Barazani Kwa Ahmed Rajab: Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barazani Kwa Ahmed Rajab: Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nguruvi3, Sep 17, 2012.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  ............  Uchambuzi wangu: Chanzo cha taarifa hii ni makala katika gazeti la Raia mwema wiki hii.

  Ili wasomaji waweze kuelewa hoja zangu vema nimeziwekea namba kwa minajili ya kuzjibu bila kupoteza maana. Ahmed Rajab amenishangaza na jinsi anavyobadili misimamo kila uchao 'change his position' kuhusu suala hili.

  Ukisoma namba (1) anasema Tanganyika ni ndugu halafu anawaita nchi ya kigeni (16). Namba (2) anasema tume itakusanya maoni ya wznz kikamilifu hata kama tume hiyo inakusanya pia kutoka Tanganyika. Hapa anaonyesha kuwa wanaolilia hatima ya muungano ni ZNZ na siyo Tanganyika. Kwa mantiki hiyo wangeweza kufanya kura ya maoni wao kuamua hatima yao bila kusubiri tume.

  Namba(3)na (8) anasema maamuzi kuhusu muundo wa muungano. Hapa anaikana hoja yake ya siku nyingi ya kutaka ZNZ ijitenge ili iwe kama Malyasia au Mauritius kama alivyowahi kuandika. Sasa anakiri kuwa WZN wanahitaji muungano. Wale wanaomfuata wamebaki njia panda kama alivyowaacha katika suala la serikali 3.

  Namba (4) anashadidia hoja kuwa WZNZ wanataka muungano. Anamkana hata Maalim anayetaka ZNZ ijitenge. Tena anarudia hoja ya mkataba

  Namba(6) anawatukana Watanganyika kuwa hawaelewi maana ya mkataba. Kwamba Watanganyika ni sawa na WZN wanaomwitikia hata pale anapoandika upuuzi. Kama anadhani hatuelewi mktaba angalia hoja zake zote ametaja mkataba bila kutuambia ni wa kitu gani(11). Huyu msomi wa ZNZ anataka tukubaliane na mawazo yake hata kama yana mapungufu, hayafai au ni ya elimu ya chini sana.

  Namba (7)anasema muungano hauna manufaa ZNZ wakati huo huo anataka muungano (3)(4)(8)

  Namba (9) anasema nchi zitaunganishwa kwa mkataba. Hajasema wa mambo gani. Namba (10)Anasema utaratibu wa ushirikiano wa nchi mbili zilzio sawa. Kwasahivi hakuna usawa kwasababu nchi moja inajiona mshiriki mkuu(12) Hasemi kuwa ushiriki mkuu unatokana na ukweli kuwa Tanganyika inatoa 100% na ZNZ 0%. wakati huo huo anataka kuwe na usawa(12) kwamba mmoja atoe sana na mwingine apokee huo ndio usawa anaouongelea.

  Namba (11) anataja mkataba na ushiriki wa mambo, asichojaribu kukiandika ni kuwa mkataba wa ushiriki wa mambo gani. Hilo hajaweza kulisema wakati huo huo anatukana Watanganyika kuwa hawajui mkataba maana yake nini. Laiti angelijua maana ya mkataba asingekuwa anahangaika kila siku kuandika kitu asichokijua

  Namba(13)anatolea mfano mzuri wa EU. Huyu mwandishi ni waajabu sana, alianza na kuvunja muungano ZNZ iwe kama Malaysia, akabadili kuwa na serikali 3, akaja mkataba sasa anatupeleka EU. Maana ya kuwa na EU ni ili WZN wafaidike na rasilimali za Tanganyika bila Watanganyika kufaidi rasilimali zao kama alivyoonyesha namba(16)(17)

  Namba (14)Anashauri tuwe na muungano kama wa Senegambia wakati huo huo anasema ule ulishindwa (15). Ahmed anataka tuige uchafu ili mradi tu tuwe na mkataba anaotaka yeye. Anaandika jambo na kulikanausha hapo hapo, ushahidi wa kiwango dhaifu sana cha uandishi.

