Barrick Gold mining yabadili jina na kujiita ACACIA

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,498
54,923
Leo Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Gold Mining imetangaza kubadili jina na Kujiita ACACIA Gold mining. Mabadiliko hayo yanaenda sambamba na kubadilisha makao makuu ya kampuni hii kutoka Africa Kusini na Kuyahamishia Tanzania.

Barrick Gold Mining inamiliki migodi ya Bulyanhulu Gold Mine, Buzwagi Gold Mine, North Mara Gold Mine. Vilevile ilikua inamiliki mgodi wa Tulawaka mine.

Wanasema ACACIA ni aina ya Mti uliopo kila sehemu barani Afrika ambao unahimili kila aina ya hali ya hewa ikiwemo ukame, ndo maana wameamua kubadili jina. Vilevile kubadili jina wanasema itasaidia kukuza biashara zao.

ACACIA wamesema wametenga dollar million 10 kwa mwaka kwa ajili ya Kusaidia jamii ya Wananchi wa Tanzania katika sehemu mbalimbali. Mia

KAMPUNI YA AFRICAN BARRICK GOLD YABADILI JINA,SASA KUITWA "ACACIA"

Kampuni ya African Barick Gold (ABG) inayo furaha kutangaza kuwa imebadili jina lake na sasa na itatambulika kama Acacia Mining plc. Mabadiliko haya ni sehemu ya jitihada kubwa za kubadilisha mtazamo na mkakati wake mpya wa kazi yetu kubwa katika uchimbaji wa madini. Mabadiliko haya yamekuja baada ya wanahisa wa kampuni kukubaliana na kupiga kura ya kupitisha maamuzi haya jana tarehe 26 mwezi Novemba mwaka 2014.

Acacia ni mti ambao ndiyo chimbuko la jina letu jipya, ni mti unaonekana kuwa ni nembo ya mandhari ya Afrika na unaweka msisitizo kwenye malengo yetu ya kiuwekezaji Afrika. Zaidi ya hayo, tutaendelea kutumia nembo ya Afrika kwenye alama zetu zote ili kusisitiza kujikita kwetu kwenye bara la Afrika. Mfuko wetu wa Maendeleo ya Jamii wa ABG sasa utajulikana kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Acacia.

Akizungumza kuhusu habari ya mabadiliko haya, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia Mining, Brad Gordon amesema:

"Bila shaka mti wa Acacia (kwa Kishwahili "Mgunga") ni mti unaojulikana kuwa ni sehemu ya utambulisho wa mandhari ya Afrika.Kwa mikakati yetu mipya, tutajenga biashara endelevu na yenye mafanikio makubwa nchini Tanzania na barani kote Afrika. Kama mti wenyewe wa Acacia ulivyo enea. Tunaamini kuwa mlinganisho wetu huu na mti wa Acacia ni madhubuti na tutaweza kustahimili mazingira magumu yoyote tutakayokumbana nayo.

Tunataka kuweka wazi kuwa mabadiliko haya ya jina hayana maana kuwa ni njia ya kukwepa wajibu waliokuwa nao ABG kama vile kulipa kodi, bali ni kuakisi hatua na mkakati wetu mpya wa biashara.

Vilevile mabadiliko haya, hayataathiri ajira zozote na hayabadilishi mfumo wa umiliki wa kampuni. Tutaendelea kuwa wachimbaji wa dhahabu tuliojitegemea na tulio orodheshwa kwenye masoko yote ya hisa ya London na Dar es Salaam. Hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya mikataba ya ajira au makubaliano (mapatano) na masharti ya ajira katika migodi yetu kufuatia mabadiliko ya jina la Kampuni."

Kufuatia jitihada hizi za kubadilisha jina la kampuni, alama zetu kwenye masoko ya hisa pia zimebadilika kutoka ABG na kuwa ACA katika masoko ya hisa ya London (LSE) na Dar es Salaam (DSE).

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia iko kwenye safari kutengeneza biashara itakayo kuwa kinara katika bara la Afrika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Ni muhimu jina hili liakisi hayo kwa usahihi. Ubadilishaji wa jina ni hatua muhimu ya kuwaleta wadau wetu pamoja kwa lengo la kuunga mkono utambulisho huu mpya wa kampuni.

