Baraza la usalama UN lachakachua sheria kuivamia Libya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la usalama UN lachakachua sheria kuivamia Libya

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Nanyaro Ephata, Mar 23, 2011.

 1. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Ndugu wanaJf
  wakati mataifa ya magharibi walipoanza kuishambulia Libya,nililaani mashambulizi na nilipost thread nikilaani mashambulizi hayo,pamoja na upinzani mkali nilioupata,bado naendelea kulaani kwa kuwa yamekiuka sheria za kimataifa,kwa kuwa Libya haijaishambulia nchi yoyote.kwa mujibu wa sheria ya UN kifungu cha 2 (7) ni marufuku kwa taifa lolote kulishambulia taifa lingine kijeshi.
  sote ni mashahidi kuwa waandamanaji wa libya,au tunisia na kwingineko hawakuomba msaada wa mataifa ya nje,
  Siafiki hata kidogo wala siamini kuwa raia wa libya ni bora kuliko wa Ivory coast,Bahrain,Somalia,na kwingineko wanapopigana..mbona wakati Waisraeli wameua zaidi ya watoto 300 wa kipalestina hamna hatua zozote zilizochukuliwa?
  Kamwe haijawi kuwa sera ya America kuwapenda raia hata kutumia gharama kubwa kiasi hiki.Ghadafi ametoa mwito wa kukaa meza moja wamekataa...
  huu ni ubeberu mpya africa na
  Ni wazi mifumo ya afya,elimuni bora kuliko ya magharibi amefanya kile ambacho kimewashinda
  lazima tupinge kwa nguvu zetu wote
  Nalaani na nitaendelea kulaani mashambulizi haya ambayo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kweli. Na mimi nitakuwa moja kati ya sauti chache zinazopinga uvamizi wa Libya. Siku hizi ulimwengu wote umetishwa kufungua midomo yao dhidi ya nchi za magharibi ambazo zimejibatiza jina la kujipamba la (Jumuiya ya Kimataifa). Zamani tukiziita nchi za kibeberu (imperialists). Siku hizi hakuna anayethubutu tusema hilo neno, hasa viongozi wetu uchwara. Wanaogopa yanayompata Gaddafi sasa hivi. Amerika na wenzake wakiisha amua basi 'Jumuiya ya Kimataifa' imeamua. Tumerudi miaka hamsini nyuma. Ni ukoloni wa kificho.
   
 3. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  napinga pia hilo la uvamizi! lakini juz clinton kasema neno flan imebidi nifikiri mara nyingine. majeshi ya gadafi yangeruhusiwa kuingia bengazi si angewachinja wote maana alikuwa tayari ameizunguka! je kusingekuwa na mauaji ya halaiki.
   
 4. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi watu wakiongelea mauaji ya halaiki Rwanda, lazima wailaumu jumuia ya kimataifa sbb waliangalia tu wakati watu wanateketezwa, kila mtu ana haki ya kutoa maoni, lkn mara nyingine tujitendee haki, Gadaffi alitangaza mapema kuwa atawateketeza wapinzani wake wote, na kweli akawashambulia kwa ndege waandamanaji! Isingekuwa busara ateketeze watu wa miji ile huku mataifa yanaangalia tu, Arab League ilishinikiza sana azimio la UN kuhusu libya lipitishwe, leo hii watu hawataji hilo! Ivory Coast kuna mgogoro mkubwa lkn kuna mchakato AU na ECOWAS unaendelea, Somalia US walipeleka majeshi huko ikashindikana, na kwa wenye kumbukumbu US walipingwa sana na mataifa ya Middle East. Mi nadhani mara nyingine tuwe tunawalaumu mataifa ya kiarabu na nchi kama China, wana uwezo wa kuingilia baadhi ya migogoro lkn kazi yao ni kupiga makelele tu na kulaumu!!
   
 5. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  "UN" ni machinjio ya Waarabu tu
   
 6. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Mkuu clinton ni nani hata aweze kutabiri kuwa Gadafi angewachinja wote?siamini hata kidogo hizi ni propaganda just to justfy the means
   
 7. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Hebu rudia hapo kwenye red, ni nani kasema? Act yew great thinker!
   
 8. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  ghadafi hapo kabla alichukua miji ya las-ranuf, al-zuwahiya, brega na adjibiya, huko kote hakufanya mauaji ya halaiki, ni vipi basi hayo mauaji angeyafanya Benghazi?.

  Kitu kingine ni kwamba, kama wao wanawalinda Raia mbona basi wanawaacha waasi wanasonga mbele na kuteka miji, kwa maana hiyo jamaa wanatake sides!.
   
 9. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka hata Iraq walikuwa na madai mengine km silaha za maangamizi na mauaji ya wapinzani. Kilichotokea ni uharibifu wa miundombinu, raia walikufa wengi kuliko kabla ya vita na wanaendelea kuuana, huduma za kijamii kama maji na matibabu zilikuwa za kuridhisha kuliko sasa na kinachoendelea ni kunyonya mafuta kama vile hawana akili timamu.
  Hali ya Libya: Walibya walikuwa na hali nzuri kimaisha kuliko baadhi ya watu wa hizo nchi hizo zinazoishambulia Libya. Huduma za kijamii km maji, umeme, nyumba, gharama za kuoa, elimu mpaka chuo kikuu vyote hivyo ni bure, je nchi hizo zinafanya hivyo kwa raia wao??

  Kitakachotokea: kama ilivyo Iraq na Afganistan yatakayojiri ni mauaji ya raia kuuana kwa mabomu ya kujilipua, kuvurugika kwa huduma za kijamii nk. Raia watakufa wengi kuliko ilivyokuwa kabla ya uvamizi wa nchi za magharibi.

  Gharama za Vita: Gharama ya kurusha ndege moja ya kivita, bei ya makombora,meli za kivita, kuweka askari kule Mediteranian ni gharama sana, nani atalipa gharama hizo?? Ni kweli walipa kodi wa nchi hizo wako tayari kugharamia vita bure eti kwa ajili ya raia wa nchi nyingine?? Je gharama za maisha hazitapanda huko mkwao?? Majibu ni rahisi; Mafuta ya Libya.

  Kusudio la vita hivi linajulikana, tusijibaraguze kwa majibu rahisi.
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160


  pamoja na mambo mengine na hasira za kuangushwa ile ndege ya pan american airline kule scotland, wanadai gaddafi is the sponsor of terrorist. By the way what is terrorism?
   
 11. wasaimon

  wasaimon R I P

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nami napingana na uvamizi wa nchi za kimagharibi kwa Libya kwani sio sawa na kama yule jamaa hafai basi ilikuwa ni juu ya walibya wao wenyewe kuamua namna ya kumtoa na si kuomba msaada wa toka nje ili kumuondoa raisi aliyeko madarakani, nasikia wameonekana kwenye Tv hao waasi wakishangalia ushindi huku wakiwa wanapeperusha bendara ya mmarekani je hii inatufundisha kitu gani? TAFAKARI
   
 12. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Napata kigugumizi kuzungumzia tena masuala ya Libya kwa kua tokea awali nimekua against sana na mataifa ya Magharibi kuhusu uvamivi wa kijeshi dhidi ya Libya,na kwa mtazamo wangu nilidhani kwamba kuna zaidi ya kuwaokoa raia...
  Well,baada ya kuona wengi wanaunga mkono mashambulizi ya Western niliamua kukaa aside na kuperuzi kurasa..kwa mara nyingine tena napata utata kuhusu mahala pa kusimama kwa kua kwa mtazamo wa haraka haraka Gadaffi ni kiongozi shupavu na mpenda so called maendeleo ya wananchi wake wakati huo huo akiwa silent killer kwa wale wote walio against na utawala wake,na kweli aliwaua na anaua as well!
  Sina hakika km ilikua sahihi kwa mataifa ya kigeni kuingilia mapigano ya Libya lakini najiuliza ni nini ingekua hatma ya mji uliokaliwa na waasi km askari wanaomtii Col Gadaffi wangeufikia mji huu!
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Angalia concept nzima ya R2P (Responsibility To Protect) na implication yake katika International Relations after Rwanda.
   
 14. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waafrika wote ni omba omba, mbona China haki za binadamu hazifuatwi na hamna nchi za magharibi inayodhubutu kutia neno. Halafu wa magharibi wana tamaa, na waarabu hawana umoja pia mpaka gaddaf anatumia ndege kuua waandamanaji wao wamekaa kimya, sasa sijui kwa sababu wamezoea kuuwana.
   
 15. crome20

  crome20 JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 833
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Lakini Semeni Ghadafi si na yeye ana sehemu ya lawama katika hili? Unawezaje kutumia ndege za kijeshi kushambulia waandamanaji? Mbona kule yemeni, Misri na Tunisia hayakutokea haya?

  Then sheria ni suala pana unataka tuamini kuwa hicho kifungu tu ulichotaja hakina provision zingine? Ina maana hata nchi za Africa zinazotuwakilisha ktk Baraza la usalama la UN hajui hii? si Wangepinga basi hlafu ionekane kuwa wamelazimisha shinikizo la No FLY ZONE lakini walikubali.

  Sasa kwa nini wasilaumiwe wote wawili ili tuonekana hatuko biased na itikadi fulani?
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Huwezi kulinganisha commonplace abuse of human rights na tyrant aliyesema "nitawasaka mlango kwa mlango" ambaye alikuwa tayari kuua makumi ya maelfu ya watu kama sio zaidi huko Benghazi.
   
 17. S

  ShockStopper Senior Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 112
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Tumekusikia, lakini wacha nikukumbushe pia hii kitu moja. Paul Kagame mpaka kesho bado analaani UN kama wewe. Ila kinyume na wewe, yeye anadai kwa nini UN haikuvamia Rwanda kuzuia ile chinjachija ya mwaka 1994.

  Sasa fanya mdahalo na Kagame tupate mshindi mmoja.
   
Loading...