Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa Serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Minerals Corporation.

Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.

======

Baada ya mgogoro uliodumu kwa takribani miaka miwili tangu mwaka 2017, Kampuni ya Barrick na Serikali zimeunda kampuni ya Twiga itakayosimamia migodi mitatu iliyokuwa chini ya kampuni ya Acacia.

Kwenye kampuni hiyo mpya, Barrick itamiliki asilimia 84 ya hisa zote huku Serikali ikiwa na asilimia 16. Utaratibu huo ni utekelezaji wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ‘sasa amezaliwa mtoto mpya baada ya Barrick kukubali kumuua mtoto wake, Acacia.’

Mgogoro kati ya Serikali na kampuni ya Acacia iliyokuwa inasimamia migodi ya Buzwagi, North Mara na Bulanhulu ulianza mwaka 2017 na Rais John Magufuli akaunda tume ya kuchunguza mwenendo wa biashara ya madini.

Tume hiyo ilibaini ukiukwaji wa sheria, utaratibu na kanuni zilizopo hivyo kuikosesha Serikali mapato inayostahili. Kutokana na hilo, Serikali iliipiga faini ya Dola 190 bilioni jambo lililosababisha kuanza kwa mzungumzo baina ya pande hizo mbili.

Bado undani wa makubaliano/mkataba huo haujawekwa wazi hadi Mwanasheria Mkuu wa Serikali apitie mkataba wa makubaliano hadi ifikapo mwezi ujao (Novemba 2019).
 
Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa Serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Minerals Corporation. Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.

Wapi Miga!!!?
 
Mbona Serikali ina % ndogo sana kweli safari ya kunufaika na madini TZ bado ndefu
Sheria mpya ya madini ndiyo imezingatiwa. Asilimia 16 ni hisa na bado watalipa asilimia 6 ya mauzo kama mrabaha na kodi ya mapato asilimia 30 ya faida baada ya gharama zote( net profit).
 
Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa Serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Minerals Corporation. Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.
Zile Noah zetu tutapewa kabla kampuni kuanza au baada ya kampuni kuanza kazi?
 
Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa Serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Minerals Corporation. Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.
Na kasema acacia imefutwa haipo tena hapa nchini
 
Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa Serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Minerals Corporation. Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.
Hii inaweza kuwa habari njema kwa Watanzania baada ya kuporwa madinibyetu miaka Mingi..!
 
Ubia, serikali imeweka nini kwenye huo ubia? Tuanzie hapo kwanza.
Sheria mpya ya madini ndiyo imezingatiwa. Asilimia 16 ni hisa na bado watalipa asilimia 6 ya mauzo kama mrabaha na kodi ya mapato asilimia 30 ya faida baada ya gharama zote( net profit).
 
Ubia, serikali imeweka nini kwenye huo ubia? Tuanzie hapo kwanza.
Hizi dili zingine zinatia mashaka sana. Mbona wakati wa majadiliano hawakuliweka wazi, wanavizia kipindi hiki cha taharuki ndipo wanaleta hizi taarifa za ubia. Je aliwaruhusu?
 
Kuna taharuki gani? Tafadhari funguka na wengine waelewe aina na chanzo cha taharuki.
 
Sheria mpya ya madini ndiyo imezingatiwa. Asilimia 16 ni hisa na bado watalipa asilimia 6 ya mauzo kama mrabaha na kodi ya mapato asilimia 30 ya faida baada ya gharama zote( net profit).
Ongezea na 1% inspection fee (kama madini watayasafrisha nje). Kwa ujumla
1. Royalities = 6%
2. Corporate tax 30%
3. Inspction fee 1%
TOTAL CONTRIBUTION = 37%. Ambapo ktk ubia GOT inachangia "LAND" wakt wao watachangia " TECHNOLOGY na MACHINE/TOOLS.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom