VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nimearifiwa na marafiki wangu wa Unguja na Pemba kuwa matangazo ya moja kwa moja ya Baraza la Wawakilishi yanafanyika. Huku kwetu Tanzania Bara,matangazo ya moja kwa moja ya Bunge yamepigwa marufuku. Yaani,BLW laonyesha mambo yake live. Bunge la Jamhuri linafichwa. Linafanyika sirini kama unyago au jando.
Inajulikana kuwa BLW lina Wajumbe karibia wote wa CCM. Mikutano ya BLW ni kama mkutano wa CCM. Ndani ya BLW la sasa hakuna mawazo kinzani kwa kiasi kikubwa na hata mawazo mbadala. Barazani humo,CCM wanajidai watakavyo. Na hawaogopi kuoneshwa live.
Huku Bungeni kwenye wapinzani wa kutosha wenye kushindana kwa hoja,kukosoa na kulipua,CCM haitaki mambo yaonekane. Hii ni taswira ya woga. Taswira ya kutojiamini katika kujenga,kujibu na kupambana kwa hoja. Ni 'udhalilishaji' kwa CCM yenye wingi wa Wabunge,maneno na matendo. Live coverage isitutishe makada wenzangu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam