Baraza la wawakilishi Zanzibar latetea matumizi ya bendera ya taifa kwa meli za Iran

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
821
335
Wakati mataifa ya Magharibi yanatishia kuiwekea vikwazo Tanzania kwa kuruhusu usajili ya meli za mafuta za Iran na kutumia bendera ya Taifa, baraza la wawakishi Zanzibar, limesema Zanzibar kama sehemu ya Muungano wa haki ya kusajili meli ya Iran au nchi yoyote ile kwa maslahi ya Wazanzibar na kuwa taarifa na kelele zinazoendelea ni njia ya kutaka kuwakatika tamaa Wazanzibar kujiletea maendeleo.

My take:

Huu ni mwendelezo wa kutaka kuhalalisha kuvunjika kwa muungano.

July 02, 2012
TAARIFA KWA BARAZA LA WAWAKILISHI JUU YA USAJILI WA MELI ZA NJE ULIOFANYWA NA SMZ KUPITIA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI ZANZIBAR MARITIME AUTHORITY – ZMA



Mhe. Spika,

Tarehe 27/06/2012 Vyombo vya Habari hapa Tanzania (The Citizen) na nchi za nje (International news Agency – Bloomberg) viliandika makala kuhusu usajili wa meli 10 za mafuta (Tankers). Ilidaiwa katika makala hayo kuwa Meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya Tanzania na kwamba zinafanya biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN. Gazeti la "The Citizen la tarehe 27 Juni, 2012 lilikuwa na kichwa cha habari "Iran Tankers adopt TZ Flag to avoid embargo" (meli za mafuta za Iran zinatumia bendera ya Tz kukwepa vikwazo.

TAARIFA YA ZMA

Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar Maritime Authority – ZMA ni Mamlaka iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).

Sheria ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006, kifungu no. 8 cha sheria hii, kinasomeka kama ifuatavyo:

Section 8 (1). There shall be established the registers of Tanzania Zanzibar ships to be Known as:-
(a). Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean going ships; and
(b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships.
(2). A ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for the purpose of this Act if that ship is registered under this part.
Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa. (Open Registry). Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.

Kama nilivyoeleza hapo awali, vyombo vya habari vimechapisha makala ya usajili wa meli 10 ambazo zinadaiwa ni meli za IRAN kulingana na makala zao hizo.

SMZ inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta ilizosajiliwa wiki mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:

Jina la meli GRT (Ukubwa) Company name Ilikotoka

1. Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta
2. Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus
3. Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta
4. Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta
5. Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus
6. Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta
7. Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta
8. Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta
9. Courage 163660 Courage Shipping Co. ltd Cyprus
10. Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus
11. valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus

Jumla ya GRT ni 1,388,368 tons

Meli hizi ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration). Meli zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta. Sambamaba na meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha usajili wao na kwenda usajili wa "TUVALU Islands".

ZMA ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizi na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya IRAN. Philtex ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis tarehe 28/06/2012 katika afisi za Philtex Corporation na Wamiliki hao wameeleza kwamba hawana uhusianao na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli ZMA kwa ridhaa yao na kwa kufata matangazo ya usajili wetu wa nje (Open Registry).

Pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza kwamba ikiwa ZMA haiko tayari kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta usajili wao na tayari wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine (PANAMA) lakini hawana nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na Malta.

Kinyume na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari juu ya uraia wa wamiliki wa meli hizi, Wamiliki wa meli hizi kama walivyojieleza katika usajili wa meli zao wana uraia wa British Vergin Islands na Sychelles.

Kulingana na "United Nations Convention Law of the Sea", Article 91, na za "Geneva convection of Registration" articles 6, 7 na 8, na kulingana na Zanzibar Maritime Transport Act of 2006, section 8, Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili meli yeyote kulingana na taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa zinazoongoza usajili huo.

Maelezo haya yanatolewa ili kutoa usahihi wa uvumi kuwa Zanzibar imesajili meli za IRAN ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya (European Union) juu ya usafirishaji na uuzaji wa mafuta kutoka Iran.

Mhe. Spika, taarifa hizi za vyombo vya habari hazina madhumuni yeyote zaidi ya kuwavunja moyo wenye Makampuni ya meli wanaotaka kusajili meli zao kwetu.

Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya nchi. Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na uchumi wake.

Hata hivyo mamlaka itafata sheria zote zilizowekwa kitaifa na kimataifa katika biashara ya usafiri baharini na itahakikisha meli zinasajiliwa chini ya mamlaka hii zinafata taratibu ilizoweka.

Mhe. Spika, kabla ya taarifa hizi za vyombo vya habari (The Citizen), Waziri wa Uchukuzi wa SMT Mhe. Harisson Mwakyembe) alipokuwa akijibu suala Bungeni hivi juzi hakuonyesha kurishika kwake katika usajili wa meli (Open Registry) inayofanywa na Zanzibar na kuahidi kufanya ziara ya kuja Zanzibar kuonana na Waziri anaehusika kuzungumzia suala hili. Taarifa za "The Citizen" zaweza kuwa ni muendelezo wa Mhe. Mwakyembe kutoridhika kwake katika usajili unaofanywa na Serikali kupitia uwakala wake huko Dubai.

Mhe. Spika, Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi yeyote.
Hili ni suala la kibiashara na kwamba kwa Serikali yetu ni njia moja ya kuongeza mapato yanayoendesha Serikali, alimradi tu usajili huo hauvunji sheria za Kimataifa.

Mhe. Spika,

Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran) na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani IRAN itaendelea kusaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo. Zanzibar haingependa kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro isiyowahusu.

Hivyo, kwa taarifa hii, Serikali inakanusha rasmi uvumi wa vyombo vya habari kuhusiana na suala hili kama taarifa hii ilivyofafanua hapo juu.

Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.

Hamad Masoud Hamad
WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO

 
Kwanini walipowasajili hawakuwawekea bendera ya Z'bar!? Si wana bendera yao? Huu ni uchokozi!
 
ROSTAM AZIZ NA BIASHARA BINAFSI KATI YA IKULU ZA TEHRAN NA MAGOGONI KUTUINGIZA MAJARIBUNI KAMA TAIFA KATIKA USO WA JUMUIA YA KIMATAIFA

... wengine tumeonya sana tu juu ya Biashara za Rostam Aziz kutuingiza motoni lakini hata siku moja hatukusikilizwa na badla yake hili li-mdudu lilipewa heko kwenye jukwaa la siasa kule Igunga na kupachikwa jina la 'Simba wa Vita'.

Yeyote anayesema kwamba kwanini tuchaguliwe marafiki;

1. kwanza tangulia kujibu swali kwamba ni lini Bunge letu tukufu kule Dodomaliliporidhia hili zoezi la Meli za Irani kupachikwa Bendera yetu ya taifa na kuchanja mbuga kwa jina letu lakini kwa faida yao?

2. Je, maridhiano kama hayo yako kwenye Hansard ya bunge letu ukurasa wa ngapi?

3. Je, kitendo cha taifa letu kuingizwa kwenye biashara HARAMU na HATARISHI kama hii mbele ya uso wa Jumuia ya Kimataifa, hadi leo hii taifa letu limenufaika kiasi gani cha fedha kwa kuamua kujitwisha 'kiroba cha bangi' kilichomshinda M-Irani?

4. Je, kati ya wabunge wetu zaidi ya 350 kule Dodoma, ni wangapi wanaojua undani wa makubaliano kati ya Rais Kikwete na uongozi wa Tehran?

5. Je, Iran imekua ikiifadhili CCM kupitia 'Mwekahazina wa Taifa Rostam Aziz' kwa miaka hiyo yote huku wao wakipata maslahi-rejea gani over the counter?

6. Je, iweje Zanzibar iruhusiwe kutumia jina la 'Tanzania' ambalo wako bize kila leo KULIKANA na kutaka Muungano ufe kwa haraka sana huku wakiendelea kufanyia biashara hatarishi kama hili kwa kutumia jina hilo hilo BAYA AMBALO WAKO RADHI WAFE KULIKO KUBAKIA NDANI YAKE kujinufaisha CCM kimtindo kwa ajili ya kukusanya fedha kupitia MCHONGO BINAFSI YA KUNDI MOJAWAPO NDANI YA CCM na Iran kuja kununulia tena madaraka 2015?

7. Viongozi wa CCM wanapoingiza taifa letu kwenye biashara za kunufaisha kile kinachosadikiwa kuwa ni 'ugaidi na juhudi za kigaidi kwa mapana na marefu yake katika ukanda wetu huu na kuchinja ovyo wananchi gizani kupitia vikundi hatari vinavyofadhiliwa na serikali hiyo hiyo ya CCM' je tutawezaje kujitenga na dhambi hii kama sisi kama walazwahoi wa taifa hili hatuoni sababu yoyote ya kumwambia Dr Kikwete kwamba huko unakotupeleka HATUKO TAYARI?

