Barrick ku occupy machimbo ya dhahabu..tufanyeje jamani?!!

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
7,564
11,478
Wakuu taarifa za vyombo vya habari wiki hii ni kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu ya barrick wana mpango wa kuongeza machimbo mengine..ikumbukwe hadi hivi sasa hawa jamaa wanamiliki machimbo na miradi ya dhahabu ikiwemo buzwagi,northmara,tulawaka, bulyanhulu na kabanga.. ikumbukwe pia shughuli hizi haziendani kabisa na thamani ambayo nchi inaipata na sio nchi tu hata maeneo husika.. viongozi wamekosa uzalendo kabisa na wameamua kutoa rasilimali hizi ilhali wao wananufaika moja kwa moja wao na familia zao..miaka iliyopita tuliona mikataba ikisainiwa kwenye mahotel kama ilivyofanywa huko la churchil na nazir karamage..katika kipindi hicho tulikuwa na tumaini jipya ambalo lilijipambanua kwa kutetea sekta ya madini (zitto kabwe) na kiukweli watanzania wote tulikuwa nyuma yake na ikamjengea heshima kubwa sana.. Kwa sasa hasikiki tena akizungumzia hizi habari na watu wanaweza sema yeye si mwenyekiti wa kamati husika lakini hata kipindi hicho hakuwa ila alisukumwa na uzalendo.. hebu watz tuamke tusiwe kama manguruwe..
 
Tuiondoe CCM mamlakani, tuwe na serikali mpya ambayo itapitia kiukweli hii mikataba. Bila hilo madini yetu yataishia mifukoni mwa Barrick.
 
sasa tufanyaje mungu wangu mbona ccm wanatutesa ivi!?

tukiandamana ndobalaa zaidi tutaleta maafa yasiyo kuwa nakifani, tukisema tuchague chadema wanachakachua matokeo, kama tulivo sikia juzi wamesema eti hata kama wakishidwa arumeru watangaze wameshinda ili kesi iende mahakamani lakini mbunge wao aweameapishwa tayari.
 
Tuiondoe CCM mamlakani, tuwe na serikali mpya ambayo itapitia kiukweli hii mikataba. Bila hilo madini yetu yataishia mifukoni mwa Barrick.

Kampuni za Mcameron mtaziondoa kweli wanachimba TZ anaenda kupitisha bakuri UK
 
Wakuu taarifa za vyombo vya habari wiki hii ni kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu ya barrick wana mpango wa kuongeza machimbo mengine..ikumbukwe hadi hivi sasa hawa jamaa wanamiliki machimbo na miradi ya dhahabu ikiwemo buzwagi,northmara,tulawaka, bulyanhulu na kabanga.. ikumbukwe pia shughuli hizi haziendani kabisa na thamani ambayo nchi inaipata na sio nchi tu hata maeneo husika.. viongozi wamekosa uzalendo kabisa na wameamua kutoa rasilimali hizi ilhali wao wananufaika moja kwa moja wao na familia zao..miaka iliyopita tuliona mikataba ikisainiwa kwenye mahotel kama ilivyofanywa huko la churchil na nazir karamage..katika kipindi hicho tulikuwa na tumaini jipya ambalo lilijipambanua kwa kutetea sekta ya madini (zitto kabwe) na kiukweli watanzania wote tulikuwa nyuma yake na ikamjengea heshima kubwa sana.. Kwa sasa hasikiki tena akizungumzia hizi habari na watu wanaweza sema yeye si mwenyekiti wa kamati husika lakini hata kipindi hicho hakuwa ila alisukumwa na uzalendo.. hebu watz tuamke tusiwe kama manguruwe..

Kulalama huko kote nilidhani utalete mpango mkakati wa kutekeleza ili kuepusha hali hiyo, Otherwise wewe ndiye unaendeleza unguruwe!
 
unajuaje kama sifanyi kitu.. mbona unanilaumu tena na kunihukumu moja kwa moja..inawezekana nilichofanya mimi hakijakidhi haja ndio maana wanaendelea kuhodhi migodi.. toa wazo lako wahusika wanaweza kuona hata wasipockia..badala ya kuni attack.. otherwise na wewe ni beneficiary wa mfumo huu..
 
Nafikiri Nyanzaga, Bugarama or somewhere in the lake zone area wamepata ore viable for commercial exploitation. So Barricck is here to stay....
 
Yah, lkn tatizo ni sheria tulizonazo. Zina mruhusu mwenye uwezo kufanya exploration maeneo aliyoyaomba na kuyapata kwa kufata taratibu au hata kuyanunua kwa watu. Na akiisha ingiza pesa yake akapata kiasi cha kutosha kujistfy kuanza uchimbaji definately ataanza kwani ndo njia pekee ya yeye kurudisha gharama na kupata faida. Inabidi sheria zibadilishwe na kwa mikataba iliyokwisha sainiwa ndo hivyo tena!
 
Waache wachimbe ila wakumbuke sio kila raisi wa Tz ni JMK!
Atakuja farao asiyemjua musa patakuwa hapatoshi!
 
Mi ntajibu swali lililopo kwenye heading.
Iondoeni Serikali iliyopo madarakani ikiwezekana hata kwa njia waliyoitumia Mali.
 
Back
Top Bottom