Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,406
- 31,387
- Thread starter
- #41
Hiyo three course meal imeniacha hoi, ha ha ha !Tanganyika hawaogopi kuvunja muungano Barubaru, as a matter of fact, mjadala ya muungano haujageuzwa kuwa three course meal kama ilivyo kwa Zanzibar. Kinacholeta shida hapa ni hizi kelele za 'divorce' lakini hakuna mtu anajaza fomu za talaka - for years! Mtu unasema unataka talaka lakini wakati huo huo unamtayarishia maji ya kuoga na chakula mezani kawa kawaida - hivi hapo unadai talaka au unataka kujua kama una bei?
Taratibu za kuachana na ndoa zinajulikana, hizi geresha za nini? Au mnatishia ili bill ya umeme mlipiwe tena?
kuhusu Talaka Mkuu Mkandara alishawahi kuweka usemi wake kuwa 'Kadhi kaingia mjini wanandoa hawataki kudai talaka' ndicho kinachoonekana.
Ukisoma makala ya Ahmed, amesema inatakiwa kuwa na mkataba ambao nchi zote zitakuwa sawa bila mmoja kuwa mshiriki mkuu. Katika mambo wanayotaka yawe ya mkataba ni pamoja na Ulinzi na Usalama ambao bajeti yake ni Bilioni 900+. Bajeti ya ZNZ ni sh Bilioni 600. Sasa hapo tukigawana usawa ZNZ watabaki na nini?
Maana ya usawa si maneno ni ushiriki ati, vinginevyo Tanganyika itabeba sehemu kubwa na hapo suala la ushiriki mkuu halitaepukika
ZNZ kamwe hawataki kuomba Passport yao kwasababu kubwa moja, wakiwa nayao tayari ni wageni.
Maana rahisi ya mkataba ni kuwa 'tuwasaidie' ili waendeleze nchi yao kwa rasilimali zetu, ukisema zao haraka haraka wanapeleka mswada kama ule wa gasi na mafuta.
Sasa tunajiuliza ni mkataba wa kitu gani ambao Mtanganyika atasema naam ushikirikiano una manufaa.
Huwezi kuwasikia wanadai sarafu yao kwasababu wanajua kuwa vitu kama umeme vitakuwa kwa dola.
Kwa ufupi mkataba wanaotaka ni wa mambo haya:
1. Urahisi wa kuwekeza bara (halinatabu hili kama wanataka maana tunakaribisha wawekezaji kwa taratibu maalumu )
2. Ardhi (linawasumbua kichwa sana, Waitaliano taratibu wanawahamisha kwenda pembezoni)
3. Soko la Ajira ( WZNZ walioajiriwa bara ni wengi kuliko walioajiriwa na SMZ,nje ya muungano kitumbua kidogo)
4. Soko la Biashara (Kontena 800 walizolalmika TRA inawawekea kauzibe zilikuwa zinaingia bara, mfano mmoja tu)
5. Ruzuku (Bajeti yao haijitoshelezi, karafuu na utalii vina ushindani sana duniani)
6. Ulinzi na usalama (Hawana bajeti hata ya senti tano, wamestarehe mgongoni wanakula halua)
7. Elimu ya juu ( Hawana bajeti hata senti tano, watoto wanasoma kwa social welfare ya Tanganyika)
8. Wastaafu na Mishahara (Yote inatoka Hazina Dar, wanataka tuendelee kuwalea wastaafu wao na wafanyakazi)
9. Supplies (Wanajua nje ya muungano na sarafu tofauti, biashara itakuwa katika mizania ya 'world currency')
10. Bandari huru (wanajua access ya bidhaa zao EA ni kupitia Tanganyika, Tanganyika ikiwa na bandari huru kwishnehi)
11. Energy(wanajua hawana vyanzo mbadala vya nishati kama umeme, nje ya muungano no free ride)
Ninachosema hapa ni kuwa mkataba maana yake ni kuweka mambo yatakyowasaidia.
Hakuna jambo hata moja, narudia hakuna jambo hata moja Tanganyika itawahitaji ZNZ! None!
Sasa tunahitaji mkataba nao wa nini?