NB: Swala la uhusiano binafsi kati ya Magogoni na Irani kamwe si salama kwa taifa letu kwa kuwa wananchi hata siku moja hatujawahi KUSHIRIKISHWA wala kuwekwa bayana faida na hasara zake zaidi ya kila kitu kuzungukwa na USIRI NA UFISADI WA KIFAMILIA kwa mgongo wa taifa zima. Hili halikubaliki hata kidogo hapa nyumbani na hata huko Ughaibuni.

Mwisho; sote tusisahau kukumbuka hili neno hapa - Dr Stephen Ulimboka kwa bahati mbaya sana itokee kwamba ataaga dunia au mwanaharakati mwingine yeyote yule kuguswa tena visivyo basi Magogoni wakae wakijua kwamba gharika la damu ya hao wote watakaodhurika leo ama kesho ndio itakayogeuka Tsunami la kulifunika kabisa CCM kabisa hata kabla ya jua la muula wake wa utawala wa kichakachuaji huu kuzama.

Wananchi sote tuamke na tuseme usiri katika biashara binafsi na Iran pale Ikulu lazima ikome mara moja.

Ulafi na ufisadi wa serikali ya Kikwete sasa unaliingiza taifa katika mgogoro wa kidiplomasia. Juzi tumeionya serikali, leo serikali ya Marekani inatoa onyo kwa Kikwete. Sababu IRAN. Watueleze ni kitu gani viongozi wa IRAN wamekuwa wakifuata Tanzania ! Mwakyembe, Membe Rostam na Kikwete Kazi Kwenu


Tanzania must stop re-flagging Iran tankers: U.S. lawmaker


WASHINGTON | Fri Jun 29, 2012 1:39pm EDT (Reuters) - Tanzania must stop the practice of "re-flagging" Iranian oil tankers or it will face the threat of U.S. sanctions and damage its ties with Washington, a U.S. lawmaker warned on Friday.

Howard Berman, the ranking member of the House Committee on Foreign Affairs, accused Tanzania of reflagging at least six and possibly as many at 10 tankers owned by the National Iranian Tanker Company.

"This action by your government has the effect of assisting the Iranian regime in evading U.S. and EU sanctions and generating additional revenues for its nuclear enrichment and weapons research program and its support for international terrorism,"

Berman said in a letter to President Jakaya Kikwete that was obtained by Reuters. Berman said if the tankers were allowed to continue sailing under the Tanzanian flag, Tanzania could face the sanctions that President Barack Obama signed into law.

He said Congress would also have "no choice" but to consider whether to continue the range of bilateral U.S. programs with Tanzania.Officials at Tanzania's embassy were not immediately available to comment on Berman's letter.

The sanctions, along with similar action by the European Union, are aimed at pressuring Iran to curb its nuclear program, which the West believes aims to develop nuclear weapons but which Tehran says is for peaceful purposes. The United States gave China a six-month reprieve from Iran financial sanctions on Thursday. The Obama administration has now spared all 20 of Iran's major oil buyers from its unilateral sanctions, rewarding them for cutting purchases of Iranian oil.

Below are some of the Super-Tankers that have been renamed, and flying the Tanzanian Flag:

Davar (previous name): Companion – Tanzania
Haraz: Freedom – Tanzania
Susangrid: Daisy – Tanzania
 
hakika huu ni uchokozi, iweje wao kama wana bendera yao na bendera hiyo ipo chini ya mamlaka yao,wasiitumie hiyo? Hapa kuna namna ya makusudi iliyofanyika.
 
Sasa hawa Wazanzibari wanataka kutuingiza kwenye matatizo, si tuvunje tu Muungano na wao? kwi kwi kwi teh teh teh!
 
ROSTAM AZIZ NA BIASHARA BINAFSI
KATI YA IKULU ZA TEHRAN NA MAGOGONI KUTUINGIZA MAJARIBUNI KAMA TAIFA
KATIKA USO WA JUMUIA YA KIMATAIFA

... wengine tumeonya sana tu juu ya Biashara
za Rostam Aziz kutuingiza motoni lakini hata siku moja hatukusikilizwa
na badla yake hili li-mdudu lilipewa heko kwenye jukwaa la siasa kule
Igunga na kupachikwa jina la 'Simba wa Vita'.

Yeyote anayesema kwamba kwanini tuchaguliwe marafiki;

1. kwanza tangulia kujibu swali kwamba ni lini Bunge letu tukufu kule
Dodomaliliporidhia hili zoezi la Meli za Irani kupachikwa Bendera yetu
ya taifa na kuchanja mbuga kwa jina letu lakini kwa faida yao?

2. Je, maridhiano kama hayo yako kwenye Hansard ya bunge letu ukurasa wa
ngapi?

3. Je, kitendo cha taifa letu kuingizwa kwenye biashara HARAMU na
HATARISHI kama hii mbele ya uso wa Jumuia ya Kimataifa, hadi leo hii
taifa letu limenufaika kiasi gani cha fedha kwa kuamua kujitwisha
'kiroba cha bangi' kilichomshinda M-Irani?

4. Je, kati ya wabunge wetu zaidi ya 350 kule Dodoma, ni wangapi
wanaojua undani wa makubaliano kati ya Rais Kikwete na uongozi wa
Tehran?

5. Je, Iran imekua ikiifadhili CCM kupitia 'Mwekahazina wa Taifa Rostam
Aziz' kwa miaka hiyo yote huku wao wakipata maslahi-rejea gani over the
counter?

6. Je, iweje Zanzibar iruhusiwe kutumia jina la 'Tanzania' ambalo wako
bize kila leo KULIKANA na kutaka Muungano ufe kwa haraka sana huku
wakiendelea kufanyia biashara hatarishi kama hili kwa kutumia jina hilo
hilo BAYA AMBALO WAKO RADHI WAFE KULIKO KUBAKIA NDANI YAKE kujinufaisha
CCM kimtindo kwa ajili ya kukusanya fedha kupitia MCHONGO BINAFSI YA
KUNDI MOJAWAPO NDANI YA CCM na Iran kuja kununulia tena madaraka 2015?

7. Viongozi wa CCM wanapoingiza taifa letu kwenye biashara za kunufaisha
kile kinachosadikiwa kuwa ni 'ugaidi na juhudi za kigaidi kwa mapana
na marefu yake katika ukanda wetu huu na kuchinja ovyo wananchi gizani
kupitia vikundi hatari vinavyofadhiliwa na serikali hiyo hiyo ya CCM'
je tutawezaje kujitenga na dhambi hii kama sisi kama walazwahoi wa
taifa hili hatuoni sababu yoyote ya kumwambia Dr Kikwete kwamba huko
unakotupeleka HATUKO TAYARI?

NB: Swala la uhusiano binafsi kati ya Magogoni na Irani kamwe si salama
kwa taifa letu kwa kuwa wananchi hata siku moja hatujawahi
KUSHIRIKISHWA wala kuwekwa bayana faida na hasara zake zaidi ya kila
kitu kuzungukwa na USIRI NA UFISADI WA KIFAMILIA kwa mgongo wa taifa
zima. Hili halikubaliki hata kidogo hapa nyumbani na hata huko
Ughaibuni.

Mwisho; sote tusisahau kukumbuka hili neno hapa - Dr Stephen Ulimboka
kwa bahati mbaya sana itokee kwamba ataaga dunia au mwanaharakati
mwingine yeyote yule kuguswa tena visivyo basi Magogoni wakae wakijua
kwamba gharika la damu ya hao wote watakaodhurika leo ama kesho ndio
itakayogeuka Tsunami la kulifunika kabisa CCM kabisa hata kabla ya jua
la muula wake wa utawala wa kichakachuaji huu kuzama.

Wananchi sote tuamke na tuseme usiri katika biashara binafsi na Iran
pale Ikulu lazima ikome mara moja.

zanzibar washa tushika makalio na mdhaifu anachekea hiki ndo kifo cha magamba bifu na mzungu hawataliweza kuna Myahudi,mmarekani na Mwingereza ...wamelikoroga!
 
Kama Zanzibar ni nchi, na nchi hiyo inabendera yake, kwa nini wasitumie bendera ya Zanzibar badala ya Tanzania?
 
