Barrick kuwapa wabunge laki tatu per day kwenye ukaguzi ni halali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barrick kuwapa wabunge laki tatu per day kwenye ukaguzi ni halali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 11, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wakati Spika wa Bunge Makinda akianza kazi aliliagiza bunge na kamati zake kwamba wanapokwenda nje kwa shughuli za bunge hupewa posho, hivyo si sahihi kupewa posho nyingine kwani ni dalili ya rushwa na inawezekana ikawafanya wasifanye kazi zao kwa haki. Sasa hii safari ya Barrick kuandaliwa ndege na kupewa sh. laki tatu kila mbunge inaashiria nini?

  Barrick yamwaga noti kwa wabunge
  • KILA MMOJA APEWA 300,000/- KWA SIKU

  UONGOZI wa mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick uliopo Nyamongo, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, juzi ulitoa sh 300,000 kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira waliokwenda mgodini hapo juzi. Tanzania Daima, limedokezwa na mmoja wa wabunge waliokuwamo kwenye safari hiyo alisema kuwa fedha hizo walilipwa kwa ajili ya safari ya siku moja na wala si kuwafumba mdomo. Mbunge huyo alisema kuwa msafara uliongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli, walibaini madudu mengi katika mgodi huo mojawapo ikiwepo ya kutokuwapo kwa visima saba vilivyodaiwa kujengwa na Barick kwa wakazi wanaozunguka mgodi huo.  kuwa walipofika mgodini hapo, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Mazingira) Dk. Terezya Luoga, alibanwa na Mbunge wa Longido, Mike Lekule Laizer aliyehoji viko wapi visima saba vinavyodaiwa kujengwa na Barick.

  Kwa mujibu wa wabunge wengine waliokuwa kwenye msafara swali hilo aliulizwa kutokana na jibu lake alilolitoa Julai mwaka huu kwa Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko, aliyetaka kujua mgodi huo umejenga visima vingapi kwa wanakijiji wanaozunguka mgodi husika ambao walikuwa wakiutegemea mto Tigite. Mto Tigite unadaiwa kuchafuliwa na maji ya sumu yanayotoka katika mgodi huo na kamati ya Bunge iliwahi kuchunguza jambo hilo na ziara ya juzi ilikuwa kwenda kuangalia shughuli zinavyoendelea katika mgodi huo.

  Tanzania Daima limedokezwa kuwa baada ya kubanwa Waziri Luoga alisema inawezekana alipewa taarifa zisizo sahihi kuhusu ujenzi huo, kwani juzi alishuhudia kutojengwa kwa visimaa hivyo. Hata hivyo, wajumbe wa kamati hiyo walimbana waziri kwa madai kuwa alilidanganya Bunge kuwa naye alifanya ziara katika mgodi huo na kuona visima hivyo. “Ilikuwa aibu kwa waziri maana Barickk walikiri kuwa hawakujenga visima hivyo bali wapo kwenye mchakato wa kuvijenga, serikali yetu iliaibika,” alisema.

  Inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja kinachopakana na mgodi huo, Omtanzania Mpima, aliwaeleza wajumbe wa kamati hiyo kuwa Barick haijajenga visima hivyo kama inavyodaiwa. Uongozi wa Barick ulidai kuwa bado hawajajenga visima hivyo na wapo kwenye mchakato wa kuvijenga, lakini kwa hivi sasa wamekuwa wakiwapa maji wananchi kwa kutumia magari.

  Tanzania Daima, liliwasiliana na Waziri Kivuli wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mazingira) Mchungaji Peter Msingwa, ambaye alisema utaratibu wa safari ile ulipitia ofisi ya Bunge, hivyo wajumbe wengi hawakujua iligharimia na Barick. Alisema wajumbe hawakuwa na wasiwasi na safari hiyo kwa kuwa ni jambo la kawaida ofisi ya bunge kugharimia safari za kamati husika. Aliongeza kuwa walibaini kuwa Barick ndiyo waliogharimia hiyo safari, lakini jambo hilo haliwezi kubadili mawazo yao na kile walichokiona kwenye mgodi huo.

  “Mimi siwezi kununuliwa na Barick au yoyote yule, ziara ile tuliifanya bila kujua nani mfadhili, lakini kimsingi tumeona kila kitu kwakuwa tulikwenda na mitambo yote ya kurekodiwa 'Hansard' na video Kamera,” alisema. Msingwa alisema katika utaratibu wa kawaida mtuhumiwa hawezi kumfadhili mpelelezi na matokeo yakawa mazuri, lakini ni vema wananchi wakawa na imani na wabunge waliokwenda kwenye mgodi huo. “Siwezi kusema wabunge tulihongwa na Barick kwa sababu ziara ile ilifanywa kwa maelekezo ya Spika kwa hiyo kama unasema tumehongwa basi ofisi ya Spika ndiyo ilikuwa ya kwanza,” alisema.

  Juzi Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilifanya ziara ya siku moja mgodini Nyamongo ikitokea mjini Dodoma, ziara ambayo kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo yake iliyoyatoa mwaka jana kuhusu athari za mazingira zilizosababisha baadhi ya wakazi wanaouzunguka kupata athari za kiafya. Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine alialikwa kuambatana na kamati hiyo, lakini safari yake iliishia Uwanja wa Ndege Dodoma baada ya kubaini kwamba ndege husika zilikuwa zimekodiwa na kampuni ya Barrick.

  Inasadikiwa zaidi ya wabunge 20 waliokuwamo kwenye msafara huo ambao ni Susan Lyimo (CHADEMA) Esther Matiko, (CHADEMA) Mary Mwanjelwa (CCM), Mbunge wa Buchosa (CCM), Dk. Charles Tizeba, Mbunge wa Kikwajuni (CCM), Hamad Yusuff Masauni na Mbunge wa Longido (CCM), Mike Lekule Laizer. Wengine ni James Lembeli (CCM), Abdulkader Shah na Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa na msafara huo unadaiwa kuongozwa na Ofisa wa Barick Deo Mwanyika.

  Tanzania Daima
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa nini Bunge linajaribu kubana ukweli huu walipoulizwa mjengoni?

  Hii laki tatu wabunge kulipwa na Barrick inashiria rushwa kukubaliwa na mhimili wa bunge au mhimili wa bunge umeadhiriwa na rushwa kama ilivyo kwa mfumo wa serikali?
   
 3. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pesa tamu eh, sasa hii wapi na wapi kukataa posho na kisha kuchukua posho? Mchungaji, je rushwa ikipitia kwa spika inakuwa sio rushwa? Where are we going with this?
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ni rushwa moja kwa moja!
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hao wabunge wote waliopokea mlungula (kama ni kweli) wafukuzwe ubunge na iwe fundisho kwa wengine.
   
 6. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  angalieni uongo unamwisho na mwisho huwa mbaya zaidi
   
 7. n

  niweze JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unajua mijambazi ya ccm wanajiita viongozi sijui ni viongozi wa nani. Hivi hakuna ethics or morals katika hii nchi? Hawa ccm walitengenezwa na nani jamani? Matumbo midomo na mikono yao siku zote ipo imepanuka kama midomo ya watoto wa ndege.Alie-suggest ccm waende wote Mara ni nani? Kwani serikali ya Tanzania ndivyo inafanya kazi na lazima wote bungeni waende safari kwa jili ya kuona machine na udongo? Time will tell .... anyway good job makinda kwa ujnga wako.

  By the way si Barrick ingewkodia ndege na familia zao pia kwani wote wana njaa.
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh njaa mbaya za wabunge watapokea
   
 9. M

  Malabata JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni rushwa kama siyo rushwa basi wabunge hao niwezi hawezi kupokea posho 2 kwa kazi 1,hao wabunge wachunguzwe na wafanyiwe kazi
   
 10. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280

  Kumbe majibu ya maswali mengi ndani ya Bunge ni fake? Je, Waziri inapobainika kadanganya kama huyu nini kinafuata?
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Ndani ya chombo hiki cha kutunga sheria kuna tatizo kubwa,lakini pia kuvamiwa na watu wasio na maadili ni sababu.
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  nchi imeoza kabisa..............................ulafi wa viongozi watisha yaani hawaridhiki na donge kubwa tunalowapa...............
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  km spika ndo alipanga safari iweje ndege zikodiwe na barrik? Na nikwanini barrik watoe posho? SPIKA NDO CHANZO CHA RUSHWA HII
   
 14. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sheria za uchafuzi wa mazingira zinasema,mwenye kiwanda ikionekana kwa namna moja ama nyingine kuharibu mazingira basi mmiliki wa hicho kiwanda ndie atakaegharamikia safari na hata uharibifu wa hizo bidhaa wa hilo eneo husika,haya maneno nimeyasikia jana kwenye chombo kimoja cha habari kuna kiongozi wa serikali alikua akifafanua hili swala,kwa wataalamu wa Sheria wanaweza kutusaidia
   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hii sheria ina utata kama inaruhusu mharibifu kuwalipa moja kwa moja wakaguzi. Ofisi ya bunge ndio ingelipwa gharama, halafu (au kabla) yenyewe ipeleke invoice kwa gharama hizo.
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sasa inmaana mbunge wangu naye alipiga foleni wakati wa kwenda kupokea bahasha ya khaki mezani kwa MTUHUMIWA Barricks sio?????????????

  Ama kweli WALAZWAHOI tumekwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiisha!!!!!!!!!!!!!!!!

  Waheshimiwa WAbunge waliokua katika timu ya kwenda kuchunguza Barricks woooote tuwamulike ipasavya wana-JF na jalada zao moja kwa moja tukazifikishe kwa wapiga kura kwa ajili ya utekelezaji wa ADHABU stahiki kwenye chaguzi zitakazofuatia.

  Kwa nini waitie AIBU Tanzania kiasi hicho kwa kushindwa kujizuia na njaa ya siku moja???????????????????
   
 17. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Labda wataalamu wa sheria na wanaojua sheria za mazingira watusaidie. Je Tz tuna sheria ya polluter pay? Kama ipo ni haki kwa Barrick kugharimia hiyo safari afterall hatuna hela za kuchezea kulipa kundi lote la wabunge ambao most of them hawana environmetal audit skills kwenda kukagua mgodi. Hapo wameenda kutalii zaidi. Mwenye uwezo wa kukagua mgodi ni lazima awe mtaalamu na masuala ya mazingira. Hence let Barrick pay if the law says so. Labda issu ni kwamba they have been paid more than what they should which could. Hapo tuwe makini na kiwango cha malipo kiwe stated na sheria. Maana kuwalipa zaidi ya perdiem ni sawa na kuwanunua na kuchezea hela za Barrick shareholders!
   
 18. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ndugu mtatupasua vichwa,wakati mwingine huwa natamani japo nikute habari ya kunifariji japo kuna maendeleo kidogo lakini wapi.je hii nchi iko vipi jamani?kichwa kinauma,ni ngumu sana kuwa mzalendo.
   
 19. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ofisi ya spika ndio tatizo. na bado tutaona madudu mengi chini ya huyu mama.
   
 20. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi hii dhambi ya rushwa itakoma lini jamani? mbona kama viongozi wa tz wamezidi kwa huu ufisadi????
   
Loading...