwa sababu sasa hivi inajulikana hakuna anayeweza kumkosoa Jiwe akabaki salama , kila mtu analinda mkate wake.

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Shemu pekee itakayoleta tofauti ni ongezeko la mrabaha na 16%.

16% ipo kwenye divident wakati makampuni mengi makubwa ya uchimbaji madini hayatoi dividents. Faida kubwa kwa wanahisa wa makampuni ya madini ni kutokana na mauzo ya shares wakati zinapokuwa zimepanda. Kwa mfano tangazo hili tu la kusema Barrick imefikia maafikiano mazuri na serikali ya Tanzania, hisa za Barrick zitapanda, na baadhi ya wanahisa watauza hisa zao na kutengeneza faida. Kwa bahati mbaya serikali haitaziuza hisa zake kipindi chote, na hivyo kutokufaidi faida itokanayo ya kuongezeka thamani kwa hisa zake.

Jambo la pili, hata kama watatoa gawio, itakuwa ni baada ya muda mrefu maana kwenye migodi uwekezaji huwa ni mkubwa na haukomi. Bahati mbaya gawio ni mpaka baada ya Barrick kurudisha pesa yake aliyowekeza. Atarudisha lini wakati uwekezaji unaendelea? Ndiyo swali la msingi.

Namwona Mwenyekiti mpya ambaye amepatikana kwa gharama kubwa sana toka Randgold, kwa mara nyingine, akifanikiwa kuonesha weledi wake wa kuweza kufanya kazi katika mazingira ya Afrika na kutengeneza faida kubwa, kama Barrick walivyotarajia. Barrick wamehangaika sana kumpata huyu bwana. Na inaonekana kuhangaika kwao haikuwa kazi bure.

Barrick katika hili wamefanikiwa sana kuliko hata mazingira ya mwanzo. Sasa wataweza kuipata hata miradi ambayo zamani wasingeipata. Maana ndani ya Barrick, sasa ipo serikali.

Kule kusakamwa kuwa mara Barrick wametiririsha maji ya sumu, mara Barrick wanawaonea wafanyakazi wazalendo, mara Barrick ni majizi na mabeberu - yote hayo sasa wameyashinda. Yamefikia mwisho. Hii sasa ni kampuni yetu. Kampuni ya Taifa letu inayobeba nembo ya Taifa, TWIGA. Mwenye kutaka kuihujumu kampuni hii kwa namna yoyote ile, anaihujumu kampuni ya serikali, atakuwa analihujumu Taifa. Na anayelihujumu Taifa amekosa uzalendo.

Hakika mazingira ya sasa, yatakuwa ya manufaa makubwa sana kwa Barrick kuliko kipindi chochote. Kwa mara nyingine tena Barrick wanaonesha uwezo wao wa kuiishi falsafa yao ya, 'Every best person must work with Barrick' . 'The biggest asset of Barrick is its people, not the machinery, not its gold in the ground, not its money in the bank, it is the PEOPLE. These are the people who have made Barrick to flourish while others were dying'. Nayakumbuka maneno haya ya Rais wa Barrick tukiwa pale Toronto, tukiwa kwenye mkutano wa wakubwa wote wa operations za Barrick Duniani kote. Kwa maneno yake ni kuwa Barrick tangu ianzishwe, kwa ujumla wake, haijawahi kushindwa kufikia malengo yake.

Kama GGM wana weledi wa kutosha, ni vema na wenyewe wakaomba kufanyiwa kama walivyofanyiwa Barrick.

Kwa ujumla, kama nchi tutafaidika zaidi na uwepo wa makampuni haya makubwa kuliko kutokuwa nao. Sawa na ilivyo - ni aheri kuwa karibu sana na mataifa haya makubwa kuliko kuwa mbali nao.

NADHANI SASA NI WAKATI WA SERIKALI KUTOA KAULI NZITO DHIDI YA YEYOTE ATAKAYETUMIA NENO MABEBERU DHIDI YA WAWEKEZAJI.
Nadhani hii imeeleweka vzur sana,hapo brother ameongelea sehem kubwa ya yaliyoandikwa kwenye mkataba..by the wale kwa wale ambao tulishindwa elewa terminologies za kibiashara katika maelekezo ya mkataba haswa neno recouping,ni meweka picture hapo chini ili tufahamu vzur maelezo yaliyotolewa na pia tujue tunabisha nini au tunabishana tu ili mradi tubishane na kuleta siasa tu... Nchi mbele mengine baadae
Screenshot_20200126-100235~3.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom