Barick against Tanzania

Kwisense

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
475
1,138
DUH?

---------------------------------------------
Anaandika Prof. Makune

Kwanza niseme ukweli nilisema hapa pia nasema Tena Tanzania ina Kundi kubwa la wenye vyeti hata hivyo wenye uelewa ni 0.01%

Ni hasara Serikali iliitangazia dunia kuwa BARICK ambao wanamiliki ACACIA na Acacia inamiliki migodi ya North Mara , Buzwagi na Bulyanhulu kuwa ni majizi na wametuibia Triilion 450 sawa na Gari 2 aina ya Noa kwa Kila mtanzania ! Rais akatangaza kuwa Wamekubali kulipa matrillion yote !

Miezi 2 ya mazungumzo
Nilisema hapa kuwa kuna kitu kinaitwa Round table , negotiation na Bargaining pia Leo majibu yametoka kama ifuatavyo tutapewa billion 600 mkono wa uaminifu na mahusiano Pia 16 % ya Barrick pia 50% ya kugawana faida !
Vilaza wanapiga makofiiii duuuu danganyika hiiii ya nyerere duuu
Ziko wapi triilion 450
Wezi Leo wanatoa mkono wa uaminifu au bilion 600 ndiyo trillion 450?

Kumiliki 16% na faida 50% Nani hajui tuna 46% pale mwadui na hatujawahi pata hata 2% ya faida japo napo kuna makubaliano ya 50% iko wapi faida pale urafiki textile tunshisa 50% na China ? Iko wapi faida NBC tunakomiliki 48% ya hisa ! Iko wapi faida NMB tuliko na 40% ya. Hisa ? Iko wapi faida Tazara tulipo na 50% ya share ? Mbona tulipata hasara ATCL tulipoingia hisa na south Africa air way 50% ! Iko wapi 50% ya Airtel iko wapi tulizeni vichwa wadanganyika .

*****************************

Kuna mambo ccm wameandika na pia yametangazwa na serikali kuwa ni makubalino na Acacia ambayo hayapo kwenye sheria yoyote, na hayapo sawa. Yawezekana kuna mahali hukuelewa au hukusikia vizuri:

1) Hakuna mrabaha (royalty) wa 16%, iwe kwa sheria ya zamani au iliyopitishwa hivi karibuni. Sheria iliyopitishwa hivi karibuni mrabaha ni 6%.

2) Kuhusu ofisi, nadhani alimaanisha operations offices.

3) dola million 300 zitalipwa in good faith ina maana hakuna kosa lililothibituka kufanywa na Acacia. Siyo sahihi kusema ni malipo ya kuanzia.

3) Hilo la ujenzi wa barabara halipo. Lakini kama sehemu ya social responsibility, kampuni itaendelea kusaidia jamii zinazowazunguka

4) Hilo la kusema watahusika na dhahabu, copper na silver pekee yaliyobakia yatakuwa mali ya Tanzania, tunataka kujiridhisha kwa ambacho hakipo. Nimefanya kazi katika migodi hiyo, zaidi ya hayo madini hakuna mengine ambayo yapo katika economic concentrations. Sharti hilo Barrick wamekubali kwa sababu halina athari yoyote kwao

5) Kuajiri na kuwafundisha watanzania, tangu makampuni haya yaanze, imekuwa ndiyo sera inanyoyaongoza. Hayo yamekuwepo wakati wote, ndiyo maana sasa hivi kuna watanzania kwenye senior managent positions. Mimi nilianza kwenye makampuni haya nikiwa junior geologist, nikapanda mpaka kuwa country manager. Nikaenda kufanya nje, nikiwa project manager, na chini yangu kukiwa na expatriates 71. Kwa hiyo ni kitu ambacho kimekuwepo. Na watanzania wengi walio na uwezo na nidhamu, wamepanda, na wengi wapo nje ya Tanzania.

6) Kutolala kwenye premises za kampuni sioni kama ni kitu cha kumsaidia mfanyakazi. Hiyo inamsaidia mwajiri. Inampunguzia gharama za kumhudumia. Pale Buly Barrick walitaka sana wafanyakazi wote wakae nje ya mgodi, tulio wengi, hasa tuliokuwa kwenye senior positions tulikataa.

7) Kazi zote kufanywa na kampuni za kitanzania. Hilo limekuwepo wakati wote. Sera inayoongoza kwenye makampuni haya kufuatia sera ya madini 2010 ni kwamba kunapokuwa na kazi, priority ya kwanza ni kampuni zilizomo ndani ya wilaya, kama hakuna unatafuta kampuni iliyomo ndani ya mkoa, kama hakuna, kazi inakuwa open kwa kampuni yoyote iliyopo Tanzania, ikishindikana unatoka nje ya Tanzania.

Mengi yaliyotajwa kwa wasiofahamu wataona ni mapya, lakini yalikuwepo siku zote. Jipya ni hilo la kugawana faida 50/50. Nalo hilo siyo la kupigia vigelegele. Huko Mwadui tulikuwa na 50/50 lakini mpaka leo tumepata nini.

Wengi wasichofahamu, makampuni haya hayapati faida kubwa kutoka kwenye mauzo ya dhahabu bali wanapata faida kubwa kutrade shares. Production inalenga kuwapa confidence shareholders ili shares ziweze kupanda. Mathalani kabla ya Brexit hisa za Acacia zilikuwa na thamani kama ya dola 2.5 hivi. Baada ya Brexit zilipanda mpaka kufikia dola 5. Walioamua kuuza hisa zao walipata faida ya 100%. Wewe kama unasubiria faida ya 50/50 unaweza kusubiri mpaka uchoke. Serikali itamiliki 16%, je tutakuwa tunauza hisa na kununua?

***********
NOTE

Acacia wametoa tamko kukanusha kuwa hakuna makubaliano yaliyofikiwa. Kwamba hayo ni maoni ya makubaliano ambayo yatajadiliwa na Kurugenzi ya uongozi wa wawekezaji wa acacia kisha ndio wataamua lipi pendekezo lipitishwe au la.

Je, wanaoshangilia wanachokishangilia ni kipi? Mafanikio yapi? Makubaliano yapi mnayosema yamefikiwa?

Ni kichaa tu anaweza kushangilia kuvuka mto wenye mamba wengi kwa mguu kabla ya kuvuka.

Kama mnajiamini na mko serious, pelekeni mikataba ya madini Bungeni na iwe wazi.

Kama mnajiamini, tekelezeni maoni ya report ya Kamati mbili za madini na kukubaliwa na Rais Magufuli.

Haya maigizo na kushangilia kuwa mmefanikiwa yanatia kichefuchefu, kinyaa, na kuonesha kuwa CCM inafanya Siasa katika mambo ya msingi ya kitaifa.

Maoni ya Kamati za madini yamefukiwa, gharama kubwa zimetumika, Rais Magufuli yuko kimya anashindwa kuchukua hatua kisha anajiita mtumbua majipu. Kisha wajinga wanashangilia. Kweli CCM ni janga la Taifa.

Solomon Kambarangwe

20/10/2017
 
Huyo mwandishi kasomea maswala ya uchumi kwenye madini au ni mwandishi wa habari za udaku?
 
Back
Top Bottom