Baraza la usalama la UN kukutana kujadili uchaguzi Congo huku Kanisa katoliki likidai washajua Mshindi nani.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
Habari wadau.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linakutana Leo kujadili matokeo ya uchaguzi Congo DRC na hatma ya Taifa hilo baada ya matokeo.

Matokeo ya awali yanapaswa kutolewa tarehe 06/01/2018 lakini mwenyekiti wa CENI Cornel Nanga anadai huenda wakashindwa kutangaza matokeo siku hiyo kwani wamehesabu 20% tu ya kura. Hii ni tofaiti kabisa na katiba hususani kipengele cha matokeo ya uchaguzi mkuu. Hali hii imeibua wasiwasi nchini humo.

Baadhi ya wananchi wameanza kukimbilia Uganda wakihofia machafuko. Kanisa katoliki lililokuwa na waangalizi 40,000 nchini kote limedai linalo jina la mshindi na huenda wakamtangaza Rais muda wowote.

Kanisa hilo linatumia matokeo yaliyobandikwa kila kituo siku ya jioni baada ya uchaguzi kukamilika.
 
Hivi vyama tawala ndio chanzo cha machafuko na migogoro ktk Afrika kwani ktk uchaguzi wowote lazima waibe kura.

Sio rahisi kwao kushinda uchaguzi kwani wanakuwa hawajafanya la maana kuweza kuwashawishi wananchi wawape kura na wenyewe kwa kulifahamu hilo wanakuwa hawana namna ila kuiba kura ili waendelee kutawala.
 
K ukoo mzima

wamuombee nani?


Waniombee kwani nani kawapa mamlaka ya yakuombea



Wanamjua hata Mungu wangu?

Lumumba mk...wako hivi mnaona kila mtu humu ni mchama sio?

Wanatetea mashoga alafu waje kuniombea Mimi.



YESU RUDI MAPEMA

Yakitokea machafuko mnawaita wawaombee, wakichukua tahadhali mapema wameingilia siasa. Hamna jema Mbulura wa Lumumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom