Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,301
- 4,681
ama kwa hakika ni tarehe 13 ya mwezi wa 9 ktk dimba la Nou Camp ambapo kutakuwa na mechi kati ya mabingwa watetezi wa klabu bingwa barani Ulaya yaani Barcelona watakapo pambana na mabingwa mara 7 wa kombe hilo na pia ni timu yenye mafanikio yaani makombe mengi zaidi ya kimataifa kuliko klabu yoyote hapa ulimwenguni hapa naizungumzia klabu ya Rosonelli au AC Milan yenye maskani yake barabara ya Turati mjini Milan Italia.
kocha wa Barca Giussepe Guardiola kama jina lake linavyotamkwa kwa kitaliano ameizungumzia AC Milan kuwa ni timu kubwa na yenye hadhi ya juu kabisa ktk utawala wa soka hapa ulimwenguni na ameeleza wazi kutoisahau kumbukumbu ya kipigo cha Mbwa koko cha goli 4-0 walichokipata Barcelona toka kwa AC Milan na yeye akiwa uwanjani kama mchezaji wa Barca mwaka 1994, ikumbukwe hii ilikuwa ni ktk mechi ya fainali ya kombe hilo.
''Sijawahi kupata fedheha kama ile, hakika Milan walitukamata, na wakatufanya walichotaka, hakika sikuweza kuwa na ujanja, Desaily na Albertini walinifunika ktk kiungo''...amenukuliwa Guardiola mapema leo.
Milan itaingia uwanjani ikiwategeme wachezaji wake mahiri kama sentahafu bora ulimwenguni Alesandro Nesta ambaye inaaminika hajawahi kutokea mkoba mahiri na imara kama yeye tangu alipoondoka Franco Baresi ambaye ni nahodha wa zamani wa AC Milan.
Pia Milan itawategemea viungo mahiri na wenye uzoefu mkubwa mno hapa nawazungumzia MVB yaani Mark Van Bommel, Brigadia Jenerali masimo Ambrosini na Dikteta wa kiungo Clarence Seedorf.
Pia Milan watakuwa na nguli mwenye uwezo wa kupiga mashuti na miguu yote hapa namzungumzia kevin Prince Boateng.
Pia safu ya ushambuliaji ya Buluda itakuwa na kiungo mwenye uwezo wa kupeleka pasi Mlandizi kisha akaifuata na kuichukua tena na kuipeleka Kigamboni kabla ya kupiga pasi ya mwisho itakayomkuta mfungaji.
Kiungo huyu ni Alberto Aquilani atakayekuwa anawalisha mipira Super Pato na Antonio ''MUSOLIN'' Casano.
Kwa upande wa Barca wao watakuwa na Refa, Line men wawili pamoja na kamisaa kama ilivyokawa kawaida yao.