Baraza la wawakilishi lafunguka: Tusilazimishane katika muungano huu. Watanganyika wanatuhadaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la wawakilishi lafunguka: Tusilazimishane katika muungano huu. Watanganyika wanatuhadaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malaria Sugu, Jun 18, 2012.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanabodi.
  Amini Usiamini UAMSHO sio UAMSHO tena. yaani Licha ya Vyombo vya habari kuripoti na kupotosha kuhusu UAMSHO. Ndani ya baraza la wawakilishi ni kinyume kabisa, hakuna mwakilishi anaejaribu kulizungumizia, na hata akijaribu kuligusa ni wazi unaweza ukahisi kama analiunga MKono japo sio moja kwa moja.

  Katika hali isiyotarajiwa na wengi. Leo hii Wazanibar wametoa madai mazito kuhusu muungano unavyoendeshwa huku Lawama za wazi wazi zikilekezwa kwa Watanganyika kwamba wanawahadaa wazanzibar

  hoja zenyewe
  1)Mh Raza: Ilikuwa ni vigelegele, makofi na hata vicheko vilitanda kila kona barazani huku Spika na Mawaziri wa SMZ wakionekana wazi kupigwa na Butwaa.
  Nini Alisema Mh Raza:
  no1:
  "Mh Spika, nina nyaraka za makubaliano kati ya Serekali ya Awamu ya 3 ya Dk Salmini na Mh Mkapa kuhusu Zanzibar kujiunga OIC. Haya sio maneno ya Mitaani, ninazo nyaraka za makubaliano, na kama serekali ya sasa wanahizaji nitawapa ambazo wenzetu walisema Tanzania itajiunga OIC kwa manufaa ya Zanzibar. Lkn wenzetu wametuhada na wanaendelea kutuhadaa. huku wao wakiwa na UBALOZI wa vertican kwa manufaa yao. Hi ni hadaa kubwa tunayoendelewa kufanyiwa Zanzibar, Hatukubali tena tunasema hatukubali, kwa muungano wa aina hii " makofi ukumbi mzima.
  eti tunaambiwa kupata uanachama wa OIC ni kazi kubwa, naimba serekali hii kazi inepe mimi, ndani ya miezi 3 Tanzania itajiunga na OIC ili tutengezewe madaraja, barabara na vyuo vikuu kama baadhi ya nchi. Zanzibar tunanjaa wao kama Watanzania bara wameshiba waache washibe

  no2:
  "Mh Spika, niliwahi kusema huko Nyuma, itafika siku vyeti vya ndoa tutakiwa tuvifate Dodoma, nikapuuzwa. sasa unaona, waziri wa nishati wa Tanzania bara leo ndio anawakilisha Wazanzibar ktk jumuia ya Afrika Mashariki huku Waziri huyo akiwa mwisho wake ni CHUMBE tu. hii ni hadaa kubwa tunayohadaiwa wazanzibar huku viongozi wetu wakiwa sio wakweli , sijui nini wanachoogopahili tunasema Tunashachoka, hatulitaki litendeke
  "
  no3: Mh spika, miaka 48 ya Muungano hadi kuna watu ndani ya tanganyika wanatuona Zanzibar hatuna maana, leo mawaziri wanakubaliana kutatua tatizo la Muunagno, kuna watu wenye nia mbaya na Zanzibar wanazuia. Muungano kama huu haufai, huu si Muungano, huu ni ulaghai" Makofi.

  mwakilishi wa Kitope
  "Mimi naona sasa hakuhitajiki viongozi wasomi kutatua matatizo ya Muungano, tuachaguliwe sisi wasio na Elimu wenye kutoa kauli. maana ndugu zetu hawataki kutusikia.
  KWA UFUPI KILA MWAKILISHI INAOENAKANA ANAKWERA NA MUUNGANO HUU UNAVYOENDESHWA licha ya waziri Aboud kudai watu wasubiri katiba mpya. sio CCM SIO CUF
   
 2. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mhhhhh! haya
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Raza bana!
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hata ukiwa na madai halali ni lazima ujue namna kujenga hoja vinginevyo utaonekana hamnazo! Ubalozi wa VATICAN na OIC wapi na wapi? halafu eti wawakilishi wanashangilia ni UJUHA!

  Mbona Raza hashangai Mbunge wa ZNZ Dr. Mwinyi kuongoza wizara ya isiyo Muungano? Au Shamsi Vuai Nahodha ni Mwakilishi ZNZ, lakini pia Mbunge wa kuteuliwa na Waziri wa ULINZI. Hivi hivyo vikao vya barala la wawakilishi huwa anahudhulia wakati gani? maana mimi namuona mda wote Dodoma.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa raza kwa nini asilete mswada wa kura ya maoni ili Zanzibar ijitoe kwenye Muungano?
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mimi naunga mkono utaratibu huu, kama kuna matatizo yasemwe kwa namna hii, sio kuchoma nyumba za ibada nk. Am against violence, anything can be resolved through dialogs.
   
 7. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Serikali ya magamaba ielewe wazi ya kuwa Muungano ulioundwa mwaka 1964 kati ya Mwalimu na Karume ulianzishwa kwa sababu fulani zilizokuwa na manufaa kwa wakati ule. Kwa sasa Muungano ule umepitwa na wakati. Sababu zilizosababishwa ufanyike hazipo tena. Wananchi wa tanzania (Watanganyika na Wazanzibari) wa 2012 tuna maoni na mtazamo tofauti kabisa. Kwa mantiki hii ni lazima kuwe na kura ya maoni ili kujua kama watu wanautaka Muungano au la. Na kama wanautaka uwe kwa namna gani. Huu sio wakati wa kuburuzana na kutishana. Ndoa hufungwa na wawili kwa hiari yao. Hakuna atakayeweza kutulazimisha watanganyika na wazanzibari kuendelea na Muungano huu uliopo kama wenyewe hatutaki!
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Malumbano,

  Ukitaka uonekane mwanasiasa mahiri Zanzibar kashifu waTanganyika[muungano] nakwambia hata kichaa atakuona wa maana.Bahati mbaya wanasiasa wa Zanzibar wameshindwa wameshindwa kutimiza matarajio ya wapiga kura wao kimbilio la kuwaadaa wananchi wa Zanzibar ni kuutukana muungano,kuukashifu muungano,kuukejeli muungano na kuchoma makanisa.

  Zipo nchi kibao zilizojiunga na OIC lakini bado zinakabiliwa na matatizo ya miundombinu,elimu na nk.OIC sijawabu la matatizo ya Zanzibar.Matatizo ya Zanzibar yatatatuliwa na wazanzibar wenyewe kwa kufanyakazi kwa bidii na maarifa.Kuna watu wa ajabu sana huko Zanzibar wanadhani dunia ya leo maendeleo yataletwa na misaada ya mataifa ya nje.

  CCM ni chama tawala ifike mahali wafanye maamuzi magumu ingawa kwangu naamini ni maamuzi mepesi sana wawape waZanzibar kisiwa chao hakuna haja ya kulazimishana hizi lawama na kejeli zimetosha tusiache hadi mambo yaharibike kabisa tufanye maamuzi sasa.
   
 9. m

  mzaire JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha!!!! Watanganyika tunawaesabia siku wanajeshi na walowezi wenu kukaa ktk ardhi tukufu ya Z'bar.

  "Tume lenu la katiba mwisho msasani" from MUAMSHO, Wazenji hawana shida ya katiba, wao wenyewe wanayo yao ya Z'bar, Tafuteni yenu ya Tanganyika.


  View attachment 56750
   
 10. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Akili nzuri ukiwa nayo. Hivi lini mlisikia Tanzania imepewa msaada na Vatican? Ubalozi si sawa na kujiunga na jumuiya ya dini. Tanzania ina ubalozi kwenye Jamhuri ya Kiislam ya Iran, hiyo inaongeza nini kwetu ukiondoa mahusiano ya kibalozi?

  Kama kuna waarabu ambao hawawezi kuwasaidia mpk mjiunge na dini yao basi mnakubali utumwa. Tena utumwa mbaya unaoanzia kichwani. Imefikia sehemu leo Zanzibar inayojifanya inataka kuwa huru ikabidhiwe kwa OIC? Kwa hiyo mnataka Zanzibar huru au Zanzibar inayomilikiwa na OIC?

  Mnapojenga hoja tumieni akili zenu. Vatican ni dola kama ilivyo Iran na Saudia, na mahusiano yake na Tanzania ni ya KIBALOZI na si kwamba Tanzania ni mwanachama wa UKATOLIKI.

  Kuna mmoja wa hao wawakilishi amekiri kuwa hawana Elimu, naunga mkono. Utumbo kama huu uliobandikwa hapa hauwezi kusemwa na mtu aliyemaliza kidato cha pili, labda awe amesoma shule ya kata
   
 11. T

  TANGANYIKA01 Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawewe nawe Songa mbele zanzibar songa mbele mpaka upate ukombozi wa kweli.Hongera Mh.Raza kiukweli nakukubali watanganyika tutabana mwisho tutaachia tu waacheni wazanzibari waende bana halafu wewe mwanakijiji unautetea muungano kwasababu umeasisiwa na juliasi nyerere tu huna lolote
   
 12. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yaani nyaraka za serikali tena za makubaliano ya viongozi wakuu yeye kaweka nyumbani?n alizipataje?
   
 13. m

  mzaire JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shujaa ni yule anaepigania ardhi yake au nchi yake takatifu, kuwa na muungano/Tanzania ni bahati mbaya sana kwa Mzanzibari yyte, wacha aonekane shujaa kwa Wazanzibari na tena sio shujaa bali ni dhahabu/lulu.
   
 14. m

  mzaire JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tunawaona Maprofesa, PHD, MBA na Elimu nyengine, Tanganyika hakuna walilolifanya zaidi ya Ufisadi, Wizi, Ulevi na Ngono uzembe, hawana la maana, maana hata hizo bajeti zenu ni utumbo mtupu tena uharo tuu.

  Elimu isio na busara ni sawa sawa na wendawazimu, ndio huo mlio nao Watanganyika.

  Kwa idadi ya wasomi mnaongoza lakini hamna la maana lenye kushawishi kuwa linafanya na usomi wenu.

  View attachment 56751
   
 15. T

  TANGANYIKA01 Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka uliza uwambiwe usikurupuke au ndio usomi wetu watanganyika kuchangia tu japo uwongo.Dr.Mwinyi si mzanzibari ni mtaanganyika kwao ni mkuranga Baba yake Mzee Ali Hassan Mwinyi ni mtu wa mkuranga na wazazi wa mzee mwinyi wote wamezikwa mkuranga fanya utafiti kidogo tu utaupata ukweli na ndio maana kipindi cha mwanzo cha ubunge wake alikuwa ni mbunge wa mkuranga mbona umesahau.kugombea zanzibar alikwenda kwa mission maalum na kimsingi alilazimishwa yeye mwenyewe alikuwa hataki alipelekwa ili baadae aje agombee uraisi jambo ambalo haliwezekani kwani mzee mwinyi hakubaliki zanzibar anaonekana kama ni msaliti mkuu wa wazanzibari kaka usikurupuke Dr.Hussein ni ndugu yetu na ni mtanganyika halisi na hana nafasi yeyote zanzibar na hata ubunge hakushinda alipewa tu ubunge kwa mtutu wa bunduki .
   
 16. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mkuu, raza hanaubavu huo kwakuwa anajua CCM waliompa huo ulimi watamnyosha! kilichobaki ni kupiga kelele na mwisho wa siku ataishia kusema anauunga mkono muungano!
   
 17. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kwa kauli hiyo Mhe.Raza, angekusikia mwanangu kirukuu angekwambia 'Safi sana mjombaaa'. Baraza la wawakilishi kama vipi litangaze kuanzishwa kwa kura ya maoni juu ya muungano. Acheni kulalamika kila siku - Fanyeni maamuzi magumu. Ili mjikomboe. Maana zenji ndio nchi pekee barani Africa ambayo bado inatawaliwa na nchi nyingine.
   
 18. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mluga!

  Mimi sichangii ila kumbukunbu yangu fupi. Kiongozi wa Uamsho na KatibuMkuu wa CUF Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Rais wa Zanzibar aliwahi kufungwa na CCM kwa kukutwa na nyaraka za Serikali baada ya kunyanganywa Madaraka ya Waziri Kiongozi. Kabla sijaendelea Raza akamatwe na ashitakiwe vinginevyo Maalim Seif aombwe radhi na CCM na ikibidi afidiwe Kama sio Yule mpwa wa Selasini Masumbuko Lamwai Seif angekuwa bado yuko jela.
  Jana Seif kasema na nilimsikia kwamba Wazanzibar wanayo katiba Yao kwa hiyo machakato wa Katiba hauwahusu ila tu waseme maoni Yao kuhusu Muungano. If your careful then Uamsho na Seif ni mapacha!
   
 19. y

  yaya JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu, wanatishia nyau tu hao.
  Umesema kweli kabisa, wao ni nchi huru, wana bunge lao tukufu (Baraza la Wawakilishi).
  Nashindwa kuelewa kelele zote hizo ni za nini? Fanyeni kama alivyopenedekeza mkuu MM, basi yaishe.

  Kajiungeni huko OIC, ili muone kama ninyi ni special zaidi ya YEMEN ambao purely ni waarabu wenzao lakini ni masikini kuliko TZ, au hata Sudan tu ambao tuliosoma nao maeneo fulani walikuwa hawataki kabisa kuitwa wa-Afrika, bali walifurahia kuitwa Wa-Arabu!!!???
  Labda hao hawaitaki misaada ya OIC. Au kule afrika ya kati je? Ambako Uislam umeshamiri zaidi ya hapo
  Zanzibar. Nao vipi OIC imewasahau. Jamani tumieni akili za tafakuri.

  Tatizo kubwa la wa TZ ni kutegemea maendeleo kutoka kwa mjomba zaidi ya kwa juhudi za ndani.
  Ndiyo maana hata wanaogombea ubunge katika ahadi zao utawasikia
  nitawatafutieni au nitawaletea wafadhili watakao wajengea shule, daraja,
  barabara na utumbo mwingine wa aina hiyo.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Muungano wetu ni ndoa ya Kikristo, unaingia kwa ridhaa na ukishaingia, umeingia hakuna kutoka!. Muungano huu ni wa milele!. Endeleeni kupiga kelele za mlango!.
   
Loading...