  Namba(16)kama hataki ZNZ iingiliwe katika mambo yake basi ashauri muungano uvunjwe. Kwanini anatapa tapa na serikali 3, mkataba au mfumo wa EU. Kitendo cha kuwa na mkataba tayari ZNZ inapoteza uhuru sasa sijui anataka mamlaka kamili yapi. Mwandishi Ahmed anajichanganya na sina uhakika anajua anaandika nini.

  Namba(17)Huko nyuma amesema mkataba utakuwa na kura ya turufu, hapa anasema kila nchi itakuwa na uhuru bila kuomba ridhaa ya nchi nyingine. Too low Ahmed

  Watanganyika, hapa tulipo hatuna sababu ya kuwa na ushirikiano na ZNZ kwasababu ZNZ haina kitu cha maana cha kutoa. Wao wanataka kuwe na ushirikiano kama wa EU ili waendelee kuinyonya Tanganyika.

  Ukweli ni kuwa yale madai kuwa Tanganyika inaizuia ZNZ sasa ni wazi ni uongo uliotukuka. Zanzibar haina ujanja inataka muungano kwa hiari au kwa lazima. Hizi habari za serikali 3, mkataba wa EU, wa Uswiss ni kutapa tapa kwa kutambua kuwa nje ya muungano atakayepigika na kuumia ni ZNZ.

  Ahmed Rajab aache kututukana kuwa hatujui mkataba, yeye ndiye hajui kwasababu hajataja jambo hata moja. Ukweli ni kuwa anataka ushirikiano ili Tanganyika itoe rasilimali zake kama alivyosema katika ulinzi na usalama ambapo ZNZ haina bajeti, elimu ya juu ZNZ haina bajeti, soko la ajira ambalo ZNZ haina, soko la Biashara ambalo ZNZ haina, Ardhi ambayo ZNZ haina n.k. Hicho ndicho anataka katika hoja ya mkataba.

  Tayari tuna EAC, SADC na UA, tukutane huko kama nchi huru. Upuuzi wa kusema eti tutawavutia wengine ni umahaluni wa hali ya juu. Tuwavutie kwanini wakati tayari tuna ushirikiano. Hatunatutakachopata kwa ushirikiano wowote ule, sisi tutakuwa losers na hapa ni wakati tuwaambie kuwa Wanatuhitaji na wafunge midomo, kinyume chake LET ZNZ GO!

 2. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Bela Mwagito, ulongile hilo. Khuuu!
   
 3. miftaah

  miftaah Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza Zanzibar... Muungano baadae na kwa hili Inshallah litawezekana.

  Uchambuzi wangu: Chanzo cha taarifa hii ni makala katika gazeti la Raia mwema wiki hii.

  [/QUOTE]
   
 4. morphine

  morphine JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 2,566
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  tutafika tu, all we need is time and wise decisions
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nguruvi3.
  Asante kwa uchambuzi wako. Kwa hakika nimejitahidi kumsoma Rajab lakini sikuelewa kabisa alichokuwa anazungumzia.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Ipi unadhani ni wise decision
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi, wakati huo huo ANAWATUSI Watanganyika kuwa hawajui mkataba, laiti wangejua wangemuunga mkono. Anataka muungano wa Senegambia anaokiri kuwa ulishindwa! yaani ni flip flop tupu.

  Kilichodhahiri ni kuwa anautaka muungano tena kwa mbinde.
  Alipokuwa UK alikuwa anadhani mambo ni rahisi sasa hivi karudi Unguja anaona kwa macho yake jinsi mtu wa kawaida anavyoutegemea muungano na Tanganyika katika survival yao.
  ZNZ watake wasitake wanautaka muungano hawana ujanja, nje ya hapo maumivu makubwa sana.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,056
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,

  ..kama sijakosea kuna kipindi CUF walikwenda mahakamani kudai kuonyeshwa mkataba wa muungano.

  ..kwa maana nyingine mkataba huo upo, na hivyo kisheria muungano tulionao sasa hivi ni muungano wa mkataba.

  ..sasa mpaka hapo utaona kwamba Mzee Rajab anatuchanganya wasomaji wake.

  ..ukimfuatilia zaidi anapendekeza kwamba Tanganyika na Zanzibar tuige nchi za ulaya kuhusu mfumo wa European Union.

  ..Well, hiyo inaitwa Europen Union, lakini tafsiri ya mfumo huo ktk lugha ya kiswahili, ni JUMUIYA YA NCHI ZA ULAYA.

  ..mpaka hapo utaona kwamba at best Mzee Rajab can not explain what he means, and at worst anawadanganya wasomaji wake.

  ..kama anachokipendekeza kiwepo baina ya Tanganyika na Zanzibar ni mfumo kama wa Jumuiya ya Ulaya, then mataifa haya mawili[Tanganyika + Zanzibar = Tanzania] tayari yapo ktk Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC. Kinachopaswa kufanyika ni kubadilisha tu toka kuwa nchi moja mwanachama kuwa nchi mbili wanachama.

  ..Mkataba wa EAC, unaofanana sana na wa EU, tayari upo, hakuna haja ya kuwa na mkataba mpya kati ya Tanganyika na Zanzibar.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Joka kuu, absolutely anawachanganya watu.
  Unajua baada ya hoja za serikali 3 na mkataba kuonekana hazina mashiko hasa kwa Tanganyika, Ahmed na Maalim Seif wanajitahidi kuingiza mambo kama EU. Tunajiuliza kama tunataka jumuiya si tayari ipo ya EAC?
  Hivi ni kwanini ZNZ inayotaka kuwa huru isijitoe katika muungano kabisa?

  Uongo unaweza kusemwa na kuwa ukweli, lakini uongo hijidhihiri wakati ukifika.
  Baada ya Watanganyika kusema hewala enendeni kwa amani, ukweli umetimia WZN wanaona muda wa kutishia nyau umekwisha.

  Ukweli usio na kificho ni kuwa ZNZ inahiitaji Tanganyika na wanahitaji muungano kuliko Watanganyika.
  Ukisoma, Ahmed anasema muungano wa miaka 48 usio na manufaa kwa ZNZ, halafu hapo hapo anasema anataka mkataba wakati huo huo anaomba mkataba wa mwaka 1964.
  Confusion tupu na sijui kama huwa anakumbuka makala iliyopita aliandika nini.

  WZNZ sasa tulieni mlelewe, fungeni midomo maana hamna hoja tena! mnautaka muungano tena kwa mbinde.
  Kitendo cha kudai serikali 3, mkataba, muungano wa EU, muungano wa Uswiss ni kwa kutambua kuwa muungano una manufaa kwenu, hata Ahmed anajua hilo.

  Tatizo ni pale Ahmed anapolazimika kutumikia pande mbili, ya WZNZ wakawaida na ile ya Sultan.
  Ndio maana anajichanganya bila mpango.
  Anawadanganya huyu Mcomoro mwisho wa siku atarudi Uingereza na kuwaacha mkisaga meno
   
 10. y

  yaya JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu jasusi, nashukuru kwamba tupo wengi ambao hatukumuelewa huyo Mhe. Rajab.
  Ameshindwa kabisa kupangilia hoja zake. Amejichanganya mno.

  Mimi naungana na wale wanaoshauri kwamba kuliko kuendelea kutokwa na povu mdomoni, kwa nini wasijitoe katika muungano wa sasa kupitia kura ya maoni kwa sheria itakayotungwa na kupitishwa na baraza lao la wawakilishi?
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,056
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,

  ..tatizo ni kwamba Maalim Seif, Ismail Jussa, Mansour Himid, na Ahmed Rajab, wameamsha hamasa za wa-ZNZ on something they r not willing to deliver.

  ..hizi kauli za ujanja-ujanja na ubabaishaji ni matokeo ya kutowaambia ukweli wa-ZNZ toka mwanzo wa harakati hizi.

  ..wa-ZNZ wanadai kwamba MUUNGANO ni sawa na UKOLONI. Wanadai waachiwe wawe huru, au "wapumue." Swali kwa Ahmed Rajab ni kwamba, je "muungano wa mkataba" siyo sawa na "UKOLONI WA MKATABA"??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Hili kundi linawafanya WZN waonekane mazuzu bila sababu. Hao ndio waliomba mkataba wa mambo 11 ya mwaka 1964.
  Wakatishia kwenda UN eti sasa wanataka muungano wa mkataba, sasa mkataba ni upi tena mbona upo tayari?

  Wakadai kuna mambo 21 yameongezwa nje ya yale 11, tukawauliza katika hayo 21 wataje moja linaloinufaisha Tanganyika, hawana jibu. Hoja ya mkataba wa mambo 11 ikafia baharini.

  Kundi hilo likwadanganya WZNZ kuwa kuna uwezekano wa serikali 3. Tutakuliza hiyo ya 3 inahitaji nini wakati ZNZ inataka kiti UN na EAC? Hawakuwa na jibu wakahamia kwingine.

  Sasa wanataka muungano wa mkataba kama wa EU. Kwanza hawajui kuwa EU siyo mkataba ni jumuiya bado wanaomba kitu wasichokilewa.

  Wamesema wanataka kuwa na mkataba kama wa Uswiss. Tukauliza huo wa Uswiss ukoje? Hawana jibu kwasababu tu kasema msomi mmoja basi wanaimba kibwagizo.

  Wanasema muungano wa sasa hauna faida kwao, vema sana kama wamelitambua hilo, sasa wanataka mkataba wa nini?
  Nimewahi kusema huko nyuma na narudia tena, tatizo la WZNZ ni umimi,ubinafsi, kujiona bora unaochagizwa na uelewa finyu sana.

  Ndio maana wanaimbishwa na kupigishwa kwata na Ahmed left right, upside down hata bila kujua wanakwenda wapi.

  Mzalendo.net fungeni mdomo kwasababu ZNZ inaihitaji Tanganyika, Tanganyika haihitaji ZNZ kwa lolote.
  Washirazi watawaweka pabaya wana ajenda yao kama hamjui ndio maana wakibwanwa wana change position kila siku.

  Tanganyika tunasema hatutaki mkataba, serikali 3 au EU kwasababu vyote hivyo ni kuwabeba na mkiwa mgongoni mnafungua vinywa na kucheza hovyo!

  Makala hiyo ya Ahmed ambayo Baru baru anasema ni msomi anayejenga hoja ni AIBU tupu.

  LET ZNZ GO!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wenzangu mna moyo.. mimi nawaona tuwaunge mkono muungano wa mkataba kwa masharti kwanza Zanzibar wajiondoe kwenye Muungano huu wa sasa. Wakishatoka ndio Tanganyika tuamue kama tunataka muungano wa kimkataba. Kwa hiyo tuwashauri Zanzibar wajitoe kwanza kwenye muungano huu.. Let ZNZ Go!
   
 14. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  katika vitu na viunga mkono kwa nguvu zote ni " Let ZNZ Go" itakuwa vyema sana likitokea hili ili tujipange manung'uniko ni dhambi aiseeeeeee
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nguruvi3,
  Unajua tuna tatizo kubwa sana na viongozi wetu hasa hawa wa Zanzibar wenye tamaa ya madaraka. Kingozi huyu huyu anayedai serikali kukusanya mawazo ya wananchi lakini yeye pia anatupa majibu hata kabla mawazo ya wananchi hayajakusanywa kwamba Wazanzibar wanataka pawepo na Muungano wa (4) nchi mbili lakini uwe Muungano wa Mkataba na si wa Katiba.

  Huyu ni kiongozi kafanya lini ukusanyaji wa mawazo haya au ndio propaganda za kuwajaza Ujinga wanchague nini!..Leo bila hata aibu, anasema yote haya toka kichwani mwake kuwa ndio maoni ya Wazanzibar wakati zoezi la kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi yanaendelea, sasa ili ijewe? kama sio yeye mwenyewe kujiona juu ya wananchi wenyewe!..

  Huku bara wananchi wanapewa Uhuru wa kufikiri na kutoa maoni yao pasipo kujazwa Ujinga lkn maajabu ya Mungu ukimya wa viongozi wa Bara unawatia wasiwasi vibaraka kama hawa wanaopenda sana kuwapachika watu madudu vichwani. Yeye alitaka viongozi wa bara waseme nini mbele ya zoezi hili la kukusanya maoni na kuyaratibu ikiwa tayari Wazanzibar wamejazwa Ujinga na watu kama hawa...

  Kwa nini asifanye hekima kidogo kusubiri maoni ya wananchi, kutozungumzia mfumo wa Muungano kwa Mkataba ili awape heshima yao wananchi wenyewe wachague ni muungano gani wanaoutaka kama tunavyofanya bara, hakuna mtu amejazwa Ujinga na viongozi wa nchi wala chama wachague ama wakubali muungano wa aina gani..
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, yaani naona wewe kama una moyo zaidi maana hata kuwapa nafasi ya pili ni moyo.
  Mimi naona tuwaunge mkono waondoke katika muungano huu usio na faida kwao kabisa, wakishajifunza watarudi kuomba mkataba wakiwa na adabu.
  Ndio maana kila siku tunasema LET ZNZ GO
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Mkandara, yaani kila mtu akiichambua hiyo makala anakuja na kitu kipya cha kushangaza.
  Hili lako pia nilikuwa sijaliona.Hivi kweli anasema watu waachwe watoe maoni halafu anasema wao wanataka mkataba! Haa!
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii article ya Ahmed Rajab ni kizunguzungu tupu! Maalim Seif anazunguka dunia sasa akishawishi wakubwa ili Zanzibar iwe na kiti chake UN. Kwa maneno mengine Maalim Seif anataka Zanzibar iwe dola kamili. Sasa kama anataka dola kamili hatua sahihi za kuchukua ni zipi, kupeleka muswada BLW au kwenda Marekani na UK kupiga porojo?

  Mambo ambayo ningeta kumuuliza Rajab:

  1. AG anataka muungano unaofanana na Switzerland - (kwa vipi, Swiss wameungana kivipi?)
  2. Rajab alikuwa anaongelea serikali 3, kabali mwelekeo lini na kwa nini?
  3. Sasa hivi Rajab anataka muungano wa mkataba. What excatly anataka kiwe kwenye mkataba, na Zanzibar wanaweka nini mezani?

  4. Kama nia ku-copy & paste EU, kwanini tusikutane Addis - AU? au Arusha - EAC?
   
 19. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bw, Nguruvi3

  Naona bora tukualike siku moja katika midahalo ya "live" hapa ZNZ ukutane na vijana wa "tuachiwe tupumue" kama hutarudi Tanganyika kwa miguu. Hapa naona mnapeana sifa za kilevi. Wanaotaka Muungano hao vingunge wenzio, juzi tu , wametuletea mamulki kutoka Tanganyika ili wapige kura uchaguzi mdogo Bububu.

  Wanaolazimisha Muungano ni hao vingunge wenzio wanao gawa hela ili watu watoe maoni ya kukubali Muungano kama ulivyo sasa. Pesa zinatoka Tanganyika ni mpango maalumu. Lakini dawa yenu iko jikoni iko siku mtajuta kulazimisha Muungano.
   
 20. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi umelewa pombe au ndio vijana wa siku hizi ...unakula vitu vya "pelle" unaoneka uko na nishai.
   
Loading...