Barcelona tumeumizwa tena. Ukuta wetu ni mbovu!

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Barcelona wenzangu Valencia wametupiga 2-1 mchezo wa fainali kombe la mfalme, nilivyoyaona magoli yote mawili tuliyofungwa ni uzembe wa wazi wa defenders ukiongozwa na Pique, hivi lini tutaimarisha ukuta wetu? Huyu Pique anasubiri nini kutimuliwa?

Ameshafungisha goli nyingi hadi sasa lakini bado yupo tu.

Nashangazwa na benchi la ufundi kutokuwa na hamasa ya kurekebisha makosa kwa kusajiri wachezaji wengi ambao si tunaowahitaji ama uwezo wao unakua mdogo.

Na hii yote ni kutegemea timu iendeshwe na viungo tu mwishowe kuwachosha.
Messi akichoka itakuwaje?

Kiukweli Messi mchezaji bora duniani inabidi awe na watu pembeni si mtu kama Suarez wa kujiangusha na kukosa nafasi za wazi kibao

Barca wenzangu nini kifanyike pale nou camp? Wenzetu wanajiandaa kwa season Moja kwa usajiri sisi tunasua tu mara tunamtaka Griezman mara hatumtaki.

Neymar siku za nyuma alionesha nia ya kutaka kurudi wakubwa pale wakambania.

Messi aliwaomba wamruhusu wakaizima hiyo issue lkn mtu kama Neymar au Mbappe ndio hasa watu wa kiwango cha kucheza na Messi.
 
Kumbe ndiyo unajuwa sasahivi Kuwa Barca haina Beki? Pale tulipowaambia Kabla ya mechi ya Liverpool mukabisha?
Nkiangalia ukuta wa barca sioni mchezaji hata mmoja anaeweza kwenda Madrid akapata namba. Mafanikio ya mess yamesababisha uongozi ujisahau katika kuimarisha kikosi upande wa ukuta, imefikia sehm mpaka mchezaji anaetumia mguu mmoja tu lenglet amekua ndo bekwa kutegemea wa kati, kiungo Sergio Roberto eti ndo beki wa kutegemea wa kulia.

Barca amekua akipigwa sana counter attack. Hata usajil wa sasa hv wanahangaika na grezman wakat wana tatizo kubwa kwenye ukuta. Barcelona ya sasa hv kuja kutisha tena labda arudi pep aanze kuisuka tena.
 
Waambie waje wachukie beki wa yanga, zahera anatafuta wateja

Tuwapeleke kwa mkopo Zana Coulibaly na Paul Bukaba. Wangefit sana kwenye hiyo beki ya kulia na ile ya kati. Yanga wazee wa kazi wanastahili Real Madrid ya Zizzou.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom