Baraza la Wawakilishi Zanzibar kila Mwakilishii Moto kuhusu Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Wawakilishi Zanzibar kila Mwakilishii Moto kuhusu Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 19, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Kero za Muungano Zatawala Mjadala wa Bajeti
  [​IMG]


  Muwakilishi wa Kwantipura Hamza Hassan
  Na Mwantanga Ame


  HUKU wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakijadili bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013, kilio cha kero za Muungano kimetawala na kutikisa michango ya wajumbe wa Baraza hilo.


  Wajumbe hao walisema kuwa kero za Muungano zimekuwa kero kubwa kwa uchumi wa Zanzibar na kwamba zinahitaji kurekebishwa hivi sasa badala ya kusubiri mchakato wa katiba mpya.


  Akichangia bajeti hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma (Kwamtipura), alisema kuwa serikali inapaswa kuja na majibu mazuri juu ya namna ya kero za Muungano zitakavyomalizwa, kwani zinakandamiza uchumi wa Zanzibar.


  Hamza alisema inasikitisha kuona serikali ya Muungano hivi sasa imekuwa na mambo mbali mbali ya serikali inayotakiwa kuyafanyia kazi lakini hakuna lililofanyika wakati serikali ya Muungano ikiwa inatekeleza vyema matakwa yake.


  Mwenyekiti huyo alisema serikali ya Zanzibar inakosa majibu juu ya suala la mgao wa Muungano wa asilimia 4.5 ambao kwa muda mrefu yametolewa mapendekezo ya asilimia 11.5 lakini BOT bado halijatekelezeka hadi sasa.


  Alisema jambo linaloshangaza kuona baada ya kupelekwa mapendekezo hayo serikali ya Muungano imeipatia gawio la asilimia 7.8 huku kukiwa hakuna muendelezo wa hatma ya suala hilo.


  Alisema kuwapo kwa gawio hilo limeifanya serikali ya Zanzibar wakati ikisubiri suala hilo kumalizwa katika vikao vya kero za Muungano imekuwa ikikosa shilingi bilioni 7,000,000,000 kati ya shilingi bilioni 15, ambazo zilitakiwa kuingia katika mfuko wa hazina ya Zanzibar kama hilo lingekuwa limemalizwa.


  Suali jengine linaloonesha kutokuwepo kwa utayari wa serikali ya Muungano kulifanyia kazi kwa haraka, ni kodi ya mishahara ya wafanyakazi wa Muungano ambao wanafanya kazi hapa Zanzibar ambapo inakosa shilingi bilioni 18.


  Alisema kama mambo hayo yangeliweza kutolewa maamuzi ya haraka, kwa kiasi kikubwa zingeweza kuisaidia serikali ya Zanzibar kupata gawio lake kwa miaka mingi badala ya hivi sasa kuendelea kutolewa kwa fedha hizo kama ni huruma.


  Aidha alisema kero pia ziko katika suala la elimu ya Juu ambapo serikali ya Zanzibar itapaswa kuona inadai serikali ya Muungano kwa mwaka ujao wa fedha kupatiwa asilimia ya gawio la Zanzibar ikiwa ni hatua itayoweza kujipanga vyema katika kutoa elimu ya juu.


  Mwenyekiti huyo, aliikosoa bajeti hiyo, kwa kueleza kuwa kodi ya umeme ambapo alisema inaweza ikachangia kuongeza gharama za maisha kwa wananchi na kuiomba serikali kuiondoa hadi kamati ya Baraza la Wawakilishi litapomaliza kufanya uchunguzi wake katika shirika la Umeme.


  Kutokana na hali hiyo Mwenyekiti huyo aliishauri serikali kufikiria kuwaangalia watendaji wake kwa kuhakikisha wanawatumikia wananchi huku serikali ikawachukulia hatua za kinidhamu wanaotajwa kuibia serikali.


  Aidha, Mwenyekiti huyo pia alieleza dhamira ya Kamati hiyo kutaka kuwasilisha maombi ya kuifanyia uchunguzi Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) baada ya kujionesha baadhi ya Watendaji katika kitengo cha Bandarini kuonekana kujihusisha na uvujaji wa mapato.


  Eneo jengine ambalo kamati hiyo imetishia kuizuia bajeti hiyo ni juu ya suala la ajira kwa vijana kutokana na hivi sasa kuwepo kwa taarifa za wageni kuajiriwa kwa wingi katika mahoteli ya kitalii huku Wazanzibari wakikoseshwa nafasi hizo.


  Kwa upande wake, Mwakilishi wa Uzini (CCM), Mohammed Raza alisema uchumi wa Zanzibar unaweza ukakosa kunawiri ikiwa baadhi ya mambo yakiachiwa moja kwa moja kutekelezwa na serikali ya Muungano likiwemo suala la kujiunga na taasisi ya kimataifa ya Kiislamu (OIC).


  Aidha Mwakilishi huyo alihoji juu ya suala la Afrika Mashariki nalo linahitaji kuangaliwa katika haki ambazo itaweza kuzipata kama Zanzibar bila ya kuingia kama ipo chini ya mwamvuli wa Tanzania.


  Naye Mwakilishi wa Kitope Makame Mshimba Mbarouk alisema serikali itapaswa kujiangalia katika miradi ya uwekezaji kutokana na baadhi ya wawekezaji kufutiwa miradi yao ikiwa analipia gharama kubwa na kupewa watu wanaolipiwa kiasi kidogo cha fedha.


  Alisema hivi sasa kuna watu wamekuwa wakiondolewa kwa chuki katika baadhi ya miradi hiyo jambo ambalo linapoteza imani ya wawekezeji kuwekeza Zanzibar na kuahidi kuizuiya bajeti hiyo hadi atapopewa maelezo ya kija juu ya suala hilo.


  Nae Mwakilishi wa Chonga (CUF), Abdalla Juma Abdalla, aliiomba serikali kuona inatekeleza vyema bajeti hiyo na kuahidi kuwa hatoacha kuiziya hadi atapopewa maelezo ya kina kutokana na kujitokeza mambo mbali mbali katika serikali.


  Mwakilishi wa Ziwani, Rashid Seif, akitoa mchango wake aliitaka serikali kuona inajipanga vyema katika suala la kusimamia sekta ya elimu kutoka an akuanza kuonekana eneo hilo huenda kukawa na wajanja wanaotumia vibaya nafasi zao.
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Haina haja ya kupiga magoti na kujizalilicha viongozi wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar hoja kwa Wazanzibar nikuvunja tu Muungano huu feki mukidile basi tutatoka katika Bad kwenda kwenye warst hawa watu wana nchi yao na sisi tuna yetu, kila moja kapata uhuru wake kivyake.
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  si muwape nchi yao..mbia mwawang'ang'ania sana??
   
 4. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  "....Suali jengine linaloonesha kutokuwepo kwa utayari wa serikali ya Muungano kulifanyia kazi kwa haraka, ni kodi ya mishahara ya wafanyakazi wa Muungano ambao wanafanya kazi hapa Zanzibar ambapo inakosa shilingi bilioni 18....."

  Hapa hapajakaa vyema. Hivi kuna Waunguja na Wapemba wangapi wanaofanya kazi huku bara?? Kuanzia mawaziri nk? hayo mapato yagawanywe kufuatana na idadi ya watu, hata kama Zanzibar ina hadhi ya kuwa nchi kamili. Hebu mumrudie Mwenyezi Mungu ni haki mapato yagawiwe nusu kwa nusu??? Wanaotaka kuvunja muungano ni wabinafsi na wanatumiwa na wenye tamaa ya madaraka.
   
 5. m

  mzaire JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wawakilishi mafala wote, si wamue tuuu kuleta kura ya maoni.

  punda.png
  Wazanzibari wakiandamana kwa Punda kuukataa muungano.
   
 6. k

  kula kulala Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi naona bora tukawaachia nchii yao hawa jamaa kwani iko siku tutakuja kujuta sana kwa hawa wazenje kikwete na pinda fanyeni kazi mambo hayo haraka iwezekanacho wasituharibie nchi
   
 7. m

  mzaire JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wee hamkuona hapo mwanzo kuwa mnataka kuungana na nchi yenye poplation ndogo, kwanini mlikubali ?

  Ndio maana Wazenji hautaki huu muungano, kwaupuuzi kama huo unaouzungumzia hapo.

  Hapo hatudiscuss poplation ila tunaaangalia nchi huru zilizoungana, ikiwa mnaona si haki waachieni Wazenji nchi yao msiwanga'nga'nie.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Kakke, kwanini wawakilishi hawakuamua kuandaa muswada wa kuuvunja muungano?
   
 9. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasas unapiga kelele za nini? kuna mtu kawakataza kutoka?
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hivi hao wazanzibari hawana kitu kingine cha kujadi zaidi ya muungano? Wao hata kwenye mambo ya feza ni muungano tu! Au kwa kuwa fedha ni moja ya mambo ya muungano?!
   
 11. P

  Physics Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kichwa kibovu.maana yake ni kodi za wafanyakazi wa z'bar wote ni muungano,mpaka tugaiwe kutoka huko.
   
 12. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao wawakilishi ni wezi mbwa, uoga wao mkubwa ni kama kamata kamata ya mafisadi style ya bara ikifika TanzaniaZanzibar
   
 13. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mbona wameacha kujadili bajeti yao wanajadili muungano
   
 14. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #14
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hao jamaa noma bwana wanasema hawatoacha kujadili muungano mpaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano iitishe kura ya maoni kwa raia wa Zanzibar....na kuhusu BOT wanasema walitoa thamani kubwa ya fedha ya kuanzishwa kwa bot na vile Nyerere aliweza kusafirisha pesa za Zanzibar $80,00000 zilizokuwepo katika bank ya Russia kule England na kuziweka katika BOT baada ya kifo cha Karume....
  Hizo ndo gadhabu zao:censored:
   
 15. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Let it go! Simple and clear they want OIC and probale Oil that it.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo utamuona mtu tena mwenye akili timamu. Akitema asali na kutamani pilipili.
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wazanzibar wakumbuke jambo moja muhimu. Muungano huu ni tunda halisi la MAPINDUZI matukufu ya tarehe 12/01/1964. Hatukuwa na Muungano kabla ya mapinduzi haya. Haiwezekani ukauchukia Muungano halafu ukayaenzi Mapinduzi haya. Watu hawataki kuwa wawazi na wakweli tu. Wangeanza kwa kuhoji kama Mapinduzi yale yalikuwa halali au ni kosa la kihistoria ambalo sasa linatakiwa kurekebishwa? Umoja wanaouonyesha Wazanzibar sasa ni kwa sababu ya uwepo wa Muungano huu. Ukishavunjwa au kuvunjika CUF itakuwa ZNP/ZPPP na CCM kule itakuwa ASP. Hotuba ile ya Mwalimu pale Kilimanjaro Hotel bado ni valid hadi kiama.
   
Loading...