Barrick imeilipa Tanzania dola milioni 100 ikiwa ni sehemu ya malipo ya dola milioni 300 ya fidia ya kodi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Kampuni ya Barrick imeilipa Tanzania dola milioni 100, sawa na takriban sh. bilioni 250, ikiwa ni sehemu ya malipo ya dola milioni 300 ambazo Kampuni hiyo ya Madini ilikubali kulipa kama fidia ya kodi.

Mfano wa Hundi ya kiasi hicho cha fedha imekabidhiwa na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Barrick, Bw. Hilaire Diarra kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, kwa niaba ya Serikali, Jijini Dodoma tarehe 26 Mei, 2020.

e30422b3-585a-41b0-b54a-3c91247a0172.jpg

Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mwenyekiti wa Timu ya Serikali ya Majadiliano na Barrick ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Kamati yake, Dkt. Mpango alisema tukio hilo ni mwanzo wa makubaliano ya mkataba wa msingi kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni hiyo yaliyofikiwa Disemba 19, 2019 na kusainiwa rasmi Januari 24, 2020.

Dkt. Mpango aliyataja makubaliano mengine yaliyofikiwa kati ya Serikali na kampuni hiyo kuwa ni kuundwa kwa Shirika la Madini la Twiga lenye umiliki wa pamoja likalofanya kazi nchini katika kusimamia uendeshaji wa migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara pamoja na migodi mingine nchini ambapo Serikali ya Tanzania itashiriki katika utoaji wa maamuzi kuhusu uendeshaji wa migodi, mipango, manunuzi pamoja na masoko ya madini.

“Tulikubaliana kuhakikisha kuwa faida za kiuchumi zinazotokana na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi pamoja na North Mara zigawanywe kwa msingi wa usawa wa asilimia 50 kwa 50 kati ya washirikania ambapo hisa za Serikali zinazotokana na faida za kiuchumi zitatolewa katika mfumo wa mrabaha, kodi pamoja na kupata asilimia 16 ya faida kutokana na makampuni hayo kufanya kazi nchini” alisema Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alisema mbali na makubaliano hayo, kampuni ya Barrick imekubali kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 5 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Mtambo wa kuchakata madini nchini (smelter).

“Kampuni ya Barrick pia imekubali kuanzisha ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuahidi kutoa hadi dola milioni 10 kwa kipindi cha miaka kumi kwa ajili ya utoaji wa mafunzo yanayohusu sekta ya madini”, aliongeza Dkt. Mpango.

Alisema Kampuni ya Barrick ilikubali kutoa dola 6 kwa kila ounce ya madini itakayouzwa (ikijumuisha mchango kwenye Mfuko wa Mandeleo ulioanzishwa na Kampuni ya Barrick Tanzania) ili kusaidia jamii zinazozunguka maeneo ya migodi pamoja na kutoa kiasi cha dola milioni 40 kwa ajili ya kuboresha kipande cha barabara kati ya Bulyanhulu na Mwanza na kujenga nyumba na miundombinu yake.

“Naipongeza Kampuni ya Barrick kwa kuanza kutekeleza makubaliano haya na natoa wito kwa kampuni nyingine za madini na wawekezaji wengine katika sekta hiyo kuiga mfano mzuri uliooneshwa na Kampuni hii katika kuhakikisha kunakuwa na hali ya usawa katika uendeshaji wa shughuli za madini nchini kwa faida ya pande zote mbili” alisisitiza Dkt. Mpango.
 
Hii habari haiko kabisa kule kws Mabeberu. Naona hii ni kwa ajili ya siasa za Tanzania.

nime Google sioni kitu huko Ulaya na Marekani. Wamelipaje pesa zote hizo bila kuwaambia shareholders wao?
Hawa watu waongo waongo ngumu kuwaamini.
 
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai
 
Hauamini kuwa tumelipwa na mabeberu?
Hii habari haiko kabisa kule kws Mabeberu. Naona hii ni kwa ajili ya siasa za Tanzania.

nime Google sioni kitu huko Ulaya na Marekani. Wamelipaje pesa zote hizo bila kuwaambia shareholders wao?
Hawa watu waongo waongo ngumu kuwaamini.
 
Tusifurahi kwanza. Kwani Lissu alisema tutashitakiwa. Tusubiri kwanza tuone. Kwani kama hao mabeberu hawatatushitaki,huenda Lissu au Zitto wakatshitaki

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao mabeberu hawawezi kwenda MIGA, wakatafute nini tena wakati wamepata wanachotaka?
Ebu jiulze yale madai US $190 bil yameyeyukia wapi? Sasa hapo mabeberu wana haja gani tena ya kushtaki? Mbona simple tu unashindwaje kuelewa?
 
Kiukweli katika maamuzi mabaya ilikuwa kusimamisha mgodi huu!! Tumepoteza ajira 2000.... pia wategemezi wao..2000*20..watu wamepoteza maisha kwa stress.. .Mapato kodi..., Biashara, viwanda, wasafirishaji... Kishika uchumba cha $300M, yalikuwa mapato ya mwezi pekee ktk mnyororo wa dhamani mgodi ukifanya kazi! Hisa 16 ,Twiga, tulikuwa nazo 15 awali ilikuwa swala kukaa mezani.
 
Kiukweli katika maamuzi mabaya ilikuwa kusimamisha mgodi huu!! Tumepoteza ajira 2000.... pia wategemezi wao..2000*20...Mapato kodi..., Biashara, viwanda, wasafirishaji... Kishika uchumba cha 300M, yalikuwa mapato ya mwezi pekee ktk mnyororo wa dhamani mgodi ukifanya kazi! Hisa 16 ,Twiga, tulikuwa nazo 15 awali ilikuwa swala kukaa mezani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Punguza ujuaji
 
Hii habari haiko kabisa kule kws Mabeberu. Naona hii ni kwa ajili ya siasa za Tanzania.

nime Google sioni kitu huko Ulaya na Marekani. Wamelipaje pesa zote hizo bila kuwaambia shareholders wao?
Hawa watu waongo waongo ngumu kuwaamini.
Nimeisoma Blumberg
 
Hao mabeberu hawawezi kwenda MIGA, wakatafute nini tena wakati wamepata wanachotaka?
Ebu jiulze yale madai US $190 bil yameyeyukia wapi? Sasa hapo mabeberu wana haja gani tena ya kushtaki? Mbona simple tu unashindwaje kuelewa?
Kama watumishi wao waliweza kupinga mkopo wa B500 wakawa wanalilia mabinti zetu wabebe tu mimba hovyo na serekali iwasomeshe. Watashindwa nini kwenye hili!?
Tatizo si mabeberu. Tatizo ni wachumia tumbo. Wenye kujipendekeza kwa mabeberu ili tu wajaze matumbo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom