Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,060
2,000
Swali ni glassi imejaa kiasi gani au imepungua kiasi gani. Toka zero shares to 16% kwa mimi layman naona tumepata kitu. Toka $190B hadi $ 300M hapo naona tumepigwa. Kwenye hizo 50% economic benefits-hakuna kikubwa kilichobadilika ukitoa hiyo 16% ya hisa. Swali jingine je 16% ndio uwezo wetu wa negotiations ulipoishia au tungeweza kupiga zaidi? Hili jibu wewe. Smelter naambiwa haimo kwenye mkataba na makinikia yataendelea kutoka kama kawa. Baba kasema hapo ni win-win situation-amua wewe ikoje hiyo. Unaweza pia ukajiuliza kelele zilizopigwa na wengine kuumizwa (achilia mbali haki za bina adamu) zinaendana na tutakachopata?
 

Onjwaria

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
926
1,000
Tuchanganyeni tu na mahesabu mnaelewa wazi haya mambo ya mikataba wengi wetu tuko mbumbumbu ila haki ya Mungu this time msije mkagusa hizo ndege
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,060
2,000
16% ni FREE CARRIED INTEREST ( FCi) japo Serikali inaweza kuziongezea kwa maana ya kununua 34% kwenye soko la mtaji zinapouzwa hisa hizo. Tanzania ni nchi ya Mfano kuweza kutunga sheria inayoifanya nchi kuanza kubakiza 16% ya hisa za makampuni yote yatakayokuja kuwekeza ktk sekta ya madini mafuta na gesi.
Kutokana na umiliki huu serikali itakuwa na Mjumbe ktk board of directors na management team kwa maana ya kujiridhisha na gharama zote za uzalishaji na matumizi mengine ili gharama zikitolewa FAIDA inagawiwa 50/50 . Nchi hii ni ya Mfano.
Tafuteni MDAs ( miming development Agreements) za kampuni mengi nchi zingine mtaona ni kwa namna gani sheria zinawapa nafasi ya mabeberu kupora maliasili zetu. Makosa yalifanyika huko nyuma lakini JPM na serikali ya Awamu ya tano wamefanya mabadiliko makubwa sana.
Watu wa Hakirasilimali wanasema hiyo 50/50 ndio imepiga nyundo ongezeko lolote, kwani kwa mkataba wao (Hisa + tozo za kodi + tozo nyingine =< 50%) hivyo itakuwa shida kuongeza hisa kwani kwa kufanya hivyo wataalamu wanasema Tanzania ingevuna zaidi ya 50% kitu ambacho mkataba hauruhusu.
 

soul provider

JF-Expert Member
Jun 21, 2014
1,274
2,000
Bado tuna safari ndefu sana hadi kufika nchi ya kaanani, angalau kila hatua tunayopiga ni tofauti na jana
 

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
3,686
2,000
Mwanamke anapobakwa na mbakaji akawa kamzidi nguvu na eneo walipo kukawa ni sehem ambayo hata dada apige vipi kelele au kufurukuta hawezi kupata msaada cha muhim anachopaswa kufanya ili asiumie ni kuiaandaa saikolojia na mwili kulienjoy tendo vinginevyo kila anavyopambana na kuresist ndivyo anavyoumia. Awam hii upinzani hamna jinsi iandaeni miili na akili Jiwe kawazidi kwa kila kitu, mnavozidi kupinga kila anachofanya haiwasaidii chochote
 

bukoba boy

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
5,350
2,000
Baada ya kulipwa 30% ya corporate tax,ile 16% ya serikali kwa maana hiyo itapata 16% kwenye hiyo 70% iliyobakia after paying corporate tax?
Ongezea na 1% inspection fee (kama madini watayasafrisha nje). Kwa ujumla
1. Royalities = 6%
2. Corporate tax 30%
3. Inspction fee 1%
TOTAL CONTRIBUTION = 37%. Ambapo ktk ubia GOT inachangia "LAND" wakt wao watachangia " TECHNOLOGY na MACHINE/TOOLS.
 

Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
4,312
2,000
Sheria mpya ya madini ndiyo imezingatiwa. Asilimia 16 ni hisa na bado watalipa asilimia 6 ya mauzo kama mrabaha na kodi ya mapato asilimia 30 ya faida baada ya gharama zote( net profit).
Dadavua Bana usimeze maneno, mwanzo tulikuwa tunapata ngapi? kma ni hivo huenda tulikuwa chini zaidi ya kiwango hicho na kwa nini! wataziba vipi hiko kilichopotea!
na waseme kinaga ubaga kwa nini walitudanganya,

Je sheria za nchi/kimataifa zinasemaje kuhusu udanganyifu wa maksudi wa serikali ya Jamhuri wa Muungano? kutubu tu haitoshi! na wabongo walioshiriki huo upotoshaji wana hali gani?

Kwa nini viwanja vya ndege viko Migodini? wakati tuna Train's cargo na Bandari za kutosha? huko ndge zinashuka na kupaa bila ukaguzi? wanaficha nini kinachopitishwa huko? kwa nini serikali inalichukulia poa jambo hili?

Nasema hivi ''tuchimbe sisi tutalipia cranes, utaalamu wao, na ushauri wao, na vifaa vyao vingine vinvyohusu uchimbaji, wao wanunue toka kwetu wasafirishe, watafute masoko. tunamega kiasi fulani tunachoona kinafaa kuwauzia.

je kila mbongo aliye shiriki mjadala mpya na wa awali alikula kiapo kabla? kwa mujibu wa sheria.

Inayobaki tunahifadhi tunavo jua. hayo ndiyo mazungumzo yanayo faa kutwambia sisi wananchi. zaidi ya hapo hamna kitu, ni porojo.
 

Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
4,312
2,000
Mibeberu ina lazima Na Mali yetu kwanini Lakini?
Mkuu sasa Mibeberu imekuja na uvumbuzi mpya ; eti vinyesi vya watu Weusi vina madini adimu sana Duniani, huku Sirari wanafumua vyoo, kwa kwenda mbele, hasa Guest house, then wanatorokea Kenya.

unajengewa kingine kipya kizuri, na mkwanja wa kutosha juu! But wazee wa kimila wamegomea hii kitu. sijui huko Bongo kwa sasa.
Wameanzia Kenya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom