Huu ni ujinga wa kupindukia sasa, tumekuwa wendawazimu wa kugeuzwa kila wawekezaji wanavyotaka. Hapa sasa kilichobaki ni kutumia nguvu ya umma kuiadabisha serikali ya vichaa hii. Haiwezekani makambuni yanayolipa mrahaba wa aslimia tatu halafu mwisho wa siku mnakuja kukaa kwenye meza kujadili kurejesha fedha tena kwa makampuni hayo. Hapa hasira imenipanda na uvumivu umeniishia. Tuamke watanzania kwani hata kipofu mwisho hutambua pale hujuma inapozidi kiasi.Yaani, we are paying them more than they put in the treasury.
point...lakini mh, kumbuka kuwa resources sio kitu kinachoisha. In the longrun, you hold the bargaining power! Hicho ndicho kitu ambacho hatujajifunza! Tatizo ni hawa viongozi wetu WAJINGA wasiokuwa na upeo. Wao wanawaza leo, leo, leo, na tumbo langu, tumbo langu, tumbo langu. Ingali ningepata nafasi ya uongozi...bongo mngelia! Sipendi ujinga kabisa!!!Ni kweli hakuna haja ya kuwa na jazba. Tulisaini mikataba, lets keep our promises maana kama mjuavyo mambo ya the race to the bottom haya. Wa kutandikwa viboko ni hao waliosaini mikataba kwa niaba ya Watanzania. Unajua nchi za Africa zinashindana kuwa the cheapest place for investors. Na nachoona hapa ni mambo ya prisoner's dilema. Nikiwawekea ngumu wawekezaje basi watahamia Ghana, na Ghana nae ana feel the same. Anayefaidika ni Investor. We need to solve that in future contracts.
Si ajabu hata huo mrahaba wa 3% wanaolipa kila mwaka tangu waanze kuchimba dhahabu, jumla yake tangu mwaka 2000 hadi sasa haijafikia $273 million.
Tungewapatia umeme wa kutosha wakailipa Tanesco ingekuwa faida kwetu, badala yake umeme wakawa wanazalisha wenyewe na serikali ilikubali kutowatoza VAT kwenye fuel lakini ili kuzuia matumizi mabaya ya hizi exemptions, VAT hukusanywa kwa kila kitu kisha wahusika wanadai refund from treasury.
Kumbuka haya ni malimbikizo ya miaka 10.
Kwa nini kulimbikiza miaka yote 10?
Kama hatutamuondoa Kikwete na mafisadi wenzake tutaendelea kulia na kusaga meno khe khe kheeeeeeeeeee huko ndiko alikojaza share zake na familia yake then mnauliza Riz anapata wapi mpunga? Hiyo ni mbinu yake lazima mmlipe hadi chozi la damu liwatoke!
Hivyo ndivyo anavyowashughulikia mafisadi khe khe kheeeeeeeeeeeeeee.
Lakini tukumbuke hii migodi zi ya wazungu 100% kuna watanzania wenzetu, ndio wenye share humo, Kama ..........., ndio waliojua weakness za watendaji wa serikali yetu, na hao watendaji AKA........... wana mgao wao hapa. Nahisi Wazungu wanawashangaa sana, manake ni Watanzania ndio wanaotoa hizo tricks,
Waziri gani ahusike wakati gani,
Katibu gani apewe nini, watanzania wenzetu, na wala si wazungu, wanaojua hongo kiasi gani apewe nani,
Mie nina hasira sana na kizazi fulani hapa nyuma,
kizazi cha viongozi wa umma, waliofilisi mashirika walioongoza, walioiba kwenye mabenki walioongoza
kwa sasa wameingia ubia na makampuni ya nje makamuni haya makubwa kama ya simu, sementi, migodi nk, kwa kweli inabidi kufuatilia mali za viongozi iwe kazi kubwa sana!!
Hopefull watoto wetu watatusamehe kwa kuwa tunajitahidi kurekebisha hii hali.
MIMI SIWEZI KUWASAMEHE HAWA WATU WALIOIBA WAKAFILISI MASHIRIKA YETU, NA SASA WANAENDELEA KUHONGA SERIKALI KUPATA MIKATABA YA AJABU AJABU KUMULIKI MAKAMPUNI MAKUBWA YANAYOENDELEA KUTUNYONYA.
Kama anavyosema Kingunge Ubinafsi kila kona.
Sasa Chadema inahusika vipi hapa? tatizo la wadanganyika kila kitu wanadhani kinahitaji kusuluhishwa kisiasa.Nadhani CDM watautaarifu umma--katika operation itakayoanza nyanda za juu kusini hivi karibuni--kuhusu haya madudu yanayofanywa na serikali ya chama cha mafisadi
Pascaldaudi,
Yule aliyesaini mkataba nina hakika anazo shares kwenye migodi ya Barrick, ndiyo maana hasumbuliwi na ripoti kama hizi. Ni kweli kisheria hakuna jinsi, unless tuwe na regime change, regime mpya ibatilishe mikataba yote kwa justification ya kwamba ilisainiwa kifisadi. Otherwise tutabaki historia tu kuwa once upon a time Tanzania was the 3rd world producer of gold, and we have nothing to show for it. Have you ever wondered why a person like Riz1 anaitwa new billionaire? Are there shortcuts for getting rich in Tanzania these days?