Kampuni ya Acacia itaendelea kuwekeza na kufanya kazi kwa karibu na jamii zinazozunguka migodi yetu kupitia miradi iliyopo na miradi/mipango mipya. Tutaendelea kuwa miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa uchumi nchini Tanzania na tutaendelea kuzingatia viwango vya juu kabisa vya ubora katika biashara yetu na pia kuendeleza uchimbaji huku usalama ukiwa kipaumbele chetu muhimu.

Chanzo: Michuzi
 
hivi kuna maana gani kubadili jina ilihali mambo mengine yanabaki kama yalivyo?na kwanini baada ya miaka mitano mitano?haya ndo mambo ya ukwepaji ulipaji kodi japo wanasema kodi wanalipa,sasa jina tu kweli linawachukulia muda?tafakari....................
 
Hapo kuna kodi inatakiwa ikwepwe,stay tuned.Hii ni international mining Company yenye makao makuu Australia if not Canada,sielewi elewi kinachoendelea
 
Kwa sasa tulawaka inamilikiwa na serikali kupitia stamico chini ya kampuni tanzu, STAMIGOLD
 
Leo Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Gold Mining imetangaza kubadili jina na Kujiita ACACIA Gold mining. Mabadiliko hayo yanaenda sambamba na kubadilisha makao makuu ya kampuni hii kutoka Africa Kusini na Kuyahamishia Tanzania.

Barrick Gold Mining inamiliki migodi ya Bulyanhulu Gold Mine, Buzwagi Gold Mine, North Mara Gold Mine. Vilevile ilikua inamiliki mgodi wa Tulawaka mine.

Wanasema ACACIA ni aina ya Mti uliopo kila sehemu barani Afrika ambao unahimili kila aina ya hali ya hewa ikiwemo ukame, ndo maana wameamua kubadili jina. Vilevile kubadili jina wanasema itasaidia kukuza biashara zao.

ACACIA wamesema wametenga dollar million 10 kwa mwaka kwa ajili ya Kusaidia jamii ya Wananchi wa Tanzania katika sehemu mbalimbali. MiaChanzo: ft.com

Hamna kitu wanataka kukwepa kodi tu, wameondoka S.Africa kwasababu kule hakuna ukwepaji wa kodi, huku kwetu unajichimbia tu dhahabu na unaisafirisha unavyotaka!
 
ilianza kmcl ikaja barick sasa wanaita sijui acica ila eleweni yote hayo ni kupata misamaha ya kijinga ya kodi
 
mkuu hao wanakwepa kodi tu ndo maana wanabadili jina
siunajua mikataba mibovu ya tz ya kuwekeana miaka 3 ikifika ndo
wawekeane tena mambo ndo mambo mabovu na madudu yanayofanywa
na serikali yetu huwezi kuwapa mkataba wa miaka 3 watu kama
hao au shirika kaka hilo halafu mnyonge mlalahoi unambana kodi
hadi kooni anashindwa hata kupumua wakati hao wanapeta kiulaini
na wanabadili majina watakavyo iilimradi tu mkataba wao umeisha
wanawaniuzi sana hawa viongozi
Leo Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Gold Mining imetangaza kubadili jina na Kujiita ACACIA Gold mining. Mabadiliko hayo yanaenda sambamba na kubadilisha makao makuu ya kampuni hii kutoka Africa Kusini na Kuyahamishia Tanzania.

Barrick Gold Mining inamiliki migodi ya Bulyanhulu Gold Mine, Buzwagi Gold Mine, North Mara Gold Mine. Vilevile ilikua inamiliki mgodi wa Tulawaka mine.

Wanasema ACACIA ni aina ya Mti uliopo kila sehemu barani Afrika ambao unahimili kila aina ya hali ya hewa ikiwemo ukame, ndo maana wameamua kubadili jina. Vilevile kubadili jina wanasema itasaidia kukuza biashara zao.

ACACIA wamesema wametenga dollar million 10 kwa mwaka kwa ajili ya Kusaidia jamii ya Wananchi wa Tanzania katika sehemu mbalimbali. MiaChanzo: ft.com
 
Hamna kitu wanataka kukwepa kodi tu, wameondoka S.Africa kwasababu kule hakuna ukwepaji wa kodi, huku kwetu unajichimbia tu dhahabu na unaisafirisha unavyotaka!
Aahhh, Maneno yako yamechana moyo wangu.Daahh!
 
Back
Top Bottom