Baraza la wawakilishi Zanzibar latetea matumizi ya bendera ya taifa kwa meli za Iran

Bora serikali moja tu Tanzania, Zanzibar ni hatari kwa usalama wa nchi ikiendelea kuwa na kajiserikali kadogo na kukumbatia ugaidi
 
Are they going to defend the Sanctions to their people? Iranians have OIL they can sell in black market 2 feed their

People; what will Zanzibar Government do to feed their people? remember it is an Island so easy to block with US

Navy Ships No food in and OUT !!!

Mkuu usitaje tena hii maneno.........loooh!
 
Kila kukicha kero kero! VIongozi pande zote kweli mnayo dhamira safi ya kudumisha huu muungano? Mnashindwa kukaa na kuamua hata maamuzi dhaifu kama yale magumu yameshindikana? waachieni wenyewe wenye nchi waamue basi! Na hakutakuwa na lawama! Kukimbilia katiba kabla ya kuweka sawa hili tatizo la Muungano, ni sawa na kuweka unga kwenye maji ambayo hayaja chemka eti unasonga ugali! Matokeo yake utakula ugali mbichi kisha ukudhuru afya yako!
JITAMBUENI!
 
.Jamani mimi nawish Tanzania iwekewe SANCTIONS kabisa .... na sactions ziwe pamoja na Travel BAN kwa Viongozi wote wa juu wa Serikali ... including Vasco Da Gama!Hii itawasaidia kufungua macho yao na kuanza kutafuta maendeleo kutokana na vyanzo vya ndani.Wanaacha hela huku wanawapa wawekezaji kwa bei ya kutupa alafu wanaenda Ulaya kuomba Vyandarua!!!!!!!...... Shame on them! .... kwa kutufanya Watanzania kudharaulika kwa Mataifa ya nje!.Piga travel ban viongozi& economic embargo kabisa hawa ..... labda watapata akili! .....
Sasa mkulu akipigwa travel ban na alivyozoea utembezi si miguu itamuota matende!?
 
bora 2 tuwekewe hivyo vikwazo labda tutapata akili jinsi ya kutumia tulivyonavyo...potelea pote!
 
Ningeiunga mkono deal hii kama ingekuwa kwa maslahi ya Tanzania. Lakini inavyoelkea imefanywa kwa moja ya sababu mbili:
1- watu binafsi wanaotaka kutiau na mfukoni marupurupu yatokanayo na ddeal hii
2-Serikali imeishiwa mno (baada ya ubadhirifu mkubwa wa safari na kununua kura) sasa inakurupuka kujaribu kupata pesa kutoka popote
Ingekuwa deal hii imefanywa kutokana na misimamo thabiti ya uhuru na uadilifu (a la Nyerere) ningesema Yes, to hell with the faggot Obama. Kwa sababu ukiangalia Marekani haina point yeyote katika sakata la Iran.
1-Iran ni NPT member therefore has the right to enrich uranium up to 20% for power generation and medicine.
2-Hakuna ushahidi wowote wa kuwa Iran ina divert uranium material kutoka kwenye vinu vinavyoangaliwa na NPT observers 24/7
3-Kama kweli Marekani is keen on nuclear non-proliferation mbona inaachia, bali kuzisaidia nchi nyingine ambazo si member wa NPT?
4- Tanzania ina haki ya kuisapoti nchi inaayosongwa, si kwa sababu ya kukiuka sheria za Kimatifa, bali kwa sababu za kutokubaliana na ubabe na u-bully wa Marekani.
Lakini, Alas, Kikwete engine hayajui yote haya na uamuzi wa serikali yake umetokana na maslahi binafsi tu. Ndio maana siungi mkono.
 
Na Nafisa Madai – WMM Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewasilisha ripoti ya usajili wa meli mbele ya wajumbe wa Baraza la wawakilishi katika mkutano wa bajeti unaoendelea Mjini Zanzibar.

Akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mh. Hamad Masoud,(Pichani) amesema kwamba Serikali imelazimika kutoa ripoti hiyo kuweka kumbukumbu sawa kuhusu madai yaliyochapishwa na kutangazwa na baadhi ya vyombo vya habari vya ndani na vile vya Kimataifa.

Waziri Masoud amesema katika mojawapo ya taarifa za vyombo vya habari vilisema “Meli za mafuta za* Iran zinatumia Bendera ya Tanzania kukwepa vikwazo”.

Waziri huyo amesema Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) imeundwa kwa mujibu wa sheria* namba* 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyingine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006.

Amesema sheria hiyo katika kifungu cha 8(1) kinaeleza kutakuwa na Mrajis wa Meli Tanzania Zanzibar ambaye atasajili meli zinzofanya safari za nje na zile za ndani.

Waziri Masoud amewaambia Wajumbe kwamba Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti Open Registry, Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General Cargo na meli za Abiria” amesema Waziri huyo.

Waziri amezitaja meli hizo na Mataifa yao kwenye mabano kuwa ni Daisy 81479* Daisy Shipping Co. Ltd (Malta) Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd (Cyprus), Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd******** (Malta) Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd ( Malta) Leadership 164241* Leadership Shipping Co. Ltd (Cyprus), Companion* 164241* Companion Shipping Co. Ltd (Malta).

*Amezitaje nyengine ni Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd ( Malta) Clove 81479* Clove shipping Co. Ltd ( Malta), Courage* 163660 Courage Shipping Co. ltd (Cyprus), Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd (Cyprus) na valor 160930 valor Shipping Co. Ltd.(Cyprus)

Amesema Meli hizo ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration).

Meli zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta.*

Sambamaba na meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha usajili wao na kwenda usajili wa “TUVALU Islands”.

Swali kwanini wapeperushe bendela ya Tanzania badala ya Zanzibar?
 
Kwa nini meli hizo zipepee bendera ya Tanzania? Na hata complain za marekani ni kuhusu Tankers kuwa na bendera ya Tanzania...

Kama hiyo mimeli yote aliyoitaja inapepea bendera yetu na sisi hatunufaiki nazo ni bora muungano uvunjwe tu maana nilidhani sisi na vilaza wa mikataba feki kumbe wenzetu ndio vilaza zaidi. Pia ikumbukwe viongozi wa CCM ndio mabingwa wa kudanganywa na huwa hawafanyi research kujiridhisha ukweli ukoje huenda ni tankers za Iran but mmedanganywa za nchi nyingine
 
Inaeleweka wazi kuwa sheria za "Zanzibar" hazi-apply kwenye masuala ambayo yapo nje ya Tanzania. Ndiyo maana hakuna kiongozi yeyote wa Zanzibar (akiwemo Rais & Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi) hana mamlaka ya kuingia mkataba wa kimataifa. Hata bilateral agreements, Zanzibar haina mamlaka ya kusaini. Ndiyo maana kama kuna agreement hata ya kisekta, na nchi hata ikiwa ya jirani kama Kenya, lazima asaini waziri wa muungano. Sasa hayo mamlaka ya kusajili meli without knowldege of Union authority wameyapata wapi? Wasije wakatuletea matatizo hawa.
 
Inaeleweka wazi kuwa sheria za "Zanzibar" hazi-apply kwenye masuala ambayo yapo nje ya Tanzania. Ndiyo maana hakuna kiongozi yeyote wa Zanzibar (akiwemo Rais & Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi) hana mamlaka ya kuingia mkataba wa kimataifa. Hata bilateral agreements, Zanzibar haina mamlaka ya kusaini. Ndiyo maana kama kuna agreement hata ya kisekta, na nchi hata ikiwa ya jirani kama Kenya, lazima asaini waziri wa muungano. Sasa hayo mamlaka ya kusajili meli without knowldege of Union authority wameyapata wapi? Wasije wakatuletea matatizo hawa.

Umenena mkuu
 
Sasa nyinyi mnajadili zanzibar kusajil meli.Angalien hizo sheria hapo juu mutaelewa. Co mufanye chuki zenu.
 
Kwa upande wangu sina tatizo kabisa na Muungano, tatizo ni namna na aina ya Muungano..... nadhani mfumo wa Muungano wetu uwe wa nchi mbili tofauti na kila moja iwe imekamilika "autonomous" na Muungano uwe kama huu tunaoujenga sasa wa Afrika Mashariki.
Huo sio Muungano, hiyo ni jumuiya tu, mbona unatumia njia ya mlango wa nyuma kusema kile kile ambacho wengine tuna balls za kukisema wazi? Tuvunje Muungano!

Iwapo sasa serikali ya Muungano itaipatia Zanzibar mamlaka ya kupeperusha bendera yake nje ya mipaka ya Tanzania, basi mambo ya Muungano yanapaswa kuainishwa wazi kwa jumuiya ya Kimataifa, na Tanganyika itumie bendera yake kwa manbo hayo pia
Bendera ni alama ya kimataifa, mataifa mengine lazima yatambue bendera ya Taifa fulani, nchi moja haiwezi kuwa na bendera mbili au tatu. Kila upande kuwa na bendera yake maana yake ndo tumevunja Muungano, na ndio dawa ya haya matatizo. Jamani mbona tunajidanganya? Utakuwaje na Muungano ambao mmoja anataka "dola huru yenye mamlaka yake kamili"?
 
Duniani kuna nchi 196 zinazotambulika na
Zanzibar si mojawapo. U.N. kuna nchi 193
zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo. Afrika
kuna nchi 54 zinazotambulika na Zanzibar si
mojawapo... Find out what i mean...
 
Duniani kuna nchi 196 zinazotambulika na
Zanzibar si mojawapo. U.N. kuna nchi 193
zinazotambulika na Zanzibar si mojawapo. Afrika
kuna nchi 54 zinazotambulika na Zanzibar si
mojawapo... Find out what i mean...
 
Back
Top Bottom