The Zanzibar government yesterday defended its move to register Iranian oil tankers, saying it didn’t break any laws as claimed by a section of the international media early this week. Zanzibar Infrastructure and Communication minister Hamad Masoud Hamad refuted reports that the Isles government had registered Iranian oil tankers as reported by Bloomberg News Agency early this week. The minister admitted however that the said Iranian oil tankers were previously registered in Cyprus and Malta islands. Briefing the House of Representatives yesterday, Hamad said the registered oil tankers were not covered by international sanctions imposed on Iranian ships by the European Union and the United States. The minister stated that according to the Zanzibar Marine Transport AuthorityAct, number 3 of 2009, and the Zanzibar Marine Transport Act of 2006, the Isles government had full autonomy to register international ships. According to the minister, Zanzibar entered into an agreement with a Dubai-based company, Philtex Ltd, to act as its agent in the registration of all international ships, known in the shipping industry as ‘open registry’. The minister added that open registry had been in effect since 2009, whereby a number of international cargo ships, oil tankers and passenger vessels were registered in Zanzibar. Contrary to the media reports, the minister said, the vessels claimed to belong to Iranian authorities were in fact owned by British nationals living in the Virgin Islands and the Seychelles. The minister warned against interference by the union government in the matter as promised by his counterpart, Dr Harrison Mwakyembe, saying marine transport in Zanzibar wasn’t a union affair. Citing relations between Iran and Zanzibar, the minister said the two countries had strong ties, adding that that was why Iran’s vice-president recently visited the Indian Ocean archipelago to discuss how to strengthen the relations. He warned that Zanzibar wasn’t ready to be dragged into the ongoing conflicts between Iran and Western countries. Speaking about the Iranian tanker flying the Tanzanian flag, the minister said since Zanzibar was part of the union, there was nothing wrong for vessels registered in the Isles to fly the union flag. “But if the Tanzanian government won’t feel comfortable with the tankers flying the union flag we are ready to let them fly the Zanzibar flag. This is no big deal and it should not be blown out of proportion,” the minister said. On Monday, Bloomberg News Agency reported that NITC, an oil-tanker company owned by Iranian pension funds, renamed at least 10 of its vessels and switched them to flying the Tanzanian flag amid increasing curbs on transactions with the Persian Gulf nation. NITC renamed five large crude oil carriers, each with a capacity to hold about 2 million barrels of oil, and five Suezmaxes, hauling 1 million barrels each, according to the Equasis shipping database maintained by the European Commission, Bloomberg reported. Ownership was switched from NITC to new companies operating from the same address in Tehran and NITC remains the operator, the data show. All the ships were previously registered in Malta or Cyprus. A European embargo on Iranian crude exports, which comes into effect on July 1, extends to insuring vessels that carry oil. Twenty-five NITC tankers are being used to store crude, the Paris-based International Energy Agency said on June 13, this year. The US and Europe said Iran’s nuclear programme was aimed at developing atomic weapons while the government in Tehran says it is for civilian purposes. Habibolah Seyedan, NITC’s commercial director, was unavailable for comment, said a person who answered a call to his office yesterday. The company lists 39 tankers on its website. Philtex Corp. operates the administrative office of the Tanzania Zanzibar International Register of Shipping from Dubai, according to the register’s website. SOURCE: THE GUARDIAN
 
Muungano mtamu lakini mchungu! Mume kaamuwa kutafuta wachumba wengine. Kwi kwi kwi teh teh teh! bado tu tuna hamu na huyo mume?

ahahahahaa! janja ya paka panya kwisa tambua!
NDOA hii haina talaka, kilicho bakia ni bakora kwa kwenda mbele, mpaka huyu mbuguma atwihi na kuendelea kupika urojo uwani! hulijui hilo bro?
 
Nahisi tunatoa mawazo yetu zaidi kwa ushabiki pengine hata kujua kiini cha mzozo wenyewe.

- Kwanza ieleweke kuwa "Si kosa kwa mujibu wa sheria zilizopo kwa Zanzibar kusajili meli za nje kwa jina na bendera ya Tanzania. Hii ni kwa mujibu wa vifungu vya sheria hii:
1): "There shall be established the registers of Tanzania Zanzibar shipsd to be known as:- (a) Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean ongoing ships, and (b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships. And a ship shall be a Tanzania ship for the purpose of this Act if that Ship is registered under this part."
Na kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa miaka sasa imekuwa ikisajili meli kwa kutumia bendera ya Tanzania kwa sababu, mpaka hapo Muungano utakapovunjika kwa wanaotaka uvunjike, Zanzibar na Tanganyika zina haki sawa ya kutuia bendera hiyo "kwa mujibu wa sheria".

- Tazizo lililopo ni kuwa meli zinazotajwa a) Wamiliki wake ni raia wa British Virgin Islans na Sychelles b) Meli hizo zimesajiliwa Malta na Cyprus

Kwa hivyo, ikiwa Tehran imefanya mizengwe ya kubadilisha usajili ni juu ya Umoja wa Ulaya kuwabana pia wamiliki wa meli hizo na zilikosajiliwa kwanza.
 
Back
Top Bottom