Wadanganyika semeni ovyo mpaka mchoke. Jamuhuri ya watu Wa Zanzibar kwanza ...shengesha baadae.Mpaka ki - kielewekeMkuu, wanatishia nyau tu hao.
Umesema kweli kabisa, wao ni nchi huru, wana bunge lao tukufu (Baraza la Wawakilishi).
Nashindwa kuelewa kelele zote hizo ni za nini? Fanyeni kama alivyopenedekeza mkuu MM, basi yaishe.
Kajiungeni huko OIC, ili muone kama ninyi ni special zaidi ya YEMEN ambao purely ni waarabu wenzao lakini ni masikini kuliko TZ, au hata Sudan tu ambao tuliosoma nao maeneo fulani walikuwa hawataki kabisa kuitwa wa-Afrika, bali walifurahia kuitwa Wa-Arabu!!!???
Labda hao hawaitaki misaada ya OIC. Au kule afrika ya kati je? Ambako Uislam umeshamiri zaidi ya hapo
Zanzibar. Nao vipi OIC imewasahau. Jamani tumieni akili za tafakuri.
Tatizo kubwa la wa TZ ni kutegemea maendeleo kutoka kwa mjomba zaidi ya kwa juhudi za ndani.
Ndiyo maana hata wanaogombea ubunge katika ahadi zao utawasikia
nitawatafutieni au nitawaletea wafadhili watakao wajengea shule, daraja,
barabara na utumbo mwingine wa aina hiyo.