Baraza la wawakilishi lafunguka: Tusilazimishane katika muungano huu. Watanganyika wanatuhadaa

Kweli wazanzibar hawafai kabisa! mpaka leo wanadha kuna wajomba wa kuwasaidia kuwapelekea maendeleo? wanaota OIC, UAE,sijui nani, nani kawambia kuna vya bure duniani? elimu bado inahitajika sana kuwakomboa wenzetu kifikra, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Mukuu,
Bajeti la Tanzania linategemea wafadhili kwa asilimia ngapi?
Wafadhili wenyewe ni akina nani?

Tukiweza kujikomboa sisi,tutaweza kuwakomboa na jirani zetu.
 
Raza alikimbilia Bara alitaka kufanyishiwa na Amani Karume,leo mhindi mwizi huyu anajifanya mjuaji? Wahame wote hapo kisiwani, kisiwa hajakirudisha Nyerere halafu irudi kwa wakoloni, Zanzibar ni sehemu ya Tanzania daima
 
Zanzibar ndio wanaohadaa, hata Wizara za Muungano mfano fedha na ulinzi ZnZ wanazo nyengine kama hizo hizo ila kwa kugeuza jina kidogo, huku za Muungano wakiwemo pia
 
Hivi, sisi Wa-Tanganyika, tutakosa kitu gani kama Muungano utavunjika! Mbona tunaonekana kama sie ndio tunaulilia sana!

Hapa unaweza kuambulia kitu. Nini kitakosekana.?

They should also convince MRC that the 1963 Lancaster agreement between the British, the Sultan of Zanzibar and the Kenyan government on the coastal strip will not expire next year as the group is claiming.

Link https://www.jamiiforums.com/kenyan-...a-kukutana-na-kundi-lisilo-halali-la-mrc.html
 
Zanzibar tangu enzi za kale ilikuwa sehemu ya pwani ya Tanganyika, Nyerere kakirudisha na kumwajiri Karume asaini kuingiza Zanzibar nyumbani, sasa asietaka ahame yeye
 
Sasa naamini ukisha kuwa muislam unaandamwa na laana .Haya wacha walie na Vatican

Hii ni zaidi ya laana.Jiulize mtu anataka ajiunge oic ajengewe daraja!hii ndo kusema anafanya kamuungano kengine ka kifikra? Hii ni sawa na mtu anayeomba talaka kisa kampata mwanaume tajiri zaidi.Nawasihi ndugu zanguni Wazenj jengeni hoja zenye mashiko.Kama bungeni ndivyo mlivyo mkibaki wenyewe itakuwaje?Angalieni msije mkawa kama wenzeni wa U arabuni wanavyopunguzana kiana.
 
Historia itajirudia tu, hakutakuwa na jipya katika hilo. Ule mkataba wa kuunganisha baadhi ya mambo ya Tanganyika na Zanzibar uliandaliwa wapi?

Ni vyema pia katika kuuvunja mswada uandaliwe huku huku Tanganyika aka Bara.

Oyaa CCM watayarishieni "magaidi" "wachoma moto makanisa" mswada wa kura ya maoni ,mambo yaishe!

Ccm hawawezi kufanya hivyo kwa sbb wanashinda kwa kura za zenz.muungano kuisha ni mwisho wa ccm bara.let zenz go.
 
hapa unaweza kuambulia kitu. Nini kitakosekana.?

they should also convince mrc that the 1963 lancaster agreement between the british, the sultan of zanzibar and the kenyan government on the coastal strip will not expire next year as the group is claiming.

