Baraza labandua matangazo ya uchochezi kupinga Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza labandua matangazo ya uchochezi kupinga Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 28, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h]


  Na Mwinyi Sadallah  28th2012
  Baraza la Manispaa Zanzibar, (ZMC), limebandua matangazo ya kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyokuwa yamebandikwa sehemu mbalimbali za manispaa hiyo.

  Matangazo na vipeperushi yalianza kubandikwa usiku wa kumkia juzi katika nyumba za ibada, majengo ya serikali na majumbani kwa watu kwenye mitaa ya mji Mkongwe wa Zanzibar.

  Matangazo hayo na vipeperushi vinasomeka “kudai utaifa wa Zanzibar ndiyo dhamira ya Mapinduzi ya 1964” walipindua Wazanzibari tujitawale” “usiseme Muungano sema wa mkataba tuu” . “Tuacheni tupumue” yanasomeka huku wanamapinduzi wakiwa katika picha ya pamoja akiwemo Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Sheikhe Amani Karume.

  “Maoni ya Wazanzibari kutaka Muungano wa mkataba yaheshimiwe” yanasema matangazo hayo yenye picha ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein, akihutubia wanachama wa CCM .

  “ Kataa malaria, kataa Ukimwi, kataa Muungano wa serikali mbili’ vinaongeza vipeperushi hivyo.

  Vipeperushi na matangazo hayo yaliibua mijadala mikubwa hapa Zanzibar kutokana na kubeba ujumbe mkali dhidi ya Muungano pia yakiwa na picha za Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Rais wa kwanza hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

  Mkurugenzi wa ZMC Rashid Ali Juma, alisema waliamua kuyabandua matangazo na vipeperushi vya kupinga Muungano kuanzia jana kwani yamebandikwa kinyume na sheria.

  Alisema kwa mujibu wa sheria matangazo yoyote yanatakiwa kabla ya kubandikwa muhusika kueleweka , pia ujumbe wake ukaguliwe, yalipiwe na yazingatie mila na utamaduni pia yasiwe ya uchochezi.

  Juma alisema matangazo ambayo yamebeba ujumbe wa uchochezi kwa mujibu wa sheria hayaruhusiwi kubandikwa na kuonya kuwa matangazo hayo na vipeperushi yamekuwa yakibandikwa katika nyumba za ibada, masoko, majengo ya serikali na katika vituo vya umeme kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

  Alisema matangazo hayo yalianza kuonekana usiku wa kumakia juzina kwamba ZMC inaendelea kuwatafuta walioyabandika.

  “Tumeyabandua kwa sababu yamebandikwa kinyume na sheria za nchi,”alisema. Masoko yote yamevamiwa na kubandikwa matangazo ya kupinga Muungano wetu tumeanza kazi ya kubandua katika soko la Darajani na Mwanakwerekwe.”alisema Mwamvua.

  Aliongeza kuwa baada ya kubandua matangazo hayo watabandika onyo kuwataka watu kuacha kubandika matangazo au vipeperushi bila kufuata taratibu na kisheria.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema CCM haihusiki na matangazo hayo ya kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Alisema kama wapo viongozi wanaopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar walitakiwa kutumia vikao au Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa maoni badala ya kuwasemea uwogo viongozi ambao wamefariki dunia.

  “Matangazo hayo na vipeperushi sio ya CCM na tuna laani vikali kitendo hicho.”alisema Vuai.

  Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Zanzibar wamekuwa wakiwekewa vipeperushi vya kupinga Muungano katika vikapu hasa wanaofika katika soko la Mwanakwerekwe na soko Kuu la darajani Zanzibar.

  Kamishna wa Jeshi la Polisi Mussa Ali Mussa, aliiambia Nipashe kuwa hadi jana polisi haijapokea taarifa kuhusu tukio hilo.
  Matangazo hayo yameibuka huku Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ikiendelea na kampeni zake msikitini za kutaka Zanzibar kujitenga.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wazanzibar Muungano hawautaki imekuwa ni sindikizo la kutumiwa vyombo vya Dola kuwakandamiza na kuwashurutisha waukubali kwa nguvu.

  Jee kwani kuna kipi cha hiari ikiwa Muungano ni Ridhaa ya nchi mbili na nchi moja imeamua kutoka katika Muungano huu ,jee nizambi?.

  Huwezi kulazimisha kitu kisicho takiwa, na hili limewafanya Wazanzibar kuukataa Muungano huu na kuono Fake pale kilipotokea kifo cha Tanganyika ambaye alikuwa ndio mshirika mkuu wa Zanzibar .
   
 3. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Waanze kujilipua ndio wataeleweka.
   
 4. B

  Bwanamdogo Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ningekua na mamlaka kilichokuwa kinatakiwa ni kuitisha kura ya maoni Zanzibar kuhusu muungano na ningeweka maswali mawili tu: 1. Ninataka Muungano 2. Sitaki Muungano. Kwani nionavyo mimi Wazanzibari wamewachoka watanganyika kisingizio cha kudai mfumo wa serikali tatu ni geresha tu maana km kweli ingekuwa ni kutaka serikali tatu Tume ya katiba inakusanya maoni hilo lingepelekwa huko. Lakini sasa hivi kinachofanywa ni kusingizia kurudisha serikali ya Tanganyika ambayo watanganyika wenyewe hatuwasikii wakiidai hivyo kwa jinsi mambo yanavyokwenda ni muda muafaka sasa watawala wawape nafasi wazanzibari wapige kura ya maoni km wanautaka muungano au la.
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,818
  Likes Received: 36,911
  Trophy Points: 280
  Free zanzibar!!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Muungano hautavunjika sababu ya kusambaza vipeperushi. Kuna njia mbadala za kuuvunja naona mnachelea kuzitumia ili kutimiza azma yenu
   
 7. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Free zanzibar
   
 8. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  kinachowafanya wakimbilie viwanja gezaulole ni nini kama hawataki muungano wajiondoe kiujumla
   
 9. W

  Wajad JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 1,131
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 180
  Baraza kubandua matangazo ni sawa na kukata jani la mgomba, kesho lin
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  kikwazo cha Zenj huru ni CCM! Ajabu Wazenj hawajui hili!
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  kikwazo cha Zenj huru ni CCM! Ajabu Wazenj hawajui hili! Wajinga kweli
   
 12. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  umaskini wafikira
   
Loading...