Barongo naye awania nafasi ya uenyekiti jumuiya ya wazazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barongo naye awania nafasi ya uenyekiti jumuiya ya wazazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 29, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na Debora Sanja, Dodoma KATIBU mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma, John Barongo, amejitosa kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa.

  Barango amejitosa kuwania nafasi hiyo baada ya kuchukua fomu mwishoni mwa wiki iliyopita katika ofisi za chama za mkoa wa Dodoma.

  Akizungumza baada ya kuchukua fomu, alisema moja ya mambo atakayoyashughulikia endapo atapata nafasi hiyo ni kuimarisha shule zote zinazomilikiwa na jumuiya hiyo.

  Alisema atahakikisha shule zote za jumuiya ya wazazi zinafanya vizuri katika mitihani yake.

  “Lazima shule zetu ziwe mfano kwa kufanya vizuri ikiwamo kuhakikisha kuwa zinakuwa na walimu wa kutosha na wenye sifa,” alisema Barongo.

  Aidha, alisema jumuiya hiyo inavyo vitega uchumi vya kutosha hivyo lazima ijiendeshe yenyewe kwa kutumia vitega uchumi hivyo.

  “Lazima tuiwezeshe jumuiya yetu iweze kujitegemea kiuchumi, hatuna sababu za kushindwa kufanya hivyo kwa kuwa tuna vitega uchumi vingi,” alisema Barongo.

  Alisema pamoja na kuitumikia Jumuiya hiyo kwa muda mrefu katika nafasi mbalimbali ameona kuna haja ya kuiongoza tena kwa nafasi ya uenyekiti wa taifa kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha.

  “Nitashirikiana na viongozi wenzangu kuhakikisha Jumuiya yetu inakuwa na nguvu kama zilivyo jumuiya zingine,’’ alisema Barongo.

  Alitaja eneo jingine ambalo atalisimamia katika uongozi wake kuwa ni kuisaidia Serikali katika malezi ya watoto na vijana kutokana na kumomonyoka kwa maadili.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
Loading...