Baraza la Wazee CHADEMA lazungumzia wazee wa CCM kuondolewa kwenye vikao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Wazee CHADEMA lazungumzia wazee wa CCM kuondolewa kwenye vikao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Feb 14, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]
  TAARIFA KWA UMMA
  [/FONT]

  [FONT=&amp]MAONI YA BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA JUU YA MAAMUZI YA CCM KUWAONDOA WAZEE KATIKA VIKAO VYA MAAMUZI
  [/FONT]

  [FONT=&amp]BAADA ya Watanzania wengi kutaka maoni ya Baraza la Wazee wa CHADEMA, juu ya uamuzi wa CCM, kupitia kwa kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, kuwaondoa wazee, wakiwemo marais ambao waliwahi kuwa wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu, tumeonelea ni vyema kusema kama ifuatavyo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Uamuzi huo wa CCM, ambao ni sehemu ya mabadiliko ya katiba ya chama hicho, mbali ya kuonekana kuwa umeiga namna CHADEMA inavyowatumia wazee, lakini uigaji huo bila shaka haukufanyika kwa makini kwa kuwa umewaengua kabisa katika nafasi ya maamuzi ya chama hicho wazee hao ambao ni makada waandamizi waliokitumikia chama hicho kwa muda mrefu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Ndani ya CHADEMA, utaratibu wa kuwawezesha wazee kuunda Baraza la Ushauri, kwa nia ya kukishauri chama umeanza kutumika tangu mwaka 2006, pale baraza hilo lilipoundwa rasmi wakati wa mabadiliko ya katiba ya chama chetu makini.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Lakini pia kwa kutambua umuhimu wa wazee hao katika uendeshaji wa chama hiki, kikilenga kuwatumikia Watanzania, kwa kufanya maamuzi kwa kuangalia nchi inakotoka, ilipo na inakokwenda, wazee ndani ya CHADEMA wana nafasi katika vikao vya maamuzi ya chama. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA ni mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA taifa; pia Wenyeviti wastaafu wa chama ni wajumbe wa kamati kuu ya chama taifa.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Aidha, Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa CHADEMA ni mjumbe wa Sekretarieti ya chama. Pia yeye pamoja na mwenyekiti wa baraza hilo, wote ni wajumbe wa vikao vya Kamati Kuu. Kwa ujumla wazee wana uwakilishi kwenye vyombo vyote vya maamuzi vya chama kuanzia ngazi ya msingi, tawi mpaka ngazi ya taifa.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Hivyo mbali ya chama kupata ushauri wa wazee kupitia baraza la washauri hao kila inapohitajika, bado kinaweza kupata busara, hekima na uzoefu wao katika maamuzi mbalimbali ya chama yanayofanyika, kupitia vikao halali na muhimu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Katika hali ya kawaida, wakati CCM inapita katika hali ngumu ya kisiasa, ikionesha kila dalili za kuchoka na mwisho wa kunyumbulika katika kuendelea kuendesha serikali, ilikuwa busara kuendelea kupata mawazo ya wazee katika vikao halali, badala ya kusubiri kuwaita na kuomba ushauri, wakati ambapo mambo yanakuwa yameshakwenda mrama.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Lakini pia CCM wasiwadanganye wananchi kuwa kwa namna ambavyo wamefikia tamati ya kuendelea kuaminiwa na Watanzania, kuwa eti wao wanaweza kusikiliza, kuamini na kufanyia kazi ushauri wa wazee hao, tena baada ya kuwaondoa katika vikao halali![/FONT]
  [FONT=&amp]
  Tunasema hivyo tukikumbuka namna mapendekezo na ushauri wa iliyokuwa kamati ya Mzee Mwinyi, iliyoundwa kutatua matokeo ya mgogoro unaoendelea kukitafuna chama hicho, yalivyotelekezwa, huku chama kikikosa uwezo, umakini, uimara na uadilifu wa kuyafanyia kazi. Kwa sababu kinalinda maslahi ya ufisadi na mafisadi na kuwatosa Watanzania.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Lakini pia CCM waambie Watanzania, uamuzi huo, unasaidiaje Tanzania na Watanzania kwa ujumla kutoka katika mtanziko mkubwa wa matatizo yanayowakabili sasa, ikiwemo kuporomoka kwa uchumi na maisha kuzidi kuwa makali, yote yakisababishwa na uongozi mbovu wa chama hicho kilichoko madarakani kwa sasa.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Imetolewa leo tarehe 14 Februari;[/FONT]


  [FONT=&amp]Nyangaki Shilungushela[/FONT]
  [FONT=&amp]Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA[/FONT]
   
 2. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani CHADEMA wahangaikie mambo yao, mambo ya ndani ya ccm whether ni ya kipuuzi au ya maana it's none of CDM business! ccm wakiboronga ni manufaa kwa cdm na wakifanya vizuri ni changamoto kwa cdm!
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa maamuzi mazuri ya wazee wa CDM
   
 4. PRISCUS JR

  PRISCUS JR JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nimependa wazee wenye busara mnavyochambua mambo bila kubwabwaja, ombi langu kwenu!
  Naomba mzunguke vijiji vyote ambapo inaaminika kuna wazee wengi wasiojua madhara ya ufisadi wa CCM mkawaelimishe.
  Nasema hivyo kwasababu kuu moja, watoa elimu ya mabadiliko vijijini wengi ni vijana, hivyo wazee wengi vijijini wanaamini vijana hawajui lolote na zaidi ni watu wa fujo na watukuza usasa.
  Uwepo wenu utawapa imani kuwa hakuna haja ya kuendelea kuikumbatia CCM.
  Utu uzima dawa wazee ni hazina. viva wazee viva CHADEMA.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine mwenzenu mweh!
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,244
  Likes Received: 3,787
  Trophy Points: 280
  Taifa likiwa na wazee wenye fikra kama hawa wa cdm litastawi vema, busara na uyakinifu vimetawala maandiko haya!
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  ..Chimbuko la Kuwaondoa wazee wa CCM kwenye vikao vya Kamati kuu....ni KIkwete.....


  Dhumuni lake ni Kuwaondoa haraka kabla ya vikao vya michakato ya uchaguzi mkuu wa ndani wa chama .....na baadaye uchaguzi mkuuu wa Taifa 2015....
  Ilijulikana wazi kuwa kutokana na uungwaji mkono wa JK kushuka....hangekuwa na nguvu ya turufu ya kupanga safu za uongozi ...chamani..na baadaye hangekuwa na nguvu ya kuweka mgombea urais anayemtaka mwaka 2015.........Mgombea yeyote ambaye angeungwa mkono na wazee ..angekuwa na nguvu kuliko mgombea ambaye angewekwa na JK.......hii ndio imepelekea JK ...anayesifika kwa siasa za "kimjini mjini" .....kuwajengea wazee zengwe...

  Wazee ...Mwinyi , mkapa,salmim,malecela,na Karume....inaelezwa kuwa wamekubali ....uamuzi huu...ili kumuacha ...abaki na ubishi wake...hasa ikizingatiwa tayari Wanayo kumbukumbu ya KIkwete kuwatenga kwenye uchaguzi mkuu wa 2010(matunda Yake Aliyaona )....sababu kuu iliyowauzi wazee ilikuwa kitendo cha KIkwete kukabidhi jukumu la kampeni kwa familia Yake....kinyume na utaratibu..hii ilipelekea chama kupoteza kura nyingi....
  Kitendo cha wazee kuwekwa kando kinatarajiwa kuongeza wito la Umbwe la uongozi kwenye utawala wa KIkwete...na anayo hatari ya kuondoka madarakani na chama ......

  Utaratibu wa wenyeviti kubaki kwenye Kamati kuu...ni utamaduni wa ccm ..iliuiga toka china,na Russia...huu unalenga kufanya smooth transition of power....kwamba rais akistaafu ....anatakiwa aendelee kuwa mwenyekiti wa chama ...Angalau kwa miaka miwili(uchaguzi mkuu wa taifa na chama unatofautiana miaka miwili)...ndani ya kipindi hichi rais mstaafu anapata fursa ya kuendelea kumshauri rais kwa mgongo wa chama...baada ya kumkabidhi rais kofia zake mbili( katakana na utashi anaweza kuamua kuondoka mapema Kama alivyofanya Mwinyi na mkapa au kumaliza miaka miwili Kama alivyofanya Nyerere na Karume wa sasa hapo Zanzibar )....baada ya kumkabidhi hubakia kwenye halmashauri kuu...

  Mtoto amelilia wembe....
   
 8. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
 9. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hongereni wazee wa CDM, nanyi ongeeni na wazee wezenu vijijini waache kukumbatia magamba na kutumiwa kuiba kura
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hao wazee wamechoka waacheni wapumzike. Waacheni watoe ushauri nyuma ya pazia, hizi siasa za dot com zitawatoa kamasi wakiamua kuingia front.
   
 11. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  There is no an iota of point in releasing this statement by Ma.gwanda. CCM's decision to relieve its elder members of their party duties should be well respected and left upon themselves. Mag.wanda should not make itself appear too meddling by questioning and deprecating each and every move taken by CCM thinking that opposition means going against anything reached by your opponent
   
 12. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  baraza la wazee chadema limefikia kutoa ushauri kwa wazee wenzao ccm ili kuwakumbusha kuwa waliloridhia kufanya litawagharimu kwa msingi kwamba siasa inazidi kukua na muda si mrefu ccm watakabidhi nchi kwa cdm so the most important thing waache kuiga kila walionalo kwa cdm,maana namna wamekuwa ccm sasa hawawezi kufikiri on their own badala yake ni mwendo wa kudense kila jambo toka cdm.wakuu ccm wataanza rasmi safari ya kukiua chama chao mara tu watakapoanza kuyatumia mabadiliko waliyoridhia juzi.
   
 13. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Suala la wazee wa CDM kutumika kuwashawishi wazee wenzao waunge mkono mabadiliko ni la muhimu sana...binafsi ninaamini hapa ndiyo tulipopigiwa bao la kisigino na CCM kule Igunga baada ya kupeleka timu ya ya wazee kama kina Mashishanga,Mangula ambao walifanya kazi nzuri sana ya kushawishi kundi hili muhimu liunge mkono CCM wakipita kila kijiji...Ni hili tu ndiyo lilo wapatia CCM zile kura 3,000 za ziada ukiachilia mbali sarakasi zao nyingine..vinginevyo CCM wasingechomoka kwenye makucha ya CDM Igunga.Kwa mfumo wa maisha ya jamii yetu,mila na desturi na hata mazoea...ni kama kijana huwa hana haki sana ya kumshauri au kumshawishi mzazi wake au mtu mzima juu ya jambo fulani na hata ikitokea basi anayeshauriwa anaweza akapuuza ushauri huo hata kama una manufaa kwa sababu tu umetolewa na kijana mdogo...Lakini mzee akifuatwa na mzee mwenzake na akashauriwa...ushauri huo huufikiria mara mbilimbili...na mwisho wa siku huukubali.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  SPLENDID!!! CCM wamekurupuka

   
 15. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Siyo lazima ufuate kila jambo ambalo mwenzio amelitoa,lakini hata hivyo kauli iliyotolewa na mwenyekiti baraza la wazee wa CDM Ujue imechekechwa si ya kukurupuka unapojibu,wazee wamekutolea mfano wa nchi mama wa socialism ambazo ni referencce kwa ccm[URUSI NA CHINA]ambako viongozi wastaafu hubaki kwenye kamati za maamuzi daima,au ndo kusema ccm ujamaa basi?
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono kwa hili
   
 17. k

  kuzou JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pilipili ya shamba yawawashia nini chadema. halafu kwa sasa ilivyo wastaaafu hawawezi kumshauri mwenyekiti mpaka awaombe ushauri lkn kwa mabadiliko haya wanaweza kumshauri rais bila yeye kuomba huo ushauri.pia wakati wapo kwenye vikao hawakua final say.ni sawa tu na wajumbe wengine
   
 18. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ni vema wazee wa CDM wakangalia mambo yao kwanza sioni sababu ya wao kuwazungumzia wenzao ikiwa wao wazee wa ccm hawakutoa tamko la kutofiki hili, binafsi naona wazee wa chadema wange jishugulisha na mambo ya chadema sijasikia wakitioa tamko juu ya changamoto zinazoiikabili nchi kama vile mfumko wa bei, kaitiba, na kadhalika ni venma wakatumia hekima na nguvu zao kukijenga chadema hasa kwa kushiriki kwenye mikutano ya kichama kuwapa nguvu wazee wenzao wajiunge chdema.
   
 19. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Well said Phillemon, lakini nina mtazamo tofauti kidogo kwenye hii issue.

  Kimsingi, both CDM, CCM na wanachama wao wanajua na kukubali umuhimu wa wazee hasa ukizingatia 'accumulated experience' wanayokuanayo kwenye masuala mbali mbali ya kiuchumi, kijamii, n.k. Umuhimu huu unajulikana duniani kote... na ndio msingi wa mabunge katika nchi nyingine za 'commonwealth' kuwa na 'upper chambers'. Mfano mzuri ninaoupenda wa 'upper chamber' ni wa bunge la Uingereza:

  • Bunge la Uingereza lina "House of Lords" ambao 'peers' wake wanakuwa watu wenye uzoefu mkubwa na mafanikio katika fani zao.
  • wanaitwa 'peers' ili kuwatenga na 'political affiliations', hivyo kuwafanya kuwa huru kwenye mijadala yao.
  • 'Peers' ni wazee wa kujitolea, hawalipwi 'salary' ispokuwa inapothibitika kwamba mhusika anahitaji msaada kushiriki kikamilifu.
  • Jukumu kubwa la 'peers' ni kupitia miswada inayopendekezwa na kushauri, na wana uwezo wa kuchelewesha mswada kupita ili ukidhi matakwa ya kitaalam.

  Kubwa hasa ninalotaka kusema ni kwamba badala ya kuwa na haya mabaraza ya wazee ya vyama tofauti, ambayo kimsingi yanatumia kodi ile ile ya Watanzania, tungependekeza kuundwa kwa baraza la wazee (la kitaalam kama hili la House-of-Lords) ambalo litaishauri Serikali kwa taratibu zitakazoonekana zinafaa.

  Ni wazi kuwa wanasiasa wote wanapigana kujenga nchi mmoja kwa sera tofauti (japokuwa wakati mwingine hata sera zinafanana), hivyo sioni mantiki kwa nini Rais mstaafu mwenye uzoefu uliotokana na makosa na mafanikio aliyoyaopata kwenye uongozi wake atekwe na chama kimoja. Worse enough, hata ushauri atakaoutoa kwenye chama chake unaweza kuminywa kwa manufaa ya chama chake hata kama utakuwa na manufaa kwa Taifa.

  Tutengeneze 'platform' ambapo wazee wetu watakuwa huru kutoa maoni hasa katika issue nyeti na pale kunapokuwa na ombwe la uongozi kama ilivyo sasa.
   
 20. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Waliokurupuka ni CDM,
  Mambo ya CCM yanawahusu vip mpaka wayatolee tamko?
   
Loading...