Barclays yapekuliwa, noti bandia zakamatwa kwenye sanduku

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,521
9,325
Pesa.jpg


Jeshi la polisi jijini Nairobi nchini Kenya linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kumiliki pesa bandia aina ya dola za Kimarekani zenye thamani ya $20 milioni (zaidi ya shilingi bilioni 46 za kitanzania) zilizopatikana ndani ya chumba cha kuhifadhia fedha cha tawi la Benki ya Barclays.

Pesa hizo ilizokuwa zimetunwa kwenye sanduku maalum la fedha zinazoingia benki (deposit box), zilikuwa zimewekwa kwa mfumo wa noti za $100, kwa mujibu wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

“Noti hizo bandia zilikuwa kwenye mfumo wa dola 100, tumezikuta kwenye sanduku salama(safe box) ndani ya benki,” akaunti rasmi ya twitter ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ikiambatisha na picha ya sanduku hilo lenye fedha.

Kati ya watu hao sita waliokamatwa Jumanne, walikuwemo watu wanaoaminika kuwa ndio wamiliki wa sanduku hilo pamoja na maafisa wawili wa Benki hiyo.

“Mteja wetu asiyemwaminifu aliyekuwa na sanduku binafsi la kutunzia fedha benki katika tawi la Queensway alikamatwa na polisi akiwa kwenye tawi hilo,” taarifa ya Benki ya Baclays imeeleza.

“Mteja huyo anadaiwa kutunza fedha bandia kwenye sanduku lake binafsi ndani ya tawi, kinyume cha sheria na kanuni za kibenki,” Barclays waliongeza.

Uongozi wa benki hiyo umeeleza kuwa wanaendelea kushirikiana kwa karibu na jeshi la polisi katika kufanikisha upelelezi wa tuhuma hizo.
 
Back
Top Bottom