link https://www.jamiiforums.com/kenyan-...a-kukutana-na-kundi-lisilo-halali-la-mrc.html

as far as i know- zanzibar ilipata uhuru kutoka kwa ukoloni wa mwingereza mwaka 1963, kisha ikafanya mapinduzi ya uhuru mpana zaidi kwa kuondoa ukoloni wa sultani mwaka 1964.
Wakati hayo yanafanyika tanganyika ishapata uhuru wake zamani tu takribani miaka 2 iliyopita, sasa sijui na wewe ni miongoni mwa wanaodhani dar-es-salaam, tanga, mtwara,mafia ni sehemu ya zanzibar?. Hii itakuwa ndoto kweli kweli.
Kiufupi ni kwamba kila mara wakubwa walipojisikia, walimpunguzia sultani eneo la kutawala, na mwishoni hata kale ka 10 miles strip kwa upande wa tanganyika, sultan barghash aliukauza kwa wajerumani.
Lakini kikubwa ni kwamba, hatumtaki mkoloni yeyote eidha awe mwingereza, mjerumani au muomani
 
wanabodi.
Amini usiamini uamsho sio uamsho tena. Yaani licha ya vyombo vya habari kuripoti na kupotosha kuhusu uamsho. Ndani ya baraza la wawakilishi ni kinyume kabisa, hakuna mwakilishi anaejaribu kulizungumizia, na hata akijaribu kuligusa ni wazi unaweza ukahisi kama analiunga mkono japo sio moja kwa moja.

Katika hali isiyotarajiwa na wengi. Leo hii wazanibar wametoa madai mazito kuhusu muungano unavyoendeshwa huku lawama za wazi wazi zikilekezwa kwa watanganyika kwamba wanawahadaa wazanzibar

hoja zenyewe
1)mh raza: Ilikuwa ni vigelegele, makofi na hata vicheko vilitanda kila kona barazani huku spika na mawaziri wa smz wakionekana wazi kupigwa na butwaa.
Nini alisema mh raza:
No1:
"mh spika, nina nyaraka za makubaliano kati ya serekali ya awamu ya 3 ya dk salmini na mh mkapa kuhusu zanzibar kujiunga oic. Haya sio maneno ya mitaani, ninazo nyaraka za makubaliano, na kama serekali ya sasa wanahizaji nitawapa ambazo wenzetu walisema tanzania itajiunga oic kwa manufaa ya zanzibar. Lkn wenzetu wametuhada na wanaendelea kutuhadaa. Huku wao wakiwa na ubalozi wa vertican kwa manufaa yao. Hi ni hadaa kubwa tunayoendelewa kufanyiwa zanzibar, hatukubali tena tunasema hatukubali, kwa muungano wa aina hii " makofi ukumbi mzima.
Eti tunaambiwa kupata uanachama wa oic ni kazi kubwa, naimba serekali hii kazi inepe mimi, ndani ya miezi 3 tanzania itajiunga na oic ili tutengezewe madaraja, barabara na vyuo vikuu kama baadhi ya nchi. Zanzibar tunanjaa wao kama watanzania bara wameshiba waache washibe

no2:
"mh spika, niliwahi kusema huko nyuma, itafika siku vyeti vya ndoa tutakiwa tuvifate dodoma, nikapuuzwa. Sasa unaona, waziri wa nishati wa tanzania bara leo ndio anawakilisha wazanzibar ktk jumuia ya afrika mashariki huku waziri huyo akiwa mwisho wake ni chumbe tu. Hii ni hadaa kubwa tunayohadaiwa wazanzibar huku viongozi wetu wakiwa sio wakweli , sijui nini wanachoogopahili tunasema tunashachoka, hatulitaki litendeke
"
no3: Mh spika, miaka 48 ya muungano hadi kuna watu ndani ya tanganyika wanatuona zanzibar hatuna maana, leo mawaziri wanakubaliana kutatua tatizo la muunagno, kuna watu wenye nia mbaya na zanzibar wanazuia. Muungano kama huu haufai, huu si muungano, huu ni ulaghai" makofi.

Mwakilishi wa kitope
"mimi naona sasa hakuhitajiki viongozi wasomi kutatua matatizo ya muungano, tuachaguliwe sisi wasio na elimu wenye kutoa kauli. Maana ndugu zetu hawataki kutusikia.
Kwa ufupi kila mwakilishi inaoenakana anakwera na muungano huu unavyoendeshwa licha ya waziri aboud kudai watu wasubiri katiba mpya. Sio ccm sio cuf

wapendwa,
wazenji wameamua kuonesha kukerwa na muungano kwa muda mrefu. Hivi wanabodi hebu leteni point za kweli juu ya faida kamili ya huu ushirika wenye mgogoro maana naona ni kama mtu kulazimisha ndoa wakati mume au mke hamtaki mwenzake. Raza anajaribu kuwahadaa wenzake kwamba oic ndo suluhisho la yote badala ya kufanya kazi kwa bidii. Anaelekeza umahiri wake wa kisiasa katika kujengewa madaraja, barabara na kuinuliwa uchumi na oic bure. Hivi hao oic hawana masharti? Hebu tujadili kidogo kauli ya raza na mbunge wa kitopeni, hivi wana faida binafsi katika hili au?
Raza acha kudanganya hao wananchi waliochoka kimaisha wape mstakabali wa maisha yao jinsi ya kuyarekebisha.
 
Malumbano,

Ukitaka uonekane mwanasiasa mahiri Zanzibar kashifu waTanganyika[muungano] nakwambia hata kichaa atakuona wa maana.Bahati mbaya wanasiasa wa Zanzibar wameshindwa wameshindwa kutimiza matarajio ya wapiga kura wao kimbilio la kuwaadaa wananchi wa Zanzibar ni kuutukana muungano,kuukashifu muungano,kuukejeli muungano na kuchoma makanisa.

Zipo nchi kibao zilizojiunga na OIC lakini bado zinakabiliwa na matatizo ya miundombinu,elimu na nk.OIC sijawabu la matatizo ya Zanzibar.Matatizo ya Zanzibar yatatatuliwa na wazanzibar wenyewe kwa kufanyakazi kwa bidii na maarifa.Kuna watu wa ajabu sana huko Zanzibar wanadhani dunia ya leo maendeleo yataletwa na misaada ya mataifa ya nje.

CCM ni chama tawala ifike mahali wafanye maamuzi magumu ingawa kwangu naamini ni maamuzi mepesi sana wawape waZanzibar kisiwa chao hakuna haja ya kulazimishana hizi lawama na kejeli zimetosha tusiache hadi mambo yaharibike kabisa tufanye maamuzi sasa.

mkuu unafatilîa malalamiko kishéria?mbona wanasheria wanaushangaa huu muungano?hauna mfano.kama kweli sema kweli utaitwa muadilifu.
 
Akili nzuri ukiwa nayo. Hivi lini mlisikia Tanzania imepewa msaada na Vatican? Ubalozi si sawa na kujiunga na jumuiya ya dini. Tanzania ina ubalozi kwenye Jamhuri ya Kiislam ya Iran, hiyo inaongeza nini kwetu ukiondoa mahusiano ya kibalozi?

Kama kuna waarabu ambao hawawezi kuwasaidia mpk mjiunge na dini yao basi mnakubali utumwa. Tena utumwa mbaya unaoanzia kichwani. Imefikia sehemu leo Zanzibar inayojifanya inataka kuwa huru ikabidhiwe kwa OIC? Kwa hiyo mnataka Zanzibar huru au Zanzibar inayomilikiwa na OIC?

Mnapojenga hoja tumieni akili zenu. Vatican ni dola kama ilivyo Iran na Saudia, na mahusiano yake na Tanzania ni ya KIBALOZI na si kwamba Tanzania ni mwanachama wa UKATOLIKI.

Kuna mmoja wa hao wawakilishi amekiri kuwa hawana Elimu, naunga mkono. Utumbo kama huu uliobandikwa hapa hauwezi kusemwa na mtu aliyemaliza kidato cha pili, labda awe amesoma shule ya kata

sisi tunataka tuwe watumwa wa OIC badala ya tanganyika,huo ndio ujinga wetu na ndo kiwango chetu cha elimu kilipo.
 
Muungano wetu ni ndoa ya Kikristo, unaingia kwa ridhaa na ukishaingia, umeingia hakuna kutoka!. Muungano huu ni wa milele!. Endeleeni kupiga kelele za mlango!.

ukristo ni mchanganyiko wa kweli na uongo mkuu,au hujui?fuatilia.
 
Back
Top Bottom