Baregu Foundation for Peace and Development (BFPD) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baregu Foundation for Peace and Development (BFPD)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TANURU, Jan 18, 2010.

 1. T

  TANURU Senior Member

  #1
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Kutokana na ujuzi alionao na umuhimu wake katika taifa letu, tumshauri Profesa Baregu aanzishe taasisi ya BAREGU FOUNDATION FOR PEACE AND DEVELOPMENT (BFPD). Naamini wengi tutamuunga mkono na hasa vyombo vya habari na wanafunzi wa elimu ya juu. Moja ya shughuli kuu za taasisi hii iwe ni kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania kila wiki kupitia televisheni na redio.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. T

  TheUchungu Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wazo zuri..afikishiwe mdau mwenyewe kwa wale aliokaribu nae
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Zipo nyingine nyingi tu kama hizo. Ajiunge nazo kuziongezea nguvu. Aende MNF kwa kuanzia ambako kunafanywa SIASA zaidi.
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Iam strongly propose the motion. Hii ndio inatakuwa komesha jeuri ya serikali kwa kumtimua chuoni.Atengeneze ya kwake hana haja ya kuungana na wengine kama ndau mmoja alivyadai.
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kama ni hivyo, isiwe NGO kiwe chama cha siasa kabisa! Aachane na CHADEMA ambacho sio chake! NGO haitampa makali anayoyataka/mnayomtakia.
   
 6. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwani chadema ni cha nani tutoe mawazo kuwa chama ni mali ya mtu ina maana akianzisha kingine kitakuwa mali yake, chama chochote kile cha siasa ni mali ya wananchi hivi CCM ni mali ya nani, hana haja ya kuanzisha chama kingine cha siasa Chadema kinamtosha si vibaya kuwa na NGO sambamba na chama cha siasa.
   
 7. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wana JF na waTZ kwa ujumla msipate taabu sana. Huu ushauri uliotolewa hapa tayari Baregu amekwisha kwenda nao hatua 10 mbele. For your tip, something like this is coming under the name Great Lakes Inst. for Peace
   
 8. B

  Bull JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Professor amekwenda kinyume na contract aliyo saini kwenye kazi yake, nimzembe na hawajibiki. Hawa ndio wale wasomi wetu wasiofuata kanuni na maadili ya kazi wanaoendeshwa na maslai bila kujali professiopnal na responsibilty zake.

  Tunachosubiri atutajie ma-professor wengine walifanya ujinga kama wake (hata kama ni CCM) tuwawajibishe

  Kama yeye kavunja sheria ya kazi yake basi hafai na haaminki tena na jamii na hakuna excuse ya kuwa kuna watu wengine wanavunjasheria namimi acha nivunje. Huyu haf
  ai
   
 9. T

  TANURU Senior Member

  #9
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera zake sana. Tunaisubiri kwa hamu.
   
 10. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sentensi hii haiitendei haki Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) iliyoanzishwa na kubarikiwa na Mwalimu mwenyewe kwa ajili ya kuendeleza yale mema ambayo alikuwa akiyasimamia kwa manufaa ya nchi yetu, Afrika na duniani kwa ujumla.

  Kumwambia Baregu aende MNF ambako kunafanywa "siasa zaidi" ni kumpotosha Baregu, kupotosha watu na kuidhalilisha Taasisi. Zogo lililotokea baada ya MNF kufanya Kongamano la Kumbukumbu ya Miaka 10 ya Kifo cha Baba wa Taifa la Tanzania na baadhi wa watu kutoa madukuduku yao ya kisiasa kusiwe sababu ya kuipaka matope Taasisi ambayo lengo lake kuu ni kusaidiana na wananchi kujenga na kuimarisha Amani, Umoja na Maendeleo ya wote.

  Baregu si 'haini' ni Mtanzania kama Watanzania wengine mwenye uchungu na nchi yake. Naamini MNF itaweza kumpokea Baregu kwa mikono miwili endapo atataka kujiunga na Taasisi hiyo kwa madhumuni ya kusaidia Taasisi itekeleze/ifanikishe malengo yake kwa kufuata misingi ya ujenzi wa amani, umoja na maendeleo ya wote kama Mwalimu Nyerere alivyoagiza.
   
 11. N

  Nanu JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bull,
  Je sheria iliyovunjwa ni ipi na sheria inaapply kwa Baregu tu?
  Dr. Mvungi ni nani?
  Late Prof. Shayo alikuwa nani?
  Nawe akili zako ni za kukurupuka kama za huyo Ghasia.
  Naomba muangalie vitu kwa undani, marefu na mapana yake na practice inayoendelea nchini bila kuwa subjective. Lets be objective in our urguments, yes we learn how to disagree but we must give reasons to support our urguments!!!!!!!!
   
 12. B

  Bull JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Huwezi kuwa na cheo kwenye chama cha siasa na wakati huohuo ni mfanyakazi kwenye public corprtion kama alivyo saini agrement.

  Kama kunawatu walivunja sheria huyu kama Professor anatakiwa kulaani uvunjaji sheria sio kujiunga kwenye mkumbo, kwakizingizio eti fulani pia kafanya

  wasomi kama hawa wanapoona mwenzake kafanya ufisadi nae anajiunga!! wasomi namna hii hatunashida nao hapa Tanzania.
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Uko off topic hapa tunazungumzia Baregu Foundation na si ajira ya Baregu, kwa taarifa yako tu Baregu alishasema hana haja ya ajira hiyo.
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  tunashukuru kwa taarifa hiyo sasa imefikia wapi tujulishane mkuu
   
 15. B

  Bull JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Tutamuamini vipi kuendesha foundation wakati anazembea katika mambo ya terms na agrements?

  Huoni wasomi kama hawa ni hatari kumpa dhamana nzito yoyote? naaliniacha ho alipo jitetea wakati wa kunyimwa ku-extend contract.
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hapa umesema ukweli kabisa ila ni kwa sababu tu ya mambo ya siasa na vile kama akitoa yupo ndani ya CHADEMA basi anaonekana ni mtu wa ajabu sana
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu Bull
  Usichanganye mambo kuongoza NGO ni tofauti na kuongoza Chama cha Siasa, hata wewe unaweza kuanzisha NGO yako kutegemea na malengo yako na uwezo wako hakuna atakaye kuuliza kwa nini wewe umejiweka Chairman mke wako treasurer binamu katibu etc. tofauti na chama cha siasa ambacho malengo yake ni kushika dora kiongozi anakuwa answerable kwa wananchi.

  Kuhusu ajira ya Baregu nimesema hii thread haihusu hilo kuna thread nyingine inasema 'kwa nini Baregu amenyimwa kazi UDSM' nafikiri bado ipo tukutane huko bye.
   
Loading...